Habari za mchana wanajamvi?
Bila shaka shughuli zimekwenda vizuri katika muda huo wote tangu tumeanza pale asubuhi na mapema!
Jamani kuna wakati Miaka ya 1980 hadi mwisho wa miaka ya 1990 kulikuwa na watu waliotambulika kuwa wana mazingaombwe walikuwa wakija mashuleni wakati ule tupo shule za msingi.
Hawa jamaa alikuwa wakionesha mambo (michezo) mbalimbali ya kimazingaombwe; mfano kijiti kugeuzwa Penseli, kishikizo kugeuka Pelemende na kadhalika, swali linakuja hivi ni kwa namna gani yale mambo yalikuwa yakitokea je kuna uhusiano na ushirikina?
Wakati mwingine walikuwa wanajiita Pawa (Power) kwa maana ya mtu mwenye nguvu za ajabu waliweza kuzuia magari na pikipiki (sikuwahi kusikia kuhusu Treni)!
Na mbona imetoweka kabisa au ni kwa sababu ya kukuwa kwa sanyansi na Teknolojia ikihusisha kuwapo kwa michezo mingi ya kiteknolojia zaidi au kuna sababu nyingine ya kutowesha hiyo michezo?
Sishangai sana AVATAR YAKOM INAONYESHA WE NI ANTI- ISLAM. LOSER kama huyo PADRI MMEGAJI WAKE ZA WATU
Mkuu umekumbuka nini hadi ulaleta 'uzi' huu hapa?
Those old good days, akina profesa ....., wakija na masanduku yao makubwa ya mazingaombwe na vibuyu. Ole wako ukiingia ukumbini na limao/ndimu au umegeuza viatu - kushoto kwenda kulia! Ofuye!
Wanafanya sana Misikitini mkuu...jitahidi kutembelea misikiti utakutana nayo tu maana mitambo ya kufanya mazingaombwe ni MAJINI
hahahaha,
Kua babu mmoja alikuwa anakuja shuleni kwetu
anajiita "POWER MABULA" duhh nilikuwa namuogopa
kipindi hicho darasa la pili. Naota mavitu ya ajabu kweli usiku..
hahahaha,
Kua babu mmoja alikuwa anakuja shuleni kwetu
anajiita "POWER MABULA" duhh nilikuwa namuogopa
kipindi hicho darasa la pili. Naota mavitu ya ajabu kweli usiku..
.duh,namkumbuka power mabula enzi hizo pale makurumla shule ya msingi(mwembechai)siku hizi kuna shule mbili sijui,yani mpaka ladha imepotea,..ndugumbi,nyerere primary school..crap..mnatuharibia historia
Hivi kuna uhusiano na majini kwenye hili sauala? Duh!
Ulishawahi kukutana na Profesa Eyesso!
Ukiingia kwenye mazingaombwe yake kwa njia za panya, lazima uwe kipofu!