Utafiti mpya wabaini:Watanzania hawana imani na mawaziri
*Dkt. Shein awafunika Lowassa, maRC
*CCM pia yashindwa kufua dafu kwa JK
*Matumaini pekee yabakia kwa Kikwete
Na Rehema Mwakasese
UTAFITI uliofanywa na Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET), umeonesha kuwa idadi kubwa ya Watanzania hawaliamini Baraza la Mawaziri, ila Rais Jakaya Kikwete.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dar es Salaam jana, Mwenyekiti Mwenza wa REDET, Bw. Laurean Ndumbalo, alisema utafiti huo ulifanyika kuanzia Oktoba mwaka jana kwa mikoa yote nchini.
Bw. Ndumbalo alisema asilimia 30 ya wasomi wanapinga uongozi wa Rais Kikwete kwa sababu mbalimbali tangu aingie madarakani, zikiwamo za hali ya uchumi kuzidi kuporomoka, kupanda kwa hali ya maisha na kutofikiwa kwa ahadi ya 'Maisha bora kwa kila Mtanzania.'
Alisema asilimia 22 ya wasomi hao wanadai Rais Kikwete hajatimiza ahadi alizozitoa kwa wananchi na asilimia 11.6 walisema Rais amekuwa hafuatilii utekelezaji wa ahadi hizo.
Alizitaja sababu zingine zilizotolewa kuwa ni kutokana na kuchagua viongozi wasio na uwezo, ambao wameshindwa kuongoza na kufanya kazi zao kwa uadilifu na ufanisi na matokeo yake, hali ya maisha kwa wananchi inazidi kupanda.
Alisema viongozi hao wameshindwa kupambana na rushwa na kusaidia hali ya uchumi kupanda, kinyume chake uchumi unaporomoka siku hadi siku.
Bw. Ndumbaro alisema takwimu za kura ya maoni iliyofanyika Oktoba mwaka jana zilionesha asilimia 67 ya watu waliohojiwa, lakini idadi hiyo imepungua na kufikia asilimia 44, Oktoba mwaka huu.
Aliongeza kwamba wananchi walioonekana kuridhika kiasi na utendaji kazi wa Serikali ya Awamu ya Nne ni asilimia 40 na waliobaki walisema utendaji kazi wa Serikali ni wa kiwango cha chini.
Pia alisema pamoja na upungufu uliopo, Rais Kikwete anapaswa kuboresha maisha ya wananchi wake, jambo linalokwamishwa kwa kiasi kikubwa na Baraza lake la Mawaziri.
"Utendaji wa Baraza la Mawaziri ni mdogo ambao ni sawa na asilimia 20, Bunge asilimia 21.8, Jeshi la Polisi 24, Mahakama 21 na Serikali za Mitaa ni asilimia 32.5," alisema.
Alisema tathmini ya jumla inaonesha hali ya utendaji kazi wa Serikali iliyopo madarakani asilimia 26.5 wanaridhika, asilimia 39 wanaridhika kiasi, asilimia 32 hawaridhiki kabisa na katika taasisi zote, TAKUKURU inaongoza kuwa na asilimia 17 ambayo ni ndogo zaidi kuliko taasisi zingine.
Aliongeza kuwa sababu zilizokuwa zinatolewa juu ya utendaji kazi za Serikali, wananchi hawaridhiki kwani haifuatilii utekelezaji kwa asilimia 32.7, rushwa asilimia 24 na inapitisha mikataba mibovu kwa asilimia 10.9
Bw. Ndumbaro alisema kutokana na kuibuka hoja mbalimbali kuhusu mikataba ya madini na maslahi yake kwa Taifa, asilimia 15 ya waliohojiwa walisema wanaridhika, asilimia 16 wanaridhika kiasi na asilimia 48.4 hawaridhiki kwa jinsi Serikali inavyosimamia raslimali za nchi yakiwamo madini.
Aliongeza kuwa kwa upande vyama vya siasa, waliohojiwa walisema utendaji wa CCM na vya upinzani kwa ujumla katika mfumo huu wa vyama vingi, asilimia 40.7 wanaridhishwa na CCM, asilimia 34.3 wanaridhika kiasi na asilimia 23.3 hawaridhishwi.
Tathmini ya waliohojiwa inaonesha kuwa hawaridhiki na utendaji kazi wa vyama upinzani kwa asilimia 38.7, ikilinganishwa na wale wanaosema wanaridhika kwa asilimia 19 na asilimia 30 wanaridhika kwa wastani.
"Hata hivyo kwa ujumla waliohojiwa wanaonekana kuwa na imani zaidi kwa Rais Kikwete (56%) kuliko CCM (45%) na hata kuliko viongozi wakuu wa Serikali yake kama vile Makamu wa Rais (46%), waziri Mkuu (43%) na wakuu wa mikoa (36%)," ulisema utafiti.
Kwa mujibu wa utafiti huo, wilaya zilizoonesha kuridhishwa sana na utendaji wa Rais Kikwete ni Kishapu (90%), Chamwino (84%), Unguja Kati (83%), Unguja Mjini (82.6%), Uyui (76%), Unguja Kaskazini A (74%) na Muleba (62%).
Wilaya zisizoridhishwa na utendaji wake ni Chake Chake (42%), Kilwa (38%), Kinondoni (38%), Kibaha (38%), Kilosa (34%), Mbarali (34%) na Moshi Mjini(32%).
"Cha kushangaza ni kwamba wilaya ya Mbarali hakuna hata mmoja kati ya waliohojiwa aliyesema anaridhika sana na utendaji wa Rais...inawezekana hatua ya Serikali kuhifadhi mazingira kwa kudhibiti matumizi ya bonde la Mto Ihefu imechangia," ulisema utafiti.
Utafiti huo ulifanywa katika mikoa 26 ya Tanzania, kuanzia Oktoba 22 mpaka 28 mwaka huu, ambapo watu 1,300 walihojiwa na kutoa mapendekezo yao wakiwamo wasomi na wasio wasomi.
Source: Majira