Maxence Melo: "Machawa" sio wawakilishi wa Vijana

Status
Not open for further replies.

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Forums, Maxence Melo akiwa katika Maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Afrika, yaliyofanyika Jijini Arusha, Tanzania amesema vijana wanaongoza katika mapambano ya rushwa na ni vema vijana wakashirikishwa katika maamuzi

Akieleze mchango wa Vijana katika Kupambana na rushwa amesema kwa takriban miaka 20 ya JamiiForums, Vijana wameshiriki kwa kiwango kikubwa katika kuibuliwa kwa mambo ya EPA, RICHMOND na mengine mengi, wamekuwa wakijadili mambo anuai mitandaoni, kwenye vyombo vya habari, vyuoni kwenye klabu mbalimbali na sehemu nyingine nyingi.

Aidha, ametoa rai kuwa Vijana washirikishwe huku akitahadharisha kuwa kumekuwa na kundi la vijana linalosema linawakilisha Vijana ila limekuwa likifanya kazi zake kama "Machawa" na kuweka bayana kuwa hao sio wawakilishi wa vijana wala wahawasemei vijana.

Amesema kuna Vijana ambao mara nyingi hawahitaji hata kulipwa, hawahitaji vyeo ila wanahitaji tu kusaidia Taifa lao, waangalie na wana uwezo wa kuwa na mchango mkubwa katika mapambano dhidi ya rushwa

Pia, amesisitiza kuwa ni bora vijana waache, wasitumiwe sheria mbaya dhidi yao. Ametolea mfano Kesi zilizokuwepo dhidi ya yake alizokuwa anawalinda toa taarifa waliokuwa wanafichua uovu, akisema walionekana kama maadui wa Serikali

Amemalizia kwa kusema zitengenezwe namna ambazo ni rafiki, sheria ziwe shirikishi ili kwa vijana wanapofichua masuala ya rushwa na mengine basi wasipitie aliyopitia yeye.

Lakini pia amegusia masuala ya uwekezaji akisema "Kuna watu wanadhani wakija hapa [Tanzania] ni sehemu ya kupiga [Kula rushwa] na wanakuja kufundisha Watanzania au Waafrika namna ya kupiga. Wanakuja kama Wawezekaji ila kwa asilimia kubwa ni wala rushwa wakubwa wenye mbinu mpya kutoka huko walikotoka. Nadhani si vizuri tuweze ku-import ufisadi"

 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom