Maxence Melo, Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, ahojiwa kwa tuhuma za kula njama za kutaka kumuua Cyprian Musiba

Nilisema kwenye mitandao hakunaga usalama 100% piga kazi rais wangu magufuli. Hivyo ni vijimambo tu.
 
Mimi naamini huyu jamaa HATA SIO MUSIBA IN REAL NAME...HILO JINA AMEPEWA KWA KAZI MAALUM...ANA JINA LAKE HALISI...NENDA GOOGLE KASEARCH BIOGRAPHY YAKE NA ALIPOPITIA HUPAONI...HUYO JAMAA MUSIBA SIO MJINGA MJINGA...NI MTU ANAYEJITAMBUA...NI MIONGONI MWA TISS AGENT...AMEJIDHATITI HASA...NA AMEWEKWA HAPO KWA KAZI HIYO...
Sidhani, yaani Agents wa hiyo Tiss ndo wanakuwa wapumbavu hivi. Very difficult to comprehend na kama ni kweli basi hatuna kabisa Intelligence.
 
Mimi naamini huyu jamaa HATA SIO MUSIBA IN REAL NAME...HILO JINA AMEPEWA KWA KAZI MAALUM...ANA JINA LAKE HALISI...NENDA GOOGLE KASEARCH BIOGRAPHY YAKE NA ALIPOPITIA HUPAONI...HUYO JAMAA MUSIBA SIO MJINGA MJINGA...NI MTU ANAYEJITAMBUA...NI MIONGONI MWA TISS AGENT...AMEJIDHATITI HASA...NA AMEWEKWA HAPO KWA KAZI HIYO...
Wenzio wanamjua alikuwa Chanel Ten

Madogo mnazingua
 
Hv musiba ndo alitakiwa kuhojiwa ili kuthiBitisha tuhuma zake za kutaka kuuliwa na watu hao au hao watu no walitakiwa kuhojiwa??ili wathibitishe nn??
 
Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anahojiwa na ofisi ya Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya jinai ( DCI) Jijini Dar Es Salaam muda huu.

Maxence anahojiwa muda mchache baada ya magazeti ya leo ya Tanzanite na Fahari Yetu kuandika kwamba Maxcence Melo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, TCRA, Balozi Emmanuel Nchimbi na Benard Membe wanapanga njama za kumuua Cyprian Musiba.

Maxence anahojiwa chini ya wakili wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania, Jones Sendodo.

Mbali na Maxence Melo, Magazeti ya Tanzanite na Fahari yetu, yamedai kwamba Mkakati huo wa kumuua Musiba unapangwa pia na baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Watumishi wa Jeshi la Polisi Nchini na Kigogo wa CCM.

Wengine walio kwenye mkakati huo wa kutaka kumuua Musiba ni Balozi wa Tanzania nchini Brazil Dkt. Emmanuel Nchimbi, Benard Membe, Ofisi ya DDP, Mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kanali Kipingu.

Magazeti hayo yamedai watumishi wa TCRA wamefunga account za Mitandao ya Kijamii ya Musiba na kufuatilia Mawasiliano yake.

Gazeti hilo limedai pia kwamba watu hao wanajipanga kifungua kesi nne, Mbili mahakama kuu na mbili mahakama ya Kisutu. Mbali na kesi pia kwamba wana mpango wa kuondoa uhai wake.

Pia Magezeti hayo yamedai kwamba hili Genge linalotaka kumtoa uhai wake, lilikuwa na mkakati wa kuhakikisha wanamuondoa rais Magufuli kupitia baadhi ya wajumbe wanaoingia katika mkutano mkuu wa CCM (NEC) na Kamati kuu(CC), ili asiweze kuendelea na kipindi chake cha pili cha Urais.

Cyprian Majura Musiba ambaye alikuwa Mtangazaji wa zamani wa runinga ya Channel Ten na radio ya Magic FM, ni Mkurugenzi wa kampuni ya CZI na Mhariri wa magazeti ya Tanzanite na Fahari yetu.

Tutaendelea kuwajuza.

======

UPDATES; 1445HRS

MAXCENCE MELO AACHIWA BAADA YA KUHOJIWA NA OFISI YA DCI KWA SAA NNE

Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Forums, Maxence Melo ameachiwa bila masharti yoyote na Ofisi ya DCI baada ya kuhojiwa juu ya tuhuma zilizotolewa na magazeti ya Fahari Yetu na Tanzanite kuwa anashirikiana na Polisi, TCRA, Bernard Membe, Balozi Emmanuel Nchimbi, Kanali Iddi Kipingu na Wakili Jonathan Mndeme kupanga njama za kumuua Ndg. Cyprian Musiba. Maxcence amekuwa mtu wa kwanza kuhojiwa saa chache baada ya gazeti kutoa habari hizo.

Amehojiwa kwa Masaa Manne.

Dar es Salaam
11.07.2019

Zaidi, soma;

View attachment 1151111View attachment 1151112
siasa mbaya sana, inachafua majina ya watu hatar sijui musiba ataacha lini hizi drama zake. kwa nini ccm wasimchukulie hatua kwa sababu naona anataka kuingiza watu kwenye game zake mbaya
 
What will Max gain from the death of Musiba?? Pure Rubbish kabisa. Watuache na JF yetu naona anaanza chokochoko huyu Musiba.
 
Duh!!!
Nionyeshe kadi yangu..

Hayo unayotaka niwe sasa subiri nikajiunge nao niwe hivyo.. na mtaisoma namba na kusaga meno humu..

Waambie waje wanipe fomu nijiunge na Mkulu wetu kabla hajamaliza muda wake 2025.

Itabidi katiba ipokee cheo kingine kipya kumpa nguvu Mh. JPM aendelee kusimamia hii nchi milele.
Asimamie hii nchi milele eenh? Mungu wa wote.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anahojiwa na ofisi ya Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya jinai ( DCI) Jijini Dar Es Salaam muda huu.

Maxence anahojiwa muda mchache baada ya magazeti ya leo ya Tanzanite na Fahari Yetu kuandika kwamba Maxcence Melo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, TCRA, Balozi Emmanuel Nchimbi na Benard Membe wanapanga njama za kumuua Cyprian Musiba.

Maxence anahojiwa chini ya wakili wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania, Jones Sendodo.

Mbali na Maxence Melo, Magazeti ya Tanzanite na Fahari yetu, yamedai kwamba Mkakati huo wa kumuua Musiba unapangwa pia na baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Watumishi wa Jeshi la Polisi Nchini na Kigogo wa CCM.

Wengine walio kwenye mkakati huo wa kutaka kumuua Musiba ni Balozi wa Tanzania nchini Brazil Dkt. Emmanuel Nchimbi, Benard Membe, Ofisi ya DDP, Mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kanali Kipingu.

Magazeti hayo yamedai watumishi wa TCRA wamefunga account za Mitandao ya Kijamii ya Musiba na kufuatilia Mawasiliano yake.

Gazeti hilo limedai pia kwamba watu hao wanajipanga kifungua kesi nne, Mbili mahakama kuu na mbili mahakama ya Kisutu. Mbali na kesi pia kwamba wana mpango wa kuondoa uhai wake.

Pia Magezeti hayo yamedai kwamba hili Genge linalotaka kumtoa uhai wake, lilikuwa na mkakati wa kuhakikisha wanamuondoa rais Magufuli kupitia baadhi ya wajumbe wanaoingia katika mkutano mkuu wa CCM (NEC) na Kamati kuu(CC), ili asiweze kuendelea na kipindi chake cha pili cha Urais.

Cyprian Majura Musiba ambaye alikuwa Mtangazaji wa zamani wa runinga ya Channel Ten na radio ya Magic FM, ni Mkurugenzi wa kampuni ya CZI na Mhariri wa magazeti ya Tanzanite na Fahari yetu.

Tutaendelea kuwajuza.

======

UPDATES; 1445HRS

MAXENCE MELO AACHIWA BAADA YA KUHOJIWA NA OFISI YA DCI KWA SAA NNE

Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Forums, Maxence Melo ameachiwa bila masharti yoyote na Ofisi ya DCI baada ya kuhojiwa juu ya tuhuma zilizotolewa na magazeti ya Fahari Yetu na Tanzanite kuwa anashirikiana na Polisi, TCRA, Bernard Membe, Balozi Emmanuel Nchimbi, Kanali Iddi Kipingu na Wakili Jonathan Mndeme kupanga njama za kumuua Ndg. Cyprian Musiba. Maxence amekuwa mtu wa kwanza kuhojiwa saa chache baada ya gazeti kutoa habari hizo.

Amehojiwa kwa Saa Nne.

Dar es Salaam
11.07.2019

Zaidi, soma Tuhuma za mauaji: Nimehojiwa na Polisi, nimetimiza wajibu wangu

View attachment 1151111View attachment 1151112
Bwana musiba unavyuna ulichopanda kwa UJINGA WAKO MWENYEWE
ALAANIWE AMTEGEMEAYE BINADAMU
 
Back
Top Bottom