Wakati Rais Samia anaibeba sekta ya michezo, TFF wanaturudisha kwenye migogoro ya enzi za FAT

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,033
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu amejipambanua kuwa mpenda michezo na amekuwa mara kadhaa akiunga mkono sekta hii kwa vitendo akitoa hamasa na zawadi mbalimbali kwa michezo tofautitofauti.

Tumeshuhudia Serikali yake ikiondoa kodi katika nyasi bandia ili kuboresha viwanja lakini pia tunafahamu ujenzi wa Arena umeanza, tunafahamu anadhamini mashindano ya CECAFA kwa wanawake lakini pia aliiwezesha timu ya Taifa ya Walemavu kushiriki mashindano ya kombe la Dunia na hivi majuzi tu ametangaza kwamba endapo timu ya Taifa itafuzu AFCON Serikali itawapa Milioni 500 na hapo hatujagusa kabisa hamasa aliyoileta kwa Simba na Yanga na ahadi ya kununua kila goli kwa shilingi Milioni 5 katika mashindano ya Kimataifa inayocheza msimu huu.

Baada ya yote haya KUNA TFF Chini ya KARIA ambayo ipo kwenye ulimwengu wake tofauti ikiendeleza migogoro, kufungiana na kukwamishana. TFF Imetoa taarifa ya kutoitambua michuano ya Ndondo Cup ambayo inafanyika kwa mara ya 10 mwaka huu (miaka 10 mfululizo).

Sote tunafahamu pengine Ndondo ina msisimko kuliko hata baadhi ya michezo ya Ligi Kuu na vipaji vingi nchini vimeibuliwa kupitia Ndondo Cup ambayo leo hii TFF wanasema hawaitambui, swali ni je kama kweli hawaitambui ilikuwaje miaka ya nyuma Rais wa TFF Karia na Katibu wake Kidao walikuwa wakihudhuria michuano hiyo (Au kwa sababu kwa wakati ule walikuwa hawajagombana na kumfungia Shaffih Dauda).

Sina lengo la kutetea kutofuatwa kwa taratibu lakini naamini kwa mashindano makubwa kama Ndondo Cup, TFF walipaswa kushughulikia suala la kibali (FACILITATION) na sio kuwa kikwazo kwa kukimbilia kutoa tamko la kutoyatambua mashindano maana athari zake kwa washiriki na wadhamini ni kubwa. TFF inaongozwa na viongozi "MABEKI" ambao kazi yao ni kuzuia tu na hawawazi kusaidia mashambulizi ya kujenga na kuibua vipaji nchini bali wanakandamiza jitihada za wadau wanaojitaoa kuinua mpira wa nchi hii.

Migogoro tulishaiacha enzi za FAT na hata Rais Samia anasisitiza maridhiano lakini Karia na wenzie wanaturudisha mulemule.

NILIWAHI KUANDIKA NA NINARUDIA TENA KARIA NA WENZIE WANAPASWA KULIWA KICHWA KABLA HAWAJATUFIKISHA PABAYA ZAIDI

- Karia anapaswa kuliwa kichwa mapema, kabla hajatufikisha pabaya zaidi
 
We ndio mpumbavu unaleta majungu hapa.

Unajionaga mjanja sana huko redioni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom