Mawazo yangu kuhusu kilimo Tanzania

Mawazo yangu kuhusu kilimo Tanzania

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
5,895
Reaction score
11,788
Mbeya_Tanzania.jpg

Wakuu Tanzania ni nchi kubwa sana na ina resources nyingi sana. Kwa muda mrefu nimekuwa nikiwaza sana hivi tukianza kuwa makini na resources zetu hatuwezi kujikomboa kutoka kwenye umasikini kweli?
Hii Tanzania ina ardhi kubwa sana, kuna madini, ardhi yenye rutuba, vyanzo vya maji, watu wengi, vivutio vya utalii na kadhalika
Mbeya_City_.jpg

Mawazo yangu ni kwamba kama serikali ikiamua kushirikiana na wananchi basi umasikini kwisha habari yake, na sasahivi Bongo tuna wasomi wengi sana na ni vijana, hakika kama vijana wakishirikiana na serikali basi tunaweza kuijenga Tanzania mpya.

Serikali inaweza kununua matrekta makubwa hata buku hivi kutoka Marekani, Ujerumani na India na kuwapa vijana wasomi wa Kitanzania wayatumie kulima mashamba makubwa sana ambayo yatakuwa yanamilikiwa na serikali.
Kuna matrekta yana nguvu sana na ni ya kisasa kabisa, mfano trekta la Maxxum 150 hp lina uwezo wa kubeba majembe 50 kwa wakati mmoja unakuta trekta limeenda round chache umeshalima hekari kibao
Steiger 715 Quadtrac.png

Mashamba yakiwa mengi na makubwa Watanzania wengi sana watanufaika. Mfano Kilombero kuna mashamba mengi ya miwa na yameajiri Watanzania 4000, ili kuweza kupata miwa inayotumika kiwanda cha sukari Kilombero.
Leo hii serikali ikianzisha mashamba ya pamba au miwa au koroshi nk itaajiri vijana waliohitimu Agricultural Engineering, Computer Science, Chemical Engineering, watu wa biashara, arts nk na wasomi tunao wengi. Aidha na wale watu wasiosoma wanahitajika pia katika mashamba hayo.
Mbalizi_Mbeya_Tanzania_-0006.jpg

Unakuta kama shamba la miwa Kilombero limeajiri Watanzania 4000 maana yake tukiwa na mashamba mia moja kama hayo tutaajiri Watanzania laki 4.
tea-pickers-on-a-tea-plantation-near-mbeya-tanzania-africa-tea-pickers-on-a-tea-plant-near-mbe...jpg

Fikiria hii, Tanzania ina mpango wa kuwa Tanzania ya viwanda, kama tukianza kuzalisha pamba kwa wingi kule Kanda ya Ziwa tunaweza pia kuanzisha viwanda vya nguo hapahapa nchini na kwa kuwa malighafi tunayo basi tunaweza kutengeneza nguo nyingi na watu waliosomea Industrial Engineering, Mechanical, sijui Business Administration, Electrical Engineering wote watanufaika na kuanzishwa kwa viwanda hivi
Screenshot_2025-07-25-15-56-08-992_com.google.android.googlequicksearchbox.png

Tukiwa na mashamba makubwa ya miwa tutaongeza viwanda vya sukari, tukiwa na mashamba mengi ya alizeti tutaongeza viwanda vya kukamua mafuta ya alizeti, tukiwa na mashamba makubwa ya karanga tutaongeza viwanda vya siagi na kukamua mafuta ya karanga nk
mpunga-2.png

Kuna mikoa kama Mbeya hapa Tanzania mazao mengi ya chakula yanastawi vizuri sana kuanzia mpunga, mahindi, maharage, kunde, mboga za majani kila kitu kinastawi. Huu mkoa na maeneo mengine yanayofanana na Mbeya tunaweza kuitumia vizuri sana kulisha Tanzania na nchi jirani. Serikali inaweza kutuma wanauchumi nchi nyingine za Africa kama DRC, Kenya, Burundi, Malawi, Zambia, Botswana, Mozambique, Botswana nk kwenda kuongea biashara vizuri na kusaini mikataba ili kupata ruhusa ya kuwauzia bidhaa zetu nyingi za kilimo na kupata soko kirahisi. Kwa hali hii utasaidia hata kupunguza njaa nchi jirani na kuongezea kipato Watanzania
Maindi-780x470.jpg

Mkoa wa Morogoro una mito mingi sana. Maana yake ni kwamba kuna vyanzo vya maji kila kona hususani vijijini. Maji haya tunaweza kuyatumia kufanya kilimo cha kisasa cha umwagiliaji kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu. Hii itatuwezesha kulima hadi kiangazi bila kutegemea mvua. Itasaidia kwa kiasi kikubwa na kama Tanzania tutakuwa na mazao mengi tutafungua fursa nyingine nyingi za kiuchumi
df32f9a3-097f-4c83-b1f9-d0b6b5db7059.jfif.jpg

Kwa sasa kwenye kilimo kuna changamoto nyingi, mfano Lindi na Mtwara wakulima wanalima korosho wanauza kwenye vyama vya kilimo halafu serikali inanunua kilo moja ya korosho kwa bei ya chini, hii inakatisha sana wakulima tamaa kwa sababu faida inakuwa ndogo na inafanya wengine kukata tamaa ya kuingia kwenye kilimo.
500px-PivotWithDrops.jpeg

Serikali ya Tanzania inapaswa kuwa namba moja kwenye ku support efforts za wakulima na pia kuhamasisha matumizi ya teknolojia kwenye kilimo ili tuanze kuwa na KILIMO CHA KISASA. Tuache kutegemea mvua na tuifanye ardhi yetu kubwa ya Tanzania iliyo na rutuba itumike kuongeza ajira kwa raia wa taifa letu pendwa
Water-Irrigation-System.jpg

Kama tukiwekeza vizuri kwenye Kilimo basi fursa nyingi za Kiuchumi zitaongezeka

Idadi ya magari yanayosafirisha mazao kutoka eneo moja hadi lingine itaongezeka kwa hiyo Watanzania wengi wataajiriwa kama madereca wa magari haya na wengine watamiliki makampuni ya kusafirisha mazao

Idadi ya wakulima successful itaongezeka, na watu wakitajirika nchini ndio mwanzo wa kufungua fursa nyingine mfano baadhi ya watu wakipata pesa za kutosha watajenga hoteli, lodges mbalimbali, wengine watanunua mabasi, wengine wataanzisha supermarket, wengine watajenga shule na private sector itakuwa nchini maana haya yote watakayojenga maana yake ni kwamba wamesaidia watu wengi kupata ajira pia maana hoteli zinahitaji kuajiri watu, mabasi yanahitaji madereva, supermarket zinahitaji watu pia yani kazi zitaongezeka
Rice-planting-machine_2,katori-city,japan.jpeg
Kama shamba moja la Kilombero limeajiri watu 4000 maana yake mashamba makubwa elfu 1 ya design uiyo yanaweza kuajiri watu milioni 4.

Na serikali ikiajiri watu milioni 4 kwenye kilimo kwa haraka haraka unaweza ukadhani umeokoa watu milioni 4 kutoka kwenye umasikini, ila kiuhalisia umeokoa watu zaidi ya milioni 10 kutoka kwenye umasikini, kwa sababu hawa watu wana familia zao zinazowategemea maana yake wakipata kipato inasaidia watu kama watano hivi kuwa na maisha mazuri maana unakuta nyumbani wana watoto, unakuwa umeeakomboa hawa watoto kutoka kwenye umasikini pia, na kupitia ajira nyingine za usafirishaji, viwanda, biashara nk ambavyo vinakuwa facilitated na kilimo basi unakuwa umesaidia kundi kubwa la watu kupata ajira
customers-buying-produce-direct-from-organic-farmers.jpg

Hiko ni kilimo tu, Tanzania inaweza kuwekeza uchumi wake kwa asilimia kubwa kwenye rasilimali mbalimbali kama rasilimali watu, madini, vyanzo vya maji, ardhi nk
Hii itasaidia sana nchi yetu kukua kwa kasi kiuchumi na kusaidia sekta nyingine za kiuchumi nazo zifanye vizuri. Watu wengi wakiona wanaweza kupata maisha mazuri hapahapa Tanzania basi yale mawazo ya kuikimbia nchi hii yatapungua, wengi watabaki hapa huku wanalisaidia taifa kimaendeleo

Mimi nahisi kama tatizo la ajira tukiwa serious kuna namna nyingi tu tunaweza kulipunguza tukitumia vizuri rasilimali zetu
 
Jipange, set soko,ingia ukalime
Usitegemee sana serikali itakuchelewesha
Ni kweli unachosema serikali
Ingekuwa serious kwenye sekta hyo watu wengi wangeinuka,na kungepunguza mindset ya vijana kukimbilia kukata mauno

Ova
 
Tatizo serikali yetu haya mambo kupambana na umasikini nchini walishayakatia tamaa kitambo sana

Sasahivi wananunua magoli huko
 
Bongo hii ni mpaka siku tukipata viongozi wenye IQ na upeo mkubwa wa kufikiri ambao hawatalazimisha vijana kuwa machawa badala yake wapige kazi ila kwa uongozi wa mama Abduli bora ujilimie mwenyewe tu 😂😂
 
Tatizo serikali yetu haya mambo kupambana na umasikini nchini walishayakatia tamaa kitambo sana

Sasahivi wananunua magoli huko
Kumbe na wewe umeona eeh kwenye vita ya umasikini wananchi tuko peke yetu, acha viongozi waendelee kuishi kifalme na kodi zetu. Bongo hatari sana 😂😂😂
 
Inauma vijana wanazidi kuwa machawa kama Lucas Mwashambwa na hawana faida yoyote kwenye maendeleo ya taifa
 
Hata ukisema bhasi nijilimie zangu tu mwenyewe, unakutana na vitimbi kama vyote kwanza mbegu unakuta imechakachuliwa(imepakwa rangi ya ukwaju) , mbolea fake , pembejeo zingine bei juu na sokoni dalali anataka akupangie bei, ukimkwepa dalali unaingia kwenye mikono ya serikali yenyewe , mara wafunge mipaka, mara wapange bei, yani mambo tafrani.
 
Bongo hii Mungu atusaidie tu
 
Umenikumbusha mwaka jana nilinunua mbegu ya mahindi ya laki 8 ambapo kila kg 10 iliuzwa 80,000 kumbe mbegu ilipakwa rangi hizo ulisema yaani ni mbegu feki
 
Aisee pole sana, bongo uhuni mwingi ndo mana watu wanasema kilimo cha bongo ni kamari kama ilivyo kubeti.
 
View attachment 3418255
Wakuu Tanzania ni nchi kubwa sana na ina resources nyingi sana. Kwa muda mrefu nimekuwa nikiwaza sana hivi tukianza kuwa makini na resources zetu hatuwezi kujikomboa kutoka kwenye umasikini kweli?
Hii Tanzania ina ardhi kubwa sana, kuna madini, ardhi yenye rutuba, vyanzo vya maji, watu wengi, vivutio vya utalii na kadhalikaView attachment 3418269
Mawazo yangu ni kwamba kama serikali ikiamua kushirikiana na wananchi basi umasikini kwisha habari yake, na sasahivi Bongo tuna wasomi wengi sana na ni vijana, hakika kama vijana wakishirikiana na serikali basi tunaweza kuijenga Tanzania mpya.

Serikali inaweza kununua matrekta makubwa hata buku hivi kutoka Marekani, Ujerumani na India na kuwapa vijana wasomi wa Kitanzania wayatumie kulima mashamba makubwa sana ambayo yatakuwa yanamilikiwa na serikali.
Kuna matrekta yana nguvu sana na ni ya kisasa kabisa, mfano trekta la Maxxum 150 hp lina uwezo wa kubeba majembe 50 kwa wakati mmoja unakuta trekta limeenda round chache umeshalima hekari kibao
View attachment 3418283

