JacksonMichael
JF-Expert Member
- Mar 22, 2012
- 339
- 61
MAWAZIRI wapya walioapishwa jana na Rais Jakaya Kikwete wameahidi kutumia uwezo wao wote kukabiliana na changamoto mbalimbali katika sekta zao.
Akizungumza na gazeti hili baada ya kuapishwa katika viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Hamis Kagasheki, alisema pamoja na kumshukuru Rais kwa heshima aliyompa kusimamia wizara hiyo, atahakikisha anakabiliana na changamoto zinazoikabili wizara hiyo.
Najua wizara hii ina changamoto nyingi likiwamo tatizo la wizi, hivyo kazi yangu ya kwanza ni kuitumia ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufichua wanaohusika na sifa hii mbaya, alisema Kagasheki.
Alisema pia atahakikisha Watanzania wanapata faida ya rasilimali zao ikiwa ni pamoja na eneo la vitalu ambalo limekuwa likikabiliwa na migogoro kila kukicha.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, alimshukuru Rais kwa kumrejesha katika wizara hiyo na kuahidi kuhakikisha mchakato unaoendelea wa Katiba mpya unafanyika vyema kwa kushirikisha kikamilifu wananchi. Alipata kuongoza wizara hiyo awali.
Naomba wananchi watarajie katika mchakato huu, kuwashirikishwa kwa wingi kwa kuwa Katiba ndiyo sheria mama, tukitunga wengi kwa maoni na mawazo mengi ya Watanzania wenyewe, ni wazi itatengenezwa Katiba bora kwa Watanzania wa sasa na baadaye, alisema.
Kuhusu sheria, alisema wizara yake itajipanga kuhakikisha inarekebisha sheria zenye utata na mwingiliano na sheria mpya zinatungwa zikiwa na ubora unaotakiwa sambamba na kushughulikia mlundikano wa kesi.
Kabla ya uteuzi huu, nikiwa Utawala Bora, nilikutana na Waziri wa Katiba na Sheria na Waziri wa Mambo ya Ndani na kuzungumzia namna ya kushughulikia suala hili hivyo nitaendeleza juhudi hizi, alisema Chikawe.
Naibu wake, Angela Kairuki, alisema uteuzi wake umekuja wakati mwafaka wa mchakato wa Katiba na kuwataka Watanzania watarajie Katiba bora ambayo itawezekana tu kwa ushiriki wao kikamilifu.
Msisitizo wangu utakuwa ni kuhimiza Watanzania kusoma na kuchambua Katiba ya sasa ili kutoa maoni mazuri yatakayozaa Katiba bora zaidi, alisema.
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, alisema hali ya usafiri nchini ni mbaya, kwa kuwa hakuna usafiri wa uhakika wa reli, anga na barabara zimekuwa zikiharibiwa na magari ya mizigo mizito kinyume cha sheria.
Alisema changamoto yake ya kwanza ofisini ni kuhakikisha Tanzania inapata usafiri wa aina zote wa uhakika. Yote haya nitashirikiana na wenzangu kuyaboresha na manufaa yake kuonekana, alisema.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, alisema moja ya malengo yake katika wizara hiyo ni kuhakikisha Tanzania inakuwa angalau na umeme wa megawati 1,200 wa uhakika usiokatikatika kila mara, hali ambayo itakuza watumiaji umeme nchini kutoka asilimia 14 hadi 75.
Naibu wake, George Simbachawene, alisema anafahamu kuwa ameingia kwenye wizara yenye changamoto nyingi kwa Taifa, kutokana na ukweli kuwa sasa kila kitu kimepanda bei kuanzia chakula, gharama za maisha na usafiri kutokana na ughali wa umeme.
Baada ya kuliona hili, nikiwa na wenzangu tutaangalia namna ya kuongeza uzalishaji umeme na njia bora tutakayotumia ni ya gesi, alisema.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda, alisema katika maendeleo ya nchi, sekta ya viwanda inapaswa kupewa kipaumbele na jambo la msingi atakaloshughulikia ni kuona uzalishaji wa viwanda unapanda mara mbili ya sasa.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Ali Mwinyi, alimshukuru Rais kwa kumrejesha kwenye wizara hiyo ambayo pamoja na kuwa na changamoto nyingi kubwa, ya sasa ni kutatua mgogoro wa madaktari.
Alisema kipaumbele chake kitakuwa ni kushirikiana na Kamati iliyoundwa kushughulikia suala hilo na kuhakikisha mapendekezo yanayotolewa yanatekelezwa.
Pamoja na mawaziri hao wengine walioapishwa jana na Rais Kikwete ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Emmanuel Nchimbi; Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe; wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani na wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza.
Wengine ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara; wa Fedha, Dk William Mgimwa na naibu mawaziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Adam Malima, wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima na wa Viwanda na Biashara, Gregory Teu.
Aidha, wengine ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais Charles Kitwanga; wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu; wa Ujenzi, Gerson Lwenge; wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid; wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba na wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba.
Wengine ni wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala; wa Maji, Dk Binilith Mahenge; wa Nishati na Madini, Stephen Maselle; wa Fedha wawili Janet Mbene na Saada Mkuya Salum.
Kati ya mawaziri sita walioachwa, aliyekuwa wa Nishati na Madini, William Ngeleja pekee ndiye alihudhuria hafla hiyo na kusema kwa uteuzi wa sasa Nishati mambo yatakuwa mazuri kwa kuwa sasa manaibu ni wawili tofauti na awali.
Waziri asiyekuwa na Wizara Maalumu, Profesa Mark Mwandosya hakuapishwa katika sherehe hizo kutokana na kuwa India akiendelea na matibabu.
sosi: HabariLeo | Mawaziri waahidi makubwa