Hotuba ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda (mb), kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa kazi za Serikali

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
UTANGULIZI

1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba, kutokana na Taarifa zilizowasilishwa katika Bunge lako Tukufu na Wenyeviti wa Kamati za Katiba, Sheria na Utawala; Kamati ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa; Kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara na Kamati ya Masuala ya UKIMWI zilizochambua Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge lako sasa lipokee na kujadili Taarifa ya Mapitio ya Utekelezaji wa Kazi za Serikali kwa mwaka 2013/2014 na Mwelekeo kwa Mwaka 2014/2015. Aidha, naliomba Bunge lako Tukufu likubali kupitisha Makadirio ya Matumizi ya Fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Taasisi zilizo chini yake pamoja na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2014/2015.


2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote na kwa masikitiko makubwanaomba nichukue fursa hii kutoa salamu za pole kwako na kwa Bungelako Tukufu kwa kuondokewa na wabunge wawili, Mheshimiwa William AugustaoMgimwa, aliyekuwa Mbunge wa Kalenga, aliyefariki tarehe 01 Januari, 2014 naMheshimiwa Saidi Ramadhani Bwanamdogo, aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, ambayealifariki tarehe 22 Januari 2014. Aidha, niwape pole Wananchi wa Mkoa waMara kwa kifo cha Mheshimiwa John Gabriel Tupa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo,kilichotokea tarehe 25 Machi 2014, na kwa Wananchi wa Wilaya ya Urambo kwakifo cha Mheshimiwa Anna Magowa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, kilichotokeatarehe 24 Septemba 2013. Vilevile, natoa pole kwa Wananchi wa Wilaya yaKalambo kwa kifo cha Mheshimiwa Moshi Mussa Chang'a aliyekuwa Mkuu waWilaya hiyo, aliyefariki tarehe 21 Aprili 2014. Naomba pia niwape poleWaheshimiwa Wabunge na Wananchi wote waliofiwa na ndugu na jamaa zaokutokana na majanga na matukio mbalimbali tangu nilipowasilisha Bajetiyangu ya mwaka 2013/2014.

Tunamwomba Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu wote mahali pema Peponi.Amina! Nichukue fursa hii pia kuwapa pole Wahanga wote wa majangambalimbali yakiwemo mafuriko na ajali za barabarani, na niwashukuru kwadhati wote waliotoa misaada ya hali na mali wakati wa ajali na maafa hayo.

3. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha 2013/2014, Bunge lakoTukufu limepata Wabunge wapya watatu ambao ni Mheshimiwa Yusuf SalimHussein, Mbunge wa Chambani; Mheshimiwa Godfrey William Mgimwa, Mbunge waKalenga; na Mheshimiwa Ridhiwan Jakaya Kikwete, Mbunge wa Chalinze.Nawapongeza kwa kuchaguliwa kuwawakilisha Wananchi katika Bunge la Jamhuriya Muungano wa Tanzania. Nawaomba watumie fursa waliyoipata kwa manufaa yaWananchi na Taifa kwa ujumla.

MAANDALIZI YA BAJETI

4. Mheshimiwa Spika, huu ni mwaka wa pili tangu tuanzeutaratibu wa Mzunguko mpya wa Bajeti ambao unatuwezesha kukamilisha Mjadalawa Bajeti ya Serikali ifikapo tarehe 30 Juni ya kila mwaka. Taarifa zaawali zinabaini kwamba utaratibu huu umeanza kuonesha mafanikio ya harakakatika utekelezaji wa kazi zilizopangwa. Bajeti hii imeendeleakutayarishwakwa kuzingatia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi yaChama ChaMapinduzi ya mwaka 2010; Awamu ya Pili ya Mkakati wa Kukuza Uchumi naKuondoa Umaskini Tanzania (MKUKUTA II); Mpango wa Kwanza wa Maendeleo waMiaka Mitano wa Mwaka 2011/12 hadi 2015/16; Dira ya Taifa ya Maendeleo2025; Malengo ya Maendeleo ya Milenia 2015; na Mfumo wa Tekeleza Sasa kwaMatokeo Makubwa (*Big Results Now – BRN*). Katika mwaka 2014/2015, Serikaliitaendelea kutekeleza miradi ya kipaumbele iliyoainishwa kwenye mipangohiyo ya Kitaifa ili kuleta maendeleo endelevu na ya harakayatakayowanufaisha Wananchi wa Tanzania.

5. Mheshimiwa Spika, nawashukuru Wajumbe wa Kamati zote zaKudumu za Bunge lako Tukufu kwa mchango wao mkubwa wakati wa uchambuzi waMakadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara, Mikoa, Wakala, Idara za SerikaliZinazojitegemea na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Kazi waliyoifanya ni kubwana ambayo imetuwezesha kukamilisha maandalizi ya Bajeti ninayoiwasilishaleo. Maoni na Ushauri wao utazingatiwa wakati wa kukamilisha mjadala waBajeti ya Serikali na utekelezaji wake.

HALI YA SIASA

6. Mheshimiwa Spika, kwa ujumla hali ya siasa Nchini ni tulivuna Vyama vya Siasa vinaendelea kutekeleza majukumu yao. Nchi yetuinapitia kwenye kipindi cha mpito ambapo tunaandika Katiba Mpya itakayowekamustakabali wa mwelekeo wa Taifa letu kwa miaka mingi ijayo. NawasihiWanasiasa na Wananchi wote kwa ujumla kutoa ushirikiano mkubwa wakati wamaandalizi ya Katiba hiyo ambayo baadaye wananchi wote wataipigia kura yamaoni. Nawaomba tushindane kwa nguvu ya hoja na si hoja ya nguvu katikakuandaa Katiba hii ambayo itatuongoza sasa na vizazi vijavyo.

7. Mheshimiwa Spika, katika jitihada za kukuza na kuimarishademokrasia ya vyama vingi Nchini, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasaimeratibu shughuli za Vyama vya Siasa kwa kuhakikisha kunakuwepo na fursasawa katika shughuli za siasa Nchini. Hadi Aprili 2014, idadi ya Vyama vyaSiasa vyenye Usajili wa kudumu imefikia 21 baada ya Chama cha Ukombozi waUmma (CHAUMMA) kupata usajili wa kudumu mwezi Juni, 2013. Aidha, Chama chaAlliance for Change and Transparency (ACT-TANZANIA), Chama cha Wananchi naDemokrasia (CHAWADE) na Chama cha Maridhiano na Uwiano (CMU) vimepatausajili wa muda. Nirejee wito wangu kwa Viongozi na Wanachama wa vyamavyote vya siasa kuendeleza utamaduni wa kuvumiliana na kutohamasisha siasaza chuki na vurugu ambazo zinaweza kutugawa na kuhatarisha amani, utulivuna umoja wa Taifa letu tulioujenga kwa miaka mingi.

ULINZI NA USALAMA

Usalama wa Raia

8. Mheshimiwa Spika, Nchi yetu imeendelea kudumisha amani nautulivu kama tunu ya Taifa iliyojengwa na kuimarishwa tangu tulipopatauhuru. Katika mwaka 2013/2014, Jeshi la Polisi limeendelea kutekelezaProgramu ya Maboresho ya Jeshi na Mkakati wa Kupunguza Uhalifu ambavyovimeongeza ushirikiano na wananchi. Jeshi hilo limeongeza Vikundi 1,778 vyaUlinzi Shirikishi na kufikia vikundi 6,798 kwa mwaka 2013 kwa Nchi nzima.Vikundi hivyo vimechangia kupunguza vitendo vya uhalifu Nchini kutokaAsilimia 4.3 mwaka 2012 hadi Asilimia 2.8 mwaka 2013 na hivyo kuchangiakupungua kwa makosa makubwa na madogo ya jinai kutoka makosa 566,702 mwaka2012 hadi makosa 560,451 mwaka 2013.

10. Mheshimiwa Spika, Serikali inalaani vitendo hivyovisivyokubalika katika jamii na itawachukulia hatua kali za kisheria walewote watakaobainika kuhusika kwa namna yoyote. Serikali imechukua hatuakadhaa za kudhibiti vitendo hivyo vya mauaji ikiwa ni pamoja na kuwakamatawatuhumiwa 26 na kati yao 13 wamefikishwa mahakamani. Vilevile, Jeshi laPolisi limeunda kikosi kazi kwa ajili ya kudhibiti hali hiyo na kufanyamikutano ya kuhamasisha jamii kuhusu kuanzisha na kuimarisha vikundi vyaPolisi Jamii. Nitoe wito kwa wananchi wema, wenye upendo na Nchi yetu kutoataarifa za uhalifu na wahalifu kwenye vyombo vya usalama ili Sheria ichukuemkondo wake.

Ajali za Barabarani


11. Mheshimiwa Spika, ajali za barabarani zimeendelea kuwa tishiokwa maisha ya watu na mali zao. Takwimu za Jeshi la Polisi zinaonesha kuwakatika mwaka 2013, kulitokea ajali za barabarani 24,480 zilizosababishavifo vya watu 4,091 na majeruhi 21,536 ikilinganishwa na ajali 23,604zilizosababisha vifo vya watu 4,062 na majeruhi 20,037 mwaka 2012. Kwaupande wa pikipiki pekee, mwaka 2012 zilitokea jumla ya ajali 5,763 nakusababisha vifo 930 na majeruhi 5,532. Mwaka 2013, zilitokea ajali 6,831na kusababisha vifo 1,098 na majeruhi 6,578. Aidha, katika kipindi chaJanuari hadi Machi, 2014 zimetokea ajali 1,449 na kusababisha vifo 218 namajeruhi 1,304. Ajali hizi ni nyingi na zinasababisha vifo vingi namajeruhi ambao wengi wao ni nguvukazi ya Taifa.

Ni vyema ikumbukwe kwamba,Serikali iliruhusu matumizi ya pikipiki kwa nia njema ya kupunguza matatizoya usafiri hususan maeneo ya Vijijini. Hata hivyo, fursa hiyo imeambatanana changamoto ya ajali nyingi barabarani. Hivyo ni wajibu wa madereva wotekuzingatia sheria za barabarani na kukidhi vigezo vyote vya kuwa na vibalihalali vya kufanya biashara hizo pamoja na leseni za udereva. SUMATRA,Jeshi la Polisi, Mamlaka za Serikali za Mitaa, na Mamlaka nyinginezinazohusika zinatakiwa kukaa pamoja ili kuweka mkakati wa kukabiliana naajali hizo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba Kanuni za Leseni zaUsafirishaji wa Pikipiki na Bajaji za mwaka 2010 zinatekelezwa ipasavyo.

Hali ya Mipaka ya Nchi

12. *Mheshimiwa Spika*, Serikali imeendelea kuliwezesha Jeshi laWananchi wa Tanzania kutimiza majukumu yake ya kulinda mipaka ya nchi yetuna raia wake. Katika mwaka 2013/2014, Serikali imewezesha Wanajeshi wetukupata mafunzo mbalimbali katika vyuo vya ndani na nje ya Nchi pamoja nakushiriki katika mazoezi ya ushirikiano kikanda. Aidha, Jeshi limeshirikikatika operesheni mbalimbali za kulinda amani zinazoongozwa na Umoja waMataifa huko Darfur (Sudan), Lebanon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo naSudan Kusini. Nafurahi kulieleza Bunge lako Tukufu kuwa Jeshi limefanyakazi kubwa, nzuri na kwa weledi mkubwa, nidhamu na kujituma hivyo kuendeleakuipatia heshima kubwa Nchi yetu. Katika jitihada za kuwapatia Askarimazingira mazuri ya kuishi, Serikali imeanza kutekeleza Awamu ya Kwanza yamradi wa ujenzi wa nyumba za Askari ambapo ujenzi wa majengo 191 kati ya6,064 unaendelea katika vikosi mbalimbali vya Jeshi Nchini.

Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa

13. Mheshimiwa Spi
ka, mwaka 2013/2014 ni wa tatu tangu Serikaliiliporejesha utaratibu wa kuwachukua Vijana wanaohitimu kidato cha sitakujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa Mujibu wa Sheria.Hadi kufikia mwezi Desemba 2013, jumla ya Vijana 15,167 wamehitimu mafunzoya JKT wakiwemo baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wa Bunge hili Tukufu. Mafunzohayo yamewapatia vijana hao fursa ya kujifunza juu ya Ulinzi, Usalama naUkakamavu, Uzalishaji mali, Uzalendo na Umoja wa Kitaifa. Katika mwaka2014/2015, Serikali itachukua vijana zaidi kujiunga na JKT kwa Mujibu wa Sheria.

SHUGHULI ZA UCHAGUZI, BUNGE, MUUNGANO, MABADILIKO YA KATIBA NA VITAMBULISHO VYA TAIFA

Tume ya Taifa ya Uchaguzi


14. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilisimamia na kuendesha chaguzi ndogo za Wabunge katika Majimbomatatu na Udiwani katika Kata 53 nchini. Chaguzi hizo zimefanyika kutokanana sababu mbalimbali zikiwemo vifo na baadhi ya Waheshimiwa Madiwani kukosasifa za kuendelea na nyadhifa hizo. Katika Uchaguzi wa Ubunge uliofanyikakatika Jimbo la Chambani - Zanzibar, CUF ilishinda kwa kupata Asilimia 84ya kura zote. CCM ilipata kura Asilimia 12.4, ADC ilipata kura Asilimia 3.5na CHADEMA ilipata Asilimia 0.4 ya kura zote. Katika Jimbo la Kalenga –Iringa, CCM ilishinda kwa kupata Asilimia 79.3 ya kura, CHADEMA ilipatakura Asilimia 20.2 na CHAUSTA ilipata kura Asilimia 0.5. Katika Jimbo laChalinze – Pwani, CCM ilishinda kwa kupata Asilimia 86.61, CHADEMA ilipatakura Asilimia 10.58, CUF ilipata kura Asilimia 1.98, AFP ilipata kuraAsilimia 0.59 na NRA ilipata Asilimia 0.25 ya kura zote. Aidha, katikaChaguzi za Madiwani zilizofanyika katika Kata 53, CCM ilishinda viti 40,CHADEMA viti 12 na NCCR – Mageuzi kiti kimoja (1).

15. Mheshimiwa Spika, Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaendelea namaandalizi ya kupata vifaa vya kisasa kwa ajili ya zoezi la kuboreshaDaftari la Kudumu la Wapiga Kura. Katika awamu hii ya uboreshaji waDaftari, Mfumo wa Biometric Voter Registration utatumika tofauti na Mfumowa awali wa Optical Mark Recognition ambao ulikabiliwa na changamoto nyingiza utendaji. Mfumo huu wa kisasa unawezesha uandikishaji na uchukuaji waalama za vidole kwa haraka zaidi na hatimaye mwananchi kupatiwakitambulisho cha kupiga kura kwa muda mfupi. Hii itasaidia sana kuokoa mudana kupata takwimu sahihi za wapiga kura watakaoshiriki kwenye chaguzi.

16. Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kuwaomba Viongozi waVyama vya Siasa kuhamasisha Wanachama na Watanzania wote wenye sifakujiandikisha kwenye Daftari hilo na kupata kitambulisho halali cha mpigakura pale zoezi hilo litakapoanza rasmi. Aidha, ninatoa wito kwa Wananchiwote wenye sifa kujitokeza kujiandikisha. Ni imani yangu kwamba tukitumiafursa hii kikamilifu tutaondoa malalamiko ya majina ya baadhi ya wapigakura kutokuwepo kwenye orodha wakati wa chaguzi. Ni muhimu tukumbukekwamba ni wananchi wenye sifa tu ndiyo watakaoandikishwa. Katika mwaka2014/2015, Tume itakamilisha zoezi la kuboresha Daftari la Kudumu la WapigaKura, kusimamia Kura ya maoni kwa ajili ya Katiba Mpya, na kuendelea kutoaelimu ya Mpiga Kura kwa Wananchi.

