Mazingaombwe ya REDET: Utafiti mpya wabaini Watanzania hawana imani na mawaziri

Keil

JF-Expert Member
Jul 2, 2007
2,214
802
Utafiti mpya wabaini:Watanzania hawana imani na mawaziri

*Dkt. Shein awafunika Lowassa, maRC
*CCM pia yashindwa kufua dafu kwa JK
*Matumaini pekee yabakia kwa Kikwete


Na Rehema Mwakasese

UTAFITI uliofanywa na Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET), umeonesha kuwa idadi kubwa ya Watanzania hawaliamini Baraza la Mawaziri, ila Rais Jakaya Kikwete.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dar es Salaam jana, Mwenyekiti Mwenza wa REDET, Bw. Laurean Ndumbalo, alisema utafiti huo ulifanyika kuanzia Oktoba mwaka jana kwa mikoa yote nchini.

Bw. Ndumbalo alisema asilimia 30 ya wasomi wanapinga uongozi wa Rais Kikwete kwa sababu mbalimbali tangu aingie madarakani, zikiwamo za hali ya uchumi kuzidi kuporomoka, kupanda kwa hali ya maisha na kutofikiwa kwa ahadi ya 'Maisha bora kwa kila Mtanzania.'

Alisema asilimia 22 ya wasomi hao wanadai Rais Kikwete hajatimiza ahadi alizozitoa kwa wananchi na asilimia 11.6 walisema Rais amekuwa hafuatilii utekelezaji wa ahadi hizo.

Alizitaja sababu zingine zilizotolewa kuwa ni kutokana na kuchagua viongozi wasio na uwezo, ambao wameshindwa kuongoza na kufanya kazi zao kwa uadilifu na ufanisi na matokeo yake, hali ya maisha kwa wananchi inazidi kupanda.

Alisema viongozi hao wameshindwa kupambana na rushwa na kusaidia hali ya uchumi kupanda, kinyume chake uchumi unaporomoka siku hadi siku.

Bw. Ndumbaro alisema takwimu za kura ya maoni iliyofanyika Oktoba mwaka jana zilionesha asilimia 67 ya watu waliohojiwa, lakini idadi hiyo imepungua na kufikia asilimia 44, Oktoba mwaka huu.

Aliongeza kwamba wananchi walioonekana kuridhika kiasi na utendaji kazi wa Serikali ya Awamu ya Nne ni asilimia 40 na waliobaki walisema utendaji kazi wa Serikali ni wa kiwango cha chini.

Pia alisema pamoja na upungufu uliopo, Rais Kikwete anapaswa kuboresha maisha ya wananchi wake, jambo linalokwamishwa kwa kiasi kikubwa na Baraza lake la Mawaziri.

"Utendaji wa Baraza la Mawaziri ni mdogo ambao ni sawa na asilimia 20, Bunge asilimia 21.8, Jeshi la Polisi 24, Mahakama 21 na Serikali za Mitaa ni asilimia 32.5," alisema.

Alisema tathmini ya jumla inaonesha hali ya utendaji kazi wa Serikali iliyopo madarakani asilimia 26.5 wanaridhika, asilimia 39 wanaridhika kiasi, asilimia 32 hawaridhiki kabisa na katika taasisi zote, TAKUKURU inaongoza kuwa na asilimia 17 ambayo ni ndogo zaidi kuliko taasisi zingine.

Aliongeza kuwa sababu zilizokuwa zinatolewa juu ya utendaji kazi za Serikali, wananchi hawaridhiki kwani haifuatilii utekelezaji kwa asilimia 32.7, rushwa asilimia 24 na inapitisha mikataba mibovu kwa asilimia 10.9

Bw. Ndumbaro alisema kutokana na kuibuka hoja mbalimbali kuhusu mikataba ya madini na maslahi yake kwa Taifa, asilimia 15 ya waliohojiwa walisema wanaridhika, asilimia 16 wanaridhika kiasi na asilimia 48.4 hawaridhiki kwa jinsi Serikali inavyosimamia raslimali za nchi yakiwamo madini.

Aliongeza kuwa kwa upande vyama vya siasa, waliohojiwa walisema utendaji wa CCM na vya upinzani kwa ujumla katika mfumo huu wa vyama vingi, asilimia 40.7 wanaridhishwa na CCM, asilimia 34.3 wanaridhika kiasi na asilimia 23.3 hawaridhishwi.

Tathmini ya waliohojiwa inaonesha kuwa hawaridhiki na utendaji kazi wa vyama upinzani kwa asilimia 38.7, ikilinganishwa na wale wanaosema wanaridhika kwa asilimia 19 na asilimia 30 wanaridhika kwa wastani.

"Hata hivyo kwa ujumla waliohojiwa wanaonekana kuwa na imani zaidi kwa Rais Kikwete (56%) kuliko CCM (45%) na hata kuliko viongozi wakuu wa Serikali yake kama vile Makamu wa Rais (46%), waziri Mkuu (43%) na wakuu wa mikoa (36%)," ulisema utafiti.

Kwa mujibu wa utafiti huo, wilaya zilizoonesha kuridhishwa sana na utendaji wa Rais Kikwete ni Kishapu (90%), Chamwino (84%), Unguja Kati (83%), Unguja Mjini (82.6%), Uyui (76%), Unguja Kaskazini A (74%) na Muleba (62%).

Wilaya zisizoridhishwa na utendaji wake ni Chake Chake (42%), Kilwa (38%), Kinondoni (38%), Kibaha (38%), Kilosa (34%), Mbarali (34%) na Moshi Mjini(32%).

"Cha kushangaza ni kwamba wilaya ya Mbarali hakuna hata mmoja kati ya waliohojiwa aliyesema anaridhika sana na utendaji wa Rais...inawezekana hatua ya Serikali kuhifadhi mazingira kwa kudhibiti matumizi ya bonde la Mto Ihefu imechangia," ulisema utafiti.

Utafiti huo ulifanywa katika mikoa 26 ya Tanzania, kuanzia Oktoba 22 mpaka 28 mwaka huu, ambapo watu 1,300 walihojiwa na kutoa mapendekezo yao wakiwamo wasomi na wasio wasomi.

Source: Majira
 
Katika maisha yangu nimewahi kupata nafasi ya kuona takwimu za utafiti, nyingi tu. Lakini lazima nikiri sijawahi kuona takwimu ziliwasilishwa kijinga kama hizi, yaani kile ambacho takwimu zinasema hawakisemi!
 
Katika maisha yangu nimewahi kupata nafasi ya kuona takwimu za utafiti, nyingi tu. Lakini lazima nikiri sijawahi kuona takwimu ziliwasilishwa kijinga kama hizi, yaani kile ambacho takwimu zinasema hawakisemi!

Hebu fafanua mzee una maana gani?. au una takwimu nyingine tofauti?
 
Nilivyoelewa mimi hii article ime-summarize opinion poll, siwezi kutegemea article hii itoe the nitty gritties.Kama kuna beef basi iwe ni jinsi ya data zilivyopatikana na authenticity. Article bomba, sijawahi kuona Tanzania tunafanya polling kama hivi.It is a good start.Kama tunaweza kupata a fuller report from the polling body itakuwa bomba.
 
Mimi nadhani Gazeti lililoripoti ndo limejaribu kuspin mambo, kiufupi Takwimu zimewekwa wazi na inaonyesha wananchi hawana Imani na utendaji wa serikali wa sasa. Mambo ya sijui ooh Kikwete safi ila baraza la mawaziri ndo baya, ninadhani watu wa gazeti hilo lililoripoti la Majira ndo wanapindisha mambo.

Kiufupi Kikwete ndo Mwenyekiti wa baraza la mawaziri, kwa hiyo kama wananchi wengi hawana imani na baraza la mawaziri basi maana yake wanatuma meseji kwa kikwete kwamba hawajaridhishwa na utendaji wa serikali yake period
 
takwimu za redet ni kichefuchefu....huwezi kusema jk ni bora kuliko chama ..wakati yeye ndio rais na mwenyekiti wa chama.....

mawaziri hawawezi kuwa wabovu ..alafu useme rais safii...kwa kuwa anawelea lea ..lazima kuna walakini na ripoti ya redet ingeenda mbali kuhalalisha hilo...

nani asiyejua mukandara...aliyetoa ripoti ya kura za maoni iliyohalalisha ...wizi wa kura utakaotokea 2005...

mukandara hana jipya...
 
Hivi kazi ya Rais ni nini kama hausiki moja kwa moja na utendaji wa vile ambavyo wananchi hawana imani navyo?!

Utendaji Baraza la Mawaziri washuka


*Wananchi hawana imani na mawaziri

*Mikataba mibovu ya madini moja ya chanzo

*Utafiti waonyesha wananchi wana imani na JK
*Wakosa imani na Takukuru, Bunge, Mahakama, Polisi


Muhibu Said na Peter Edson


IMANI ya wananchi kuhusiana na utendaji kazi wa serikali, Bunge na Mahakama imeporomoka huku ule wa Rais Jakaya Kikwete binafsi ukiwa si mbaya ukilinganisha na taasisi hizo.


Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia (Redet) iliyo chini ya Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kiwango cha wananchi kuridhika sana na utendaji wa vyombo vikuu kama Baraza la Mawaziri na Bunge umepungua katika kipindi cha kati ya Oktoba mwaka jana na Oktoba mwaka huu, huku kiwango cha kutoridhika kikiongezeka mara dufu.



Katika utafiti huo, wananchi wameelezea sababu za kutoridhika na utendaji kazi wa taasisi hizo ni kuwa ni kushindwa kutofuatilia utekelezaji, kujihusisha na rushwa, kupitisha mikataba mibovu ya madini na kutokutoa mikopo au mitaji. Sababu nyingine ni kutopandisha mishahara ya wafanyakazi.


Taarifa hiyo ya Redet, inaonyesha kwamba kiwango cha kuridhika sana na utendaji kazi wa Bunge umepungua kutoka asilimia 39.2 mwaka 2006 hadi asilimia 21.8 mwaka 2007, huku kwa wananchi wasioridhika na utendaji kazi wa chombo hicho ukiongezeka kutoka 11.3 mwaka 2006 hadi asilimia 25 mwaka 2007.


