Mawifi kuingilia mapenzi ya kaka zao

Mawifi kuingilia mapenzi ya kaka zao

Labda huwezi vitu vya namna i ati
398964866.gif
 
Hayo ni matatizo ya kuishi nyumba za familia...mimi yalishanikuta kwa my wife kupigwa kidomo tena kipindi kifupi tu cha uzazi home kwangu nilimwambia avumilie baada ya uzazi atagundua ameolewa na mwanamme au mvulana.....Hivi sasa kila jambo lisipopitia kwake ndie limezikwa hadi yeye mwenyewe anawaombea pooo. Mmeo ndio mwenye uwezo wa kukufanya wewe first lady wake ila kama una aina ya wanaume wanaotegemea ndg hata namna ya kupanga uzazi wa familia yake pole na tena pole saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaana.
Hatukai nyumba ya familia, tunakaa kwetu wao ndiyo wanakaa wote nyumba moja ya familia baada ya kuachika. Mume wangu anawaelewa sana dada zake kuwa wana matatizo kiasi kwamba hata wakija kwetu kaka yao anakuwa busy na shughuli zake au anatoka kabisa. Na sasa baada ya kuona wamezidi chokochoko amewambia wasikanyage kwake kabisa kama wana shida atawafuata huko huko wanakoishi.
 
ukileta hapa maneno ya taarabu eti ndugu wa mume hawachukuliki mi naona unakosea kwakuwa utakuwa una generalize tu. mi nadhan chamsingi wapotezee tu jua maisha yako na mumeo. na ujaribu sn kuwa nao mbali kma ushaona ni threat kwa ndoa yako. KUMBUKA MAISHA NI KUPANGA NA KUPANGA NI KUCHAGUA!

Sina ukaribu nao tena. Na kaka yao amewapiga marufuku kukanyaga kwake, kama kuna shida kubwa inayohitaji uwepo wake amewambia atawafuata huko huko kwao.
 
mpaka akanioa KIMETAH nimequalify kila idara na hajawahi kujuta kuwa nami!!! Sijui hao dada zake walioachika wameachika kwa sabau zipi.
Labda huwezi vitu vya namna i ati
398964866.gif
 
Sina ukaribu nao tena. Na kaka yao amewapiga marufuku kukanyaga kwake, kama kuna shida kubwa inayohitaji uwepo wake amewambia atawafuata huko huko kwao.

huo sasa ndo mpango mzima! saiv jitaidi kumuenzi mumeo sasa, ucje ukawa umemtenga na dada zake halafu tena mtu mwenyewe ukawa PASUA KICHWA tu!
 
kweli kabisa.. hata mi niliwahi letewa makasheshe mengi tu, mpaka kufikia hatua ya kutukanwa mbele za watu. nilipotetewa, alitishiwa kutengwa, hakujali.
ilipofika wkt wana shida na ada za wtt wao, akasema muombeni mke wangu. wakalalamika, akawaambia kama mlimkosea mke wangu muombeni msamaha, akiwasamehe atawapa hizo hela. tokea hapo heshima mbele
Wewe nawe umeolewa na Mwanamme..... hatujisifii ila tuko wachache sana kama kufananisha timu iliyo uwanjani na mashabiki wa majukwaani. Unajua wanaume tunapooa ndg wanafurahia harusi tuu ila ndani ya mioyo yao hawapendi kwani kwa kiasi wanajua tayari tunaenda kujenga familia nyingine na milango iliyokuwa wazi inazibwa ili kujenga mstakabathi wa maisha....Lazima sheria isimame na itoke kwa mwanamme na siyo mvulana.
 
Hatukai nyumba ya familia, tunakaa kwetu wao ndiyo wanakaa wote nyumba moja ya familia baada ya kuachika. Mume wangu anawaelewa sana dada zake kuwa wana matatizo kiasi kwamba hata wakija kwetu kaka yao anakuwa busy na shughuli zake au anatoka kabisa. Na sasa baada ya kuona wamezidi chokochoko amewambia wasikanyage kwake kabisa kama wana shida atawafuata huko huko wanakoishi.
Okay kumbe nae ni mwanamme....la kufanya acha kuwasilikiliza na kuwasemea kwa yeyote ubaya wanaokufanyia....Kwa kifupi unaishi yako na familia yako mkikutana salamu wifu mkipeana visogo ndio hadi litokee tena... Usiwaendekeze kuwapigia au kupokea simu zao mara kwa mara kama kuna shida watampigia mmeo hivyo usiwe daraja lao...Baada ya muda matusi na kejeli wanazokutolea zitawarudia kwani zitakosa kituo kwako na wataanza kukuogopa, hapo unakuwa umefunga la kisigino kama una harufu ya soka utanielewa.
 
Hii tabia ya mawifi kuingilia ndoa na mapenzi ya kaka zao naichukia sana. Yani mtu unajitahidi kuwaonyesha wema na upendo lakini mwisho wa siku unaonekana mbaya. Sasa najiuliza hawa watu huwa wanataka nini na sometimes wengine ni wake za watu kabisa wameolewa lakini hawaishi kufuatilia maisha ya kaka yao na familia yake. Wanakera sana.

hao mawifi zako wanashughuli gani? maana mi nina wifi mmoja yaani mke wa kaka yangu jinsi nilivyobusy sidhani hata kama huwa na muda wa kufuatilia maisha yao.
 
viwifi vingine unakuta hata kuolewa bado ndo kwanza vimemaliza chuo au viko chuoni lkn chokochoko kibao
 
Hapana mimi siyo PASUA KICHWA.
huo sasa ndo mpango mzima! saiv jitaidi kumuenzi mumeo sasa, ucje ukawa umemtenga na dada zake halafu tena mtu mwenyewe ukawa PASUA KICHWA tu!
 
kila mwanamke/msichana mwenye kaka kuna siku atakua na wifi/mkwe na lawama hii itendelea hii ni chuki ya asili ambayo wanwake wamezaliwa nayo
 
Asante Tamatheo nimekuelewa vizuri. Nashukuru.
Okay kumbe nae ni mwanamme....la kufanya acha kuwasilikiliza na kuwasemea kwa yeyote ubaya wanaokufanyia....Kwa kifupi unaishi yako na familia yako mkikutana salamu wifu mkipeana visogo ndio hadi litokee tena... Usiwaendekeze kuwapigia au kupokea simu zao mara kwa mara kama kuna shida watampigia mmeo hivyo usiwe daraja lao...Baada ya muda matusi na kejeli wanazokutolea zitawarudia kwani zitakosa kituo kwako na wataanza kukuogopa, hapo unakuwa umefunga la kisigino kama una harufu ya soka utanielewa.
 
mwambie mumeo awatafutie mtaji hata laki mbili wawe wanachukua matunda/mboga kariakoo wawe wanatembeza mtaani nadhani hawatapata tena muda wa kufuatilia maisha yako
 
Duh.. Pole sana mdada, Muombe Mungu akusimamie katika Ndoa yako. Hayo ni Mapito tu!!
 
Ukiona wifi anakusumbua sana mwambie aje yeye kukaa na kaka yake. Ni wivu na Stress za maisha tu vinawasumbua wengi wao halafu wanataka kusambaza na wengine nao wapate.

Duh....
 
Lincon, mume wangu aliwapa mtaji wakawa wanapika mama lishe lakini wakala mtaji wakapewa tena bado wakaharibu mara ya mwisho nikawapa mimi lakuni bado wanashindwa kutulia na kufanya biashara.
mwambie mumeo awatafutie mtaji hata laki mbili wawe wanachukua matunda/mboga kariakoo wawe wanatembeza mtaani nadhani hawatapata tena muda wa kufuatilia maisha yako
 
Ukishakuwa na dada ni shida sijui anataman yy awe ndo kaka!!!!
 
Back
Top Bottom