Sugar wa Ukweli
JF-Expert Member
- Jun 25, 2009
- 373
- 40
Asante sana kaka PJ kwa kutuwakilisha,na hii inaonyesha tuko na umoja!!!
Fanya ya KiJF zaid basi Kiongozi!
Thanx alot Fidel180.Nawashukuru kwa kunipa moyo, nimeamini kuwa kumbe together we can move mountains here!...BBlessed!
Nimejisikia raha saana, Utadhani mimi ndo mfiwa!
PJ endelea na moyo huo wa upendo, Mungu atakubariki, lakini hii yote ni kupitia JF.
Sasa mbona unatubagua? How about ambao tupo ughaibuni ???hahaaa, kama kawaida.
ujue kwasasa JF ni kama familia kubwa iliyotapakaa kila kona. wazo langu ni kwamba hata wamikoani wajikusanye na kufanya get tugeza zao itasaidia kufahamiana nje ya JF kama wapwa na mabinamu wa hapa dar ndani ya zero pub, chawote bar na kwingineko utatukuta tu!.
Ndugu WanaJF,kama mlivyoona hiyo introduction hapo juu, ni kwamba muda huu ndo nawasili mjini Arusha tokea eneo yalikofanyika mazishi ya Babu Mpendwa wa mwanaJF wetu mahiri, SIPO.
Mimi kama mjuavyo niko huku Arusha, na baada ya kukutana na thread hiyo hapo juu, nilim`PM huyu bwana SIPO nikimsihi anijulishe kuhusu tarehe na Eneola mazishi mara atakapowasili Arusha, ambapo kweli alinifahamisha kwamba wangemzika leo [j3,23/11/2009], katika eneo liitwalo Bangata, umbali wa KM10 toka Arusha mjini, miguuni mwa Mlima Meru.
Nami bila ajizi nimeaga kazini kwangu mapema, na kuelekea pande za eneo hilo geni kwangu, huku nikijiamini kuwa naenda kuiwakilisha JAMII-FORUMS katika mazishi hayo, japo kwa uhakika simjui kabisa kwa sura mwenyeji wangu SIPO!
Kikwetu wanasema "Nyumba yenye matanga haijifichi"! Kwa Neema za Mungu niliwasili mahala huko baada ya kuulizia njia kwa kila niliyemwona usoni akikatiza!
Misa rasmi ya kumwombea Marehemu huyo, Mzee Michael Tomito(81), ambaye alikuwa pia Mchungaji wa KKKT, ilianza mida ya saa 7mchana katika kanisa dogo la kijijini hapo, ambapo ilihudhuriwa na Maaskofu wa2, Askofu Thomas Laizer wa Dayosisi ya Arusha na Askofu Akyoo wa Meru. Pamoja na wakuu hao, alikuwepo pia EL, Wachungaji tele toka mji mzima wa Arusha, na ujumbe wa vyama vya siasa na wa kiserikali.
Lakini kikubwa zaidi nilichoshuhudia na kupigwa nacho butwaa ni umati wa watu, ambapo kwa hesabu za haraka walizidi 2000.
Baada ya Misa hiyo, Msafara wa kuelekea Kaburini umeanza, ambapo ni shambani kwake Marehemu, na muda wa saa 9.00mchana Mzee huyo amepumzishwa mahala pake pa kudumu, na kuachana moja kwa moja na dhiki za dunia hii!
Aidha, Mzee huyo Mchungaji Veterani hapa Arusha ameacha watoto 7, wajukuu 16(INCLUDING SIPO), na vilembwe 2, ambapo mkewe alishatangulia kunako haki mwaka2007.
Katika salamu za rambirambi zilizotolewa na vikundi, mbalimbali vya kijamii, vimeeleza kuwa Mzee huyu aliyezaliwa mwaka 1928 alikuwa msomi wa wakati wake, na kabla ya kuanza kusomea Uchungaji katika chuo cha Makumira, alisomea na kufanya kazi katika fani za Kilimo, Afya Chama tawala na sekta nyingine lukuki.
Aidha ameelezewa kuwa alikuwa Mfano wa kuigwa katika jamii na Taifa kwa ujumla.MUNGU AILAZE PEMA ROHO YA MAREHEMU MZEE HUYU!
Hadi najipanga kuondoka eneo hilo, kwa hakika sijafanikiwa kumfahamu Mwanaharakati SIPO, japo nimesalimiana na watu kadha MBAPO HUENDA MMOJAWAPO NDIYE. Anyway, labda ndiyo raha/Karaha ya JF!
Lakini naamini nimetimiza wajibu wangu kama MwanaJF, wa KUWAWAKILISHA, ipasavyo, na nadhani wanaJF mtanisupport na kunipa BIG-UP kwa kazi hiyo!.
NAWASASILISHA .[/QUOTE
pamoja mkuu hiyo ni safi sana, sasa nakumbuja jamaa moja aliwahi kuongea hapa kuwa wakati unatoa maoni yako lazima uwe mwangalifu sana maana unaweza kuwa unamtukana hata mzazi wako, na huwezi jua mtu atakuja kukusaidia lini na nini sasa kama hata njiani unaweza kuwa unapita ukapata tatizo hata kama uko na gari inaweza kupata shida na pengine ni usiku au ni karibu na vibaka akajitokeza mwana jf mmoja akakusaidi hata kwa kukupatia fundi tayari ni msaada lakini kwavile tu hamjuani kwamba wote ni wana jf na pengin e mlikwishakuwa na tofauti katika huku mtandao. nimeona somo kubwa sana hapa la kujifunza, many thanks pj n b blesi
Jamani nakosa cha kuandika kusema kweli nimefarijika sana.
Jamani nakosa cha kuandika kusema kweli nimefarijika sana. Ninachoweza kusema PakaJimmy Mungu akubariki sana kwa kufika, ilikuwa bahati mbaya tu hatukuonana. Nashukuru sana tena sana kwa WanaJF wote. Nimepungukiwa na maneno kabisa ya kusemea wema wa mioyo yenu. Be blessed all the days
hongera sana kaka!Ndugu WanaJF,kama mlivyoona hiyo introduction hapo juu, ni kwamba muda huu ndo nawasili mjini Arusha tokea eneo yalikofanyika mazishi ya Babu Mpendwa wa mwanaJF wetu mahiri, SIPO.
Mimi kama mjuavyo niko huku Arusha, na baada ya kukutana na thread hiyo hapo juu, nilim`PM huyu bwana SIPO nikimsihi anijulishe kuhusu tarehe na Eneola mazishi mara atakapowasili Arusha, ambapo kweli alinifahamisha kwamba wangemzika leo [j3,23/11/2009], katika eneo liitwalo Bangata, umbali wa KM10 toka Arusha mjini, miguuni mwa Mlima Meru.
Nami bila ajizi nimeaga kazini kwangu mapema, na kuelekea pande za eneo hilo geni kwangu, huku nikijiamini kuwa naenda kuiwakilisha JAMII-FORUMS katika mazishi hayo, japo kwa uhakika simjui kabisa kwa sura mwenyeji wangu SIPO!
Kikwetu wanasema "Nyumba yenye matanga haijifichi"! Kwa Neema za Mungu niliwasili mahala huko baada ya kuulizia njia kwa kila niliyemwona usoni akikatiza!
Misa rasmi ya kumwombea Marehemu huyo, Mzee Michael Tomito(81), ambaye alikuwa pia Mchungaji wa KKKT, ilianza mida ya saa 7mchana katika kanisa dogo la kijijini hapo, ambapo ilihudhuriwa na Maaskofu wa2, Askofu Thomas Laizer wa Dayosisi ya Arusha na Askofu Akyoo wa Meru. Pamoja na wakuu hao, alikuwepo pia EL, Wachungaji tele toka mji mzima wa Arusha, na ujumbe wa vyama vya siasa na wa kiserikali.
Lakini kikubwa zaidi nilichoshuhudia na kupigwa nacho butwaa ni umati wa watu, ambapo kwa hesabu za haraka walizidi 2000.
Baada ya Misa hiyo, Msafara wa kuelekea Kaburini umeanza, ambapo ni shambani kwake Marehemu, na muda wa saa 9.00mchana Mzee huyo amepumzishwa mahala pake pa kudumu, na kuachana moja kwa moja na dhiki za dunia hii!
Aidha, Mzee huyo Mchungaji Veterani hapa Arusha ameacha watoto 7, wajukuu 16(INCLUDING SIPO), na vilembwe 2, ambapo mkewe alishatangulia kunako haki mwaka2007.
Katika salamu za rambirambi zilizotolewa na vikundi, mbalimbali vya kijamii, vimeeleza kuwa Mzee huyu aliyezaliwa mwaka 1928 alikuwa msomi wa wakati wake, na kabla ya kuanza kusomea Uchungaji katika chuo cha Makumira, alisomea na kufanya kazi katika fani za Kilimo, Afya Chama tawala na sekta nyingine lukuki.
Aidha ameelezewa kuwa alikuwa Mfano wa kuigwa katika jamii na Taifa kwa ujumla.MUNGU AILAZE PEMA ROHO YA MAREHEMU MZEE HUYU!
Hadi najipanga kuondoka eneo hilo, kwa hakika sijafanikiwa kumfahamu Mwanaharakati SIPO, japo nimesalimiana na watu kadha MBAPO HUENDA MMOJAWAPO NDIYE. Anyway, labda ndiyo raha/Karaha ya JF!
Lakini naamini nimetimiza wajibu wangu kama MwanaJF, wa KUWAWAKILISHA, ipasavyo, na nadhani wanaJF mtanisupport na kunipa BIG-UP kwa kazi hiyo!.
NAWASASILISHA .
Jamani nakosa cha kuandika kusema kweli nimefarijika sana. Ninachoweza kusema PakaJimmy Mungu akubariki sana kwa kufika, ilikuwa bahati mbaya tu hatukuonana. Nashukuru sana tena sana kwa WanaJF wote. Nimepungukiwa na maneno kabisa ya kusemea wema wa mioyo yenu. Be blessed all the days
Jamani nakosa cha kuandika kusema kweli nimefarijika sana. Ninachoweza kusema PakaJimmy Mungu akubariki sana kwa kufika, ilikuwa bahati mbaya tu hatukuonana. Nashukuru sana tena sana kwa WanaJF wote. Nimepungukiwa na maneno kabisa ya kusemea wema wa mioyo yenu. Be blessed all the days
secondedhongera sana kaka!
tunashukuru kwa kutualika.
karibu get tugedha yetu ya december tukufanyie maisha