Kwa upande wa Baraza la Mawaziri, kiwango cha kuridhika sana na utendaji kazi wa baraza hilo kimepungua kutoka asilimia 33.8 mwaka 2006 hadi asilimia 20.1 mwaka huu.


Katika kukosa imani ya utendaji kwa taasisi hizo, wananchi wameonyesha wasiwasi mkubwa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (PCCB) ikiongoza kwa kuwa na asilimia ndogo zaidi ya utendaji kazi kati ya taasisi zote za serikali katika kipindi hicho.


Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti Mwenza wa Redet, Dk Laurean Ndumbaro, alisema utafiti huo ulifanywa Oktoba 22-28, mwaka huu, kwa kuendesha kura ya maoni kwa kuwahoji wananchi katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na Visiwani.


Dk Ndumbaro alisema kulinganisha na kura ya maoni iliyofanyika Oktoba mwaka jana kutathmini mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Kikwete tangu aingie madarakani, asilimia ya waliohojiwa ambao wanasema wanaridhika sana na utendaji wake, imepungua kutoka asilimia 67.4 mwaka jana hadi asilimia 44.4 mwaka huu.


Alisema waliohojiwa, walitakiwa kutoa maoni yao iwapo wanaridhishwa au la ambapo asilimia 44.4 walisema kuwa wanaridhishwa sana wakati asilimia 35.0 walisema wanaridhika kiasi na asilimia 18.6 wakasema hawaridhiki na utendaji kazi wa Rais Kikwete.


Mbali na hilo, Dk Ndumbaro alisema pia idadi ya waliohojiwa na kusema hawaridhiki na utendaji kazi wa Rais Kikwete, imeongezeka maradufu kutoka asilimia 7.8 hadi asilimia 18.6 na kwamba, idadi ya waliohojiwa wanaosema wanaridhika kiasi, imeongezeka kutoka asilimia 23 ya mwaka jana hadi asilimia 35.


Alisema wale ambao walisema wanaridhika kiasi na wale ambao hawaridhiki, walitakiwa kueleza sababu za tathmini yao ambapo theluthi moja ya wahojiwa (sawa na asilimia 30.4), walisema Rais Kikwete ameshindwa kuboresha hali ya maisha wakati takriban asilimia 22, walisema hajatimiza ahadi na asilimia 11.6 walisema imetokana na kutofuatilia utekelezaji.


Dk Ndumbaro alisema sababu nyingine zilizotolewa na wahojiwa, ni Rais Kikwete kuteua viongozi wabovu (asilimia 9.1) na kushindwa kupambana na rushwa (asilimia 5.6).


Hata hivyo, alisema utafiti huo pia ulijaribu kutathmini kiwango cha imani ya wananchi kwa viongozi wao wa ngazi za juu na matokeo kuonyesha kwamba pamoja na Rais Kikwete kupata asilimia 44.4 ya wahojiwa waliosema wanaridhika sana na utendaji kazi wake, zaidi ya nusu ya wahojiwa (asilimia 56), walisema kwamba wana imani naye.


"Imani hii ya wananchi kwa Rais Jakaya Kikwete inajidhihirisha hata pale wahojiwa wanapoulizwa kutaja jina la mwanasiasa mashuhuri anayewafurahisha katika utendaji wake wa kazi," alisema Dk Ndumbaro.


Alisema katika swali hilo, pia Rais Kikwete anaongoza kwa kumzidi anayemfuatia ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kwa zaidi ya mara tatu.


Dk Ndumbaro alisema Rais Kikwete alitajwa na asilimia 32 akifuatiwa na Zitto aliyetajwa na asilimia 10 na Lowassa aliyetajwa na asilimia 5.8 ya wahojiwa wote na kwamba, wanasiasa wengine wametajwa kwa asilimia ndogo.


Alisema wahojiwa waliosema wanaridhika sana na utendaji kazi wa Baraza la Mawaziri, ni asilimia 20, huku Bunge likiwa na asilimia 21.8 na idadi ndogo pia kwa Jeshi la Polisi (asilimia 24), Mahakama (asilimia 21) na serikali za mitaa (asilimia 32.5).


"Maoni haya yanashabihiana na pale wahojiwa wanapoulizwa kutoa tathmini ya jumla ya utendaji kazi wa serikali nzima iliyopo madarakani. Asilimia 26.5 walisema wanaridhika sana, asilimia 39 walisema wanaridhika kiasi na asilimia 32 walisema hawaridhiki," alisema Dk Ndumbaro.


Alisema kati ya taasisi zote, PCCB inaongoza kwa kuwa na asilimia ndogo zaidi ya wahojiwa waliosema kwamba wanaridhika sana na utendaji wake wa kazi (asilimia 17), huku ikiwa na idadi kubwa ya wahojiwa waliosema hawaridhiki (asilimia 33).


Hata hivyo, Dk Ndumbaro alisema matokeo hayo yanaonyesha kwamba, wahojiwa wanaridhika zaidi na utendaji kazi wa Rais Kikwete kuliko wanavyoridhishwa na utendaji kazi wa serikali yake.


"Hii inajidhihirisha pale ambapo tunaona kwamba wakati asilimia 44 ya wahojiwa wote walisema wanaridhika sana na utendaji kazi wa Rais Kikwete, kiwango cha kuridhika sana na utendaji kazi wa serikali nzima ni asilimia 26.5 na asilimia 20 kwa Baraza la Mawaziri. Hii inaonyesha kwamba watu wengi wana imani na Rais Kikwete hata pale ambapo utendaji kazi wa baadhi ya taasisi zilizo ndani ya serikali yake haziwaridhishi sana," alisema Dk Ndumbaro.


Alisema tathmini ya utendaji kazi wa serikali nzima iliyopo madarakani, wahojiwa ambao walisema wanaridhika au hawaridhiki, walitakiwa watoe sababu za maoni yao ambapo baadhi ya sababu zilizotolewa ni pamoja na serikali kutofuatilia utekelezaji (asilimia 32.7), kujihusisha na rushwa (asilimia 24) na kupitisha mikataba mibovu ya madini (asilimia 10.9).


Dk Ndumbaro alisema kutokana na kuibuka kwa hoja mbalimbali kuhusu mikataba ya madini na maslahi yake kwa taifa, wahojiwa walitakiwa kutoa maoni yao kuhusu tathmini yao iwapo wanaridhika au la na namna serikali inavyosimamia rasilimali za nchi, hasa madini ambapo asilimia 15 ya wahojiwa wote ndio walisema wanaridihika sana wakati asilimia 16 walisema wanaridhika kiasi.


Hata hivyo, alisema karibu nusu ya wahojiwa wote (asilimia 48.4), walisema hawaridhiki kwa jinsi serikali inavyosimamia rasilimali za nchi, yakiwamo madini.


Alisema kulinganisha maoni ya wahojiwa ya Oktoba mwaka jana na yale ya Oktoba mwaka huu, utendaji kazi wa vyombo vikuu, kama Baraza la Mawaziri na Bunge, kiwango cha 'kuridhika sana', kimepungua, wakati kiwango cha kuridhika kiasi, kimeongezeka na kile kiwango cha wahojiwa wanaosema 'hawaridhiki' kimeongezeka maradufu.


Dk Ndumbaro alisema kiwango cha kuridhika sana na utendaji kazi wa Bunge, kimepungua kutoka asilimia 39.2 mwaka jana hadi asilimia 21.8 mwaka huu na kwamba, kile cha wasioridhika na utendaji kazi wa Bunge, kimeongezeka kutoka asilimia 11.3 mwaka jana hadi asilimia 25 mwaka huu.


Alisema kwa upande wa Baraza la Mawaziri, kiwango cha kuridhika sana na utendaji kazi wa baraza hilo, kimepungua kutoka asilimia 33.8 mwaka jana hadi asilimia 20.1 mwaka huu ambapo kiwango cha wasioridhika, kimeongezeka kwa asilimia 10 katika kipindi hicho.


Dk Ndumbaro alisema upande wa utendaji kazi wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Amani Abeid Karume, ni asilimia 35.5 ya wahojiwa wote wa Zanzibar ndio walisema wanaridhika sana, asilimia 30.6 wanaridhika kiasi na asilimia 31.5 walisema hawaridhiki.


Alisema walipoulizwa sababu za kuridhika kiasi au kutoridhika na utendaji kazi wa rais huyo, wahojiwa walitaja sababu mbalimbali, ikiwamo kushindwa kuboresha hali ya maisha (asilimia 37.5), kutotimiza ahadi (asilimia 17.3), kutofuatilia utekelezaji (asilimia 11.7), kuteua viongozi wabovu (asilimia 10) na kushindwa kupambana na rushwa (asilimia 6).


Dk Ndumbaro alisema kulinganisha na matokeo hayo na yale ya utafiti wa Oktoba mwaka jana, idadi ya wahojiwa wanaosema wanaridhika sana na utendaji wa rais huyo, imepungua kutoka asilimia 47.8 Oktoba mwaka jana hadi asilimia 35.5 Oktoba mwaka huu.


Hata hivyo, alisema kuna takriban theluthi moja ya wahojiwa ambao wanasema hawaridhiki na utendaji kazi wa baraza la wawakilishi (asilimia 30.2) na serikali nzima ya SMZ (asilimia 31.9).


Kuhusu utendaji kazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vyama vya upinzani, Dk Ndumbaro alisema wahojiwa waliulizwa kutoa tathmini yao na asilimia 40.7 walisema wanaridhika sana na utendaji kazi wa CCM ambapo wale waliosema wanaridhika kiasi ni asilimia 34.3 na asilimia 23.3 walisema hawaridhiki.


Alisema kwa upande wa vyama vya upinzani, tathmini ya wahojiwa ya utendaji kazi wa vyama hivyo, inaonyesha kuwa idadi kubwa ya wahojiwa hawaridhiki na utendaji wao (38.7) kulinganisha na wale wanaosema wanaridhika sana (19) au wanaridhika kiasi (30.3).


Dk Ndumbaro alisema wahojiwa waliulizwa sababu za kuridhika kiasi au kutoridhika na utendaji kazi wa CCM na kutaja kuwa hakitimizi ahadi (asilimia 19.6), viongozi wake ni wabovu (asilimia 10.8) na viongozi wake ni wala rushwa (10.1).


