Mawaziri waahidi makubwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawaziri waahidi makubwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JacksonMichael, May 8, 2012.

 1. J

  JacksonMichael JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 339
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MAWAZIRI wapya walioapishwa jana na Rais Jakaya Kikwete wameahidi kutumia uwezo wao wote kukabiliana na changamoto mbalimbali katika sekta zao.

  Akizungumza na gazeti hili baada ya kuapishwa katika viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Hamis Kagasheki, alisema pamoja na kumshukuru Rais kwa heshima aliyompa kusimamia wizara hiyo, atahakikisha anakabiliana na changamoto zinazoikabili wizara hiyo.

  “Najua wizara hii ina changamoto nyingi likiwamo tatizo la wizi, hivyo kazi yangu ya kwanza ni kuitumia ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufichua wanaohusika na sifa hii mbaya,” alisema Kagasheki.

  Alisema pia atahakikisha Watanzania wanapata faida ya rasilimali zao ikiwa ni pamoja na eneo la vitalu ambalo limekuwa likikabiliwa na migogoro kila kukicha.

  Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, alimshukuru Rais kwa kumrejesha katika wizara hiyo na kuahidi kuhakikisha mchakato unaoendelea wa Katiba mpya unafanyika vyema kwa kushirikisha kikamilifu wananchi. Alipata kuongoza wizara hiyo awali.

  “Naomba wananchi watarajie katika mchakato huu, kuwashirikishwa kwa wingi kwa kuwa Katiba ndiyo sheria mama, tukitunga wengi kwa maoni na mawazo mengi ya Watanzania wenyewe, ni wazi itatengenezwa Katiba bora kwa Watanzania wa sasa na baadaye,” alisema.

  Kuhusu sheria, alisema wizara yake itajipanga kuhakikisha inarekebisha sheria zenye utata na mwingiliano na sheria mpya zinatungwa zikiwa na ubora unaotakiwa sambamba na kushughulikia mlundikano wa kesi.

  “Kabla ya uteuzi huu, nikiwa Utawala Bora, nilikutana na Waziri wa Katiba na Sheria na Waziri wa Mambo ya Ndani na kuzungumzia namna ya kushughulikia suala hili hivyo nitaendeleza juhudi hizi,” alisema Chikawe.

  Naibu wake, Angela Kairuki, alisema uteuzi wake umekuja wakati mwafaka wa mchakato wa Katiba na kuwataka Watanzania watarajie Katiba bora ambayo itawezekana tu kwa ushiriki wao kikamilifu.

  “Msisitizo wangu utakuwa ni kuhimiza Watanzania kusoma na kuchambua Katiba ya sasa ili kutoa maoni mazuri yatakayozaa Katiba bora zaidi,” alisema.

  Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, alisema hali ya usafiri nchini ni mbaya, kwa kuwa hakuna usafiri wa uhakika wa reli, anga na barabara zimekuwa zikiharibiwa na magari ya mizigo mizito kinyume cha sheria.

  Alisema changamoto yake ya kwanza ofisini ni kuhakikisha Tanzania inapata usafiri wa aina zote wa uhakika. “Yote haya nitashirikiana na wenzangu kuyaboresha na manufaa yake kuonekana,” alisema.

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, alisema moja ya malengo yake katika wizara hiyo ni kuhakikisha Tanzania inakuwa angalau na umeme wa megawati 1,200 wa uhakika usiokatikatika kila mara, hali ambayo itakuza watumiaji umeme nchini kutoka asilimia 14 hadi 75.

  Naibu wake, George Simbachawene, alisema anafahamu kuwa ameingia kwenye wizara yenye changamoto nyingi kwa Taifa, kutokana na ukweli kuwa sasa kila kitu kimepanda bei kuanzia chakula, gharama za maisha na usafiri kutokana na ughali wa umeme.

