Maxence Melo aanza kujitetea Kesi Namba 456 Jamhuri vs JamiiForums juu ya Oilcom na Uchakachuaji Mafuta Bandarini

Masikini Policcm wanafungua kesi hata hawajui wanafungua ya nini, ina husu nani na wapi, hawajui tofauti ya Jamii Media na Jamii forums, wala hawajui walichofungulia kesi ni jamii forums au jamii forum.

Aibu sana hii.
Sio Policcm pekee Bali hata ofisi ya mwendesha mashtaka wa serikali ni bure kabisa maana wao ndio wanajiridhisha kwanza na mashtaka na Ku frame charge.
Sasa kundi zima lililopo huko hizo LLB zao ni za kuangulia madafu au kusongea ugali?
Au hizo digrii wanasomea Kaole?
 
Hahaha utashangaa wakiona wameshindwa, watamuongezea shitaka la uhujumu uchumi na utakatishaji.
 
Hamia tu somalia si bado.unazo pesa ulizolipwa na Acacia?
Watu kama nyie maneno ya kuwa define vyema yakitolewa yaweza kuonekana kama matusi, lakini acha tuwavumilie tuu kama vile kinyesi pamoja na kuwa ni uchafu kinatokea tumboni
 
Hivi huyo FUHRER aliwai andika tena chochote baada ya pale
Hivi Leo Magufuli akijitokeza na kusema Mimi ndio huyo FUHRER hawa wanafiki sii ni dakika hiyo hiyo kesi ya Max itafutwa na ataanza kuitwa shujaa? Tutasikia matamko ya Kangi , Sirro na hata DPP wakimsifu kwa kubuni wazo la kuanzisha JF?
Tunakwenda hovyo sana kuliko nchi zilizokuwa na kina Mobutu, Bokassa,Nguema au hata PK na M7
 
MARA NYINGI WATU WENYE RANGI NYEUPE WA JINSIA ZOTE KE, NA ME, MFANO KIKWETE, MWINYI, MAJALIWA, MEMBE. MANDELA. WINNIE, JERY RAWLING, SALIM AHMED SALIM, WALTER SISULU, OBAMA, JESSE JACKSON, nk
WANA ROHO NZURI SANA..

LAKINI WENYE RANGI NYEUSII WA-AFRICA ORIGINAL, LOOOOL!
WANA ROHO ZA KOROSHO NI USIPIME. KWA NINI?
KAMA X- WANGU, JACKLINE M. NA JIWE. MOBUTU, AMIN, BOKASA, GRACE MUGABE SAMWEL DOE FANYA KAUCHUNGUZI
wataalamu wa geneology mtusaidie hapa mtujuze, kuna uhusiano gani kwenye Pituitary grand za watu hawa ambazo hu-determine Melanin productions. hivo kumfanya mtu kuwa na rangi ya ngozi nyeusi ilo kolea , Pia hufanya ngozi za watu wengine wawe weupe weupe hivi, akikaa na wazungu anakuwa km wao.

Na wengine huwafanya wawe na rangi nyeusi kama ya jiwe na wenzake nilowataja hapo juu, sijui kwa nini hii kupelekea kuwa na chembechembe za, Umimi, Unafiki, Uchawi, roho mbaya, tena isiyotulia kusaka ubaya tuuu? (nasema walio wengi)

Ni simple tu Chunguzeni , hata wana familia, wasema hovyo na wachawi wengi ni rangi nyeusi. majirani, ukoo, nk. then mlete mrejesho
Nimecheka kama mazuri vile! Inamaana ngozi nyeupe inamfanya mtu kuwa mwema?
Mfano yule Keisha (mjumbe wa KK ya CCM aliyefukuzwa) atakuwa na roho njema?
Mbona amewahi kurekodiwa akimkejeli Lissu aliyekuwa mgonjwa kitandani? Au albino sio rangi nyeupe bali kasoro ya kimaumbile?
 
