Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Zamani wa Monduli (CCM) Hayati Edward Lowassa anazikwa leo Nyumbani kwake, Monduli. Mazishi haya yamehudhuriwa na viongozi wakuu wa Nchi wakiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Waombolezaji wametoa Salamu za Mwisho kwenye Jeneza la Hayati Lowassa, wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kisha famili ya Lowassa, viongozi wengine wa kitaifa pamoja na Viongozi waandamizi kutoka vyama vya upinzani, Freeman Mbowe na Zitto Kabwe.

Mazishi haya yataendeshwa kwa Sehemu mbili, Kidini na Kiserikali. Kwa upande wa Dini, Askofu Mkuu wa KKKT, Dkt. Alex Malasusa ataongoza ibada hiyo, kisha Jeshi la Wananchi la Tanzania litashiriki sehemu ya pili ya Mazishi hayo.

Kwa mujibu wa taratibu za Kijeshi, Hayati Lowassa atapigiwa mizinga 17 kwa heshima yake.

Saa 6:25 Mchana, Maafisa wa JWTZ wenye cheo cha Kanali wanauingiza Mwili wa Hayati Lowassa Kaburini. Zoezi hili linafuatiwa na kuweka mchanga kaburini kama sehemu ya kuaga.

Waache "WAFU" wazike "WAFU" wao...
 
CCM ni kundi kubwa sana la watu wasio na haya.

Jinsi walivyokuwa wanamtusi, wanamnyanyasa Lowassa na familia yake, walivyomuita "maiti", wakamtweza kwa Kila Hali, leo wanajifanya kububujikwa na machozi.

CCM walimdhadhalilisha sana Lowassa kiasi kwamba Leo tunapowaona wameongozana kwenda kwenye mazishi yake, tunajiuliza, KULIKONI???
Na wale waliowahi kumuita fisadi papa na kumuweka kwenye list of shame...na baadae kuja kutuambia kuwa mgombea wao na kumnadi kila pembe ya nchi nao tuwaweke kwenye kundi gani....????
 
Nafikiri siku ya leo TANESCO/serikali ingefumba macho kuruhusu umeme nchi nzima ili wananchi wafuatilie yanayojiri Monduli. Anyway kama kuna mkono wa mtu basi naye siku zake kuwe na mikwamo kwa watu wake
 
CCM ni kundi kubwa sana la watu wasio na haya.

Jinsi walivyokuwa wanamtusi, wanamnyanyasa Lowassa na familia yake, walivyomuita "maiti", wakamtweza kwa Kila Hali, leo wanajifanya kububujikwa na machozi.

CCM walimdhadhalilisha sana Lowassa kiasi kwamba Leo tunapowaona wameongozana kwenda kwenye mazishi yake, tunajiuliza, KULIKONI???
Unawezakuta msukuma na nape nao wapo msibani.
 
Na wale waliowahi kumuita fisadi papa na kumuweka kwenye list of shame...na baadae kuja kutuambia kuwa mgombea wao na kumnadi kila pembe ya nchi nao tuwaweke kwenye kundi gani....????
List of shame ilihusu Nini???

Aliyekuwa anamuita Lowassa fisadi Papa ni Lipumba na siyo CHADEMA.
 
Attachments

  • images (2).jpeg
    images (2).jpeg
    33.9 KB · Views: 2
Nipo tabata (temporarily), kwa ndugu na jamaa, tumeshindwa kuona matukio kwa sababu ya HAKUNA UMEME, mnaolea huu uzembe.......!, nisije kutukana, nimechukizwa mno!
 
Back
Top Bottom