Bunge

17. Mheshimiwa Spika, kuanzia mwezi Julai, 2013 hadi Aprili 2014,Ofisi ya Bunge imeendesha Mikutano Mitatu ya Bunge na Mikutano mitatu yaKamati za Bunge. Maswali ya Msingi 410 pamoja na maswali 73 ya papo kwapapo kwa Waziri Mkuu yaliulizwa na Waheshimiwa Wabunge na kujibiwa. Aidha,Miswada minane (8) ya Sheria ilipitishwa na Bunge. Pia, Bunge limekamilishaukarabati wa Ukumbi wa Bunge na Miundombinu yake kuwezesha Mkutano wa Bungela Katiba kufanyika na ujenzi wa Ofisi za Wabunge Majimboni umeendeleakufanyika. Vilevile, Ofisi ya Bunge imewajengea uwezo Wabunge na Watumishiwake kupitia semina mbalimbali katika masuala ya Utawala Bora. Katika mwaka2014/2015, Ofisi ya Bunge itaendelea kuratibu Mikutano ya Bunge, Vikao vyaKamati za Kudumu za Bunge pamoja na kuimarisha miundombinu na majengo yaBunge.

Muungano

18. Mheshimiwa Spika, tarehe 26 Aprili 2014, tumeadhimisha Miaka50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Miaka 50 kwa lugha yoyote ilesiyo kipindi kifupi. Tumeweza kufika hapa tulipo kutokana na misingi imaraya Muungano iliyowekwa na Waasisi wetu na kuendelezwa na Viongoziwalioongoza Taifa letu katika awamu zilizofuatia. Tunajivunia kwambaMuungano wa Tanzania umejengeka kwenye historia ya muda mrefu yaushirikiano wa watu wa pande hizi mbili. Jamii hizi zina uhusiano wa damu,kifikra na mapambano ya pamoja dhidi ya wakoloni waliotawala kwa vipinditofauti.

Walichofanya waasisi wetu mwaka 1964 ni kurasimisha ushirikianowetu wa muda mrefu. Nichukue fursa hii kuwashukuru na kuwapongezaWatanzania wote kwa kuadhimisha Miaka 50 ya Muungano. Aidha, ninawashukurukwa dhati Viongozi wote walioongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania naZanzibar tangu kuasisiwa kwa Muungano. Kwa namna ya pekee namshukuruMheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania na Mheshimiwa Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Zanzibar naMwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa Uongozi wao ambao umezifanya pandembili za Muungano kuwa karibu zaidi.

19. Mheshimiwa Spika, tumeadhimisha Miaka 50 ya Muungano tukiwana takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012. Takwimu hizo zinawekajambo moja wazi kwa Muungano wetu; kwamba zaidi ya asilimia 90 yaWatanzania wote wamezaliwa baada ya Muungano. Hivyo, tuliozaliwa kabla yaMuungano ni chini ya asilimia kumi. Kwa mujibu wa takwimu hizo, Tanzanianzima ina watu 44,926,923. Kati yao, watu 40,640,425, sawa na Asilimia90.6 ni wa umri wa siku moja hadi miaka 50. Kwa upande wa Tanzania Bara,idadi ya watu ilikuwa 43,625,354, kati ya hao, watu 39,456,065 sawa naasilimia 90.5 wamezaliwa baada ya Muungano. Kwa upande wa Zanzibarkulikuwa na watu 1,303,569, ambapo watu 1,184,360 sawa na asilimia 90.9wamezaliwa baada ya Muungano. Takwimu hizo zina maana kwamba, asilimia90.6 ya watu wote wamezaliwa ndani ya Muungano na nchi wanayoifahamu niJamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sote tunawajibika kuwatendea haki watuhawa kwa kuulinda, kuuimarisha na kuudumisha Muungano wetu.

20. Mheshimiwa Spika, tuna kila sababu ya kuadhimisha Miaka hii50 ya Muungano kwa furaha. Katika maadhimisho ya mwaka huu, tuliandaa maonesho maalum, makongamano na shughuli nyingine ambazo zilisaidia wananchi kuelimishwa kuhusu masuala ya Muungano. Aidha, kimeandaliwa kitabu maalum kinachoelezea historia, utekelezaji wa mambo ya Muungano, mafanikio,changamoto, fursa na matarajio ya Muungano kwa miaka ijayo. Kitabu hichokitatumika kama rejea kwa kizazi chetu na vizazi vijavyo.

21. Mheshimiwa Spika, tutaendelea kuulinda Muungano wetu kwanguvu zote tukiwa na uelewa kwamba, katika kipindi cha miaka 50 iliyopita Watanzania wameishi kwa amani na kufanya kazi zao za kujiletea maendeleowakiwa upande wowote wa Muungano. Tunatambua changamoto zilizopo natumeweka utaratibu mzuri wa vikao ili kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo. Vikao hivyo vitaendelea kufanyika katika ngazi ya wataalam, Watendaji Wakuuna Viongozi wa Kitaifa. Ni imani yangu kwamba, Muungano huu utaendeleakudumu na watu watapata maendeleo makubwa kwani Jamhuri ya Muungano waTanzania ina fursa nyingi zinazoweza kutumika kwa manufaa ya wote. Sotetukumbuke kuwa, UTANZANIA WETU NI MUUNGANO WETU, TUULINDE, TUUIMARISHE NAKUUDUMISHA!

Mabadiliko ya Katiba


22. Mheshimiwa Spika, tarehe 30 Desemba 2013, Tume ya Mabadilikoya Katiba ilikamilisha Rasimu ya Pili ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano waTanzania na kuikabidhi kwa Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Raiswa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Napenda kuishukuru Tumeya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa ikiongozwa na Mheshimiwa Jaji JosephSinde Warioba kwa kuandaa Rasimu ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano waTanzania. Rasimu hiyo imeliwezesha Bunge Maalum la Katiba kuanza mjadala.Nitumie fursa hii kuwashukuru Watanzania wote kwa kutoa maoni yaliyowezeshaTume kuandaa Rasimu hiyo ya Katiba.

23. Mheshimiwa Spika, Bunge Maalum la Katiba linaundwa na Wabungewa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge wa Baraza laWawakilishi na Wajumbe 201 walioteuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabadilikoya Katiba ya mwaka 2011. Naomba nitumie fursa hii kuwapongeza Wajumbe wotewa Bunge Maalum la Katiba kwa kupata fursa hii ya kuwawakilisha Watanzaniakatika kuandaa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni dhahirikuwa dhamana hii ni kubwa sana!

24. Mheshimiwa Spika, Bunge Maalum la Katiba lilianza kazi rasmitarehe 18 Februari, 2014 kwa kumchagua Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho kuwaMwenyekiti wa muda wa Bunge hilo. Nichukue fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kulisimamia Bunge Maalum hadi kuwezesha kupatikana kwa Kanuni za kuliongoza Bunge hilo. Aidha, niwapongeze Mheshimiwa Samwel John Sitta kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum laKatiba.

Nampongeza Katibu wa Bunge la Katiba Bwana Yahaya Hamadi Khamis naNaibu wake Dkt. Thomas Kashililah pamoja na Wajumbe wote waliochaguliwakuwa Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Kamati 12 za Bunge Maalum. Baada yakukutana kwa muda wa siku 67, Bunge Maalum limeahirisha Mkutano wake tarehe25 Aprili, 2014 ili kupisha majadiliano ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwamwaka 2014/2015. Ni matumaini yangu kwamba, Bunge Maalum la Katibalitakaporejea litakamilisha kazi hiyo kwa umakini na kupata Rasimu ambayohatimaye itapelekwa kwa wananchi kwa ajili ya kura ya maoni.


Vitambulisho vya Taifa

25. Mheshimiwa Spika, katika hotuba yangu ya Bajeti ya mwaka2013/2014 nilielezea dhamira ya Serikali ya kutoa Vitambulisho vya Taifakwa Wananchi wake. Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba, Serikaliimekamilisha usajili na utambuzi wa watu kwa upande wa Zanzibar, Watumishiwa Umma na vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na wakazi wa Mkoa wa Dar esSalaam. Serikali pia, imekamilisha ujenzi wa vituo vya kuingiza na kuhakikitaarifa, kituo cha kutengeneza Vitambulisho na kuhifadhi kumbukumbu pamojana kituo cha uokozi na majanga ya taarifa na takwimu. Katika mwaka 2014/2015, Serikali itaendelea na zoezi la Utambuzi na Usajili waWatanzania katika Mikoa mingine ili kwa pamoja tuweze kunufaika na Vitambulisho vya Taifa katika nyanja za kijamii, kiuchumi na kiusalama.

Sensa ya Watu na Makazi

26. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014, Serikaliimeendelea kutoa machapisho mbalimbali ya matokeo ya Sensa ya Watu naMakazi ya mwaka 2012. Machapisho hayo yanajumuisha Taarifa ya Mgawanyo waWatu kwa Maeneo ya Utawala; Mgawanyo wa Watu kwa Umri na Jinsia na Taarifaza Msingi za Kidemografia, Kijamii na Kiuchumi. Taarifa hizo zimebainikuwa, katika miaka kumi iliyopita kumetokea mabadiliko makubwa ya kiuchumina kijamii katika nchi yetu. Kiwango cha watu wanaojua kusoma na kuandikakimeongezeka kutoka asilimia 69 mwaka 2002 hadi asilimia 78 mwaka 2012.Aidha, uandikishaji halisi katika shule za msingi umeongezeka kutokaasilimia 69 mwaka 2002 hadi 77 mwaka 2012. Idadi ya watu wanaoishi kwenye nyumba zenye kuta imara ni asilimia 74 na asilimia 65.4 wanaishi kwenye nyumba zilizoezekwa kwa bati. Hata hivyo, pamoja na mafanikio hayo, hali ya utegemezi nchini ni kubwa kutokana na ukweli kuwa kati yaWatanzania Milioni 44.9, Asilimia 50.1 ni watoto wenye umri chini ya miaka18. Aidha, takwimu zimebainisha kuwa Asilimia 7.7 ya Watanzania ni watotoyatima. Kutokana na hali hiyo, ni jukumu letu kama Taifa kuweka mipangomadhubuti ya kukabiliana na changamoto hizo katika sekta za huduma za jamiiili hatimaye kila mwenye uwezo wa kufanya kazi achangie ipasavyo katikakukuza uchumi na maendeleo ya nchi yetu.

MASUALA YA UCHUMI

Hali ya Uchumi


27. Mheshimiwa Spika, Pato la Taifa katika mwaka 2013 lilikua kwaAsilimia 7.0 ikilinganishwa na ukuaji wa Asilimia 6.9 mwaka 2012. Ongezekohilo limetokana na ukuaji mzuri wa shughuli za huduma za mawasiliano,viwanda, ujenzi na huduma za fedha. Kutokana na ongezeko hilo, wastani waPato la Mtanzania limeongezeka kutoka Shilingi 1,025,038 mwaka 2012 hadiShilingi 1,186,424 mwaka 2013, sawa na ongezeko la Asilimia 15.7. Mfumukowa Bei umepungua kutoka Asilimia 9.8 Machi 2013 hadi Asilimia 6.1 Machi2014. Kupungua kwa mfumuko wa bei kumechangiwa na kupungua kwa kasi yakupanda bei za bidhaa na vyakula hasa mahindi, mchele na aina nyingine yanafaka.

28. Mheshimiwa Spika, pamoja na uchumi wetu kukua kwa kasi yaasilimia 7.0 kwa mwaka 2013 na Pato la Mtanzania kuongezeka, kiwango hichosiyo kikubwa sana kuwezesha umaskini wa wananchi kupungua kwa kasi.Utafiti wa kitaalam unaonesha kwamba, ili umaskini upungue kwa kasi kubwa,uchumi unatakiwa kukua kwa zaidi ya Asilimia 8 kwa kipindi cha miaka 10mfululizo. Ukuaji huo pia unatakiwa kulenga Sekta ambazo zinagusa maishaya watu wengi, hususan kilimo, mifugo na uvuvi. Mwelekeo wa Serikali nikuweka mazingira wezeshi kwa Sekta za kipaumbele kukua kwa kushirikisha Sekta Binafsi.

Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano

29. Mheshimiwa Spika, Serikali inatekeleza Mpango wa Maendeleo waMiaka Mitano 2011/2012 – 2015/2016 ambao unatekelezwa katika kipindi chamwaka mmoja mmoja. Katika mwaka 2013/2014, Serikali ilitekeleza Mpango huokupitia Kauli mbiu ya Tekeleza Sasa kwa Matokeo Makubwa. Msingi wa kaulimbiu hii ni kuainisha maeneo machache ya kimkakati na kuyatengearasilimali za kutosha, kusimamia na kufuatilia utekelezaji kwa karibuzaidi. Chombo maalum cha Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi yakimkakati chini ya Ofisi ya Rais kinachojulikana kama President's Delivery Bureau – (PDB) kimeanzishwa na Watendaji Wakuu wameteuliwa.Ninapenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba, matunda ya utekelezaji waMfumo huo yameanza kuonekana katika maeneo makuu sita ya kipaumbele kitaifaambayo ni Nishati ya Umeme, Uchukuzi, Kilimo, Elimu, Maji na Ukusanyaji waMapato. Utekelezaji wa miradi hiyo na mafanikio yaliyoanza kupatikana yatatolewa maelezo na Mawaziri katika Sekta husika.

Maendeleo ya Sekta Binafsi na Uwekezaji

30. Mheshimiwa Spika, njia ya uhakika ya kuliwezesha Taifa kuwana uchumi imara na wa kisasa utakaohimili ushindani katika masoko yaKikanda na Kimataifa ni kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji. Katikakufikia azma hiyo, tarehe 31 Januari, 2014 nilizindua rasmi Taarifa yaTathmini ya Sera, Sheria na Kanuni mbalimbali zinazosimamia UwekezajiTanzania. Mapendekezo ya Taarifa hiyo yatatumika kuihuisha Sera ya Taifa yaUwekezaji ya mwaka 1996 pamoja na Sheria ya Uwekezaji Tanzania ya mwaka1997. Aidha, ili kuwawezesha Wawekezaji na Wafanyabiashara kupata hudumana taarifa zote muhimu kama vile Sheria, Kanuni na Taratibu mbalimbalikuhusu biashara na uwekezaji kwa njia ya mtandao, Serikali imezindua upyaTovuti ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania. Kupitia Tovuti hii, Wawekezajipopote duniani wanaweza kupata taarifa kuhusu usajili wa Kampuni naviwango vya kodi kwa njia ya mtandao.

Dhamira ya Serikali ni kuboresha mazingira ya uwekezaji na kupunguzagharama za kufanya biashara nchini ili kukabiliana na ushindani mkubwakutoka nchi nyingine zilizotekeleza maboresho ya mifumo yao ya udhibiti wabiashara.