Maxence: Tulifungua shauri hili Mahakama Kuu baada ya kupata barua nyingi Mfulizo kutoka Polisi na TCRA tukiiomba Mahakama isaidie kutafsiri barua hizo kwani tuliona haki ya faragha inaenda kuvunjwa. Kesi hii tuliifungua ni kabla sijafunguliwa kesi hii (Machi 2016)

Kibalata: Angalia hii hukumu unaitambua?

Maxence: Naikumbuka. Ni hukumu ya Mahakama Kuu.

Kibatala: Mkabidhi Wakili wa Jamhuri kama kielelezo.

(Wakili wa Serikali Sylvia Mitanto, anapinga kutopokelewa kwa hukumu hiyo kama kielelezo).

Sylvia Mitanto: Sikubali hiki kielelezo Sababu ni COPY sio original. Pia nahitaji nipate muda wa kutosha wa kuipitia hii hukumu.

Hakimu Simba: Tunatakiwa tupate majibu ya upande wa pili kuhusu hili pingamizi lilowekwa, hivyo Kibatala mnatakiwa mjibu tarehe 28. Na Nitatoa hukumu ndogo siku hiyo hiyo juu ya hili pingamizi kwamba hii hukumu ikubaliwe au la.
Hii Kesi yetu haitakiwi kuvuka mwezi Septemba 2019 kabla ya hukumu.

Tarehe ya kujibu pingamizi la ushahidi ni 28 na 29 mwezi wa 8. Lazima tumalizane na kesi hii mwezi huu tusubiri hukumu.

Kesi imeahirishwa hadi Tarehe 28/08/2019.

Pole Max na Wenzako! Penye nia kuna Njia!
 
Kesi namba 456

https://www.jamiiforums.com/threads...bandarini-kufanyiwa-marekebisho-tena.1308937/

inayowakabili Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media Maxence Melo na mwanahisa mwenzake Mike William, imeendelea leo Katika Mahakama ya Kisutu Dar Es Salaam kwa Hakimu Thomas Simba.

Wakili wa Jamhuri aliyekuwepo ni Sylvia Mitanto na Mawakili wa Utetezi walikuwa Peter Kibatala na Jebra Kambore.

Baada ya kula kiapo, Peter Kibatala anamuongoza kwa Mahojiano Maxence Melo:

Kibatala: Wanasema ulizuia uchunguzi wa Jeshi la Polisi katika eneo la Mikocheni wewe na Mwenzako mkiwa kama wakurugenzi wa Jamii Media inayoendesha JamiiForums; Polisi walitaka kuchunguza taarifa za kampuni ya Oilcom (T) Ltd kuhusu tuhuma za member FUHRER JF-Expert member, Je, ulikuwa Mkurugenzi wa Jamii Media LTD?

Maxence: Ni kweli kwa wakati huo nilikuwa Mkurugenzi.

Kibatala: Wengine ni Wakina nani? Wataje.

Maxence anawataja baadhi ya wakurugenzi.

Kibatala: Mike alikuwa Mkurugenzi?

Maxence: Mike William hayumo. Hakuwa Mkurugenzi. Hata shahidi wa BRELA simkumbuki jina, alisema Mike sio Mkurugenzi. Hakuna mtandao unaoendeshwa chini ya Jamii Media. Jamii Media ilisajiliwa kuendesha na kufanya kazi ya matangazo sio mitandao ya kijamii. Ndiyo leseni yake ya biashara.

Kibatala: Kuna ushahidi wowote uliwahi kuletwa kuonesha kwamba Jamii Media imesajiliwa kuendesha Mitandao ya Kijamii?

Maxence: Hakuna ushahidi wowote ulioletwa.

Kibatala: JamiiForums ni nini?

Maxence: Ni mtandao wa kijamii ulianzishwa mwaka 2006 Machi mwanzoni ikiitwa Jambo Forums. Ni Social Network kwa ajili ya watu kutoa maoni mbalimbali na kushiriki mijadala anuai.

Kibatala: Kuna uhusiano gani wa kisheria kati ya Jamii Media na JamiiForums?

Maxence: Shahidi wa BRELA alisema ‘ule ni mwavuli’ tu. Hakuna uhusiano wowote wa kisheria. Shahidi yule alidai ni kwakuwa aliona jina langu katika kampuni ya Jamii Media.

Kibatala: Watu wanatoaje maoni JamiiForums?

Maxence: Mtandao wa JamiiForums unatoa nafasi ya mtu yeyote kujisajili na kutoa maoni yoyote kwa jina lolote.

Kibatala: Kwenye Hati ya mashtaka wanasema ninyi mnameneji, mnafahamu vipi Identity ya mtu?

Maxence: Hatuna namna ya kufahamu identity ya member. Tunachoangalia ni maoni yake tu.

Kibatala: Hivi ni “Jamii Forum” au JamiiForums?

Maxence: Ni JamiiForums, ina "S".

Kibatala: Mlikataa kutoa identity yake, Fuhrer JF Expert Member, mngewezaje?

Maxence: Hatukuwa na uwezo huo.

Kibatala: Mahakama ingependa kufahamu Privacy ni nini?

Maxence: JamiiForums inaelezea haki za mwanachama anapotumia mtandao huo. Sera yetu ya faragha ipo mtandaoni na kila mtu anaikuta kabla ya kujisajili anaisoma.

Kibatala: Ninapotaka kujiunga naiona?

Maxence: Mtu anapojiunga anaiona kwanza Sera ya faragha.

Kibatala: Haya mambo ya faragha ni kwanini?

Maxence: Sheria za kimataifa zinazoongoza mitandao zinataka Wamiliki wa Mitandao kuwa Sera ya Faragha pia tuliangalia Katiba ya Tanzania Ibara ya 18 pia inalinda faragha ya mtu.

Kibatala: Mtu akijiunga JamiiForums, Wewe unachokiona kinachomhusu ni nini?

Maxence: Tunaona jina alilojisajili na email(mpaka yeye aruhusu) kama hajataja email huwezi kujua.

Kibatala: Kuna ushahidi wowote uliletwa mahakamani kuhusu hii kesi ya Oilcom?

Kibalata: Kuna computer ililetwa mahakamani wakamuonesha hakimu kwamba taarifa za Oilcom zilizoandikwa JamiiForums ni hizi hapa?

Maxence: Hakuna

Kibatala: Kuna printout yoyote iletwa mahakamani kumuonesha Hakimu kwamba FUHRER JF Expert Member, maneno yake aliyoyaandika ni haya hapa?

Maxence: Hakuna.

Kibatala: Wenzetu wa mashitaka wanasema walikuandikia barua, Barua ya 23/2/2016 ilisainiwa na Fatma Kigondo. Ikiihusu Jamii Forum, Jamii Forum ni kitu gani?

Maxence: Sikijui.

Kibatala: Je, kwenye Barua hiyo wanayosema walikuandikia, walitaja kifungu chochote cha Sheria kinachowapa Mamlaka ya kukuandikia Barua? Walisema ni kifungu gani cha sheria?

Maxence: Hawakutaja.

Kibatala: Wanasema Barua walimkabidhi Chrispine, ni lini Chrispine Muganyizi mwenye namba za simu 0714 xxxxx alikuja kutoa ushahidi Mahakamani kudhibitisha kama kweli alipewa barua?

Maxence: Hajawahi kuja.

Kibatala: Ni lini mtandao wa tiGO walikuja kuthibitisha kwamba hizi namba walizotaja ni za Chrispine Muganyizi?

Maxence: Hakuna mtu aliyekuja.

Kibatala: Kuna Dispatch iliyoletwa hapa Mahakamani kuthibitisha kupokewa kwa hii barua ya Polisi?

Maxence: Hapana

Kibatala: Kuna nyaraka barua ya 29/02/2016 ilisainiwa na Benedict Alex ambayo ipo hapa, ni (ID 1), Je unaitambua?

Maxence: Naitambua.

Kibatala: Huyo wakili unamfahamu?

Maxence: Ndio

Kibatala: Ana uhusiano wowote na Jamii Forums?

Maxence: Hapana. Aliandika kwa niaba ya Jamii Media Co. LTD na naomba Mahakama iitambue kama ni majibu yetu kwa Jeshi la Polisi. (Kielelezo).

Kibatala: Hii barua ilikuwa inajibu nini?

Maxence: Tulikuwa tunarejea barua yao waliyotuandikia

Kibatala: Je, barua ilikuwa inaijibu P1?

Maxence: Ndio

Kibatala: Ilikuwa inajibu nini, soma hakimu asikie

Maxence: (Anasoma kilichojibiwa, anamsomea hakimu) kwamba tupo tayari kutoa ushirikiano iwapo watatueleza ni kifungu gani cha Sheria wametumia kinachowapa Mamlaka ya kutaka data za wateja wetu.

Kibatala: Je, mshawahi kujibiwa hiyo barua?

Maxence: Hatujawahi kujibiwa.

Kibatala: Mliahidi nini kwenye barua?

Maxence: Tuliahidi kutoa ushirikiano mkubwa endapo wangeeleza ni kwa mujibu wa sheria gani.

Kibatala: Polisi waliwahi kuja kuomba mahakama itoe amri ya kuwaamrisha ili nyie mtimize matakwa wanayoyataka?

Maxence: Haikuwahi kutokea kitu kama hicho.

Kibalata: Kuna maamuzi ya Mahakama Kuu ya Jaji Korosso na Wenzake (Kitusi na Alfani) ambayo ni hukumu ya Kesi ya Jamii Media dhidi ya Mwamasheria Mkuu wa Serikali(AG) na mkuu wa Polisi(IGP) maamuzo yaliyotolewa Machi 8, 2017. Inakuhusuje?

Maxence: Tulifungua shauri hili Mahakama Kuu baada ya kupata barua nyingi Mfulizo kutoka Polisi na TCRA tukiiomba Mahakama isaidie kutafsiri barua hizo kwani tuliona haki ya faragha inaenda kuvunjwa. Kesi hii tuliifungua ni kabla sijafunguliwa kesi hii (Machi 2016)

Kibalata: Angalia hii hukumu unaitambua?

Maxence: Naikumbuka. Ni hukumu ya Mahakama Kuu.

Kibatala: Mkabidhi Wakili wa Jamhuri kama kielelezo.

(Wakili wa Serikali Sylvia Mitanto, anapinga kutopokelewa kwa hukumu hiyo kama kielelezo).

Sylvia Mitanto: Sikubali hiki kielelezo Sababu ni COPY sio original. Pia nahitaji nipate muda wa kutosha wa kuipitia hii hukumu.

Hakimu Simba: Tunatakiwa tupate majibu ya upande wa pili kuhusu hili pingamizi lilowekwa, hivyo Kibatala mnatakiwa mjibu tarehe 28. Na Nitatoa hukumu ndogo siku hiyo hiyo juu ya hili pingamizi kwamba hii hukumu ikubaliwe au la. Hii Kesi yetu haitakiwi kuvuka mwezi Septemba 2019 kabla ya hukumu.

Tarehe ya kujibu pingamizi la ushahidi ni 28 na 29 mwezi wa 8. Lazima tumalizane na kesi hii mwezi huu tusubiri hukumu.

Kesi imeahirishwa hadi Tarehe 28/08/2019.

Kila la kheri Maxe. Mwenyezi Mungu akulinde na kukutangulia katika yote.
 
Nimecheka kama mazuri vile! Inamaana ngozi nyeupe inamfanya mtu kuwa mwema?
Mfano yule Keisha (mjumbe wa KK ya CCM aliyefukuzwa) atakuwa na roho njema?
Mbona amewahi kurekodiwa akimkejeli Lissu aliyekuwa mgonjwa kitandani? Au albino sio rangi nyeupe bali kasoro ya kimaumbile?
Mkuu ni walio wengi, hata ukikumbana na kaka jambazi mweupe, ndo wanakuwaga wa kwanza kutamka neno tusimuue!
Yaani mkuu baba kama halifulani hivi inawalazimishaga kufanya ubaya. but siyo wao kabisaaa!
 
Nimecheka kama mazuri vile! Inamaana ngozi nyeupe inamfanya mtu kuwa mwema?
Mfano yule Keisha (mjumbe wa KK ya CCM aliyefukuzwa) atakuwa na roho njema?
Mbona amewahi kurekodiwa akimkejeli Lissu aliyekuwa mgonjwa kitandani? Au albino sio rangi nyeupe bali kasoro ya kimaumbile?
Yaani iko hivi; Layers of Melanin kwa weusi na weupe ni tofauti, Mzungu anazo tatu,Sun violet zina muathiri vibaya hata kupelekea upofu, Wahindi na Waarabu wanazo km 5 hivi, Waafrika 12 sun violet hazimuathiri hata akielekeza macho yake kwenye jua ni poa tu, Albino Baadhi ni ''0 layers,some hawaoni vizuri hivo basi Mzungu anakaribia U-Albinism.
Mkusanyiko mkubwa wa melanin uko kwenye Macho, Kwenye vizalio, na Nywele. Usishangae kuona papuchi ya kitoto kichanga cha leo leo ikiwa nyeusi ni Melanin.
hata mtu mzima ni hivo. fungus wanapenda sana kula hii kitu. hawa waafrica weupe kiasi imepungua .
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii Forums, Maxence Melo amedai sheria za kimataifa zinazoongoza mitandao zinataka wamiliki wa mitandao kuwa na sera ya faragha.

Melo na mwenzake Mike William wanakabiliwa na kesi namba 456 ya mwaka 2016 ya kuzuia Jeshi la polisi kufanya uchunguzi,

Akiongozwa na Wakili wa utetezi, Peter Kibatala jana Jumanne mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, Melo alidai kulingana na Katiba ya Tanzania Ibara ya 18 inalinda faragha ya mtu.

Alidai barua ya Februari 2, 2016 iliyosainiwa na Benedict Alex iliandikwa kwa niaba ya Jamii Media Co. LTD ilikuwa na majibu kwa Jeshi la Polisi.

Melo alidai katika majibu ya barua hiyo walieleza (Polisi) wapo tayari kutoa ushirikiano iwapo wataeleza ni kifungu gani cha sheria wametumia kinachowapa mamlaka ya kutaka data za wateja wao. #KwanzaHabari
 
KILA LA HERI Maxence Melo MUNGU AKUSIMAMIE USHINDE KESI YAKO

UNATULINDA SANA
 
Kesi namba 456

https://www.jamiiforums.com/threads...bandarini-kufanyiwa-marekebisho-tena.1308937/

inayowakabili Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media Maxence Melo na mwanahisa mwenzake Mike William, imeendelea leo Katika Mahakama ya Kisutu Dar Es Salaam kwa Hakimu Thomas Simba.

Wakili wa Jamhuri aliyekuwepo ni Sylvia Mitanto na Mawakili wa Utetezi walikuwa Peter Kibatala na Jebra Kambore.

Baada ya kula kiapo, Peter Kibatala anamuongoza kwa Mahojiano Maxence Melo:

Kibatala: Wanasema ulizuia uchunguzi wa Jeshi la Polisi katika eneo la Mikocheni wewe na Mwenzako mkiwa kama wakurugenzi wa Jamii Media inayoendesha JamiiForums; Polisi walitaka kuchunguza taarifa za kampuni ya Oilcom (T) Ltd kuhusu tuhuma za member FUHRER JF-Expert member, Je, ulikuwa Mkurugenzi wa Jamii Media LTD?

Maxence: Ni kweli kwa wakati huo nilikuwa Mkurugenzi.

Kibatala: Wengine ni Wakina nani? Wataje.

Maxence anawataja baadhi ya wakurugenzi.

Kibatala: Mike alikuwa Mkurugenzi?

Maxence: Mike William hayumo. Hakuwa Mkurugenzi. Hata shahidi wa BRELA simkumbuki jina, alisema Mike sio Mkurugenzi. Hakuna mtandao unaoendeshwa chini ya Jamii Media. Jamii Media ilisajiliwa kuendesha na kufanya kazi ya matangazo sio mitandao ya kijamii. Ndiyo leseni yake ya biashara.

Kibatala: Kuna ushahidi wowote uliwahi kuletwa kuonesha kwamba Jamii Media imesajiliwa kuendesha Mitandao ya Kijamii?

Maxence: Hakuna ushahidi wowote ulioletwa.

Kibatala: JamiiForums ni nini?

Maxence: Ni mtandao wa kijamii ulianzishwa mwaka 2006 Machi mwanzoni ikiitwa Jambo Forums. Ni Social Network kwa ajili ya watu kutoa maoni mbalimbali na kushiriki mijadala anuai.

Kibatala: Kuna uhusiano gani wa kisheria kati ya Jamii Media na JamiiForums?

Maxence: Shahidi wa BRELA alisema ‘ule ni mwavuli’ tu. Hakuna uhusiano wowote wa kisheria. Shahidi yule alidai ni kwakuwa aliona jina langu katika kampuni ya Jamii Media.

Kibatala: Watu wanatoaje maoni JamiiForums?

Maxence: Mtandao wa JamiiForums unatoa nafasi ya mtu yeyote kujisajili na kutoa maoni yoyote kwa jina lolote.

Kibatala: Kwenye Hati ya mashtaka wanasema ninyi mnameneji, mnafahamu vipi Identity ya mtu?

Maxence: Hatuna namna ya kufahamu identity ya member. Tunachoangalia ni maoni yake tu.

Kibatala: Hivi ni “Jamii Forum” au JamiiForums?

Maxence: Ni JamiiForums, ina "S".

Kibatala: Mlikataa kutoa identity yake, Fuhrer JF Expert Member, mngewezaje?

Maxence: Hatukuwa na uwezo huo.

Kibatala: Mahakama ingependa kufahamu Privacy ni nini?

Maxence: JamiiForums inaelezea haki za mwanachama anapotumia mtandao huo. Sera yetu ya faragha ipo mtandaoni na kila mtu anaikuta kabla ya kujisajili anaisoma.

Kibatala: Ninapotaka kujiunga naiona?

Maxence: Mtu anapojiunga anaiona kwanza Sera ya faragha.

Kibatala: Haya mambo ya faragha ni kwanini?

Maxence: Sheria za kimataifa zinazoongoza mitandao zinataka Wamiliki wa Mitandao kuwa Sera ya Faragha pia tuliangalia Katiba ya Tanzania Ibara ya 18 pia inalinda faragha ya mtu.

Kibatala: Mtu akijiunga JamiiForums, Wewe unachokiona kinachomhusu ni nini?

Maxence: Tunaona jina alilojisajili na email(mpaka yeye aruhusu) kama hajataja email huwezi kujua.

Kibatala: Kuna ushahidi wowote uliletwa mahakamani kuhusu hii kesi ya Oilcom?

Maxence: Hakuna ushahidi wowote ulioletwa.

Kibalata: Kuna computer ililetwa mahakamani wakamuonesha hakimu kwamba taarifa za Oilcom zilizoandikwa JamiiForums ni hizi hapa?

Maxence: Hakuna

Kibatala: Kuna printout yoyote iletwa mahakamani kumuonesha Hakimu kwamba FUHRER JF Expert Member, maneno yake aliyoyaandika ni haya hapa?

Maxence: Hakuna.

Kibatala: Wenzetu wa mashitaka wanasema walikuandikia barua, Barua ya 23/2/2016 ilisainiwa na Fatma Kigondo. Ikiihusu Jamii Forum, Jamii Forum ni kitu gani?

Maxence: Sikijui.

Kibatala: Je, kwenye Barua hiyo wanayosema walikuandikia, walitaja kifungu chochote cha Sheria kinachowapa Mamlaka ya kukuandikia Barua? Walisema ni kifungu gani cha sheria?

Maxence: Hawakutaja.

Kibatala: Wanasema Barua walimkabidhi Chrispine, ni lini Chrispine Muganyizi mwenye namba za simu 0714 xxxxx alikuja kutoa ushahidi Mahakamani kudhibitisha kama kweli alipewa barua?

Maxence: Hajawahi kuja.

Kibatala: Ni lini mtandao wa tiGO walikuja kuthibitisha kwamba hizi namba walizotaja ni za Chrispine Muganyizi?