Mashamba yakiwa mengi na makubwa Watanzania wengi sana watanufaika. Mfano Kilombero kuna mashamba mengi ya miwa na yameajiri Watanzania 4000, ili kuweza kupata miwa inayotumika kiwanda cha sukari Kilombero.
Leo hii serikali ikianzisha mashamba ya pamba au miwa au koroshi nk itaajiri vijana waliohitimu Agricultural Engineering, Computer Science, Chemical Engineering, watu wa biashara, arts nk na wasomi tunao wengi. Aidha na wale watu wasiosoma wanahitajika pia katika mashamba hayo. View attachment 3418301
Unakuta kama shamba la miwa Kilombero limeajiri Watanzania 4000 maana yake tukiwa na mashamba mia moja kama hayo tutaajiri Watanzania laki 4.
View attachment 3418307
Fikiria hii, Tanzania ina mpango wa kuwa Tanzania ya viwanda, kama tukianza kuzalisha pamba kwa wingi kule Kanda ya Ziwa tunaweza pia kuanzisha viwanda vya nguo hapahapa nchini na kwa kuwa malighafi tunayo basi tunaweza kutengeneza nguo nyingi na watu waliosomea Industrial Engineering, Mechanical, sijui Business Administration, Electrical Engineering wote watanufaika na kuanzishwa kwa viwanda hivi
View attachment 3418314
Tukiwa na mashamba makubwa ya miwa tutaongeza viwanda vya sukari, tukiwa na mashamba mengi ya alizeti tutaongeza viwanda vya kukamua mafuta ya alizeti, tukiwa na mashamba makubwa ya karanga tutaongeza viwanda vya siagi na kukamua mafuta ya karanga nk
View attachment 3418313
Kuna mikoa kama Mbeya hapa Tanzania mazao mengi ya chakula yanastawi vizuri sana kuanzia mpunga, mahindi, maharage, kunde, mboga za majani kila kitu kinastawi. Huu mkoa na maeneo mengine yanayofanana na Mbeya tunaweza kuitumia vizuri sana kulisha Tanzania na nchi jirani. Serikali inaweza kutuma wanauchumi nchi nyingine za Africa kama DRC, Kenya, Burundi, Malawi, Zambia, Botswana, Mozambique, Botswana nk kwenda kuongea biashara vizuri na kusaini mikataba ili kupata ruhusa ya kuwauzia bidhaa zetu nyingi za kilimo na kupata soko kirahisi. Kwa hali hii utasaidia hata kupunguza njaa nchi jirani na kuongezea kipato Watanzania
View attachment 3418325
Mkoa wa Morogoro una mito mingi sana. Maana yake ni kwamba kuna vyanzo vya maji kila kona hususani vijijini. Maji haya tunaweza kuyatumia kufanya kilimo cha kisasa cha umwagiliaji kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu. Hii itatuwezesha kulima hadi kiangazi bila kutegemea mvua. Itasaidia kwa kiasi kikubwa na kama Tanzania tutakuwa na mazao mengi tutafungua fursa nyingine nyingi za kiuchumi
View attachment 3418351
Kwa sasa kwenye kilimo kuna changamoto nyingi, mfano Lindi na Mtwara wakulima wanalima korosho wanauza kwenye vyama vya kilimo halafu serikali inanunua kilo moja ya korosho kwa bei ya chini, hii inakatisha sana wakulima tamaa kwa sababu faida inakuwa ndogo na inafanya wengine kukata tamaa ya kuingia kwenye kilimo.
View attachment 3418352
Serikali ya Tanzania inapaswa kuwa namba moja kwenye ku support efforts za wakulima na pia kuhamasisha matumizi ya teknolojia kwenye kilimo ili tuanze kuwa na KILIMO CHA KISASA. Tuache kutegemea mvua na tuifanye ardhi yetu kubwa ya Tanzania iliyo na rutuba itumike kuongeza ajira kwa raia wa taifa letu pendwa
View attachment 3418353

Kama tukiwekeza vizuri kwenye Kilimo basi fursa nyingi za Kiuchumi zitaongezeka

Idadi ya magari yanayosafirisha mazao kutoka eneo moja hadi lingine itaongezeka kwa hiyo Watanzania wengi wataajiriwa kama madereca wa magari haya na wengine watamiliki makampuni ya kusafirisha mazao

Idadi ya wakulima successful itaongezeka, na watu wakitajirika nchini ndio mwanzo wa kufungua fursa nyingine mfano baadhi ya watu wakipata pesa za kutosha watajenga hoteli, lodges mbalimbali, wengine watanunua mabasi, wengine wataanzisha supermarket, wengine watajenga shule na private sector itakuwa nchini maana haya yote watakayojenga maana yake ni kwamba wamesaidia watu wengi kupata ajira pia maana hoteli zinahitaji kuajiri watu, mabasi yanahitaji madereva, supermarket zinahitaji watu pia yani kazi zitaongezekaView attachment 3418367Kama shamba moja la Kilombero limeajiri watu 4000 maana yake mashamba makubwa elfu 1 ya design uiyo yanaweza kuajiri watu milioni 4.

Na serikali ikiajiri watu milioni 4 kwenye kilimo kwa haraka haraka unaweza ukadhani umeokoa watu milioni 4 kutoka kwenye umasikini, ila kiuhalisia umeokoa watu zaidi ya milioni 10 kutoka kwenye umasikini, kwa sababu hawa watu wana familia zao zinazowategemea maana yake wakipata kipato inasaidia watu kama watano hivi kuwa na maisha mazuri maana unakuta nyumbani wana watoto, unakuwa umeeakomboa hawa watoto kutoka kwenye umasikini pia, na kupitia ajira nyingine za usafirishaji, viwanda, biashara nk ambavyo vinakuwa facilitated na kilimo basi unakuwa umesaidia kundi kubwa la watu kupata ajiraView attachment 3418373
Hiko ni kilimo tu, Tanzania inaweza kuwekeza uchumi wake kwa asilimia kubwa kwenye rasilimali mbalimbali kama rasilimali watu, madini, vyanzo vya maji, ardhi nk
Hii itasaidia sana nchi yetu kukua kwa kasi kiuchumi na kusaidia sekta nyingine za kiuchumi nazo zifanye vizuri. Watu wengi wakiona wanaweza kupata maisha mazuri hapahapa Tanzania basi yale mawazo ya kuikimbia nchi hii yatapungua, wengi watabaki hapa huku wanalisaidia taifa kimaendeleo

Mimi nahisi kama tatizo la ajira tukiwa serious kuna namna nyingi tu tunaweza kulipunguza tukitumia vizuri rasilimali zetu
Naomba nikusanue,shida ya Tanzania ni wizi,ukitumia uwekezaji kama mfano wabongo wanaanxa kuiba kuanzia diesel,spare,Mbegu na mavazi ya shamba na bado wanafanya robbing ya bei sokoni.

Laana ya Tanzania Iko katika roho mbaya na fitna na wizi kama wote
 
Unaweza kusolve hiyo issue pia, kwa mawazo yangu lakini. Ni suala la kukaa chini kufikiria tu vikwazo vyote vya miradi yenu na kuamua namna ya kukabiliana na vikwazo hivyo
Kwa mfano hapa Tanzania wanajeshi wengi ni wazalendo, mkianzisha mradi kama huo wa kilimo, mnatuma wanajeshi kadhaa kila kona ya Tanzania ambapo mmeanzisha hayo mashamba, wanaenda kule kama raia wa kawaida (wanakuwa spies) na watakuwa wanatoa report kwa siri juu ya jinsi mradi unavyoenda. Kukiwa na any suspicious activity wawe wanareport
Uhalifu kama huu utapungua tu maana watakaofanya hiyo mipango watakamatwa na kuwajibishwa bila kujua ni nani kawachoma serikalini
 
Kwa taifa letu haiwezekani ndugu
Inawezekana shida ni kwamba tuonaongozwa na watu wenye akili gani.
Mtu kama mchengerwa
Bashe
Na wengine wa namna hiyo badala ya kuinua kilimo wameua zao la pamba! Nasikia watu washapoeza imani na zao hilo imagine unalima pamba kwa miezi6 halafu siku unauza unakopwa kwa miezi 2.

Kuna mwaka ilikuwa kuipata hela yako hadi uhonge ndo upewe yaani unazungushwa tu. Utegemee watu wataendelea kulima kwa hali hiyo?
 
Back
Top Bottom