Alisema wahojiwa waliulizwa kutaja sababu za kuridhika kiasi au kutoridhika na utendaji kazi wa vyama vya upinzani na kutaja sababu mbalimbali, ikiwamo kuwa na migogoro (asilimia 15), kutokuwa na sera (8.6) na kutokuwa na uwezo wa kuongoza nchi (asilimia 8.4).


Dk Ndumbaro alisema kulinganisha matokeo hayo na yale ya Oktoba mwaka jana , idadi ya wahojiwa waliosema wanaridhika sana na utendaji kazi wa CCM, imepungua kutoka asilimia 60 Oktoba mwaka jana hadi asilimia 40.7 Oktoba mwaka huu na kwamba, idadi iliyoongezeka ni ya wale ambao wanasema wanaridhika kiasi (kutoka asilimia 25.5 hadi 34) na ya wale wanaosema hawaridhiki (asilimia 12 hadi 23).


"Ukiangalia kwa makini kwa upande wa upinzani, ingawa kuna idadi ndogo ya wahojiwa wanaosema wanaridhika sana na utendaji kazi wa vyama vya upinzani katika tafiti zote mbili, hata hivyo kuna mabadiliko ya maoni katika vipengele vingine. Idadi ya wale wanaosema wanaridhishwa kiasi imeongezeka kutoka asilimia 23 hapo Oktoba 2006 hadi asilimia 30 Oktoba mwaka huu. Pia asilimia ya wale ambao wanasema hawaridhiki na utendaji kazi wa vyama vya upinzani imepungua kutoka asilimia 51 hapo Oktoba 2006 hadi asilimia 38.7 Oktoba mwaka huu.


"Hata hivyo, ingawa kiwango cha kuridhika sana na utendaji kazi wa CCM umepungua kwa takriban asilimia 20, haimaanishi kwamba kiwango cha kuridhika sana na utendaji wa kazi wa vyama vya upinzani umeongezeka. Idadi ya wahojiwa wanaosema wanaridhika sana na utendaji kazi wa upinzani umeongezeka kwa asilimia 0.8 tu," alisema Dk Ndumbaro.


Alisema kati ya viongozi wote waliofanyiwa tathmini hiyo ya imani ya wananchi kwao, ni mawaziri ndio wanaopata kiwango cha chini cha wahojiwa wanaosema wana imani sana (asilimia 23.5) na kiwango cha juu cha wahojiwa wanaosema wana imani kiasi na mawaziri (aslimia 40.5) na kwamba, kiongozi anayeongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wahojiwa wanaosema hawana imani, ni mbunge ambapo asilimia 32 walisema hawana imani na mbunge wao.


Dk Ndumbaro alisema wahojiwa pia waliulizwa kuhusu imani yao kwa CCM na vyama vya upinzani na matokeo kuonyesha kwamba, wengi wao wanasema wana imani sana na chama hicho kwa asilimia 45 kuliko vyama hivyo (asilimia 14).


Alisema wale wanaosema hawana imani, ni wengi zaidi kwa upande wa vyama vya upinzani (asilimia 38 kuliko CCM (asilimia 17) na kwamba, wahojiwa wanaonekana kuwa na imani zaidi kwa Rais Kikwete (asilimia 56) kuliko CCM (asilimia 45) na hata kuliko viongozi wakuu wa serikai yake, akiwamo Makamu wa Rais, Dk Ali Mohamed Shein (asilimia 46), Lowassa (asilimia 43) na wakuu wa mikoa (asilimia 36).


Dk Ndumbaro alisema wahojiwa waliulizwa kutaja tatizo moja kubwa ambalo wanaliona kama kero kwao ambalo linahitaji ufumbuzi na kuonyesha kuwa ni huduma mbaya za jamii, kama vile afya, elimu, maji, umeme na barabara ambalo lilitajwa na theluthi moja ya wahojiwa wote (asilimia 31) na kufuatiwa na kupanda kwa gharama za maisha (asilimia 28), ukosefu wa ajira (asilimia 7), rushwa (asilimia 6), viongozi walioko madarakani (asilimia 4) na mikataba mibovu/isiyo na maslahi kwa taifa (asilimia 3).


Alisema anatarajia kuwa matokeo hayo, yatatoa mwanga kwa viongozi wa serikali kuhusu uchapakazi wao pamoja na masuala ambayo wananchi wangependa yapewe kipaumbele.


Alisema maoni ya wote waliohojiwa, yalichangiwa kwa kiasi fulani na matukio makubwa yaliyojitokeza katika kipindi hicho.


Dk Ndumbaro alisema katika utafiti huo, sampuli nasibu ilitumika kuchagua wilaya moja katika mkoa na kwamba, jumla ya wahojiwa, ilikuwa ni 1,300, ikiwa ni wahojiwa 50 kutoka katika kila wilaya iliyochaguliwa.


"Lengo kuu la utafiti huu ni kuboresha shughuli za serikali kwa kuleta maendeleo kwa watu walio wengi na kuimarisha demokrasia nchini," alisema Dk Ndumbaro.


Akielezea mfumo wa ukusanyaji maoni, Dk Ndumbaro alisema utafiti huo ulifanyika katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani. Sampuli ilichaguliwa kwa kutumia ngazi tatu ambazo ni wilaya, vijiji/mitaa na wahojiwa. Katika kila ngazi, sampuli ilipatikana kwa kutumia mtindo wa sampuli nasibu (random sampling method)

Source link: Mwananchi.