31. Mheshimiwa Spika, Sekta Binafsi inaendelea kupewa nafasikubwa katika kukuza uchumi Nchini. Takwimu zinaonesha kwamba, Miradiiliyosajiliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania imeongezeka kutoka 869 yenyethamani ya Shilingi Bilioni 31.5 mwaka 2012 hadi miradi 885 yenyethamani ya Shilingi Bilioni 141.2 mwaka 2013.Napenda pia kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba Nchi nyingi dunianizinaendelea kuiamini Tanzania kama Kituo maarufu cha uwekezaji Duniani.Mwezi Novemba, 2011 nilizindua Mpango wa Ushirikiano kati ya Tanzania naUingereza unaojulikana kama Partnership in Prosperity. Mpango huo umelengakuongeza uwekezaji kutoka Sekta Binafsi ya Uingereza kwenye mafuta na gesi,kilimo na Nishati jadidifu. Lengo ni kuongeza uwekezaji kutoka Nchi hiyokwa zaidi ya maradufu ya kiwango cha sasa. Aidha, tumekubalianakushirikiana kuimarisha mazingira ya biashara ili kurahisisha uwekezajikatika sekta hizo.

32. * Mheshimiwa Spika, *baadhi ya Kampuni za Uingereza tayarizimeanza kutekeleza makubaliano hayo kwenye Sekta ya kilimo. Kampuni yaUnilever kwa mfano, itawekeza zaidi ya Shilingi Bilioni 275 kwenye kilimocha chai kwa kushirikiana na wakulima wadogo. Tayari Kampuni hiyo imeanzakupanua Kiwanda cha Chai Kibwele, Mufindi na kufungua zaidi ya Hekta 300 zamashamba ya chai katika Wilaya ya Mufindi. Aidha, Kampuni hiyo imeingizanchini vipando 250,000 vya miche bora ya chai. Pia, Kampuni inaandaa zaidiya miche milioni 2 kwa ajili ya kuwagawia wakulima wadogo Wilayani Njombeili waongeze uzalishaji wa chai Nchini.

33. *Mheshimiwa Spika, *katika mwaka 2013/2014, Kituo cha Uwekezajikimeshirikiana na Uongozi wa Mikoa mbalimbali Nchini kuratibu maandalizi yaMakongamano ya Uwekezaji yenye lengo la kuhamasisha, kukuza na kutangazafursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo kwenye Mikoa hiyo. Jumla ya Mikoa 11imeshiriki kikamilifu kuandaa na kufanikisha Makongamano ya Uwekezajikatika maeneo yao. Mikoa hiyo ni Mwanza, Mara, Kagera, Geita, Simiyu,Shinyanga, Tabora, Manyara, Tanga, Kilimanjaro na Arusha. Makongamano hayoyamechangia kwa kiasi kikubwa kuzitangaza fursa za uwekezaji zilizopokwenye Mikoa hiyo, pamoja na kuihamasisha Mikoa na Halmashauri za Wilayandani ya Mikoa hiyo kuainisha na kutenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji.Aidha, Wawekezaji wengi walioshiriki kwenye Makongamano hayo wameonesha niana utayari wa kuwekeza kwenye Mikoa husika. Jitihada hizi zitaendelezwakatika kipindi kijacho.

Majadiliano na Sekta Binafsi

34. *Mheshimiwa Spika,* kwenye hotuba yangu ya Bajeti mwaka 2013/2014,nilieleza kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Majadiliano ya Ushirikiano kwaManufaa ya Wote. Mkutano huo ulifanyika kuanzia tarehe 28 Juni hadi tarehe1 Julai 2013, Jijini Dar es Salaam chini ya Uenyekiti wa Mheshimiwa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mkutano huoulitoa fursa ya kipekee kwa Viongozi wa Serikali kujadiliana na kupatamaoni ya makundi mbalimbali ya Wananchi kuhusu mbinu za kuongeza kasi yamaendeleo ya kiuchumi na kijamii. Serikali imedhamiria kufanya Majadilianoya Ushirikiano kwa Manufaa ya Wote kila mwaka kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoahadi Taifa kwa kuzingatia fursa kubwa za maendeleo shirikishi zilizopokwenye maeneo husika.

35. *Mheshimiwa Spika, *Baraza la Taifa la Biashara lilifanya Mkutano wakewa Saba tarehe 16 Desemba 2013 chini ya Kauli Mbiu ya "Ukuaji Shirikishi waUchumi". Maazimio ya Mkutano huo ni pamoja na kuunda Kamati Tatu ambazozitashughulikia Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Mazingira Wezeshi ya Biasharana Matumizi Endelevu ya Maliasili za nchi. Kamati ya Mazingira Wezeshi yaBiashara imeanza kuishauri Serikali kuhusu mikakati ya kuwavutia wawekezajiwa ndani na nje na kuongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania. Kazi hiyoimefanyika kwa utaratibu wa Maabara chini ya Mfumo wa Tekeleza Sasa kwaMatokeo Makubwa. Utaratibu huo ulianzisha maeneo sita muhimu ambayoyakishughulikiwa yataboresha mazingira ya biashara nchini. Maeneo hayo nikuboresha Kanuni na Taasisi zinazosimamia biashara; upatikanaji wa ardhi nahaki za umiliki wake na kuimarisha ukusanyaji wa kodi na kupunguza wingi wakodi na tozo mbalimbali. Maeneo mengine ni kuzuia na kupambana na rushwa;kuboresha Sheria za Kazi na kuimarisha mafunzo na stadi za kazi pamoja nakusimamia utekelezaji wa mikataba na utawala wa sheria. Katika mwaka2014/2015, Baraza la Taifa la Biashara litaendelea kuratibu utekelezaji wamaazimio hayo ya Mkutano wa Saba sanjari na kusimamia mikutano ya Mabarazaya Wilaya na Mikoa.

UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI

36. *Mheshimiwa Spika,* dhamira ya Serikali ya kubuni na kutekelezaSera ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004 ni kuhakikisha kwambaWatanzania wananufaika na rasilimali za nchi yao badala ya kubaki kuwawatazamaji. Kwa kutambua umuhimu wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, katikaMwaka 2013/2014 Serikali imeanzisha Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindaniwa Kibiashara (*Tanzania Entrepreneurship Competitiveness Centre*).Taasisi hiyo itatekeleza jukumu la kutoa miongozo ya uandaaji wa mitaala yaujasiriamali katika ngazi tofauti na kuhamasisha uzalishaji wa bidhaa borazitakazohimili ushindani. Aidha, Serikali imeendelea kusimamia Mifuko yaUwezeshaji Wananchi Kiuchumi na kuongeza ufanisi wake. Hadi kufikia mweziFebruari 2013, Mfuko wa Uwezeshaji wa Mwananchi ulikuwa umepokea ShilingiBilioni 2.1 zilizotumika kudhamini mikopo ya wajasiriamali kupitia Benki yaCRDB kwa makubaliano ya kukopesha mara tatu ya dhamana ya Serikali.Kutokana na makubaliano hayo, hadi kufikia mwezi Desemba 2013, mikopo yenyethamani ya zaidi ya Shillingi Bilioni 9.5 ilikuwa imetolewa kwaWajasiriamali 9,790 waliojiunga kwenye Vikundi 283 na Vyama vya Akiba naMikopo (SACCOS) 51 katika Mikoa 12 na Wilaya 27.

37. *Mheshimiwa Spika,* Kwa upande wa Mfuko wa KuendelezaWajasiriamali Wadogo na wa Kati, hadi kufikia Desemba 2013, ulikuwaumetoa mikopo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 36.39 kwaWajasiriamali 62,720. Aidha, Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ulikuwa umetoamikopo kwa Vijana yenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.22 kupitiaSACCOS 244; na Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake ulikuwa umetoa mikopoyenye thamani ya Shilingi Bilioni 5.44 kwa Wanawake 500,000Nchini. Vilevile, Mradi wa Mikopo kwa Wajasiriamali Wadogo (SELF) ulikuwaumetoa mikopo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 57.1 kupitia Asasi 375 zaKifedha ambapo Wajasiriamali 95,034 walinufaika.Mfuko wa Maendeleo ya Jamii – TASAF

38. *Mheshimiwa Spika, *Serikali kupitia Awamu ya Tatu ya Mfuko waMaendeleo ya Jamii (TASAF III) inatekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskinizilizo katika Mazingira Hatarishi Tanzania Bara na Zanzibar. Katikakutekeleza Mpango huo, utaratibu wa uhawilishaji fedha kwa kaya maskiniulifanyika katika Mamlaka za Serikali za Mitaa 22 ambapo kaya 138,032katika Vijiji na Shehia 1,179 zilitambuliwa na kuandikishwa katika Mfumo waMasijala wenye walengwa 464,552. Hadi sasa, Shilingi Bilioni 5.5zimehawilishwa katika kaya hizo. Lengo ni kuziwezesha kaya hizo kupatachakula na kujiongezea fursa ya kipato.