  “Baada ya kuliona hili, nikiwa na wenzangu tutaangalia namna ya kuongeza uzalishaji umeme na njia bora tutakayotumia ni ya gesi,” alisema.

  Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda, alisema katika maendeleo ya nchi, sekta ya viwanda inapaswa kupewa kipaumbele na jambo la msingi atakaloshughulikia ni kuona uzalishaji wa viwanda unapanda mara mbili ya sasa.

  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Ali Mwinyi, alimshukuru Rais kwa kumrejesha kwenye wizara hiyo ambayo pamoja na kuwa na changamoto nyingi kubwa, ya sasa ni kutatua mgogoro wa madaktari.
  Alisema kipaumbele chake kitakuwa ni kushirikiana na Kamati iliyoundwa kushughulikia suala hilo na kuhakikisha mapendekezo yanayotolewa yanatekelezwa.

  Pamoja na mawaziri hao wengine walioapishwa jana na Rais Kikwete ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Emmanuel Nchimbi; Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe; wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani na wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza.

  Wengine ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara; wa Fedha, Dk William Mgimwa na naibu mawaziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Adam Malima, wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima na wa Viwanda na Biashara, Gregory Teu.

  Aidha, wengine ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais Charles Kitwanga; wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu; wa Ujenzi, Gerson Lwenge; wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid; wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba na wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba.

  Wengine ni wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala; wa Maji, Dk Binilith Mahenge; wa Nishati na Madini, Stephen Maselle; wa Fedha wawili Janet Mbene na Saada Mkuya Salum.

  Kati ya mawaziri sita walioachwa, aliyekuwa wa Nishati na Madini, William Ngeleja pekee ndiye alihudhuria hafla hiyo na kusema kwa uteuzi wa sasa Nishati mambo yatakuwa mazuri kwa kuwa sasa manaibu ni wawili tofauti na awali.

  Waziri asiyekuwa na Wizara Maalumu, Profesa Mark Mwandosya hakuapishwa katika sherehe hizo kutokana na kuwa India akiendelea na matibabu.

  sosi: HabariLeo | Mawaziri waahidi makubwa
   
 2. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Tunawatakia kila la Heri,ila kumbuka hiyo ya kutoka asilimia 15 hadi 75 utahukumiwa nayo wewe na chama chako 2015 wakati wa uchaguzi Mkuu
   
 3. c

  collezione JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Tanzania bwana. ukisikiliza ahadi, unaweza kusema, baada ya miaka 2, tutakuwa kama NewYork. Haha

  Any way, sasa hivi hamna cha excuse tena. 2015 we want new gvt.
   
 4. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  hawawezi kufikia za mteuzi wao na tumeshawazoea.
  tafakari hizi.
  1.reli mpya ya kati.
  2.meli mpya kila ziwa.
  3.barabara za juu dar
  4.machinga complex kila mkoa.
  5.viwanja vya ndege mikoa kadhaa.
  6.maisha bora kwa kila mtanzania
  7..............
  8.................
  9....................

  SASA KATI YAO NANI AMEAHIDI HATA ROBO YA HIZO?
   
 5. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Huyu profesa kaanza kutokota kabla hajaanza yaani ahadi za hovyo kabisa
   
 6. c

  collezione JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Sijamsikia waziri wa mambo ya ndani, ujenzi, uchukuzi wakiongelea swala la usalama barabarani.

  Ajali za barabarani zimekuwa janga la taifa kwa sasa
   
 7. c

  collezione JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Hizo ahadi ukimuuliza JK, ameshasahau (it was just a joke in fact). Sasa hivi yuko kwenye kilimo kwanza.
   
 8. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2012
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,421
  Likes Received: 3,770
  Trophy Points: 280
  Hii ni nchi ya ahadi... Lakini tunakoelekea tutafika mwisho wa kupata nafasi za kuchaguliwa kwa ahadi. Nina uhakika ule msululu wa ahadi za JK utawatesa sana uchaguzi wa 2015 majukwaani. Maana kwa mujibu wa mtazamo wangu, sioni kama kuna uwiano wowote kati ya muda uliopita na ahadi zilizotekelezwa, au muda uliobaki na ahadi zilizobaki achilia mbali thamani ya ahadi.
   
