ERTUGRUL BEY
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 11,631
- 21,699
Mawazo yako ndio fomula ambayo yatafanya maisha yako yawe ya namna gani
Kila wazo ni picha halisi ambayo inaenda kuhifadhiwa katika subconscious mind yako kwa ajili ya matumizi ya baadae
Kila wazo ambalo lipo katika mfumo wa picha ndio litakuwa mustakabali wa kufuatwa au ramani ya kufuatwa katika kufikia mafanikio yako
Na mawazo yako yatafanyiwa kazi mpaka ufikie lengo lako kamili ambalo huwa unaliwaza kila siku
Ni mafundisho ya baadhi ya dini kwamba hakika unakuwa vile unavyowaza
Ameandika mwanafilosofa wa zamani wa Rome Marcus Aurelis " maisha yetu yanatokana na mawazo tuliyokuwa nayo"
Mwanasaikolojia maarufu William James wa Havard anasema "imani inaweza kuifanya picha kwenye mawazo yetu kuwa ni kweli"
Your mental pictures are completed into reality by being converted into power by your subconscious
Ni hayo tu!