39. *Mheshimiwa Spika,* Serikali pia imejenga uwezo kwa Viongozi naWataalam kutoka maeneo ya utekelezaji wa Mpango huo. Uwezo umejengwa kwakutoa mafunzo katika masuala ya utambuzi, uandikishaji na ukusanyajitaarifa za kaya maskini. Aidha, mafunzo ya usanifu wa miradi ya ujenziyalitolewa kwa wataalam kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa. Pia, Wajumbe17 wa Baraza la Wawakilishi na Wakuu wa Mikoa na Wilaya kutoka Zanzibarwalitembelea Vijiji vya Pongwe-Kiona na Malivundo (Bagamoyo) na Gwata(Kibaha) ili kujifunza kuhusu utekelezaji bora wa Mpango huo. Katika mwaka2014/2015, Serikali itaendelea kufanya utambuzi na uandikishaji wa kayamaskini kufikia maeneo yote 161 ya utekelezaji wa Mpango Tanzania Bara naZanzibar. Lengo ni kutambua na kuandikisha Kaya 920,000 kutoka Vijiji,Mitaa na Shehia 9,000.

UZALISHAJI MALI Uzalishaji wa Mazao


40. *Mheshimiwa Spika*, hali ya upatikanaji wa chakula ni yakuridhisha katika maeneo mengi nchini kufuatia mavuno mazuri ya msimu wa2012/2013. Uzalishaji wa mazao ya chakula kwa msimu huo ulikuwa TaniMilioni 14.38 ikilinganishwa na mahitaji ya chakula ya Tani 12.15 kwa mwaka2013/2014 ikiwa ni ziada ya Tani Milioni 2.3 za chakula. Ongezeko hilolimefanya Taifa kujitosheleza kwa chakula kwa Asilimia 118 na hivyo,kufanya wastani wa bei za mazao ya chakula katika masoko Nchini kuwa zachini katika kipindi chote cha mwaka 2013/2014.

Ruzuku ya Pembejeo za Kilimo

41. *Mheshimiwa Spika*, Serikali imeendelea na juhudi za kuongezatija katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara kulingana na Mipangoinayotekelezwa chini ya Kaulimbiu ya KILIMO KWANZA, na Mpango wa Tekelezakwa Matokeo Makubwa Sasa. Katika mwaka 2013/2014, Serikali imesambaza jumlaya vocha za ruzuku 2,796,300 zenye thamani ya Shilingi Bilioni 83 kwa ajiliya mbolea na mbegu bora za mpunga na mahindi kwa Kaya 932,100. Pia,Serikali ilitoa ruzuku ya dawa za korosho kiasi cha lita 158,845 na Tani620 zenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.5. Vilevile, ruzuku ilitolewa kwaajili ya uzalishaji wa mbegu bora za pamba Tani 4,000 zenye thamani yaShilingi Bilioni 4.8, miche ya kahawa 350,000 yenye thamani ya ShilingiMilioni 100 na miche ya chai 1,850,000 yenye thamani ya Shilingi Milioni300.

42. *Mheshimiwa Spika*, ongezeko la tija katika uzalishaji wa mazaounategemea sana huduma bora za ugani kwa wakulima. Serikali katika mwaka2013/2014, ilitoa kibali cha kuajiri Maafisa Ugani 1,452 ili kufanikishakufikiwa kwa malengo ya kuwa na Afisa Ugani wa Kilimo mmoja kwa kilakijiji. Vilevile, Serikali imeongeza Mashamba Darasa kutoka 16,330 yenyewakulima 344,986 mwaka 2012/13 hadi 16,543 yenye wakulima 345,106 mwaka2013/2014 ili kuimarisha utoaji wa mafunzo kwa wakulima.

43. *Mheshimiwa Spika*, Serikali imeendelea kushirikisha Washirikawa Maendeleo kuchangia Programu ya Kuendeleza Kilimo katika Ukanda waKusini mwa Tanzania (SAGCOT). Miongoni mwa malengo ya Programu hiyo nikuwaunganishawakulima wadogo na mnyororo wa thamani wa kibiashara wa Makampuni makubwaya ndani na nje ya nchi. Ili kufikia lengo hilo, Serikali imeanzisha MfukoChochezi wa Uendelezaji wa Kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania(SAGCOT Catalytic Trust Fund). Mfuko huo utatoa mitaji itakayogharamiahatua za awali za miradi inayotoa tija ya haraka ambayo imebainishwa kwenyeMpango Mkakati wa Uwekezaji.

Vilevile, Mfuko huo utahamasisha biasharainayolenga kumuinua Mkulima mdogo kwa kumuunganisha na mnyororo wa thamanina kampuni kubwa kupitia madirisha makuu mawili. Dirisha la kwanza niMatching Grant Fund linalolenga kuwezesha kampuni kubwa zilizoanzishabiashara ya Kilimo Nchini, kuimarisha minyororo ya thamani inayowahusishawakulima wadogo zaidi au kuanzisha kilimo cha Mkataba kati ya wakulimawakubwa na wakulima wadogo. Dirisha la pili ni Social Venture Capital Fund,linalolenga kuziwezesha biashara changa na za kati kwenye Sekta ya Kilimoau kuwezesha Kilimo cha mkataba kati ya wakulima wakubwa na wakulimawadogo. Tayari Bodi ya Mfuko imeteuliwa na Mtendaji Mkuu wa Mfukoameajiriwa.

44. *Mheshimiwa Spika*, katika mwaka 2014/2015, Serikali kupitiaMfumo wa Tekeleza Sasa kwa Matokeo Makubwa, inategemea kuvutia uwekezaji nakuanzisha Kilimo cha mashamba makubwa 25 ya Kilimo cha kibiashara kwa mazaoya mpunga na miwa kwa utaratibu wa kuwaunganisha wakulima wakubwa na wadogowanaozunguka mashamba hayo. Aidha, itaanzisha, itaboresha na kuendeshakitaalamu maghala 275 ya kuhifadhi mahindi kwa kuwaunganisha wakulimakatika umoja wa kibiashara kwa ajili ya kupata masoko ya pamoja.

Umwagiliaji

45. *Mheshimiwa Spika*, katika juhudi za kuendeleza Kilimo chaumwagiliaji Nchini, Sheria ya Umwagiliaji Namba 5 ya mwaka 2013 imeanzakutumika Mwezi Januari, 2014. Sheria hiyo itaiwezesha Serikali kuanzishaTume ya Umwagiliaji ambayo ni chombo cha kitaifa chenye dhamana yakusimamia, kuendeleza na kudhibiti shughuli za Umwagiliaji Nchini. Sheriahiyo pia itaanzisha Mfuko wa Taifa wa Umwagiliaji utakaosaidia kutekelezamipango ya umwagiliaji kwa kulipia gharama za umwagiliaji zinazofanywa namkulima mmoja mmoja na wawekezaji kupitia mikopo na dhamana. Serikali piailiendelea na ujenzi na ukabarati wa skimu 24 za umwagiliaji zilizopokatika wilaya 15 Nchini. Katika mwaka 2014/2015, Serikali itaendeleza Skimuza Umwagiliaji 39 kwa ajili ya Kilimo cha mpunga.

