Mazingaombwe ni ujuzi gani?

Mazingaombwe ni ujuzi gani?

Wakati niko shule ya msingi Nyakabungo mwanza alikuja mwana mazingaombwe mmoja,kwa macho yangu nilishuhudia mfuko mtupu ambao ulikung'utwa na nilijiridhisha haukuwa na kitu chochote ndani jamaa yule aliuwekea makaratasi tupu ambayo niliyachana kutoka kwenye daftari langu ambalo nilikuwa sijaliandikia chochote na mara baada ya kumwaga chini makarasi yale zilitoka blue blue tupu yaani noti za elfu kumi elfu kumi maana kipindi kile zilikuwa za blue.Mpaka leo huwa najiuliza maswali kama kaweza kufanya uchawi wa kugeuza karatasi kuwa pesa ameshindwa nini kutoa nyingi za kutosha ili azitumie mwenyewe na badala yake alituchangisha wanafunzi shiling hamsini hamsini za kutazama onesho lake!!???

Sent from my DRA-LX5 using JamiiForums mobile app
Hakuna uchawi hapo ni ujanja tu wa kuwazidi akili.
Ngoja nikuelezee wanachokifanya hapo,yule anayefanya huo mchezo anakuwa amevaa shati lenye mikono mirefu na ndani ya hiyo mikono ya shati anakuwa amezificha hizo noti kwa hiyo anavyokuwa anaingiza mikono yake kwenye bahasha huku akijifanya kuomba hapo anakuwa abazishusha hizo hela taratibu bila ya watazamaji kujua helazikishashuka ndio atajifanya kuita mtazamaji mmoja aje kuzitoa.
Siku ukikutana nao tena ukitanga kuwapa changamoto waambie wafanyie kwenye sahani iliyo wazi badala ya kutumia bahasha uone kama watafanya
 
Toa codes kuhusu hiyo elimu.

Au kama ni mwiko kuweka hadharani njoo PM unipe tips kidogo.
Mkuu; hakuna cha eti ni mwiko wowote au nini. Wala huko PM siji/siendi. Naweka hapa👇👇
1. Mazingaombwe ni ujanja wa kuficha na kufichua. Unaficha sirini na unafichua hadharani mbele za watazamaji.
Kwa mfano gari kushindwa kuondoka: Mwoneshaji anajitahidi sana tairi isikanyage chini walau hata kwa sm0.3. Hakuna tairi iliyogusa ardhi -Gari itaendaje? Ni muhimu sana dereva anayeendesha gari la maonesho awe ni sehemu ya maonesho hayo.
 
N

Ndo ubaya wa kumwelewesha mtu ambaye anaangalia Mazingaombwe youTube.

Hiyo ndizi ilishikwa na Mwanafunzi na ilikuwa nzima kabisa.

Kuna baadhi ya Mazingaombwe kweli ni tricks ila mengine yamevuka ukomo.
Mkuu usiwe mbishi mbinu zote za mazingaombwe huwa zinafanana na huwa zinasambaa duniani kote,ukienda America utazikuta,ukienda India utazikuta na ukija Africa utazikuta mbinu hizo hizo.
Hiyo ndizi kama alikuja nayo mwenyewe kuna namna inakuwa imechokonolewa kwa ndani,na nje pia inakuwa ishakatwa halafu inaunganishwa na gundi yenye rangi sawa na ndizi ili kukuzubaisha wewe usione kitu.
Ukitaka kujua hilo siku ukiwaona waambie unakuja na ndizi yako mpya kutoka gengeni waifanyie kazi kama watakubali
 
Wiki mbili zilizopita kuna Kijana (Jina kapuni).
Alipigwa 100k.

Kwenye mchezo huo kulikuwa na kete tatu moja ilikuwa na picha na ziingine mbili hazikuwa na picha, Sasa Bwana si dogo alijichanganya alipigwa za uso. Cha kushangaza ukiwa mpenzi mtazamaji unaona kabisa ile pale yenye picha ila ukijitosa utaimba HALLELUJAH.

Tuacheni na hilo tukio katika maisha yangu mpaka sasa nimeshuhudia Mazingaombwe mbalimbali.

Mwana-mazingaombwe kutafuna wembe na kutoa sindano mdomoni, Mwana-mazingaombwe kugeuza karatasi kuwa biscuits, Kuna ile ya kuvuta pikipiki kwa shingo (Sina hakika kama zile ni nguvu za wahusika au ni Mazingaombwe), Kuna nyingine iliyonishangaza pia Mwana-mazingaombwe alisimama kama mita tatu kutoka kwa Kijana aliyebeba ndizi ila cha ajabu Mwana-mazingaombwe akiwa ameshikilia kisu aliweza kukata ndizi kwa distance hiyo.

Ningependa tujadili hii WanaJamiiForums.
Je, Hii ni elimu gani? Inafikirisha.

Kiranga , Infropreneur
Kuna elimu au Ujuzi wa magic na unafundishwa ukitaka sema tukupeleke kwa mtaalam
 
Kha! Mkuu unapenda nikufundishe japo kidogo kile ninachafahamu cha Mazingaombwe??? Ndizi Ilikuwa nzima kivipi? Nimekuuliza: Uliikagua kabla? No reply. Nikakuuliza tena: Nani alileta hizo ndizi? No reply. Halafu mwisho nikuulize: Unafahamu uhusiano baina ya huyo mwanafunzi na mwonesha mazingaombwe na ilivyopatikana hiyo ndizi? Nadhani hapo utaweza kupata walau mwanga kidogo. Mathalani mm ninaweza kusoma makaratasi mliyoandika nikiwa sipo tena mkayakunja-kunja say watu 30 kwa kutumia kisogo changu. Ni vi-tricks vya kijinga tuu hakuna lolote na kila mtu anaweza kufanya Mkuu.
Ni tricks ndio ushawah ona mtu anakatwa kichwa live kinatengwa na Anaongea?
 