Habari hizo kwenye Gurdian:
JK eclipses Govt in performance rating

2007-12-05 08:51:52
By Austin Beyadi


The public rating of President Jakaya Kikwete`s performance over the past year is a lot better than that of the Government as a whole, according to a recent study.

The study was conducted by the University of Dar es Salaam`s Research and Education Democracy in Tanzania (REDET) project.

It showed State organs as having attracted rising levels of public discontent and disillusionment during the period under review.

Revealing the findings of the study to journalists in Dar es Salaam yesterday, REDET Acting Chairman Laurean Ndumbaro said the level of public dissatisfaction has risen from 7.8 per cent last year to 18.6 per cent this year.

He pointed out a bigger number of Tanzanians put more trust in the President than in the larger State machinery.

Elaborating, he explained that an average of one in every five Tanzanians contacted for comment said they were not satisfied with the performance of the cabinet ministers.

Another 17 per cent of the respondents said that they were not satisfied with the performance of the recently reconstituted Prevention and Combating of Corruption Bureau.

According to the study, the schools.

Districts where most respondents said they were satisfied with President Kikwete's performance are Kishapu (90 per cent rating), Chamwino (84), Unguja Central (83), Unguja Urban (82.6), Unguja West A (74), and Muleba (62).

Meanwhile, districts where the President's performance had the lowest rating are Chake Chake (42 per cent), Kilwa (38), Kinondoni (38), Kibaha (34), and Moshi Urban (32).

The REDET executive noted none of the respondents in Mbarali District expressed satisfaction with the President`s performance, the blanket explanation given being that the President had failed to improve the lives of Tanzanians as per his election-time promise.

But Ndumbaro hinted that the negative response could mainly be attributed to the decision by government authorities there to conserve the environment by banning the use of Ihefu Valley.

The REDET study was conducted between October 22 last year and October 28 this year and involved one district in each of the country`s 26 regions, five of them in Zanzibar.

Each district had 50 respondents picked randomly down to the village level.

SOURCE: Guardian
Source link: Ippmedia.

SteveD.
 
Gamba wewe hujui wabongo tulivyo na mambo ya kujigonga gonga kwa big men.Hapo gazeti linaandika huku linajishtukia.Al Pacino anakwambia if you wanna shoot shoot, don't talk.If you want to blast the government blast, don't flip flop mara Kikwete mzuri wabaya mawaziri.Ndiyo hawa hawa wanaotuambia Kikwete mzuri wabaya washauri. If that is the case then by virtue of not knowing to appoint or by virtue of not knowing bad advice he is more dangerous as a president, due to inability to judge.
 
Inawezekana lengo la REDET ni kurudisha imani ya wananchi kwa Rais wao. Hapa naona REDET wanafanya kazi ya kuokoa jahazi kwa kuwa mawaziri watakuja kujiokoa wenyewe kwenye majimbo yao ya uchaguzi come 2010! Ila kwa sasa kinachotakiwa ni kuonyesha kwamba Kikwete bado ni bomba wakati wengine wanambondea kwamba kashindwa kazi ya urais.
 
''Districts where most respondents said they were satisfied with President Kikwete's performance are Kishapu (90 per cent rating), Chamwino (84), Unguja Central (83), Unguja Urban (82.6), Unguja West A (74), and Muleba (62). ''


such disrticts ?. Actually they have right to admire him ...........????? Labda wanendelea kuadmire haiba ya Muungwana
 
Naomba mtu akiweza a-post article ya Tanzania Daima. I think that it provides a more accurate picture. Ukweli ni kwamba JK kapoteza umaarufu 23%! NOw that's news siyo kwamba maarufu kuliko baraza. That was the case October last year.
Mi nadhani analysis iliyofanywa na waandishi ni bomu. We need to get the study itself! Kama mtu anayo naomba atume, au ndiyo wimbo tuliokuwa tunasubiri from Mzee Mwnkjj?
 
Mimi nafikiri hiyo research ya REDET inawakilisha maoni ya Watanzania. Uchunguzi wangu binafsi hata kama sio wa kisayansi
unatoa matokeo ambayo yanakaribiana na hayo.

Pamoja na serikali ya JK kuboronga lakini watu walio wengi bado
wanampa nafasi JK na badala yake wanapeleka lawama kwa watu wengine kama baraza la mawaziri na watendaji wengine. Je hilo ni kweli? Hata mimi zamani nilikuwa naamini hivyo lakini sasa naanza kuona kwamba huenda tatizo liko kwa mkuu mwenyewe.

Matokeo ya REDET ni mabaya sana kuliko hata nilivyotegemea, pamoja na mwandishi kuyaonyesha in a positive way kwa JK lakini
ukimpa mchambuzi wa siasa anaweza kutoa maana ambayo ni mbaya sana kwa JK. Popularity ya rais iko chini (56) na wanaoridhika na utendaji wake asilimia 44, hizo namba ni mbaya mno hasa kwa rais aliyeingia madarakani kwa asilimia zaidi ya 80.

