Maxence Melo aanza kujitetea Kesi Namba 456 Jamhuri vs JamiiForums juu ya Oilcom na Uchakachuaji Mafuta Bandarini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
Kesi namba 456

Kesi namba 456: Jamhuri vs JamiiForums juu ya Oilcom na Uchakachuaji mafuta bandarini kufanyiwa marekebisho tena!

inayowakabili Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media Maxence Melo na mwanahisa mwenzake Mike William, imeendelea leo Katika Mahakama ya Kisutu Dar Es Salaam kwa Hakimu Thomas Simba.

Wakili wa Jamhuri aliyekuwepo ni Sylvia Mitanto na Mawakili wa Utetezi walikuwa Peter Kibatala na Jebra Kambore.

Baada ya kula kiapo, Peter Kibatala anamuongoza kwa Mahojiano Maxence Melo:

Kibatala: Wanasema ulizuia uchunguzi wa Jeshi la Polisi katika eneo la Mikocheni wewe na Mwenzako mkiwa kama wakurugenzi wa Jamii Media inayoendesha JamiiForums; Polisi walitaka kuchunguza taarifa za kampuni ya Oilcom (T) Ltd kuhusu tuhuma za member FUHRER JF-Expert member, Je, ulikuwa Mkurugenzi wa Jamii Media LTD?

Maxence: Ni kweli kwa wakati huo nilikuwa Mkurugenzi.

Kibatala: Wengine ni Wakina nani? Wataje.

Maxence anawataja baadhi ya wakurugenzi.

Kibatala: Mike alikuwa Mkurugenzi?

Maxence: Mike William hayumo. Hakuwa Mkurugenzi. Hata shahidi wa BRELA simkumbuki jina, alisema Mike sio Mkurugenzi. Hakuna mtandao unaoendeshwa chini ya Jamii Media. Jamii Media ilisajiliwa kuendesha na kufanya kazi ya matangazo sio mitandao ya kijamii. Ndiyo leseni yake ya biashara.

Kibatala: Kuna ushahidi wowote uliwahi kuletwa kuonesha kwamba Jamii Media imesajiliwa kuendesha Mitandao ya Kijamii?

Maxence: Hakuna ushahidi wowote ulioletwa.

Kibatala: JamiiForums ni nini?

Maxence: Ni mtandao wa kijamii ulianzishwa mwaka 2006 Machi mwanzoni ikiitwa Jambo Forums. Ni Social Network kwa ajili ya watu kutoa maoni mbalimbali na kushiriki mijadala anuai.

Kibatala: Kuna uhusiano gani wa kisheria kati ya Jamii Media na JamiiForums?

Maxence: Shahidi wa BRELA alisema ‘ule ni mwavuli’ tu. Hakuna uhusiano wowote wa kisheria. Shahidi yule alidai ni kwakuwa aliona jina langu katika kampuni ya Jamii Media.

Kibatala: Watu wanatoaje maoni JamiiForums?

Maxence: Mtandao wa JamiiForums unatoa nafasi ya mtu yeyote kujisajili na kutoa maoni yoyote kwa jina lolote.

Kibatala: Kwenye Hati ya mashtaka wanasema ninyi mnameneji, mnafahamu vipi Identity ya mtu?

Maxence: Hatuna namna ya kufahamu identity ya member. Tunachoangalia ni maoni yake tu.

Kibatala: Hivi ni “Jamii Forum” au JamiiForums?

Maxence: Ni JamiiForums, ina "S".

Kibatala: Mlikataa kutoa identity yake, Fuhrer JF Expert Member, mngewezaje?

Maxence: Hatukuwa na uwezo huo.

Kibatala: Mahakama ingependa kufahamu Privacy ni nini?

Maxence: JamiiForums inaelezea haki za mwanachama anapotumia mtandao huo. Sera yetu ya faragha ipo mtandaoni na kila mtu anaikuta kabla ya kujisajili anaisoma.

Kibatala: Ninapotaka kujiunga naiona?

Maxence: Mtu anapojiunga anaiona kwanza Sera ya faragha.

Kibatala: Haya mambo ya faragha ni kwanini?

Maxence: Sheria za kimataifa zinazoongoza mitandao zinataka Wamiliki wa Mitandao kuwa Sera ya Faragha pia tuliangalia Katiba ya Tanzania Ibara ya 18 pia inalinda faragha ya mtu.

Kibatala: Mtu akijiunga JamiiForums, Wewe unachokiona kinachomhusu ni nini?

Maxence: Tunaona jina alilojisajili na email(mpaka yeye aruhusu) kama hajataja email huwezi kujua.

Kibatala: Kuna ushahidi wowote uliletwa mahakamani kuhusu hii kesi ya Oilcom?

Kibalata: Kuna computer ililetwa mahakamani wakamuonesha hakimu kwamba taarifa za Oilcom zilizoandikwa JamiiForums ni hizi hapa?

Maxence: Hakuna

Kibatala: Kuna printout yoyote iletwa mahakamani kumuonesha Hakimu kwamba FUHRER JF Expert Member, maneno yake aliyoyaandika ni haya hapa?

Maxence: Hakuna.

Kibatala: Wenzetu wa mashitaka wanasema walikuandikia barua, Barua ya 23/2/2016 ilisainiwa na Fatma Kigondo. Ikiihusu Jamii Forum, Jamii Forum ni kitu gani?

Maxence: Sikijui.

Kibatala: Je, kwenye Barua hiyo wanayosema walikuandikia, walitaja kifungu chochote cha Sheria kinachowapa Mamlaka ya kukuandikia Barua? Walisema ni kifungu gani cha sheria?

Maxence: Hawakutaja.

Kibatala: Wanasema Barua walimkabidhi Chrispine, ni lini Chrispine Muganyizi mwenye namba za simu 0714 xxxxx alikuja kutoa ushahidi Mahakamani kudhibitisha kama kweli alipewa barua?

Maxence: Hajawahi kuja.

Kibatala: Ni lini mtandao wa tiGO walikuja kuthibitisha kwamba hizi namba walizotaja ni za Chrispine Muganyizi?

Maxence: Hakuna mtu aliyekuja.

Kibatala: Kuna Dispatch iliyoletwa hapa Mahakamani kuthibitisha kupokewa kwa hii barua ya Polisi?

Maxence: Hapana

Kibatala: Kuna nyaraka barua ya 29/02/2016 ilisainiwa na Benedict Alex ambayo ipo hapa, ni (ID 1), Je unaitambua?

Maxence: Naitambua.

Kibatala: Huyo wakili unamfahamu?

Maxence: Ndio

Kibatala: Ana uhusiano wowote na Jamii Forums?

Maxence: Hapana. Aliandika kwa niaba ya Jamii Media Co. LTD na naomba Mahakama iitambue kama ni majibu yetu kwa Jeshi la Polisi. (Kielelezo).

Kibatala: Hii barua ilikuwa inajibu nini?

Maxence: Tulikuwa tunarejea barua yao waliyotuandikia

Kibatala: Je, barua ilikuwa inaijibu P1?

Maxence: Ndio

Kibatala: Ilikuwa inajibu nini, soma hakimu asikie

Maxence: (Anasoma kilichojibiwa, anamsomea hakimu) kwamba tupo tayari kutoa ushirikiano iwapo watatueleza ni kifungu gani cha Sheria wametumia kinachowapa Mamlaka ya kutaka data za wateja wetu.

Kibatala: Je, mshawahi kujibiwa hiyo barua?

Maxence: Hatujawahi kujibiwa.

Kibatala: Mliahidi nini kwenye barua?

Maxence: Tuliahidi kutoa ushirikiano mkubwa endapo wangeeleza ni kwa mujibu wa sheria gani.

Kibatala: Polisi waliwahi kuja kuomba mahakama itoe amri ya kuwaamrisha ili nyie mtimize matakwa wanayoyataka?

Maxence: Haikuwahi kutokea kitu kama hicho.

Kibalata: Kuna maamuzi ya Mahakama Kuu ya Jaji Korosso na Wenzake (Kitusi na Alfani) ambayo ni hukumu ya Kesi ya Jamii Media dhidi ya Mwamasheria Mkuu wa Serikali(AG) na mkuu wa Polisi(IGP) maamuzo yaliyotolewa Machi 8, 2017. Inakuhusuje?

Maxence: Tulifungua shauri hili Mahakama Kuu baada ya kupata barua nyingi Mfulizo kutoka Polisi na TCRA tukiiomba Mahakama isaidie kutafsiri barua hizo kwani tuliona haki ya faragha inaenda kuvunjwa. Kesi hii tuliifungua ni kabla sijafunguliwa kesi hii (Machi 2016)

Kibalata: Angalia hii hukumu unaitambua?

Maxence: Naikumbuka. Ni hukumu ya Mahakama Kuu.

Kibatala: Mkabidhi Wakili wa Jamhuri kama kielelezo.

(Wakili wa Serikali Sylvia Mitanto, anapinga kutopokelewa kwa hukumu hiyo kama kielelezo).

Sylvia Mitanto: Sikubali hiki kielelezo Sababu ni COPY sio original. Pia nahitaji nipate muda wa kutosha wa kuipitia hii hukumu.

Hakimu Simba: Tunatakiwa tupate majibu ya upande wa pili kuhusu hili pingamizi lilowekwa, hivyo Kibatala mnatakiwa mjibu tarehe 28. Na Nitatoa hukumu ndogo siku hiyo hiyo juu ya hili pingamizi kwamba hii hukumu ikubaliwe au la. Hii Kesi yetu haitakiwi kuvuka mwezi Septemba 2019 kabla ya hukumu.

Tarehe ya kujibu pingamizi la ushahidi ni 28 na 29 mwezi wa 8. Lazima tumalizane na kesi hii mwezi huu tusubiri hukumu.

Kesi imeahirishwa hadi Tarehe 28/08/2019.
***

UPDATE
Kesi namba 456 iliyopo kwa Hakimu Simba, imeahirishwa hadi tarehe 24/09/2019.

Sababu iliyotolewa na hakimu ni kwamba leo kuna kesi nyingi za watu waliopo Mahabusu zimeletwa, hivyo ni vyema waanze na kesi za waliopo Mahabusu.

Kamaliza kwa kusema "Mtuwie radhi".
****

UPDATE
Leo Septemba 24, kesi hii imeendelea lakini imeahirishwa mpaka Oktoba 7, 2019

Sababu ya kuahirishwa ni upande wa Jamhuri kuomba tarehe nyingine kutokana na Wakili wa Jamhuri anayeliendesha shauri hili kupata dharura

Hakimu ameomba mpaka Oktoba 15 kesi iwe imekwisha kwasababu imeshaenda kwa muda mrefu
*****

UPDATE
Kesi namba 456 (Jamhuri v JamiiForums) ya kwa Hakimu Simba imeshindwa kuendelea leo Oktoba 7 na imeahirishwa hadi 29 Oct 2019.

Wakili Msomi wa Utetezi Peter Kibatala ambaye ndiye aliyemuandaa Mkurugenzi wa JamiiForums ndugu Maxence Melo, hakuwepo Mahakamani, alikuwa kwenye majukumu mengine Mahakama Kuu
******

Kesi hii imeendelea leo. Kusoma Kilichojiri Mahakamani Kisutu, soma:
 
Umenikumbusha rafiki yangu mmoja Mtanzania mwenzetu. Yeye aliniambia kwamba kwa mambo yanayoendelea nchini miaka hii ya karibuni akisikia jina Tanzania anachukia sana na kujawa na hasira za hali ya juu. Huyo mtu ni mtu hatari sana kwa Taifa letu na pia na janga kubwa sana. Miaka mine tu nchi inawaka moto kiasi hiki imagine kama atakaa madarakani miaka 10. Mwenyezi Mungu atunusuru Watanzania na hili balaa kubwa lililopo nchi ni mwetu ambalo chanzo chake kikubwa ni huyo dhalimu wa chato.

Najisikia fedheha kuwa mtanzani kwa sasa!!!
 
Bahati mbaya kuna wajinga hawaoni hali hii mpaka yawakute!!

Wengine wako busy wakisifu na kutukuza!!

Katika huu Ulimwengu,huenda hakuna binadamu mbinafsi kama mbongo!!
 
Kesi namba 456 https://www.jamiiforums.com/threads...bandarini-kufanyiwa-marekebisho-tena.1308937/
inayowakabili Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media Maxence Melo na mwanahisa mwenzake Mike William, imeendelea leo Katika Mahakama ya Kisutu Dar Es Salaam kwa Hakimu Thomas Simba.

Wakili wa Jamhuri aliyekuwepo ni Sylvia Mitanto na Mawakili wa Utetezi walikuwa Peter Kibatala na Jebra Kambore.

Baada ya kula kiapo, Peter Kibatala anamuongoza kwa Mahojiano Maxence Melo:

Kibatala: Wanasema ulizuia uchunguzi wa Jeshi la Polisi katika eneo la Mikocheni wewe na Mwenzako mkiwa kama wakurugenzi wa Jamii Media inayoendesha JamiiForums; Polisi walitaka kuchunguza taarifa za kampuni ya Oilcom (T) Ltd kuhusu tuhuma za member Fuhrer JF-Expert member, Je, ulikuwa Mkurugenzi wa Jamii Media LTD?

Maxence: Ni kweli kwa wakati huo nilikuwa Mkurugenzi.

Kibatala: Wengine ni Wakina nani? Wataje.

Maxence anawataja baadhi ya wakurugenzi.

Kibatala: Mike alikuwa Mkurugenzi?

Maxence: Mike William hayumo. Hakuwa Mkurugenzi. Hata shahidi wa BRELA simkumbuki jina, alisema Mike sio Mkurugenzi. Hakuna mtandao unaoendeshwa chini ya Jamii Media. Jamii Media ilisajiliwa kuendesha na kufanya kazi ya matangazo sio mitandao ya kijamii. Ndiyo leseni yake ya biashara.

Kibatala: Kuna ushahidi wowote uliwahi kuletwa kuonesha kwamba Jamii Media imesajiliwa kuendesha Mitandao ya Kijamii?

Maxence: Hakuna ushahidi wowote ulioletwa.

Kibatala: JamiiForums ni nini?

Maxence: Ni mtandao wa kijamii ulianzishwa mwaka 2006 Machi mwanzoni ikiitwa Jambo Forums. Ni Social Network kwa ajili ya watu kutoa maoni mbalimbali na kushiriki mijadala anuai.

Kibatala: Kuna uhusiano gani wa kisheria kati ya Jamii Media na JamiiForums?

Maxence: Shahidi wa BRELA alisema ‘ule ni mwavuli’ tu. Hakuna uhusiano wowote wa kisheria. Shahidi yule alidai ni kwakuwa aliona jina langu katika kampuni ya Jamii Media.

Kibatala: Watu wanatoaje maoni JamiiForums?

Maxence: Mtandao wa JamiiForums unatoa nafasi ya mtu yeyote kujisajili na kutoa maoni yoyote kwa jina lolote.

Kibatala: Kwenye Hati ya mashtaka wanasema ninyi mnameneji, mnafahamu vipi Identity ya mtu?

Maxence: Hatuna namna ya kufahamu identity ya member. Tunachoangalia ni maoni yake tu.

Kibatala: Hivi ni “Jamii Forum” au JamiiForums?

Maxence: Ni JamiiForums, ina "S".

Kibatala: Mlikataa kutoa identity yake, Fuhrer JF Expert Member, mngewezaje?

Maxence: Hatukuwa na uwezo huo.

Kibatala: Mahakama ingependa kufahamu Privacy ni nini?

Maxence: JamiiForums inaelezea haki za mwanachama anapotumia mtandao huo. Sera yetu ya faragha ipo mtandaoni na kila mtu anaikuta kabla ya kujisajili anaisoma.

Kibatala: Ninapotaka kujiunga naiona?

Maxence: Mtu anapojiunga anaiona kwanza Sera ya faragha.

Kibatala: Haya mambo ya faragha ni kwanini?

Maxence: Sheria za kimataifa zinazoongoza mitandao zinataka Wamiliki wa Mitandao kuwa Sera ya Faragha pia tuliangalia Katiba ya Tanzania Ibara ya 18 pia inalinda faragha ya mtu.

Kibatala: Mtu akijiunga JamiiForums, Wewe unachokiona kinachomhusu ni nini?

Maxence: Tunaona jina alilojisajili na email(mpaka yeye aruhusu) kama hajataja email huwezi kujua.

Kibatala: Kuna ushahidi wowote uliletwa mahakamani kuhusu hii kesi ya Oilcom?

Maxence: Hakuna ushahidi wowote ulioletwa.

Kibalata: Kuna computer ililetwa mahakamani wakamuonesha hakimu kwamba taarifa za Oilcom zilizoandikwa JamiiForums ni hizi hapa?

Maxence: Hakuna

Kibatala: Kuna printout yoyote iletwa mahakamani kumuonesha Hakimu kwamba Fuhrer JF Expert Member, maneno yake aliyoyaandika ni haya hapa?

Maxence: Hakuna.

Kibatala: Wenzetu wa mashitaka wanasema walikuandikia barua, Barua ya 23/2/2016 ilisainiwa na Fatma Kigondo. Ikiihusu Jamii Forum, Jamii Forum ni kitu gani?

Maxence: Sikijui.

Kibatala: Je, kwenye Barua hiyo wanayosema walikuandikia, walitaja kifungu chochote cha Sheria kinachowapa Mamlaka ya kukuandikia Barua? Walisema ni kifungu gani cha sheria?

Maxence: Hawakutaja.

Kibatala: Wanasema Barua walimkabidhi Chrispine, ni lini Chrispine Muganyizi mwenye namba za simu 0714 xxxxx alikuja kutoa ushahidi Mahakamani kudhibitisha kama kweli alipewa barua?

Maxence: Hajawahi kuja.

Kibatala: Ni lini mtandao wa tiGO walikuja kuthibitisha kwamba hizi namba walizotaja ni za Chrispine Muganyizi?

Maxence: Hakuna mtu aliyekuja.

Kibatala: Kuna Dispatch iliyoletwa hapa Mahakamani kuthibitisha kupokewa kwa hii barua ya Polisi?

Maxence: Hapana

Kibatala: Kuna nyaraka barua ya 29/02/2016 ilisainiwa na Benedict Alex ambayo ipo hapa, ni (ID 1), Je unaitambua?

Maxence: Naitambua.

Kibatala: Huyo wakili unamfahamu?

Maxence: Ndio

Kibatala: Ana uhusiano wowote na Jamii Forums?

Maxence: Hapana. Aliandika kwa niaba ya Jamii Media Co. LTD na naomba Mahakama iitambue kama ni majibu yetu kwa Jeshi la Polisi. (Kielelezo).

Kibatala: Hii barua ilikuwa inajibu nini?

Maxence: Tulikuwa tunarejea barua yao waliyotuandikia

Kibatala: Je, barua ilikuwa inaijibu P1?

Maxence: Ndio

Kibatala: Ilikuwa inajibu nini, soma hakimu asikie

Maxence: (Anasoma kilichojibiwa, anamsomea hakimu) kwamba tupo tayari kutoa ushirikiano iwapo watatueleza ni kifungu gani cha Sheria wametumia kinachowapa Mamlaka ya kutaka data za wateja wetu.

Kibatala: Je, mshawahi kujibiwa hiyo barua?

Maxence: Hatujawahi kujibiwa.

Kibatala: Mliahidi nini kwenye barua?

Maxence: Tuliahidi kutoa ushirikiano mkubwa endapo wangeeleza ni kwa mujibu wa sheria gani.

Kibatala: Polisi waliwahi kuja kuomba mahakama itoe amri ya kuwaamrisha ili nyie mtimize matakwa wanayoyataka?

Maxence: Haikuwahi kutokea kitu kama hicho.

Kibalata: Kuna maamuzi ya Mahakama Kuu ya Jaji Korosso na Wenzake (Kitusi na Alfani) ambayo ni hukumu ya Kesi ya Jamii Media dhidi ya Mwamasheria Mkuu wa Serikali(AG) na mkuu wa Polisi(IGP) maamuzo yaliyotolewa Machi 8, 2017. Inakuhusuje?

Maxence: Tulifungua shauri hili Mahakama Kuu baada ya kupata barua nyingi Mfulizo kutoka Polisi na TCRA tukiiomba Mahakama isaidie kutafsiri barua hizo kwani tuliona haki ya faragha inaenda kuvunjwa. Kesi hii tuliifungua ni kabla sijafunguliwa kesi hii (Machi 2016)

Kibalata: Angalia hii hukumu unaitambua?

Maxence: Naikumbuka. Ni hukumu ya Mahakama Kuu.

Kibatala: Mkabidhi Wakili wa Jamhuri kama kielelezo.

(Wakili wa Serikali Sylvia Mitanto, anapinga kutopokelewa kwa hukumu hiyo kama kielelezo).

Sylvia Mitanto: Sikubali hiki kielelezo Sababu ni COPY sio original. Pia nahitaji nipate muda wa kutosha wa kuipitia hii hukumu.

Hakimu Simba: Tunatakiwa tupate majibu ya upande wa pili kuhusu hili pingamizi lilowekwa, hivyo Kibatala mnatakiwa mjibu tarehe 28. Na Nitatoa hukumu ndogo siku hiyo hiyo juu ya hili pingamizi kwamba hii hukumu ikubaliwe au la. Hii Kesi yetu haitakiwi kuvuka mwezi Septemba 2019 kabla ya hukumu.

Tarehe ya kujibu pingamizi la ushahidi ni 28 na 29 mwezi wa 8. Lazima tumalizane na kesi hii mwezi huu tusubiri hukumu.

Kesi imeahirishwa hadi Tarehe 28/08/2019.
Masikini Policcm wanafungua kesi hata hawajui wanafungua ya nini, ina husu nani na wapi, hawajui tofauti ya Jamii Media na Jamii forums, wala hawajui walichofungulia kesi ni jamii forums au jamii forum.

Aibu sana hii.
 
Yaani Mkuu inashangaza sana kuona jinsi ya baadhi ya Watanzania wasivyojali kabisa maovu mbali mbali wanayofanyiwa Watanzania wenzao ambao hawana hatia yoyote ile bali kutumia haki yao ya kikatiba kuikosoa Serikali au kufanya kazi zao kama waandishi wa habari. Wengine wamefikia hata kufurahia kubambikiwa kesi kwa Watanzania wenzao hata kuuawa.

Nchi yetu imefikia mahali pabaya sana na upumbavu uliokithiri nchini kwa baadhi ya Watanzania kutojua haki zao kama raia ndiyo chanzo cha maovu yoye haya kwani wengi wa hawa wapumbavu wanaunga mkono kila aina ya maovu yanayoendelea nchini. Mkuki kwa nguruwe.

Bahati mbaya kuna wajinga hawaoni hali hii mpaka yawakute!!

Wengine wako busy wakisifu na kutukuza!!

Katika huu Ulimwengu,huenda hakuna binadamu mbinafsi kama mbongo!!
 
Yaani Mkuu inashangaza sana kuona jinsi ya baadhi ya Watanzania wasivyojali kabisa maovu mbali mbali wanayofanyiwa Watanzania wenzao ambao hawana hatia yoyote ile bali kutumia haki yao ya kikatiba kuikosoa Serikali au kufanya kazi zao kama waandishi wa habari. Wengine wamefikia hata kufurahia kubambikiwa kesi kwa Watanzania wenzao hata kuuawa.

Nchi yetu imefikia mahali pabaya sana na upumbavu uliokithiri nchini kwa baadhi ya Watanzania kutojua haki zao kama raia ndiyo chanzo cha maovu yoye haya kwani wengi wa hawa wapumbavu wanaunga mkono kila aina ya maovu yanayoendelea nchini. Mkuki kwa nguruwe.
Alafu Jumapili na wengine Ijumaa utawakuta wako katika nyumba za ibada eti wanaabudu!!!

Kibaya zaidi,hata hao wanaoitwa/wanaojiita ni viongozi wa dini ,nao wamebaki kusifu kama sio kukaa kimya!!

Ukweli ni bora waliochagua kuwa wapagani kuliko sisi wanafiki tunaojidai kumjua Mungu!!
 
Hawa jamaa bana
 
Naam Mkuu Wanafiki! Wanataka kumdanganya hata Mwenyezi Mungu ambaye anaona jinsi walivyo na roho mbaya na chuki za kutisha hadi kufikia kutoa uhai wa binadamu wenzao ili tu wajione wako salama madarakani.

Alafu Jumapili na wengine Ijumaa utawakuta wako katika nyumba za ibada eti wanaabudu!!!

Kibaya zaidi,hata hao wanaoitwa/wanaojiita ni viongozi wa dini ,nao wamebaki kusifu kama sio kukaa kimya!!

Ukweli ni bora waliochagua kuwa wapagani kuliko sisi wanafiki tunaojidai kumjua Mungu!!
 
Daa nilifanya kosa sana kule mwanzoni ningejua ningejikita kwenye sheria zaidi..
hua napenda sana huo mtiririko wa vijiswali vya wakili
 
Back
Top Bottom