Toa hiyo elimu kuhusu namna unavyoweza kusoma majina yaliyokunjwa kwenye karatasi au kama haupo willing kuiweka public nicheki PM. Mana nipo interested walau kujua baadhi ya tricks.

Napenda kujifunza vitu vipya kila siku.
Mkuu; wewe ni mdadisi sana. Kongole. Unataka uitumie kujipatia maokoto? Nimesema hapo juu PM siji naweka hapa-hapa hadharani ujinga/ujanja unaotumika:
1. Ni lazima/Sharti (Muhimu sana hii) awepo mmoja kati yenu msiyemjua/kumdhania ninafahamiana naye awe naye ameandika na ataandika kitu tutakachokuwa tumekubaliana kabla ya onesho. Huyu ni msiri wangu.
Mimi nitakapofika hapo mlipo na mkiwa tayari mmeshaandika mliyo yaandika na kuzikunja karatasi; nitachukua karatasi lolote miongoni mwa makaratasi yenu mliyokunja-kunja. Nitasoma kwa sauti kwa kuliweka kisogoni kwangu bila hata ya kulikunjua kile msiri wangu alichoandika. Naye atanyosha mkono kukubali kwamba ameandika yy. Then nitalifungua na kulisoma kiukweli. Tahadhari; Hakuna mtu kukaa nyuma yangu-manake siri itabumbuluka. Kuanzia hapo nitakuwa nasoma kile nilichokisoma kwenye karatasi la kwanzaalilokubali msiri wangu. Kamchezo hako ka kijinga kataendelea vivyo hivyo mpaka namaliza karatasi zote.:3Dance: Siri inabaki kati yangu mimi na Msiri wangu. Aaamen.
 
Ni tricks ndio ushawah ona mtu anakatwa kichwa live kinatengwa na Anaongea?
Ndio -tena sio mara moja. Jitahidi uhudhurie Maadhimisho ya kitaifa au kikanda(maonesho) e.g. Nane-Nane pale Uwanja wa Themi Arusha au Sabasaba pale Dodoma. (Hicho kichwa huwekwa kwenye beseni na kuzungushiwa pamba au kitambaa cheupe -ujiulize why ? si angekatwa kama kuku tu halafu aachwe hapo?? .Ukienda kwenye matamasha au maadhimisho ya Kitaifa Utaweza kubahatika kuona. Yapo pia maonesho ya Mtu anakatwa panga kichwani hadi linazama nusu ya kichwa au mtu anachomwa kisu ubavuni hadi kinatokeza upande wa pili na damu imevuja nyingi :KEKBye: na bado anaendelea kuongea kwa mbwembwe zote na maonesho yake.
 
Mkuu usiwe mbishi mbinu zote za mazingaombwe huwa zinafanana na huwa zinasambaa duniani kote,ukienda America utazikuta,ukienda India utazikuta na ukija Africa utazikuta mbinu hizo hizo.
Hiyo ndizi kama alikuja nayo mwenyewe kuna namna inakuwa imechokonolewa kwa ndani,na nje pia inakuwa ishakatwa halafu inaunganishwa na gundi yenye rangi sawa na ndizi ili kukuzubaisha wewe usione kitu.
Ukitaka kujua hilo siku ukiwaona waambie unakuja na ndizi yako mpya kutoka gengeni waifanyie kazi kama watakubali
Kama mpaka hapo hajaelewa basi tena: Case dismissed. Cooooooourt.
 
Wachungaji wengi tu mbona Ni wanamazingaumbwe si mkawaulize!
Na kuna mtu anafundisha hayo mambo yupo pale mkata njia panda ya kwenda kwa msisi tanga!
Uko sahihi,pia hata wale waganga wa kienyeji wa mjini wengi wanatumia mbinu kama hizi za wanamazingaombwe kuwarubuni watu ila wengi wao hawana dawa yoyote na wala hawajui chochote kuhusu tiba.
Kwa mfano kuna mchezo mmoja hivi anaweza akachukua yai akalipasua kitundu kidogo kisha anatoa nje kile kiini na yale majimaji ya yai kwa kuvuta na bomba la sindano/syringe baada ya hapo wanaingiza damu ndani kwa kutumia hilo hilo bomba la sindano kisha wakishamaliza wanaziba hilo tundu kwa kutumia maranda ya mbao wanayanasisha na gundi kisha wanapiga msasa yai linakuwa kama jipya kwa nje.
Sasa mteja akienda atajifanya kupiga ramli kwa kutumia hilo yai kisha baadae analivunja linatoka damu kisha anakutafsiria kwamba ukiona yai linatoka damu ujue maisha yako yapo hatarini maana yake wabaya wako wako karibu kukumaliza kinachofuata hapo anakutoa mpunga ili akupe dawa ya kuzuia mashambulizi ya adui,hahahaha
 
Mkuu usiwe mbishi mbinu zote za mazingaombwe huwa zinafanana na huwa zinasambaa duniani kote,ukienda America utazikuta,ukienda India utazikuta na ukija Africa utazikuta mbinu hizo hizo.
Hiyo ndizi kama alikuja nayo mwenyewe kuna namna inakuwa imechokonolewa kwa ndani,na nje pia inakuwa ishakatwa halafu inaunganishwa na gundi yenye rangi sawa na ndizi ili kukuzubaisha wewe usione kitu.
Ukitaka kujua hilo siku ukiwaona waambie unakuja na ndizi yako mpya kutoka gengeni waifanyie kazi kama watakubali
Dogo hujawahi kuona Mazingaombwe kakojoe ulale.
 
Back
Top Bottom