Maarifa ambayo huyaelewi usiyaite uchawi.Kete 3 ni sawa na Karata 3 ni Utaperi...!
Mchezeshaji ndo anaamua ule wakati Gani, wakati Gani uliwe.
Mazingaombwe ni Uchawi/Majini.
Wewe umeshindwa kuelewa ni namna gani huyo jamaa anaweza kumeza hiyo hela, Halafu unasema ni uchawi.Kuna jamaa tulisoma nae alikua akimeza ela inatokea mfukoni kwa mtu yoyote atakaemchagua...ikafika hatua walimu wakamtishia kumfukuza shule maana tulikua hatusomi ni mazingaombwe tu. uchawi upo.
1. Nimehudhuria mara nyingi sana maonesho live ya mazingaombwe nilipokuwa Shule ya msingi. Nikawa interested na ninashangaa sana. inakuwaje mchanga unageuka sukari, magazeti yanakuwa noti (fedha) mpya moto unawaka bila kiberiti n.k.Hujanishawishi, Hivi umeshawahi kushuhudia Mwana-mazingaombwe live au unaangalia kwenye simu?
Siongelei tricks nyepesi unazozisemea wewe, Ila kama wewe ni wa kishua huwezi elewa pia.
Mkuu; mbona unakubali ununuliwe kwa bei rahisi hivo? Hizo ndizi nani kazileta hapo? Je, ulizikagua vizuri kabla ya tendo la kukata? Zilikuwa ndizi mbivu au mbichi zile za kumenya? Hayo na maswali mengine yataweza kukupa mwanga wa nini kiliendelea.Basi tuachane na hilo la kuchanganya mikono kwa haraka.
Tuongelee hii ya Mwana-mazingaombwe kukata ndizi kwa distance ya mita 3, Yani assume wewe ni Mwana-mazingaombwe mkononi umeshikilia kisu na Mimi nipo distance ya mita 3 kutoka kwako lakini unafanikiwa kukata ndizi nilioshikilia mkononi. Je, hichi kitendo kinatokeaje? Hii nilishuhudia LIVE sijahadithiwa wala kuangalia YOUTUBE.
Zile ni tricks tu ukizijua utashangaa ulidanganywaje,ingia you tube andika breaking magician codesMagic na Witchcraft ni maneno tu hayaondoi ukweli kuwa Mazingaombwe ni sanaa ya kushangaza sana.
Basi nimekubali ni magic. Je, hii magic inafanyikaje mpaka ipumbaze akili ya binadamu!!! Inashangaza.
We wa kishua huwezi kuelewa Mazingaombwe ninayoongelea.Acha uvivu, nenda youtube tricks zote zipo zinaelezewa step by step!
Siamini kwenye kuamini.Hivi wewe unaamini uwepo wa majini?
Aluta continua!Kazi inaendelea!!!
Achana na vya YouTube, Naongelea Mazingaombwe kweli kweli, Au ile ya kuvuta pikipiki nayo kuna code wanafanya . Wakati kwa macho unashuhudia Mkulungwa akivuta pikipiki kwa shingo. C'mon man kuwa serious kidogo.Zile ni tricks tu ukizijua utashangaa ulidanganywaje,ingia you tube andika breaking magician codes
Mkuu; hongera sana. Kumbe ww ni school mate wangu! Mimi nilisoma S/M Mirongo.Wakati niko shule ya msingi Nyakabungo mwanza alikuja mwana mazingaombwe mmoja,kwa macho yangu nilishuhudia mfuko mtupu ambao ulikung'utwa na nilijiridhisha haukuwa na kitu chochote ndani jamaa yule aliuwekea makaratasi tupu ambayo niliyachana kutoka kwenye daftari langu ambalo nilikuwa sijaliandikia chochote na mara baada ya kumwaga chini makarasi yale zilitoka blue blue tupu yaani noti za elfu kumi elfu kumi maana kipindi kile zilikuwa za blue.Mpaka leo huwa najiuliza maswali kama kaweza kufanya uchawi wa kugeuza karatasi kuwa pesa ameshindwa nini kutoa nyingi za kutosha ili azitumie mwenyewe na badala yake alituchangisha wanafunzi shiling hamsini hamsini za kutazama onesho lake!!???
Sent from my DRA-LX5 using JamiiForums mobile app
Ndo ubaya wa kumwelewesha mtu ambaye anaangalia Mazingaombwe youTube.Mkuu; mbona unakubali ununuliwe kwa bei rahisi hivo? Hizo ndizi nani kazileta hapo? Je, ulizikagua vizuri kabla ya tendo la kukata? Zilikuwa ndizi mbivu au mbichi zile za kumenya? Hayo na maswali mengine yataweza kukupa mwanga wa nini kiliendelea.
Mimi sihitaji kuamini.Ila hauamini katika kuendelea kwa mapambano
Dah! Wewe kama unashangaa pikipiki cjui Toyo, Kinglion, Houjue, T-Better nk. Ugeshagaaje? mana kuna mwamba mmoja aliitwa kwa jina Power Mabula (sijui kama yupo hai au vp). Huyo mwamba alikuwa na uwezo wa kuzuia gari aina ya Land-rover Mandolin isiondoke hata kama dereva ataweka (ataengage) 4WD kwa kutumia nywele za kichwa chake. Hiyo nilishuhudia mm mwenyewe live Sengerema Sec.School. Baada ya onesho tulipata bahati ya kufanya naye mazungumzo na katika urafiki ule wa kiuanafunzi tulijifunza baadhi ya vitu kutoka kwake. Hakuna Uchawi wowote aliokuwa akitumia ila ujanja/kificho wa mazingaombwe.Achana na vya YouTube, Naongelea Mazingaombwe kweli kweli, Au ile ya kuvuta pikipiki nayo kuna code wanafanya . Wakati kwa macho unashuhudia Mkulungwa akivuta pikipiki kwa shingo. C'mon man kuwa serious kidogo.
By the way ushawahi kushuhudia mazingaombwe live Zaidi ya hayo huko YouTube?
Kwanza hakuna ushahidi, uthibitisho wala uhakika wa uwepo wa huyo Mungu.Sasa ulijuaje kwamba Mungu hayupo
Kha! Mkuu unapenda nikufundishe japo kidogo kile ninachafahamu cha Mazingaombwe??? Ndizi Ilikuwa nzima kivipi? Nimekuuliza: Uliikagua kabla? No reply. Nikakuuliza tena: Nani alileta hizo ndizi? No reply. Halafu mwisho nikuulize: Unafahamu uhusiano baina ya huyo mwanafunzi na mwonesha mazingaombwe na ilivyopatikana hiyo ndizi? Nadhani hapo utaweza kupata walau mwanga kidogo. Mathalani mm ninaweza kusoma makaratasi mliyoandika nikiwa sipo tena mkayakunja-kunja say watu 30 kwa kutumia kisogo changu. Ni vi-tricks vya kijinga tuu hakuna lolote na kila mtu anaweza kufanya Mkuu.N
Ndo ubaya wa kumwelewesha mtu ambaye anaangalia Mazingaombwe youTube.
Hiyo ndizi ilishikwa na Mwanafunzi na ilikuwa nzima kabisa.
Kuna baadhi ya Mazingaombwe kweli ni tricks ila mengine yamevuka ukomo.