Mawazo kuhusu biashara ya wasaidizi wa kazi za ndani

nelvine

JF-Expert Member
Nov 8, 2015
1,109
1,855
Habari wanajamvi, msaada wa mawazo yenu hapa.

Nilikuwa nina wazo la bihashara ya wasichana wa kazi ( house girls) mwaka jana, lilikua niwe nawatafuta mabinti nawapa mafunzo kiasi jinsi ya kufanya kazi na kujifunza ujuzi mdogo mdogo, pia niwachambue wale bora na kuwatafutia kazi za ndani.

Lengo kuu ni mimi kupata kipato, pia kuwasaidia na wao pia. Lakini pia nitasimamia baadhi ya haki zao za msingi wawe wanazipata toka kwa waajiri wao( nakua mwamvuli).

Sasa kwasasa nimeanza kuliendesha hili wazo, lakini changamoto kubwa napata mabinti wadogo umri kuanzia miaka 12 hadi 17, na wengi hawajawahi kwenda shule kabisa, na baadhi yao wana historia ya kuishi kwenye ndoa.

Japo wakifika kwangu nawapa mafunzo ya mwezi mzima na kuzijua baadhi ya tabia zao na kuwafundisha angalau kusoma na kuandika.

Je, hili wazo langu kisheria lipoje?

Je, nipo halali kisheria kuwatafutia kazi hawa mabinti? Maana wanatoka kwenye mazingira magumu sana.

Hadi sasa ninao 20 nawapa mafunzo na kuzijua tabia zao, wakiwa na vigezo nawatafutia kazi.

NB: Wana ruhusa za wazazi wao.
 
Wewe wewe wewe, Nakuita mara tatu ndugu Kwa umri huo Tena Kwa mtoto wa kike watafuta kiyama shekhe!

Wanatakiwa wawe shule hao Kama unataka kuwasaidia nenda human rights foundation kawapeleke naamini utapata nishani ya amani na utapata hata connection nzuri tu itakayokutoa maisha.

Alisikika mwanaharakati huru!
 
ni wazo zuri kwa kweli, mimi binafsi nimeshalifikiria kwa mara kadhaa, ni vizuri uwe unatupa update tunaweza kuja kuwa na mashirikiano mbeleni huko.

Ila mkuu kuwa makini usiji kuanza kuwala mwenyewe
 
ni wazo zuri kwa kweli, mimi binafsi nimeshalifikiria kwa mara kadhaa, ni vizuri uwe unatupa update tunaweza kuja kuwa na mashirikiano mbeleni huko.

Ila mkuu kuwa makini usiji kuanza kuwala mwenyewe
Kiukweli naona ni bihashara inayolipa, kuhusu kuwala mkuu hapana najitahidi sana kuwafanya km wadogo zangu.
 
Kuna dada anafanya hyo shughuli nimemsahau jina, tena alikuwa ana kituo cha kuwapa trainings kabla hawajaanza kazi
Natamani siku ikifika nifungue kituo pia, maana siku hizi wadada wa kazi ni changamoto sana .
 
Umepita kwa watu wa Sheria?? Nahis watakupa mrejesho.... Wazazi wao wa sign pia picha muhimu wakiwa wanasign
 
ni wazo zuri kwa kweli, mimi binafsi nimeshalifikiria kwa mara kadhaa, ni vizuri uwe unatupa update tunaweza kuja kuwa na mashirikiano mbeleni huko.

Ila mkuu kuwa makini usiji kuanza kuwala mwenyewe
inalipaje. Mfano binti mmoja anaweza kukuingizia shingapi.
 
Habari wanajamvi, msaada wa mawazo yenu hapa.

Nilikuwa nina wazo la bihashara ya wasichana wa kazi ( house girls) mwaka jana, lilikua niwe nawatafuta mabinti nawapa mafunzo kiasi jinsi ya kufanya kazi na kujifunza ujuzi mdogo mdogo, pia niwachambue wale bora na kuwatafutia kazi za ndani.

Lengo kuu ni mimi kupata kipato, pia kuwasaidia na wao pia. Lakini pia nitasimamia baadhi ya haki zao za msingi wawe wanazipata toka kwa waajiri wao( nakua mwamvuli).

Sasa kwasasa nimeanza kuliendesha hili wazo, lakini changamoto kubwa napata mabinti wadogo umri kuanzia miaka 12 hadi 17, na wengi hawajawahi kwenda shule kabisa, na baadhi yao wana historia ya kuishi kwenye ndoa.

Japo wakifika kwangu nawapa mafunzo ya mwezi mzima na kuzijua baadhi ya tabia zao na kuwafundisha angalau kusoma na kuandika.

Je, hili wazo langu kisheria lipoje?

Je, nipo halali kisheria kuwatafutia kazi hawa mabinti? Maana wanatoka kwenye mazingira magumu sana.

Hadi sasa ninao 20 nawapa mafunzo na kuzijua tabia zao, wakiwa na vigezo nawatafutia kazi.

NB: Wana ruhusa za wazazi wao.
Sheikh hii ni mojawapo ya biashara ya UTUMWA POPOTE ULIPO

Hacha kufanya ivyo, unless otherwise huwe na kibali kutoka mamlaka usika .
 
inalipaje. Mfano binti mmoja anaweza kukuingizia shingapi.

Mimi bado sijapanga kwenye suala la training , Mpaka sasa mchakato wangu upo kwenye mipango ya kuwa niwe mtu wa kati tu. Ila hilo suala la training ni jambo zuri sana linahitaji kufikiriwa.
 
Mmh ila hii biashara ina ukakasi. Wataalamu wa uchumi wanasema biashara ikiwa na risk kubwa ina faida kubwa pia lakin hapa naona mleta mda hii biashara yake ina risk kubwa ila haina faida kubwa au haina kabisa.

Wazazi wa watoto kukubali sidhani kama ndio inakupa wewe go ahead moja kwa moja. Mamlaka za serikali zinasemaje kuhusu hilo? Umefatilia huko??
Kua na mbinti 20 kinyemela ni biashara haramu iyo mkuu, unaweza kuzushiwa kesi kua unawauza hao.

Mabinti 20 wanalala wapi mkuu?? Umewapangishia nyumba??
 
Mm ninavyoelewa sheria inamtaka mtoto kuanzia miaka 13 ndyo aanze kufanya hzo Kaz so ukiwa below hyo age hapo utapambana na mkono wa Sheria na si miaka 18 Kama weng wanafikiri umri kwa mtoto kufanya kazi
 
inalipaje. Mfano binti mmoja anaweza kukuingizia shingapi.
Binafsi uwa nakaa na mabint wiki moja na zaidi , gharama hutegemeana, mi nakua n mtu wa kati, kumtafutia kazi na kumfundisha baadhi ya kazi na hasa nidhamu
 
Binafsi uwa nakaa na mabint wiki moja na zaidi , gharama hutegemeana, mi nakua n mtu wa kati, kumtafutia kazi na kumfundisha baadhi ya kazi na hasa nidhamu
Unajua mambo mengine kwenye forum unaweza kukosoa bila kujua hali halisi. Wasichana kama hao unaosema wengi unakuta wametoka familia maskini sana na huko walikukuwa walikuwa wanaishi kwenye mazingira magumu. Hata kama sheria inazuia kuajiri watoto wa umri huu lakini kiuhalisia wasipoajiriwa wataishia kubebeshwa mimba au kuolewa huko kwao na maisha kuwa mabaya zaidi. Mimi nadhani serikali inatakiwa kuangalia haya mambo kwa uhalisia wake. Mimi nakushauri ufanye hii shughuli kwa kuzingatia haki na uhakikishe unasimamia haki za hao wasichana kwani waajiri wengine wanaweza kuwatumikisha kama watumwa.
 
Back
Top Bottom