Mazingira ya Lupaso Mtwara tumeyaona, tufanye marekebisho

Papa1

JF-Expert Member
Apr 21, 2012
2,017
2,208
Ndugu zangu, kwanza niwape pole kwa msiba mkubwa tulioupata kwa kuondokewa na jemedali wetu, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu William Benjamin Mkapa.

Moja kwa moja kwenye mada.

Wote tuliofuatilia maziko ya Bwana Benjamin huko Lupaso tumeona mazingira ya Lupaso. Nashawishika kusema kwamba huenda Rais Mstaafu hakupaendeleza kwa kuhofia kelele kama zile za taa za barabarani za Chato. Sasa Mzee keshajipumzikia, lakini eneo hilo sasa ni sehemu nyeti na litendelea kulindwa miaka yote, au miaka mingi ya hivi karibuni.

Ili kuweka kumbukumbu za viongozi wetu, napendekeza eneo hilo lijengwe kitu kisichofutika kirahisi kwa makusudi kabisa ya kuhifadhi kumbukumbu ya Mkapa.

Mimi napendekeza kijengwe chuo kikuu cha Benjamini Mkapa. Hiki ndio kitega uchumi endelevu kinachoweza kuhifadhi kumbukumbu yake nakuepuka sehemu hiyo kutupiliwa mbali na viongozi wa baadae wasiokuwa na karama ya kuthamini na kujali juhudi za waliotangulia.

Majirani walipwe fidia wapewe eneo jingine. Sehemu hiyo iwe ya Serikali na iwe sehemu ya museum.

Wewe una mawazo gani?
 
Mkuu, unawaza kila mahali atapozikwa basi tuwekeze mabilioni kwa ajili ya kumbukumbu yake! Ni upotevu wa raslimali na kutojua unachohitaji, nchi yetu tuko nyuma sana na tunatakiwa kutumia vema kila shilingi tunayoipata.
 
Back
Top Bottom