 9. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #9
  May 8, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Tatizo ukiingiza utaalam wako na sisas unapotea,Prof umeteuliwa huchaguliwa acha ahadi za jukwaani we tekeleza halafu tusomee mafanikio tutakuona tu wewe na mafanikio yako,kama miaka 50 mna 14 asilimia hiyo mitatu mtafikisha 75 asilimia? Au ndo jina lako linaanza kazi(muhongo)
   
 10. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #10
  May 8, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Wanasema watatumia uwezo wao wote wakati uwezo wao ni Mdogo kiutendaji hawana jipya hawa nawashauri waboreshe magereza kwasababu ndio kinachofuata
   
 11. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #11
  May 8, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,973
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Wabongo kwa talalila ndo wenyewe. Maneno matupu yangekuwa yanaleta maendeleo sasa hivi tungekuwa zaidi ya New York.
   
 12. Ufipa-Kinondoni

  Ufipa-Kinondoni JF-Expert Member

  #12
  May 8, 2012
  Joined: Jan 3, 2012
  Messages: 4,488
  Likes Received: 2,147
  Trophy Points: 280
  Hawa mioyoni wamejaa unyang'anyi na ufisadi raslimali zetu. Kwani hawajui kuwa nchi inatakiwa kusimamia wazawa katika ajira za ndani, haiwezekani Mchina mmoja anajiandiksha kuja kuuza mitumba harafu analeta wataalam wake 20 wakati kuna watanzania wenye ujunzi zaidi yao. Mambo mengi yanahitaji uzalendo zaidi kuliko kutoa ahadi zisizowasaidiz watz.
   
 13. v

  victor11 Member

  #13
  May 8, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Jamani hawa mawaziri hawahitaji kufanya makubwa wala uchawi ili kuikwamua hii nchi. Kwanza kuna quick wins, ambazo ni kuhakikisha makusanyo ya serikali yanakusanywa kama ilivyopangwa, hakuna misamaha isiyokuwa na tija, uchumi unasimamiwa kama policy zinavyohitaji, mabarabara yanajengwa kama mipango iliyokwisha pitishwa na bunge, sera zipo kinachohitajika ni kuhakikisha zinaheshimiwa, reli zinafanya kazi kwani biashara iliyopo ni kubwa sana, bandari ndo usiombe, pia kuhakikisha kila mtu katika nafasi aliyopo anatimiza wajibu wake.
   
 14. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #14
  May 8, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,347
  Likes Received: 2,683
  Trophy Points: 280
  Hilo mbona walishalitolea ufafanuzi Magamba kupitia domokaya wao wa kipindi hicho Mzee Makamba, kuwa ilikuwa ni danganya toto tu ili Wadanganyika watoe kura za ndio kwa JK.
   
 15. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #15
  May 8, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Wamuulize mama Tibaijuka kilichompunguza speed, wasifikiri kwa mfumo uliopo itakua rahisi kama wanavyoahidi, watakapotaka kwenda mbele watashangaa wamevutwa mashati, speed inapungua taaratibu. This country bwana!!!!!
   
 16. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #16
  May 8, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wamuombe mungu maana watajeuka simba asiye na meno ama nyoka asiye na sumu!
   
 17. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #17
  May 8, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  wote wanaanzaga hivo hivo...wanaahidi so much...but then they deliver soo little...tushawazoea..hata bosi wao alituahidi mambo mengi
   
 18. K

  Katufu JF-Expert Member

  #18
  May 8, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 433
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Ngoja tusubiri tuone vitu vyao kama nao hawatakuwa walaji tu
   
Loading...