Lazima pia muelewe jamii za kiafrika, kunapokuwa na makosa tunalaumu wasaidizi, ndio maana hata kwenye bao, mkubwa anajamba, wanasingiziwa watoto. Hao PCCB inaelekea wameshindwa kabisa kufanya kazi, ili wafanikiwe inatakiwa wananchi wawe na imani nao, watapataje ushirikiano wa wananchi, kama zaidi ya asilimia 80 ya wananchi hawana imani nao?

JK amka, serikali yako inaenda pabaya, rudisha imani za wananchi kwa kutimiza uliyoahidi wakati wa uchaguzi. Huhitaji maajabu, kinachotakiwa ni wewe mwenyewe kuwajibika na kuwafanya viongozi chini yako kuwajibika.

Somo kwa upinzani, watch out huko wilayani, wananchi bado nwanamjua JK tu.
 
"Cha kushangaza ni kwamba wilaya ya Mbarali hakuna hata mmoja kati ya waliohojiwa aliyesema anaridhika sana na utendaji wa Rais...inawezekana hatua ya Serikali kuhifadhi mazingira kwa kudhibiti matumizi ya bonde la Mto Ihefu imechangia," ulisema utafiti.

sasa hiyo ya mbarali ambako hakuna hata mtu mmoja anayeridhishwas na utendaji wa muungwana si ingepaswa iwe sifuri???????? 0%
 
Unajua hawa REDET wanajishushia hadhi kwa kutoa majibu contradictory kama fadhila Mkandala keshapewa au anaogopa atanyanganywa fadhila?
Haingii akilini ati raisi safi mawazili hovyo ni kujikosha tuu!
Yeye ndo anaewachagua hao wote na kwake they are the best among all the Tanzanians akijua watadeliver accordingly leo unasema wateule hao hovyo.Indirectly ni sawa na kusema aliyewateua nae hafai.
REDET msimpake mju mafuta kwa mgongo wa chupa "A SPADE IS A SPADE NOT A BIG SPOON"
 
"Who said data are important? What is important is how you interplate them" Mtanzania

Poll: Kikwete approval rating dips to 44 per cent (Thisday)


DAMAS MWITA
Dar es Salaam

PRESIDENT Jakaya Kikwete’s popularity has dipped to 44.4 per cent, with the majority of Tanzanians who responded to a new opinion poll saying the fourth phase government has so far failed to improve their living conditions.

A previous opinion poll conducted about a year ago put the president’s approval rating at 67 per cent.

About a third of the respondents in the latest opinion poll said they disapprove of the performance of the entire government currently in office.

The findings represent a further significant decline in Mr Kikwete’s approval ratings after recording a landslide victory of over 80 per cent of votes cast across the country in the 2005 presidential elections.

A total of 1,300 adult Tanzanians from the mainland and Zanzibar were interviewed for the latest opinion poll results unveiled yesterday by the Research and Education for Democracy in Tanzania (REDET).

While 44.4 per cent of Tanzanians polled said they ’’approved’’ of Kikwete’s handling of his job as president, another 35 per cent ticked the box showing only ’’slight approval’’, 18.6 said they ’’disapproved’’ and two per cent were undecided.

The number of Tanzanians who said they disapproved of the president’s leadership more than doubled, from just 7.8 per cent recorded last year.

Among the sampling of Tanzanians who said they disapprove of Kikwete’s leadership, 30.4 per cent said he has failed to improve the people’s living conditions, while 21.6 per cent said he has not fulfilled his campaign promises.

Other reasons cited for the president’s rising disapproval rate include not making keen follow-ups on implementation of government policies (11.6 per cent), appointing shoddy leaders (9.1 per cent), and failing to tackle corruption (5.6 per cent).

About 1.8 per cent of the respondents in the sample of those who disapprove of Kikwete said they did not know why, while 19.8 per cent gave other reasons not afore-mentioned.

According to REDET co-chairperson Dr Laurean Ndumbaro, the researchers found a direct co-relation between those who approve or disapprove of the president’s handling of national affairs and their education levels.

Speaking at a news conference in Dar es Salaam yesterday, Dr Ndumbaro said most of the educated Tanzanians polled expressed disapproval of Kikwete’s performance, compared to most of the less-educated respondents who said he was doing a good job.

The opinion poll was conducted from October 22 to 28 this year in one district from each of the 26 regions in both mainland Tanzania and Zanzibar.

On the government as an entity and certain specific public institutions, 33.4 per cent of the respondents said they were not satisfied with the performance of the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB).

The PCCB�s disapproval rating was followed closely by the entire fourth phase government currently in office, which received a thumbs-down from 32 per cent of Tanzanians polled.

About 30 per cent of the respondents said they were not satisfied with the performance of the country’s police force, while disapproval ratings for other government institutions were as follows: Judiciary (28.4 per cent), parliament (25 per cent), ministerial cabinet (19.2 per cent) and local government authorities (16.2 per cent).

Only 20.2 per cent of respondents stated clearly that they ’’approved’’ of the current cabinet of ministers, as another 41.4 per cent preferred to say they only ’’slightly approved’’.

The number of people who said they actually ’’disapproved’’ of the cabinet was again more than double at 19.2 per cent this year, compared to 9.2 per cent last year.

Meanwhile, according to the REDET poll, the approval rating of Zanzibar president Amani Abeid Karume also slumped to 35.5 per cent this year from last year’s 47.8 per cent.

