Mawazo yangu kuhusu siasa za 2030

Mawazo yangu kuhusu siasa za 2030

theprogrammer C++

Senior Member
Joined
May 17, 2013
Posts
139
Reaction score
334
Hii ni stori nimeiskia ikizungumzwa kinyemela kwenye vijiwe vyetu vya kahawa Kariakoo. Sijui kama ni kweli au ni soga tu za wazee. ila nimeona niilete hapa tujadili.

Habari nzuri na uwajibikaji, uchapakazi mzuri wa DCEA unaonekana mtaani na faida zake. Tani za dawa zinakamatwa, mamia ya watuhumiwa wanafikishwa mahakamani, kesi nzito zinaendelea na conviction rate ya taasisi yetu ni nzuri sana.

Kuna wanaodai kila operesheni kubwa inayofanikiwa inaongeza imani ya wananchi kwa viongozi wa vyombo vya usalama kuliko hata baadhi ya wanasiasa wanaotafuta kura..... Kuna wanaonong'ona kwamba kama hali hii itaendelea mpaka 2030, huenda akatokea mtu ambaye hatahitaji kuzunguka na ilani ndefu ya CCM. Watu watakuwa wanamtambua kwa rekodi ya operesheni, kukamata wahalifu na kusimamia sheria.

Sisemi ndiyo itatokea. Sina uthibitisho. Ila siasa za Tanzania zina tabia ya kutushangaza.

Nauliza tu, je, inawezekana uchaguzi wa 2030 ukaandikwa mapema kupitia mafanikio ya vita dhidi ya dawa za kulevya???
 
Cha msingi cha kukumbuka ni kwamba historia ya siasa za Tanzania haijawahi kufuata formula ya hisabati. Huwa highly unpredictable. Kumbuka jinsi Magufuli alivyotokea upande ambao hakuna mtu aliyetarajia mwaka 2015, kwa hiyo, hii nadharia ya kwamba mkuu wa DCEA au chombo chochote ataandika historia ya 2030 sasa hivi inaweza kuwa kweli, lakini pia inaweza kuwa distraction tu huku mtu mwingine kabisa asiyetarajiwa akijipanga kimyakimya chini ya kapeti. We just have to wait and see how the cards play out.
 
Ila the guy is playing his card well and underdog.. mtoa mada ametoa hint flani hii farfetched ila kwa siasa za Tanzania inawezekana.
 
I agree.. 2030 anaweza akatoka mgombea kutoka kwenye vyombo vya utendaji vyenye pr nzuri. Mpaka sasa DCEA wanafanya kazi na PR yao ipo topnotch.
 
Uzi wa makachero huyo mwamba toka yuko kahama alikua msumbufu kaenda mwanza wanamjua smart sana ilo zao mfumo Tiss mwenye akili anaechukia vibunda na rushwa Lymo
 
Naunga mkono hoja
Napongeza DCEA
PPP
TUME YA MADINI
TPA
TRC
HIZI TAASISI ZINAKWENDA KUIBEBA TENA CCM KWA MARA NYINGINE NA INASHINDA MAPEMA TU
 
Cha msingi cha kukumbuka ni kwamba historia ya siasa za Tanzania haijawahi kufuata formula ya hisabati. Huwa highly unpredictable. Kumbuka jinsi Magufuli alivyotokea upande ambao hakuna mtu aliyetarajia mwaka 2015, kwa hiyo, hii nadharia ya kwamba mkuu wa DCEA au chombo chochote ataandika historia ya 2030 sasa hivi inaweza kuwa kweli, lakini pia inaweza kuwa distraction tu huku mtu mwingine kabisa asiyetarajiwa akijipanga kimyakimya chini ya kapeti. We just have to wait and see how the cards play out.
Kama mlikuwa hamtarajii Magufuli kuibuka kinara basi hamjui kufuatilia trend za siasa mnaenda kwa mkumbo tu.
2015 kulikuwa na factors nyingi sana zinazoashirian Magufuli kuwa candidate.
Cc Pascal Mayalla
 
Kumbuka hata Membe, Pinda, na Bilal walikuwa na kambi zenye nguvu sana kuliko Magufuli. Magufuli hakuwa na kambi ya kisiasa ndani ya chama, yeye alikuwa anajulikana kama mtendaji tu mkorofi mtaani. Kwenye siasa za CCM, kutokuwa na kambi huwa ni tiketi ya kukatwa mapema sana. Kupenya kwake kulikuja kama compromise candidate baada ya kambi kubwa za kina Lowassa na Membe kuchinjana na kuleta hatari ya kukivunja chama.
 
Unazungumziaje ya 2030 angali 2025 hakukuwa na uchaguzi bali mauaji makubwa yaliwaweka madarakani wauaji ..

Kwasasa yafuatayo yanapaswa kuzungumzwa.

1. Nani alitoa Order ya shoot to kill
2. Maiti za Ndugu zetu zipo wapi tuzike
3. Waliohusiks wote na mauaji makubwa ya Kihistoris wawajibishwe.
4. Uchaguzi mkuu urudiwe
5. Katiba mpya
 
Ni nani atampitisha?
Kikwete atamkubali??

Back
Top Bottom