Maxence Melo: Viongozi wanapenda kuhubiri “Uhuru wenye Mipaka” kwa wananchi, mipaka kwao ipo wapi?

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Mkurugenzi wa Jamii Forums, Maxence Melo na Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti ya Twaweza, Aidan Eyakuze walifanya mahojiano asubuhi ya leo Azam Tv, mjadala ulikuwa unahusu Kanuni za Maudhui ya Mtandaoni za Sheria ya EPOCA (Electronic and Postal Communication Act).

5D3131F3-3452-4AF2-9B84-5B2B51B07CAE.png




Maxence ameeleza kuwa Sheria ya EPOCA ilikuwepo tangu 2010 ila kanuni hizi zimekuja sasa tena kupitia Wizara ya Habari na maoni ya wadau yametakiwa ndani ya siku 7 tu‬.

Maxence anaendelea kusema Kanuni zenyewe zimeandikwa kwa Kiingereza na zinawalenga watanzania. Yawezekana nia ni njema lakini uharaka unatia shaka.

Maxence: Kwa Kanuni za Maudhui Mtandaoni za Sheria ya EPOCA (2010), Mamlaka zimetoa siku 7 wadau wawe wametoa maoni. Muda hautoshi! ‬

Aidan Eyakuze: Kanuni zitapelekea watu kufanya censorship kwa kiwango kikubwa. Vijana watashindwa kufanya kazi kwa ubunifu kwa uoga ‬

Maxence: Sheria, Kanuni au Sera zinazokuwa zinaua ubunifu(innovation) kwa namna yoyote hazifai katika ulimwengu wa sasa ‬

Maxence: Mamlaka zifafanue “Maadili ya Mtanzania” ni yepi kabla ya kutunga sheria za kudhibiti wanaoenda kinyume na ‘maadili’ hayo ‬

Maxence: Viongozi wetu wanapenda kusema “Hatuwezi kuwa na uhuru usio na mipaka” ila mipaka hiyo mara nyingi inawalenga wananchi tu ‬

Aidan Eyakuze: Dola pia inatakiwa kuwekewa mipaka kisheria. Sio suala la kuweka mipaka kwa wananchi wakati Katiba imetoa uhuru huo

Maxence: Waandishi wana maadili ya uandishi; mtandaoni wananchi ndio waandishi. Tunakosea kuwachukulia raia kama waandishi wa habari ‬

Aidan: Internet cafe zitatakiwa kuweka kamera kufuatilia kinachofanywa na wateja wao, hii ni kuingilia uhuru wa wananchi kupita kiasi‬

Maxence: Kuweka kamera si jambo jipya, hata hotelini zinakuwepo ila si vyumbani. Surveillance inayopendekezwa na kanuni haikubaliki ‬

Maxence: Kanuni zinapendekeza maudhui kuchujwa kabla hayajaenda kwa umma; uchujaji huu nauona kama [HASHTAG]#censorship[/HASHTAG] isiyofaa karne hii

Aidan: Kwa mwenye ukurasa Facebook au Blog kupitia maoni yote itakuwa kazi kubwa. Mwandishi aliyekuwa anaibuka atakata tamaa ku-blog ‬

Maxence Melo: Kanuni hizi pia zinataka wenye mitandao kukusanya taarifa za wateja wao. Si wote wana uwezo kiteknolojia kufanya hivyo

Maxence Melo: Kanuni zinataka ukiambiwa uondoe taarifa kwenye mtandao ufanye hivyo ndani ya saa 12. Ni muda mfupi na ni mtego unasao

Maxence Melo: Kimataifa, kuna utaratibu wa kuondoa taarifa mtandaoni. Mhimili wa Mahakama ndo ungethibitisha taarifa gani iondolewe. Ametolea mfano wa Chile walivyoamua kuhakikisha Mahakama ndiyo inasimamia haki katika hili. Amesema kwa namna ilivyokaa, watu binafsi na taasisi binafsi watautumia mwanya huu kuipoteza maana nzima ya Take Down Notice.

Maxence: Kuna vijana wana mawazo mazuri na wanatamani kuwa zaidi ya JamiiForums, Facebook, Instagram, WhatsApp, Twitter n.k; mazingira yanayoandaliwa yanaua ubunifu.

Maxence: Tulitakiwa kuhakikisha vitu vya kitanzania tunavitengenezea mazingira ya kukua na kuonekana kimataifa. Tuhamasishe ubunifu ‬

Maxence Melo: Mataifa kadhaa niliyotembelea nimebaini huwa yanakazana kuhamasisha maudhui na ubunifu wa ndani. Huo ndio uzalendo. Tusione haya kuwataja wanaofanya vyema nchini. Kataja baadhi ya blogs.

Maxence Melo: Sijajua maana ya neno “Uzalendo” kwa wenye mamlaka ni ipi; nadhani ni vyema tukaelezwa kwao mtu mzalendo ni yupi.‬

Maxence: Kama wao ndio wazalendo, kwanini kanuni zinazotengenezwa kuhudumia waswahili ziandaliwe kwa Kiingereza na zipitishwe haraka?‬

Maxence: Tunahitaji Kanuni/Sheria ila tunatakiwa kuwa na ushiriki wa wadau ili Mamlaka zipate maoni tofauti. Tusijenge Taifa la Waoga‬

Maxence: Kanuni zinataka Blogs na Mitandao isajiliwe na TCRA. Ieleweke, mtu anaweza kukataliwa usajili pia! Hili pia linashangaza ‬

Maxence: Wanaweza fanikiwa kudhibiti wabunifu wa ndani; wabunifu wa nje kama Facebook, Twitter hawawezi kudhibitiwa kirahisi hivyo

Maxence: Mwanasiasa awe Upinzani au Chama Tawala, asingependa akosolewe na mwananchi kirahisi. Kanuni zinatakiwa kuwalinda wananchi

Maxence: Katiba imetaja umuhimu wa faragha ya raia; Kanuni zinataka watumiaji wa mtandao taarifa zao nyeti zikusanywe na watoa huduma‬

Maxence Melo: Tukiwaogofya wabunifu hapa Tanzania, watakimbilia nchi nyingine na tunaweza kujikuta tunawapokea kama wawekezaji ‬

Aidan: Mwaka 2015 wakati wanajaribu kupitisha Sheria 4 tuliambiwa tusiwe na wasiwasi; kwa sasa wameshawakamata wengi kwa sheria hizo.

Maxence Melo: Bahati mbaya, mtoa taarifa (whistleblower) ambaye Mamlaka zinamtambua ni yule aliyeenda kwao(mamlaka) na si vinginevyo!‬
 
Kwa taratibu hizo mpya, watafungwa wengi. Mpaka leo watu hawaijui hii sheria ya mitandao na wanapatikana na makosa. Hizo mpya ndio vichwa vingi vitakutana magerezani.
 
Niulize swali la kizushi, hivi Jamiiforums leo isipokuwepo, itakuwa hasara ya nani kwa mfano?
Mangapi ulishawahi jifunza humu tokea kujiunga kwako mkuu?
Unapowazia hasara fikiria kwanza juu yako wewe.

Je? Huoni kuwa waanzilishi wa jamii forum ndipo sehemu yao ya kujipatia riziki?
 
Chupaku wote ila Serikali ndiyo itakayoathirika,kwani kwanza itakosa eneo la kupatiwa ushauri na maoni ya wananchi,pia itakosa mapato ya kodi!
Serikali hawategemei ushauri kutoka mitandao ya kijamii wala hata wanahabari mkuu, wao ndiyo wanachopanga ndicho kinafanyika labda mipango ya Mungu tu,

NB... Ikiwa wangekuwa wanafanyia ushauri wanaopewa kazi ona leo watu kila wanachoshauri hakifanyiwi kazi.
 
Niulize swali la kizushi, hivi Jamiiforums leo isipokuwepo, itakuwa hasara ya nani kwa mfano?
Ni faida kubwa sana kwa walioko madarakani,lakini ni hasara kubwa sana siku wakitoka madarakani na kuwa wananchi wa kawaida.
 
Mwambie akagombee ubunge ili atanue uwanja wa kutetea uhuru wa habari.
 
Kinachoshangaza kwa huyu Baba, ni kuwa kwani haijui ile kanuni inayosema kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza?

Sasa kama yeye anaamini anawafanyia mazuri watanzania, kitu gani kinachomsumbua kutaka kufungia vyombo ya habari huru??

Hii nchi tumeikabidhi watu washamba na malimbukeni.
By Zitto Kabwe
 
Katiba mpya ni muhimu sana. Hii iliyopo haina mipaka yoyote kwa rais.

Kwenye katiba hii, rais ni sawa na mungu mtu.
 
Niulize swali la kizushi, hivi Jamiiforums leo isipokuwepo, itakuwa hasara ya nani kwa mfano?

Unaweza kuwa yule malaika unayeshuka kuja kufunga mitandao ya kijamii. Kwa taarifa yako kuna mambo mengi tu yamefanyiwa kazi tokea katika hoja za watu mitandaoni. Kama huamini waombe kuwapima mapigo ya moyo wale watu wasiojulikana.
 
Maxence: Mwanasiasa awe Upinzani au Chama Tawala, asingependa akosolewe na mwananchi kirahisi. Kanuni zinatakiwa kuwalinda wananchi

Hilo ni jiwe la ukweli linalowanyoosha waliopinda pande zote. Ajabu ya TZ wanakuja wafuasi wa magwanda ya kijani wanaona Kiongozi wao ni mtukufu hakosei utajuta kushauri, wanakuja wa magwanda ya kaki wanaona Mbowe, Lissu etc ndo malaika wa kuikomboa TZ hawakosei (hawa wametubeba katika umoja wetu tunakofundishwa kutokubali kukosolewa).

Kuna wale wengine wa magwanda ya zambalau ndo usiseme Mwami wao anaonekana safiii ukimkosoa wanakua wakali kukuuliza unamkosoa una elimu gani?

Mjinga siku zote hujiona ni mwerevu kweli kweli.
 
Back
Top Bottom