However, a good 40.7 per cent of respondents said they ’’approved’’ the performance of the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM), while just 19 per cent ticked in favour of the opposition political parties.

The majority of pollsters who said they ’’disapproved’’ of the opposition parties said they were put off by internal party leadership squabbles, lack of good policies, and what they perceived as a general lack of ability to lead the country.

On the main problems facing Tanzanians at present, the respondents cited poor services in social sectors like health, education, water, electricity and roads (30.8 per cent); rising costs of living (28.3 per cent); unemployment (7.4 per cent); corruption (6 per cent); current leadership (3.9 per cent); bad government contracts (3.1 per cent); and others.
 
Yaani ukiona REDET wamefikia hatua ya kutoa data zenye sura hasi kiasi hiki kwa utawala wa Muungwana, ujue hali ni mbaya sana! Ni kwamba hapo kilichotolewa kitakuwa kimiesha brashiwa na kun'galishwa vya kutosha na hicho kilicho toka ndo walau kitamuachia muungwana usingizi!

Ila utafiti ungetoka live bila kupembuliwa mhhhhh!
 
sasa hiyo ya mbarali ambako hakuna hata mtu mmoja anayeridhishwas na utendaji wa muungwana si ingepaswa iwe sifuri???????? 0%

Nyambala,

Si unajua Waandishi wa habari TZ hawajui hesabu? Fuatilia maandishi yote yanayohusu namba utagundua wanavyovurunda.

Ndio maana kwa wenzetu huwezi kwenda university bila kuwa na
angalau C kwenye hesabu na lugha.

Sitashangaa hapo kama waandishi wa habari ndio wamechemsha.
 
Heshima mbele.
Mimi ninshangaa kuona tunamtofautisha rais na serikali yake anayoiongoza na chama ambacho yeye ni mwenyekiti wa taifa. Kama kweli tunataka kumsaidia rais wetu na kuinusuru Tanzania ni lazima tuanze kusema ukweli ili wahusika waone aibu na rais awajibike kwa watu kwa kutekeleza matakwa yao. Mengine yote ni chai ya rangi isiyo na kitafunio.
 
Maana ya hizi takwimu ni kuwa rais ameshindwa kazi ya kuongoza nchi.

Hapa inavyoonekana ni kuwa kama kwa kipindi cha miaka miwili ya utawala wake ambapo aliingia kwa kupata 80% anashuka hadi kuwa 44% maanana yake ni kuwa kama kura zikipigwa anaweza kujikuta kwenye wakati mgumu sana .

Pili, ukiangalia matokeo ya maeneo ya mijini ndio ambao wanamkataa JK chini ya 40% ,hii maana yake ni kyuwa muamko wa wananchi ni mkubwa na hawa ni kwa kuwa wanapata taarifa kila wakati na wapo informed.

Tatu, kusema eti JK bado anapendwa ni kutafuna maneno kwani takwimu zinaonyesha kuwa ameanguka kwa 23%ndani ya mwaka mmoja , hapa kuna maana kuwa kama akiendelea kuanguka umaarufu wake kwa wananchi kiasi hiki kwa kila mwaka kwa miaka mitatu ya utawala wake iliyobakia , 2010 atakuwa kwenye negative popularity, na hapo huenda uchaguzi ukamuwia mgumu sana ama labda CCM wanaweza kufanya miujiza na kumweka mgombea mwingine....

Tuendelee kutafuta ripoti kamili ya REDET na huenda tukaipata nitapita ofisi za REDET leo jioni ili kuweza kuangalia kama wanaweza kunipa copy.
 
takwimu za redet ni kichefuchefu....huwezi kusema jk ni bora kuliko chama ..wakati yeye ndio rais na mwenyekiti wa chama.....

mawaziri hawawezi kuwa wabovu ..alafu useme rais safii...kwa kuwa anawelea lea ..lazima kuna walakini na ripoti ya redet ingeenda mbali kuhalalisha hilo...

nani asiyejua mukandara...aliyetoa ripoti ya kura za maoni iliyohalalisha ...wizi wa kura utakaotokea 2005...

mukandara hana jipya...


Hapa wa kushangawa sio REDET, bali ni hao watoa maoni. I am not amused neither am I suprised. Watanzania ndivyo wanavyofikiria, wanaona Rais wao ni mzuri isipokuwa anaharibiwa na hao waliomzuguka. Inaonekana wengi wetu hapa hatujawajua wananchi wetu vizuri. Tusimlaumu messanger, tuwalaumu wenye ujumbe kama ndivyo tunataka.

Katika ku-challenge utafiti huwa hatuwi concerned sana na matokeo, tunaangalia jinsi haya matokeo yalivyofikiwa: ni kwa kiasi gani sampuli inawakilisha population, ametumia njia zipi, etc.

Pamoja na matatizo yangu na REDET, nafikiri this time huu utafiti wao ni far more credible kuliko tafiti za huko nyuma.

PS: Ili kuweza ku-challenge au ku-corroborate matokeo REDET huko mbele tunahitaji pollster organisation ingine TZ, vinginevyo kwa sasa hawa ndio wanaotegemewa na kuaminiwa na wananchi walio wengi. It is the only respectable academic institution undertaking this delicate research at present.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom