Inakua shida.Kabisa Lizzy umenena....Wengine wanakuwa treated very rude kwenye ndoa zao sasa ngoja wakukute unaishi kimahaba na mkeo...
Inakua shida.
Yani we kaka mtu mkeo kila siku kapendeza, lugha nzuri nyumbani, mnakula na kuvaa vizuri, unamsaidia saidia mkeo vitu vidogo vidogo mkiwa nyumbani, unajali watoto wenu wakati dada yako ye ana ndoano au hana kabisa? Lazima atafute namna ya kuwavuruga aisee.
Btw salama Mkirua . Nimekukosa;-)
Unaishi jirani na hao dada wa kaka yako?
Ni kweli Mwallu, hao wifi zangu wameachika na wote wamerudi kwao kwenye nyumba ya familia wanaishi pamoja, inawezekana ndiyo maana hawaishi kunichimba wanaona nafaidi sana na wakati na mimi nafanya kazi na wala siyo mama wa nyumbani tu wa kungoja kuletewa.pole dada..wengine frustrations za maisha yao zinasababisha wawe hivyo
thank God naelewana na wake za kaka zangu wote
Idimi sisi tunakaa Mbezi Msakuzi na wao wanakaa Kimara Baruti kwenye nyumba ya familia baada ya kuachika.
Ni wivu tu huwasumbua wanaona unafaidi wakati hata na wao wanawafaidi kaka za watu,
Halaf napenda mawifi wenye midomo ili nicheze nao movie kabisaa
Ni kweli Mwallu, hao wifi zangu wameachika na wote wamerudi kwao kwenye nyumba ya familia wanaishi pamoja, inawezekana ndiyo maana hawaishi kunichimba wanaona nafaidi sana na wakati na mimi nafanya kazi na wala siyo mama wa nyumbani tu wa kungoja kuletewa.
Kumbe ndo maana, yani ukitaka kuiona ndoa chungu basi olewa kwenye familia ambayo mawifi wapo tu nyumbani kwao wamekosa waume au waliolewa lakini maisha ya ndoa yakawashinda UTAJUTANi kweli Lizzy maana hao wifi zangu wako wanne. Watatu wote wameachika wapo nyumbani wanatanga na njia. Huyo mmoja ameolewa ana maisha yake mazuri na hana tabia za chokochoko kama hao wengine.
pole, ila jichunguze, pengine kweli kuna tatizo somewhere
Pole dada.
Hapo kwenye bold na rangi pamenipa picha halisi ya hao mawifi zako!
kama una maelewano mazuri na mumeo hakuna haja ya kuhangaika nao
Tatizo kama lipi kibella24? Maana sijawatendea ubaya wowote tena wakati mwingine wanaweza kuomba msaada kaka yao akakataa kutoa mimi ndiyo natoa hela zangu nawapa. Sikukuu nanunua vitu nawaita wanakuja kuchukua. Nifanye nini tena kingine? Kila kukicha maneno mafumbo. Kweli ndugu wa mume hawachukuliki kuna muimba taarabu mmoja aliimba hakukosea.
Hayo ni matatizo ya kuishi nyumba za familia...mimi yalishanikuta kwa my wife kupigwa kidomo tena kipindi kifupi tu cha uzazi home kwangu nilimwambia avumilie baada ya uzazi atagundua ameolewa na mwanamme au mvulana.....Hivi sasa kila jambo lisipopitia kwake ndie limezikwa hadi yeye mwenyewe anawaombea pooo. Mmeo ndio mwenye uwezo wa kukufanya wewe first lady wake ila kama una aina ya wanaume wanaotegemea ndg hata namna ya kupanga uzazi wa familia yake pole na tena pole saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaana.