Naona Wote wasafi humu jf....haya bwana....sawa hakuwa makini ndg yetu huyu, ila cha muhimu ni kumshauri akapime ili ajue hali ya afya yake.... Bila kupima kupata uhakika ataendelea kuwa na mawazo tu....
Usipime, jifanye umesahau yaliyotokea ila uwe unakula balance diet na upige mazoezi, kama una wazaz wanakutegemea jaribu kuwajengea nyumba halafu jaribu kuokoka. Ndo ushauri wangu
By king'astikwa taarifa yako huduma za hospitali na kitabibu hazibagui. Yeyote ambaye anahisi amepata accidental exposure ana haki ya kupata hii huduma. Acha kupotosha, kama mnahukumu watu huko unakosali basi hospitali huduna hazibagui.
Inaingia akili umnyime mtu pep halafu akishapata hiv usiulize uliipata wapi na uanze tu kumpa huduma na art? Ni akili matope ama? Kila liwezekanalo kupunguza uwezekano wa mtu mmoja kupata hiv linafanyika, kwa upendo na bila
kuhukumi. Spare us your 'holier than thou' attitude.
MBONA MBIO HIVYO! BY THE WAY [kwa taarifa yako huduma za hospitali na kitabibu hazibagui] ,HIYO TAARIFA UNAYONIPA UMEITOA WAPI? BONGO HII HII AU KUNA NYINGINE YA MABOX ULIYOJITENGENEZEA ? KAMA HUDUMA HIZO HAZIBAGUI REFFERAL ZINAZOLALAMIKIWA HUZIJUI! NI ZA WATU WA DARAJA GANI?[MALARIA KUTIBIWA INDIA,
S.AFRICA],WAKATI HOSPITALI HAZINA ALU WALA PANADOL,HUO SIO UBAGUZI?,..
NDIO MAANA NIKAKARIBISHA MASWALI
KWA MAELEZO MAFUPI UTOAJI WA KINGA HIZO UMEGAWANYWA KATIKA SEHEMU ZIFUATAZO
HIV PEP in Occupational Exposure
HIV PEP in Sexual Exposure[(rape/sexual assault), as well as in the
case of slipped or broken condom during sex with discordant partner. ]
HIV PEP INAYOTOLEWA KWENYE AJALI ZA VYOMBO VYA MOTO[kwa waliokutana na damu wakati wakitoa msaada kwa wahanga wa ajali,na hata kwa majeruhi wenyewe kama walikuwa zaidi ya mmoja hii itategemea degree and severity of injury,maaana pia zinaweza kumplicate matibabu]
MPAKA SASA KWA UFAHAMU WANGU KITAALUMA NA KIKAZI, KINGA ZILIZOPEWA KIPAUMBELE NI
Occupational Exposure[ KWA AJILI YA HEALTH CARE PROVIDERS]
HIV PEP in Sexual Exposure[(rape/sexual assault). HII HUTOLEWA IKIAMBATANA NA UJAZAJI WA VIAMBATANISHO VYA KISHERIA[POLICE, N.K]
HIV PEP INAYOTOLEWA KWENYE AJALI ZA VYOMBO VYA MOTO[MTA]
Inaingia akili umnyime mtu pep halafu akishapata hiv usiulize uliipata wapi na uanze tu kumpa huduma na art? Ni akili matope ama?
.WOTE NI WADAU WA NGONO,.HILO HALIPINGIKI NA NI MOJAWAPO YA SABABU ILIOTULETA DUNIANI [nendeni mkazaane na muongezeke muijaze dunia].LAKINI KILA MMOJA WETU NI MUOGA WA MAAMBUKIZI .KUNA WATU WENGINE HATA BAADA YA KUTUMIA KINGA[CONDOM] BADO WANA WASIWASI WA MAAMBUKIZI.
AJALI YA KUPASUKIWA NA KINGA[CONDOM KUTOKUWA KATIKA UBORA UNAOTAKIWA,UHIFADHI USIOKIDHI VIWANGO, UVAAJI USIO SAHIHI N.K
KUTOKUAMINIANA KWA WENZA [WANANDOA,WAPENZI], HAWA WOTE WANAKUWA KATIKA HALI YA WASIWASI WA MAAMBUKIZI MUDA WOTE
NGONO BILA KINGA [NGONO ZEMBE] N.K
SABABU;
HAYO MAKUNDI YOTE NILIYOYATAJA HAPO JUU YAPO KATIKA UHITAJI WA KINGA, LAKINI UKIANGALIA ,NI KUNDI LA UOGA WA MAAMBUKIZI LENYE WATU WENGI KULINGANISHA NA WAATHIRIKA WA VVU AMBAO WAPO KWENYE MATIBABU .
KIASI CHA DAWA KILICHOPO NI KIDOGO UKILINGANISHA NA MAHITAJI. KUNA WAKATI[MWAKA JANA] WAGONJWA WALIFIKIA HATUA YA KUGAWANA DAWA ,KOPO MOJA WATU WAWILI ,KUNA WAKATI ILIFIKIA KOPO KWA WATU WATATU. SASA HIYO ILITOKEA KWENYE BIG CTC CENTRES.HIZO NDOGO SIJUI ILIKUWAJE WE PATA PICHA.
ALIYEATHIRIKA AKIANZA KUTUMIA ARV,HATAKIWI KUSIMAMA WALA KUACHA MPAKA MWISHO WA MAISHA YAKE,KWANI KUSIMAMA AUKUACHA MADHARA YAKE NI MAKUBWA.[ REF ,POST LOLIONDO HIV REPORT]
SASA WEWE UNATOKA POVU MDOMONI , BILA LOGIC YOYOTE, UNATAKA KILA MTU AGAWIWE,.BASI UNDA PROGRAM YAKO YA MABOKSI, UGAWIE KILA MTU,NA ZINGINE ZIWEKE KWENYE MAGEST KABISA ILI KILA ANAYEJIHISI KAAMBUKIZWA APEWE KOPO LAKE NA NYINGINE GAWIA WANA NDOA WASIOAMINIANA;HAPO NDIPO ITAKAPOKUINGIA AKILINI KAMA UNATUMIA UBONGO KUFIKIRI , NA KAMA UNAFIKIRI KWA KUTUMIA YALE YA WABUNGE WA DARISALAMA! BASI KY ITATUMIKA NA ITAINGIA KULE KUNAKOTAKIWA BILA TABU,ASUBUHI UKIONA MATOPE USILIE, UJUE UMESHAKUWA, NA HAPO PEP HAITAHITAJIKA AMINI NAKUAMBIA.
Inaingia akili umnyime mtu pep halafu akishapata hiv usiulize uliipata wapi na uanze tu kumpa huduma na art??! WEWE NI DAKTARI KWELI? MHmhhm ,,..
Spare us your 'holier than thou' attitude. SABATO MASALIA HUWA HAMJIFICHI,..vipi ile safari yenu ya kwenda ulaya bila pasi na tiketi iliishia wapi?au ndio umerudi na ushuda huo wa kimabox ,
.,,,,,, MY TAKE AGAIN ACHENI KUPOTOSHA WATU ,MPAKA SASA TANZANIA HIV PEP HAITOLEWI KWA MAELEZO YA NGONO ZEMBE,,,........
jamaa alivyoongea nikajua labda ni coordinator wa CTC. lakini post exposure prophylaxis hutolewa hata kwa waliobakwa, waliopasukiwa condom na watu wote walio kwenye risk ya kupata ngoma. wenye risk kubwa walikuwa wanapewa dawa tatu na ndogo dawa mbili
WEWE NDIO POYOYO KABISA USIYEELEWA HATA UNACHOKISOMA NA KUKIANDIKA,[lakini post exposure prophylaxis hutolewa hata kwa waliobakwa] YAANI HUWEZI KUTOFAUTISHA NGONO ZEMBE NA KUBAKWA,!!. HATA UTARATIBU WAKE WA KIMATIBABU UKOJE PIA HUJUI? LOh!.
....MY TAKE KINGA YA PEP SIO KWA AJILI YA KUJIKINGA BAADA YA NGONO ZEMBE,...TAFADHALINI ACHENI KUHADAA WATU
NI TOPIC INAYOZUNGUMZIA TUKIO LILILOTOKEA, TANZANIA KWENYE MAZINGIRA TULIYOPO,.. MUATHIRIKA WA TUKIO HILO AMEOMBA MSAADA WA USHAURI, ULITAKIWA KUMSHAURI NINI CHA KUFANYA ,NA JINSI YA KUJIELEZA KWA MAELEZO MBADALA AMBAYO YANGEWEZA KUTATUA TATIZO LILELILE , UKIZINGATIA UKIZINGATIA PEP YA NGONO ZEMBE HAINA KIPAUMBELE SO FAR IN TZ. BADALA YA KUFANYA HIVYO WEWE UNAKIMBILIA KUGOOGLE NA KUPASTE KUWA HIYO PEP HUTOLEWA HATA KWA WALIOBAKWA,..BAADALA YA KUELEWA KINACHOZUNGUMZIWA NA MAZINGIRA YA TUKIO,..WEWE UNAKIMBILIA ULIYOYASOMA YA WALEEE,..NA KUNGANGANIZA KUWA NI YA TZ,…pole
NILITOA NAFASI YA MASWALI UNGEULIZA.,,,,,…
jamaa alivyoongea nikajua labda ni coordinator wa CTC.,wenye risk kubwa walikuwa wanapewa dawa tatu na ndogo dawa mbili
WALIKUWA WANAPEWA HIZO NI ENZI ZILEE,..NADHANI ILIKUWA NI VIDONGE[ dawa zipo katika mfumo wa kimiminika,hewa na yabisi [solid kama sijasahau ambazo hujulikana kama tembe au vidonge] .
,wenye risk kubwa walikuwa wanapewa dawatatu na ndogo dawa mbili ,..
HIYO NI HADIDU YA ENZI ZILLEE,AMBAYO KIUHALISIA HAIKUBALIKI KABISAA….MTU YUPO KWENYE HATARI YA KUATHIRIKA UNAJUA KABISA KUATHIRIKA HUKO KUNAWEZA KUMSABABISHIA MAGONJWA NYEMELEZI NA HATA KUMGHARIMU MAISHA,.BADALA YA KUMSAIDIA KWA UMAKINI WA HALI YA JUU ,.UNAANZA KUMTENGENEZEA MAJEDWALI YA MATIBABU eti RISK KUBWA NA NDOGO,…BE SERIOUS WEWE ! UKIWAPA WOTE DAWA YA RISK KUBWA HAZITAFANYA KAZI ILE ILE? FIKIRI KABLA YA KUTENDA WEWE,….
ULIMALIZA SHULE LINI ? HUWA UNA UPDATE SHULE YAKO KWELI,?MBONA UNA DATA ZA KIZAMANI? HIZO DAWA TATU NA MBILI ZISAHAU ,KIDONGE KIMOJA TU CHA ART AMBACHO UNASHAURIWA KUMEZA USIKU KWA MUDA WA MWEZI MMOJA KINATOSHA .
Ningeiona hii post mapema ningekushauri ukatimie PEP... Maana ukiwahi ndani ya saa 72 inazuia. Otherwise usijali. .. mi naamini kama ulipaka mafuta hukuchubuka na hivyo hukuupata...
Onyo: usijaribu kwenda kupima...
atakuwa muumini wa kanisa uchwara huyu, anayejihisi mtakatifu kwa sababu yeye hazini, ila anamuibia muajiri muda kwenda kwenye maombi na anapiga dili la kutumia per diems ama mali za muajiri kwa kazi za kanisani.
we unwaza kanisa tu,na uumini.,,,,vimekusaidia nini tangu umezaliwa mpaka ,leo ,....ulikuwa na bwana padri nini?!! ! Ufanatiki mbaya sana,....niambie basi kanisa lako la ukweli likowapi nami nijiunge katika kundi la wajinga waliwao,...muumini mzuri sana wewe,.unamwelekeza mdau ,.aende maria stopes,.!.wale ni mbingwa wa kutoa mimba,..sasa wakiivuta dushedede kwa kudhania mimba inatoka huku mkono wa mtoto ukiwa umetangulia mimi simo,...mwenzio anataka pep bwana na sio kutoa mimba
Habarini wadau
Member mwenzenu yamenikuta, dunia naiona chungu.
Nilikua na mazoea ya kupitia bar flani hivi napiga mbili tatu kisha narudi nyumbani. Nikaweka mazoe na barmaid (ya kawaida tu) ambae alikua mcheshi siku zote nizokua nikifika hapa. Alikua anapenda kuketi nami na kunielezea mambo mengi tu ya kimaisha matatizo anayopitia kiasi cha kumuonea huruma. Dada ni mzuri kwakweli. tukafikia hatua hadi ya kubadilishana namba ya simu.
Majuzi wakati niko kwa ofc akanipigia akinambia yule bosi wake (alokua akimtaka kimapenzi) amemtimua kazi na ashaenda kukata tiketi ya kurudi kwao , na kule geto alikokua akiishi na wenzake ashatimuliwa.
Huruma ikaniingia. Nikamwambia anisubiri nikitoka kazini nitaonana nae.
Jioni niotoka nikampitia nikamkuta kweli amepaki mabeji yake nikamfanyia booking ya chumba ajihifadhi mpaka kesho akielekea kituoni.
Nikamwacha room lakini hakuridhia akanisihi tukae kidogo japo tupige stori mbili tatu. Kwakua nje yake kulikua na bar, basi nkamsihi tukae hapo bar tupige hizo stori
Nikaanza kuzifakamia huku stori zikiendelea, alikua ana habari nyingi sana kila nikitaka kuondoka ameanzisha hii. Na kama ujuavyo bar unavoendelea kukaa ndivo unavoendelea kuzinywa.
Hata nivomuaga mara ya mwisho akanisihi kua muda umekwenda mno na kwa hali ile nisingefika niendako.
Nikazama nae mpaka room huku nikiwa na ndomu za kutosha tu kama ikitokea zitasave.
Time ya game ilivofika nilivaa kwa makini ile kitu lakini ilichukua muda mrefuu bila mi kumaliza nahisi ni kutokana na mapombe nilokunywa, mwenzangu akalalamika kua anaumizwa sana na kitu nilovaa.
Akatoa mafuta akanambia nivulie mbali ile ndom na nipakae mafuta ambayo ameniaminisha kua nikipaka sitapata mchubuko na tutakua safe wote. Pombe zangu kichwani zikaamini njia hiyo na nikatumika bila kinga!
Ivofika asubuhi mipombe isheniisha kichwani ndo naanza ku recall, Ayyaaaah metumika bila kinga miye!
Nikaamka zangu na kumwacha yule barmaid akijitayarisha kwa safari.
Basi wadau nina mawazo mwenzenu mpaka naumwa hivi nimesalimika kweli miye? Daaaah! Sijui nikapime miye! Uff!
kunguru ni kunguru tu hata ukimchanganya na kuku kuna saaaa atajisahau atalia kwaaaaaaaa kwaaaaaaaaa!we anza kugawa mirathi tu safari yako ndo ishaiva!!!
wewe ulivyomaliza si ulioga ?kama ulioga hamna noma maana hata kamanda wa chama la pekupeku ni bomba
Zuma alioga na ikawa poa kabisa mpaka leo ni presidar na wewe jiandae
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.