PakaJimmy
JF-Expert Member
- Apr 29, 2009
- 16,202
- 8,781
Nimepata Msiba WanaJF
Sipo18th November 2009, 04:40 PM![]()
Rating:(1 votes - 5.00 average)![]()
Ndugu wana JF leo mchana nimepata msiba wa Babu yangu Mzaa Mama anayeishi huko Arusha. Huu msiba mzito sana kwangu kutokana na maisha niliyoishi. Kwa wale ambao hawakukulia kwa Baba na Mama wanajua role ya Babu na Bibi nami ndio inayonifanya niomboleze sana. Kwa kifupi alikuwa ni Baba mzazi. Bwana alitoa na Bwana ametwaa. Jina la Bwana lihimidiwe milele. AmeN
Ndugu WanaJF,kama mlivyoona hiyo introduction hapo juu, ni kwamba muda huu ndo nawasili mjini Arusha tokea eneo yalikofanyika mazishi ya Babu Mpendwa wa mwanaJF wetu mahiri, SIPO.
Mimi kama mjuavyo niko huku Arusha, na baada ya kukutana na thread hiyo hapo juu, nilim`PM huyu bwana SIPO nikimsihi anijulishe kuhusu tarehe na Eneola mazishi mara atakapowasili Arusha, ambapo kweli alinifahamisha kwamba wangemzika leo [j3,23/11/2009], katika eneo liitwalo Bangata, umbali wa KM10 toka Arusha mjini, miguuni mwa Mlima Meru.
Nami bila ajizi nimeaga kazini kwangu mapema, na kuelekea pande za eneo hilo geni kwangu, huku nikijiamini kuwa naenda kuiwakilisha JAMII-FORUMS katika mazishi hayo, japo kwa uhakika simjui kabisa kwa sura mwenyeji wangu SIPO!
Kikwetu wanasema "Nyumba yenye matanga haijifichi"! Kwa Neema za Mungu niliwasili mahala huko baada ya kuulizia njia kwa kila niliyemwona usoni akikatiza!
Misa rasmi ya kumwombea Marehemu huyo, Mzee Michael Tomito(81), ambaye alikuwa pia Mchungaji wa KKKT, ilianza mida ya saa 7mchana katika kanisa dogo la kijijini hapo, ambapo ilihudhuriwa na Maaskofu wa2, Askofu Thomas Laizer wa Dayosisi ya Arusha na Askofu Akyoo wa Meru. Pamoja na wakuu hao, alikuwepo pia EL, Wachungaji tele toka mji mzima wa Arusha, na ujumbe wa vyama vya siasa na wa kiserikali.
Lakini kikubwa zaidi nilichoshuhudia na kupigwa nacho butwaa ni umati wa watu, ambapo kwa hesabu za haraka walizidi 2000.
Baada ya Misa hiyo, Msafara wa kuelekea Kaburini umeanza, ambapo ni shambani kwake Marehemu, na muda wa saa 9.00mchana Mzee huyo amepumzishwa mahala pake pa kudumu, na kuachana moja kwa moja na dhiki za dunia hii!
Aidha, Mzee huyo Mchungaji Veterani hapa Arusha ameacha watoto 7, wajukuu 16(INCLUDING SIPO), na vilembwe 2, ambapo mkewe alishatangulia kunako haki mwaka2007.
Katika salamu za rambirambi zilizotolewa na vikundi, mbalimbali vya kijamii, vimeeleza kuwa Mzee huyu aliyezaliwa mwaka 1928 alikuwa msomi wa wakati wake, na kabla ya kuanza kusomea Uchungaji katika chuo cha Makumira, alisomea na kufanya kazi katika fani za Kilimo, Afya Chama tawala na sekta nyingine lukuki.
Aidha ameelezewa kuwa alikuwa Mfano wa kuigwa katika jamii na Taifa kwa ujumla.MUNGU AILAZE PEMA ROHO YA MAREHEMU MZEE HUYU!
Hadi najipanga kuondoka eneo hilo, kwa hakika sijafanikiwa kumfahamu Mwanaharakati SIPO, japo nimesalimiana na watu kadha MBAPO HUENDA MMOJAWAPO NDIYE. Anyway, labda ndiyo raha/Karaha ya JF!
Lakini naamini nimetimiza wajibu wangu kama MwanaJF, wa KUWAWAKILISHA, ipasavyo, na nadhani wanaJF mtanisupport na kunipa BIG-UP kwa kazi hiyo!.
NAWASASILISHA .