Maxence: Hakuna mtu aliyekuja.

Kibatala: Kuna Dispatch iliyoletwa hapa Mahakamani kuthibitisha kupokewa kwa hii barua ya Polisi?

Maxence: Hapana

Kibatala: Kuna nyaraka barua ya 29/02/2016 ilisainiwa na Benedict Alex ambayo ipo hapa, ni (ID 1), Je unaitambua?

Maxence: Naitambua.

Kibatala: Huyo wakili unamfahamu?

Maxence: Ndio

Kibatala: Ana uhusiano wowote na Jamii Forums?

Maxence: Hapana. Aliandika kwa niaba ya Jamii Media Co. LTD na naomba Mahakama iitambue kama ni majibu yetu kwa Jeshi la Polisi. (Kielelezo).

Kibatala: Hii barua ilikuwa inajibu nini?

Maxence: Tulikuwa tunarejea barua yao waliyotuandikia

Kibatala: Je, barua ilikuwa inaijibu P1?

Maxence: Ndio

Kibatala: Ilikuwa inajibu nini, soma hakimu asikie

Maxence: (Anasoma kilichojibiwa, anamsomea hakimu) kwamba tupo tayari kutoa ushirikiano iwapo watatueleza ni kifungu gani cha Sheria wametumia kinachowapa Mamlaka ya kutaka data za wateja wetu.

Kibatala: Je, mshawahi kujibiwa hiyo barua?

Maxence: Hatujawahi kujibiwa.

Kibatala: Mliahidi nini kwenye barua?

Maxence: Tuliahidi kutoa ushirikiano mkubwa endapo wangeeleza ni kwa mujibu wa sheria gani.

Kibatala: Polisi waliwahi kuja kuomba mahakama itoe amri ya kuwaamrisha ili nyie mtimize matakwa wanayoyataka?

Maxence: Haikuwahi kutokea kitu kama hicho.

Kibalata: Kuna maamuzi ya Mahakama Kuu ya Jaji Korosso na Wenzake (Kitusi na Alfani) ambayo ni hukumu ya Kesi ya Jamii Media dhidi ya Mwamasheria Mkuu wa Serikali(AG) na mkuu wa Polisi(IGP) maamuzo yaliyotolewa Machi 8, 2017. Inakuhusuje?

Maxence: Tulifungua shauri hili Mahakama Kuu baada ya kupata barua nyingi Mfulizo kutoka Polisi na TCRA tukiiomba Mahakama isaidie kutafsiri barua hizo kwani tuliona haki ya faragha inaenda kuvunjwa. Kesi hii tuliifungua ni kabla sijafunguliwa kesi hii (Machi 2016)

Kibalata: Angalia hii hukumu unaitambua?

Maxence: Naikumbuka. Ni hukumu ya Mahakama Kuu.

Kibatala: Mkabidhi Wakili wa Jamhuri kama kielelezo.

(Wakili wa Serikali Sylvia Mitanto, anapinga kutopokelewa kwa hukumu hiyo kama kielelezo).

Sylvia Mitanto: Sikubali hiki kielelezo Sababu ni COPY sio original. Pia nahitaji nipate muda wa kutosha wa kuipitia hii hukumu.

Hakimu Simba: Tunatakiwa tupate majibu ya upande wa pili kuhusu hili pingamizi lilowekwa, hivyo Kibatala mnatakiwa mjibu tarehe 28. Na Nitatoa hukumu ndogo siku hiyo hiyo juu ya hili pingamizi kwamba hii hukumu ikubaliwe au la. Hii Kesi yetu haitakiwi kuvuka mwezi Septemba 2019 kabla ya hukumu.

Tarehe ya kujibu pingamizi la ushahidi ni 28 na 29 mwezi wa 8. Lazima tumalizane na kesi hii mwezi huu tusubiri hukumu.

Kesi imeahirishwa hadi Tarehe 28/08/2019.
I am proudly working with and at JamiiForums.

Ahsante sana Maxence Melo and Team for standing firmly and logical.
 
Back
Top Bottom