Mawazo yenu juu ya hili eneo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawazo yenu juu ya hili eneo

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by BelindaJacob, Feb 14, 2012.

 1. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #1
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Wakuu habari za leo.

  Ninaomba ushauri madhubuti kuhusu eneo nililonalo.

  Ni heka 20 eneo la Kibaha Misufini. Zaidi ya kupimwa na kusafishwa mara kwa mara hamna kinachoendelea kwenye hilo eneo na sina mpango wa kujenga huko kwa muda huu.

  Eneo hilo lina ardhi nzuri pia maji mengi sana. Sasa mimi nipo mbali nalo lakini nilipenda nifikirie kitu na kuweza kuliweka hilo eneo katika hali ya kutumika. Mtu wa kuniangalizia ninaweza kupata ambaye atasimamia shughuli nitakayodhamiria kuiendeleza kutokana na mawazo nitakayopata na kuyashambua.

  Natanguliza shukrani kwa mawazo/ushauri wenu.
   
 2. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Kwa kuwa umesema eneo-------- lina rutuba nzuri--------maji ya kutosha-----na unaweza kumpata kijana wa kuliangalia------- i mean kufyeka nk--------- ushauri wangu--------

  wapo wafugaji wengi wa ngombe dsm--- hawa wafugaji wa mjini-----hawana-----majani------

  Ligawe hilo eneo katika vipande vya nusu ekari------tafuta aina tofautitofauti ya majani ya ngombe------yaoteshe kwa kila eneo----baada ya muda------utaanza kuvuna-----na kuuza majani-------ukiweza kufanya kwa umakini uatashangaa ------kila kukicha majani yanafuatwa huko huko shambani----

  Uwekezaji wa namna hii hautakusumbua saana-----hauhitaji mtaji mkubwa-----na wala hautachukua muda wako kufuatilia

  Kila La kheri

  PS
   
 3. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hapo kwenye red ndio wapi? Au Kibaha? Kama ndio, vipi umeshawacheki watu wa ardhi ili ujue matumizi yake? Mimi ninalo la heka 25 Visiga. Nilipotaka kulipima, niliambiwa mtu mmoja hawezi kupimiwa eneo kubwa hivyo kwa sasa (labda heka tatu tatu). Kucheki matumizi, nikakuta ni industrial area/residential na wanalichikulia kama ni kibaha mjini.

  Baada ya kuona hiyo nikaamua kupanda miembe (ili serikali ikilitaka kwa matumizi yake) nipate kitu cha kuthaminisha (ile inayoota kwa muda mfupi). Hata hivyo kwa sasa nataka nilisurvey na kuligawe viwanja vya makazi. Unaweza ukapitia nyao zangu kama ukiona inafaa
   
 4. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #4
  Feb 14, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Mkuu ukishagawa kwa ajili ya makazi tuambie na sisi tuambulie kidogo!!
   
 5. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Usijali kamanda humu jamvini mtakuwa wa kwanza kujua
   
 6. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  niuzie hapo heka 10, then utaona nachofanya na wewe utacopy na kupest kutoka kwangu
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kwanza kabisa onana na maofisa ardhi wakupe mipango ya serikali vinginevyo unaweza kupoteza rasilimali uliyo nayo.

  Ukiona wanakupa jibu la kutatanisha bora kata vipande vipande na kuza viwanja vya makazi, kisha pesa hiyo tafuta eneo linalofaa kwa kilimo
   
 8. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #8
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Mkuu PS,

  Asante sana kwa ushauri mwanana nitauzingatia. Nafanya SWOT analysis zake na kujipanga!


  Nilikosea nimeshasahihisha mkuu, ni Kibaha. Kwakweli zaidi ya kulipima sijawacheki watu wa ardhi, bora umenifumbua macho nifuatilie haraka iwezekanavyo.
  Nitazingatia ushauri wako pia kuhusu upandaji wa hiyo miembe.
   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Feb 14, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Hivi hawa serikali wanasurvey viwanja vya watu bila kuwapa info wakazi wa hapo maana yake nini? Belinda nakushauri panda mitiki tu hapo serikali hawatachukua kabisa na hata wakichukua watakupa mpunga mrefu sana hapo!!!!
   
 10. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #10
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Mwaga ushauri basi Jino kwa Jino..huwezi jua, utanufaisha na wengine pia. Mwenyewe hii ni asset yangu kuuza sasahivi ni ngumu mkuu. Maisha yenyewe haya kama unavyoyaona!


  Candid Scope nashukuru kwa mwangaza wako. Hilo suala la maofisa wa ardhi ni priority na wiki hii nafuatilia kwa hali&mali. Asante mkuu!
   
 11. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #11
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Serikali yetu si unaijua tena King Kong!!..Shukrani pia kwa ushauri wa mitiki, acha nijipange sasa mkuu! asante
   
Loading...