Miundombinu ya Masoko ya Mazao

46. *Mheshimiwa Spika*, katika mwaka 2013/2014, Serikali kupitiaProgramu ya Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za KifedhaVijijini imekarabati kilometa 352 za barabara za vijijini kwa kiwango chachangarawe katika Halmashauri za Iringa Vijijini, Njombe Vijijini, SingidaVijijini, Mbarali, Lushoto, Same, Mbulu, Msalala na Mpanda. Halmashaurinyingine ni Maswa, Songea Vijijini, Rufiji, Karatu na Kwimba. Vilevile,imejenga maghala matano yenye uwezo wa kuhifadhi tani 1,000 za mazao kilamoja katika halmashauri za Iringa Vijijini, Njombe Vijijini, Same, Songeana Mbarali na kukarabati maghala matatu katika Halmashauri za Sumbawanga,Mbulu na Kahama. Aidha, Programu hiyo imezijengea uwezo benki tisa zawananchi/ushirika ili kuimarisha mfumo wa kifedha Vijijini.

47. *Mheshimiwa Spika*, katika mwaka 2014/2015, Serikali kupitiaProgramu hiyo imepanga kukarabati kilometa 434 za barabara kwa kiwango chachangarawe, kujenga maghala 14 na masoko saba katika Halmashauri 64 zaTanzania Bara na Wilaya 10 za Zanzibar. Aidha, wazalishaji wadogo kutokaMikoa 24 ya Tanzania Bara na Mikoa mitano ya Zanzibar watajengewa uwezo wakuhifadhi mazao na mbinu za kufikia masoko ambapo zaidi ya wananchi 100,000watanufaika na mafunzo hayo.

Maendeleo ya Ushirika

48. *Mheshimiwa Spika*, Sheria ya Ushirika Namba 6 ya mwaka 2013imetungwa na imeanza kutumika Mwezi Januari, 2014. Sheria hiyo itawezeshakuanzishwa kwa Tume ya Maendeleo ya Ushirika ambayo itakuwa na majukumu yakusimamia moja kwa moja Vyama vyote vya Ushirika. Aidha, kupitia Sheriahiyo, Serikali imetoa Waraka Namba 1 wa mwaka 2014 unaotoa ufafanuzi kuhusuChaguzi katika Vyama vya Ushirika. Ili kuondoa migogoro ya kimaslahi,Waraka huo umewaondoa Viongozi wa Siasa na Serikali katika uongozi waVyama vya Ushirika katika ngazi zote. Katika mwaka 2014/2015, Serikaliitaimarisha uratibu wa Vyama vya Ushirika kulingana na mahitaji ya Wananchina kuunganisha Vyama vya Ushirika na Taasisi za fedha ili kuboresha utoajiwa huduma za kifedha kwa Vyama vya Ushirika.

Maendeleo ya Sekta ya Mifugo

49. *Mheshimiwa Spika*, kupitia Mpango wa Ruzuku ya dawa yakuogeshea mifugo, Serikali ilitoa jumla ya lita 11,020 zenye thamani yaShilingi Milioni 181.8 na kusambazwa nchini. Vilevile, ilitoa chanjo kwaajili ya kudhibiti magonjwa ya mifugo ambapo dozi 150,000 za chanjo yaUgonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa zenye thamani ya Shilingi milioni 119ilitolewa katika Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Tanga na Dodoma.Vilevile, Serikali imeimarisha Kituo cha Uhamilishaji kilichopo katika eneola Usa River, Arusha pamoja na Vituo vingine vitano vya Kanda kwa kusimikamitambo ya kuzalisha kimiminika cha naitrojeni na kujenga Vituo vitano vyamadume bora.

Vilevile, ng'ombe walionenepeshwa wameongezeka kutoka 132,246mwaka 2011/2012 hadi kufikia 175,000 mwaka 2013/2014. Ili kuboreshaupatikanaji wa maziwa Nchini, Serikali imeongeza uzalishaji mitamba katikamashamba yake kutoka mitamba 943 kwa mwaka 2012/2013 hadi mitamba 1,046mwaka 2013/2014 na kusambaza Mbuzi wa maziwa 9,530 kupitia Mpango wa KopaMbuzi lipa Mbuzi. Jitihada hizi, zimesaidia wafugaji kuongeza tija na hivyokuchangia ongezeko la uzalishaji wa maziwa kutoka lita Bilioni 1.9 mwaka2012/2013 hadi lita Bilioni 2 mwaka 2013/2014.

50. *Mheshimiwa Spika*, katika mwaka 2014/2015, Serikali itatoaruzuku ya dawa za kuogesha mifugo na kununua dozi milioni moja kwa ajili yachanjo ya ugonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa kwa Mikoa ya Arusha, Tanga,Tabora na baadhi ya mikoa katika Kanda ya Ziwa. Vilevile, Serikaliitaimarisha Vituo vya uhamilishaji, mashamba ya kuzalisha mifugo bora nayale yanayozalisha mbegu bora za mifugo pamoja na kununua mifugo wazazi.

Maendeleo ya Sekta ya Uvuvi

51. *Mheshimiwa Spika, *katika mwaka 2013/2014, Serikali kwakushirikiana na wadau ilihuisha Sera ya Taifa ya Uvuvi ya mwaka 1997 naSheria ya Uvuvi Namba 22 ya mwaka 2003 ili ziendane na mabadiliko yakiuchumi, kisayansi na kiteknolojia. Katika kuimarisha ufugaji wa samaki,wakulima 2,604 walipewa mafunzo ya ufugaji bora wa samaki na mabwawa 64yalichimbwa. Hatua hiyo imeongeza idadi ya mabwawa ya Samaki kufikia 20,198yenye uwezo wa kuzalisha Tani 3,029.7 za samaki ikilinganishwa na mabwawa20,134 yaliyokuwepo mwaka 2012/2013. Vituo vya kuzalisha vifaranga wasamaki kwa wingi kwa kutumia teknolojia ya ndani viliongezeka kutoka *kituokimoja* mwaka 2012/2013 hadi kufikia *vituo vitano* mwaka 2013/2014 vyenyeuwezo wa kuzalisha vifaranga bora vya samaki Milioni 10 kwa mwaka. Serikalipia, ilijenga matanki sita yenye lita za ujazo 8,000 kila kimoja kwa ajiliya kuzalisha vifaranga vya samaki.

52. *Mheshimiwa Spika*, katika mwaka 2014/2015, Serikali itaanzishaVituo vya kuzalishia vifaranga vya samaki katika maeneo ya Bacho Dareda -Manyara, Hombolo – Dodoma, na Kigoma. Vilevile, itajenga bwawa la kufugasamaki katika Kituo cha Mafunzo ya Kilimo cha Kilimanjaro – KATC; na kutoaruzuku kwa ajili ya kuchimba mabwawa na kuzalisha vifaranga wa samaki.

Ufugaji Nyuki

53. *Mheshimiwa Spika*, Sekta ya ufugaji nyuki imeendelea kuimarikana kuchangia kuongeza ajira na kupunguza umaskini. Mwaka 2013, thamani yamauzo ya asali nje yalifikia Shilingi Milioni 287.3 ikilinganishwa na mauzoya Shilingi Milioni 262 mwaka 2012. Katika kipindi hicho, jumla ya Tani384 za nta zenye thamani ya Shilingi Milioni 4,660 ziliuzwa njeikilinganishwa na Tani 277 zenye thamani ya Shilingi Milioni 2,583zilizouzwa mwaka 2012.

Nchi zilizoongoza katika ununuzi wa Asali na Nta yaTanzania ni Ujerumani, Oman, China, Japan, Yemen, India, Ubelgiji,Botswana, Kenya na Marekani. Kutokana na maendeleo haya mazuri katika mwaka2013/2014, Serikali imetenga maeneo 20 yenye ukubwa wa Hekta 58,445 sehemumbalimbali Nchini kwa ajili ya hifadhi za nyuki. Aidha, imetoa mafunzokwa wafugajinyuki 924 na vikundi 49 kutoka Wilaya 12 pamoja na kutoa elimu ya miongozona sheria za ubora wa mazao ya nyuki kwa wafanyabiashara wa mazao ya nyuki.

54. *Mheshimiwa Spika*, katika mwaka 2013/2014, Tanzania ilishirikikwenye Kongamano la Ufugaji nyuki lililofanyika Kiev, Ukraine. KatikaKongamano hilo, mazao ya nyuki kutoka Tanzania yalikuwa kivutio kikubwa nayaliwezesha kupata medali ya Banda Bora la Asali kutokana na asali yake kuwana viwango vya ubora na usalama vinavyokubalika Kimataifa. Aidha, kampunimbalimbali zilionesha nia ya kuwekeza kwenye Sekta ya ufugaji nyukiNchini.
 
waziri mkuu ahsante kwa bajeti yako..lakini kama waziri mkuu wa Tanzania sioni kitu cha mana kwa upande wa Zanzibarkatika bajet yako ya 5 triliioni.
ofisi yako inaonekana ni kamaya Tanganyika tu japo ukweli hautakiwi ....kuitaja Tanganyika ni nongwa..lakini mfumo huu haujengi
 
Ukurasa wa mwisho wa hotuba ya Waziri mkuu (Mh.Pinda) wakati akiomba bunge lipitishe bajeti yake na ya TAMISEMI alisema hivi:

"Halmashauri zote zinaombewa jumla ya Shilingi Trilioni Nne, Bilioni Mia Mbili Thelathini na Moja, Milioni Mia Nne Arobaini na Mbili, Mia Tisa Sabini na Nne Elfu (4,231,442,974,000).....

..... Kati ya fedha hizo, Shilingi Trilioni Tatu na Bilioni Tisini, Milioni Mia Tatu Sabini, Mia Tatu na Nane Elfu (3,090,370,308,000) ni za Matumizi ya Kawaida na Shilingi Bilioni Mia Sita Themanini na Mbili, Milioni Mia Sita na Mbili na Arobaini na Nne Elfu (682,602,044,000) ni za Miradi ya Maendeleo."

UNAELEWA HII INAMAANISHA NINI?
Hii inamaanisha kuwa Sh.3,090,370,308,000/= sawa na 73.03% ni za matumizi ya kawaida kama kunywa chai, safari, warsha, semina, posho za vikao etc. Na Sh.682,602,044,000/= sawa na 26.96% tu, ndio za miradi ya maendeleo.

Yani watu watatumia 74% ya bajeti ili wazalishe 26%. Nahisi bado hujanielewa. Yani ni sawa na kumlipa mtu laki moja ili akufanyie kazi ambayo itakuingizia elfu 10..!

Bado nahisi hujaelewa. Ni hiviiii...... Ni sawa na ununue simu ya elfu 25, halafu uiwekee screen protector ya laki tatu...!

KARIBU TANZANIA.!!!
 
CHUKUA CHAKO MAPEMA
CHAMA CHA MAFISADI
CHAMA CHA MAJANGILI
Hiyo bajeti itaungwa mkono kwa 100% na wabunge wote wa CHUI, CHATU na MAFISI

Ngoja nijihami na Dengu kwanza
 
Si.ndio.maana viongizi huwa wanawaza kwa kutuma kabaaaang kwa sababu wanakula sana
 
Usijali hii inapatikana Tanzania tu.Yaani kiinglish wanasema 'Made in Tanzania only":A S cry:
 
Jamani Watanzania!!! Watanzaniaaaaaaaaaa!!! Tangu lini mkawa Wagalatia!!!!! Huku sio kulogwa ni kuchizi, kurukwa akili, we.u na uzez.eta uliopita kipimo ......... naita Watanzaniaaaaaaaaaaaaaa!! Stop being sleeping dogs, hii ni dharau kubwa sana. IS THIS NOT A NATION OF YOU?????
 
Jamani Watanzania!!! Watanzaniaaaaaaaaaa!!! Tangu lini mkawa Wagalatia!!!!! Huku sio kulogwa ni kuchizi, kurukwa akili, we.u na uzez.eta uliopita kipimo ......... naita Watanzaniaaaaaaaaaaaaaa!! Stop being sleeping dogs, hii ni dharau kubwa sana. IS THIS NOT A NATION OF YOU?????


wewe ni mutu ya kenya au ya museven aloo
 
nakuona mweupe kabisa kichwani. wala hujaelewa kitu. ni vizuri ukauliza ueleweshwe kuna wataalamu wengi tu humu. au unaweza kum-PM yule mchumi na 1 tanzania -mwingulu!

Ukurasa wa mwisho wa hotuba ya Waziri mkuu (Mh.Pinda) wakati akiomba bunge lipitishe bajeti yake na ya TAMISEMI alisema hivi:



UNAELEWA HII INAMAANISHA NINI?
Hii inamaanisha kuwa Sh.3,090,370,308,000/= sawa na 73.03% ni za matumizi ya kawaida kama kunywa chai, safari, warsha, semina, posho za vikao etc. Na Sh.682,602,044,000/= sawa na 26.96% tu, ndio za miradi ya maendeleo.

Yani watu watatumia 74% ya bajeti ili wazalishe 26%. Nahisi bado hujanielewa. Yani ni sawa na kumlipa mtu laki moja ili akufanyie kazi ambayo itakuingizia elfu 10..!

Bado nahisi hujaelewa. Ni hiviiii...... Ni sawa na ununue simu ya elfu 25, halafu uiwekee screen protector ya laki tatu...!

KARIBU TANZANIA.!!!
 
Ambae hatakuelewa kwa mifano uliyoitoa hakika atakua amekunywa maji ya bendera ya CCM Alaf at the same time ana dalili za ugonjwa wa Dengu
 
Kuna ndugu yangu mmoja katoa mfano mmoja rahisi kua ni sawa na unanunua simu kwa laki1 then wanakuuzia ile screen protector kwa Millioni 1,nahisi huyu mzee aliandikiwa hii bajeti na yeye mwenyewe hajaisoma au ndo kwa matumizi ya 2015?
 
Kuna ndugu yangu mmoja katoa mfano mmoja rahisi kua ni sawa na unanunua simu kwa laki1 then wanakuuzia ile screen protector kwa Millioni 1,nahisi huyu mzee aliandikiwa hii bajeti na yeye mwenyewe hajaisoma au ndo kwa matumizi ya 2015?

Hali hii tutaendelea nayo mpaka lini?
 
Kama umesikiliza hotuba yote kwanini usituwekee mchanganuo wa hiyo bilioni 3????

Mishahara nayo italipwa na hela za miradi????
 
Ninavyojua TAMISEMI inashughulikia kila kitu sehemu husika. Ningetegemea nisikie kinyume chake hiyo hela ilivtotengwa yaani ya maendeleo iwe ya matumizi ya kawaida. Hii ni kwa sababu kwa jinsi ilivyotolewa bado itatuchukua zaidi ya miaka kumi kupata madarasa na madawati ya kutosha watoto wetu, vituo vya afyapamoja na huduma nyingine za kijamii!

Hivi mbona huwa hatuelezwi kwa mwaka fulani wa fedha tutapunguza deni letu la taifa kwa kiasi gani? Kuna wananchi wengine tuko tayari kuchangia dola moja kwa mwaka!
 
Mimi nawaambieni ccm ni janga lakitaifa bado tuu watu wabishi. Hebu tuache ubishi kila mmoja amshawishi rafiki ndugu jamaa yake mmoja tu na kumsisitiza amweleze mwenzake mmmoja tu ili tujaribu chama kingine pia kenya wamejaribu mbona
 
Back
Top Bottom