Mayweather hutumia mamilioni kubadilisha oil ya gari yake

Ndio akili za kiafrika.
Angekua bilgates ni mtu mweusi nadhani hata kuja Tanzania asingekuja. Watu weusi tuna matatizo ya akili na IQ ndogo.

Mtu mweusi akipata pesa anafikiria starehe na umaarufu, bilgates hatujawahi kusikia anafanya huo ujinga
We bilgate matumizi yake unayajua lkini. ...Au unafikiri anashindia ugali tembele,Mtu usafiri anaotumia Mara kwa Mara ni ndege tena yake binafsi sasa ukiambia na yeye akimwaga oil kwenye ndege ni sh.ngapi? sijui utaanza kusema mitume hawakuishi hivyo,acha mtu atumie pesa yake aliyoipigania bna,ndo maisha ya ndoto zake hayo
 
Hata 50 cent na tyson walitetewa hivyo hivyo mwisho wakaanza kuuza majumba haikusaidia

pia mi sijakosa nna hela ya kunitosha mm na familia yangu na ela ya mafuta na service ya gar langu maisha yanasonga ila sina za maonyesho ambazo ukifulia unaingia uvunguni
Service kama mayweather...
 
Huyoo Jamaa sidhani Hata Charity kama huwa anafanya pamoja na Mali zote hizoo...!! Ni ushambaaa na kulewaa pesaa...

Sema anyway ni zakee lakini Pesa ni mauaa
 
Ni kweli niko bara la giza nikiwa na fikra huru sio za kitumwa na siutukuzi uzungu najivunia kuzaliwa afrika

Siwezi kujaribu kuwaza kumpangia floyd matumizi kwa kuwa hata wazazi tu walionisomesha au kunitafutia kazi hawana uwezo wa kunipangia matumizi ya pesa zangu
Niko huru na nna uwezo wa ku manage kipato changu
kwa mtu mwenye akili ya kimaskini kama floyd miaka 20 baadae atakuwa maskini tu kwa kuwa ana roho ya kimaskini utajiri sio saizi yake
Nadhani mi nitakuwa levo nyingine sana wakati huo
anatumia kutokana na pesa aliyonayo....unataka ajibane akifa wafaidi wengine? mwache ale matunda ya jasho lake.....halafu maisha hayana formula kuna mcheza tennis anaitwa boris becker aliinvest pesa yake kwenye oilcompany dola biliion moja ikazama sasa hivi ni masikini wa kutupwa
 
Tofautisheni matumizi ya mtu na mtu ku expose maisha yake..inawezekana kabisa Bill gates akawa na matumiz ya fedha makubwa ila hajasema tu tofaut hyo mwanangumi kajiachia na mambo yake na pia hata akifilisika mtamsaidia nin??
 
habari nyingine huwa sio za kuamini huwa hiyo mitandao inalipwa na hao mastaa kuandika habari ambazo zitaendelea kuwaweka kwenye spotlight pale wanapokuwa hawana mambo au shughuli za kuwafanya kuongelewa

mfano kwa sasa mayweather amestaafu ngumi na kwa kiasi kikubwa ile spotlight aliyokuwa nayo imepotea... ndani ya mwaka mzima kasikika kwa mambo mawili kugombaniwa na wanawake yaani huyu aliyenaye sasa badmedinna na yule wazamani

na ghafla TMZ wamekuja na hili la matumizi ya pesa (kuna walakini)

gari hubadilishwa OIL baada ya kutembea KM kadhaa na sio kila baada ya muda fulani

mayweather ndani ya mwezi mzima hilo gari anaweza kulieendesha mara mbili tu.. sasa hapo oil inabadilishwa ya nini

rudi kwenye pointi yangu habari kuhusu mastaa nyingi huwa ni za kutunga na sometimes huwa wanafikia hatua hadi kuwalipa waandishi ili wawaandike ili tu waendelee kuwa kwa spotlight...

NAWASILISHA HOJA... GARI HUBADILISHWA OIL KILA BAADA YA KUTEMBEA KM KADHAA 1000-4000 INADEPEND NA GARI NA AINA YA OIL NA SIO KILA BAADA YA MUDA FULANI HAPO TUMEDANGANYWA ....OVER...
 
Kwenye kutumia pesa kila mtu huwa anataratibu zake za matumizi ya pesa yake uwezi kuanza kumtabiria mtu eti mwisho wake utakua hivi kwani wewe Mungu pengine unaongea hivyo kumbe wewe huna na pia huna uwezo wa kufanya hivyo ila ukipata unafanya mengi zaidi yake ukiwa huna unona anaharibu pesa.
 
Nina hakika matumizi ya huyo billget kwa wiki ni zaidi ya billion,ulinzi alionao vyombo vya usafiri anavyotumia,chakula,ma Dr wake,wapishi n.k,service ya vitu vyake vodgo vidgo n.k,Hakuna utofauti na huyu Mwana utofauti wao uko kwenye kuanika mambo
 
Acha fix kawa danganye jamaa zako wa kijiwe cha kahawa..

Nyie madogo mpo jf kibahati mbaya wakubwa tunapoongea mambo hatunaga utani.

Rapper 50 Cent baada ya kutawala kwenye vichwa vya habari kuhusu kufirisika kwake na mali alizonazo hivi sasa hati yake inayoonyesha kufirisika kwake imepatikana.

proxy

Hati hiyo ya ufirisi imepatikana na kutupiwa online na Daily mail ikiwa inaonyeshwa thamani na kiasi cha pesa alichonacho.

Rapper huyo mwenye umri wa miaka 40 aliandikiwa jarada la ufirisi mwezi juni ambapo kulitokana na kushindwa kumlipa Lastonia Leviston $7 milion kwasababu ya kuachia sex tape ya mwana dada huyo.

proxy

 
Nyie madogo mpo jf kibahati mbaya wakubwa tunapoongea mambo hatunaga utani.

Rapper 50 Cent baada ya kutawala kwenye vichwa vya habari kuhusu kufirisika kwake na mali alizonazo hivi sasa hati yake inayoonyesha kufirisika kwake imepatikana.

proxy

Hati hiyo ya ufirisi imepatikana na kutupiwa online na Daily mail ikiwa inaonyeshwa thamani na kiasi cha pesa alichonacho.

Rapper huyo mwenye umri wa miaka 40 aliandikiwa jarada la ufirisi mwezi juni ambapo kulitokana na kushindwa kumlipa Lastonia Leviston $7 milion
Wee jamaa bado inaonekana mambo mengi sana huyajui..

50 cent alitangaza kufilisika ili kukwepa kumlipa huyu demu hzo hela..
 
Wee jamaa bado inaonekana mambo mengi sana huyajui..

50 cent alitangaza kufilisika ili kukwepa kumlipa huyu demu hzo hela..

Sio maneno yangu nimekuwekea hadi ripot ya uchunguzi wewe nani ataamini maneno yake bila kukaguliwa au huon ripot ya mahakama hiyo?
 
Back
Top Bottom