Bunge halina siri,kuna waandishi....pia zama za akina Lamwai,Lwekama,Mutungirehi,Mrema,Slaa hakukuwa na bunge laivu na walitingisha.....kama wangekuwa na hoja wasingekimbilia kiki ya maafa.
Acha uongo.
Ungewajuaje kama vyombo vya habari vingekua vinadhibitiwa kama ilivyo leo.
Tena ushukuru tu mana sheria sasa hivi inatungwa kichama. Ukiwa CCM hata utukane mtu kwenye vyombo vya habari na usiku kucha uwe unakashfu wapinzani hakuna hatua itakayochukuliwa. Tuliona vifo vya Mawazo na Dr. Mvungi.
Hata bungeni tunaona wale tunaofuatilia bunge CCM haina wabunge wenye hoja zaidi ya kupitisha miswada kama ilivyoletwa na serikali kwa kugonga meza tu.
Na nikukumbushe pia kuwa tangu wakati wa utawala wa Mwingereza bunge lilikua linatangazwa redioni na wananchi hasa wa vijijini walikua wanafuatilia sana matangazo ya Bunge.
Tusingewajua hao wakina Lamwai ,Mrema , Slaa na wengine kama sio matangazo ya bunge kupitia redio na Tv.
Dr. Slaa alipata umaarufu wakati wa bunge live likiongozwa na Samweli Sita. Kama JK na Sita wangebana bunge na vyombo vya habari tusingewajua watu kama akina Dr. Harison Mwakyembe na hata Viongozi wengi waliopo madarakani.
Kudharau uhuru wa matangazo ya bunge ni ujinga mkubwa kwani utawaumiza zaidi CCM kwani tutarejea enzi zile za kiongozi hakosei. Wale wa mitandao mtabaki mitandaoni tu na hamtaweza kuonyesha jamii uwezo na vipaji vyenu.
Leo hii mwaka mmoja sasa umepita lakini mpaka sasa hakuna mtanzania anayejua kuwa ni mbunge gani kijana wa CCM ambaye ameonyesha uwezo na kipaji cha kujenga hoja kama tulivyowaona enzi za akina January, Nchemba, Kigwangala. Serukamba, Lusinde n.k. achilia mbali wale wa upinzani.
Kwa nchi ya kidemokrasia ambapo watu wanaomba ajira ya uongozi kupitia kura za wananchi ni jambo la hatari sana endapo watu hawataachwa wakaonekana kwenye vyombo vya habari na kwenye shughuli za kisiasa. Ukibana shughuli za kisiasa unazalisha shughuli haram za kisiasa kama zile za siasa kwenye dini na mara nyingine ugaidi. Mana yule anayeonekana sana na kujulikana kwenye nyumba za ibada anaweza kugeuka na kujipigia debe kidini na akapata kura.
Tusifurahiye siasa za gizani kwani tuna shindwa kujua nani anaweza akatufaa kuongoza jamii yetu , nani anatetea maslahi yetu na nani anatoa lugha chafu na nani hana nidham.
Mfano hai upo kwa madiwani. Hawa wameharibu sana mipango ya serikali kwenye halmashauri nyingi kwa sababu wanafanya maamuzi yao gizani. Wengi hawana uwezo kabisa wa kiuongozi na kimipango lakini wanaendelea kuchaguliwa kutokana na ukweli kuwa wananchi hawajui kuwa diwani wa kata nyingine amemzidi kwa kiwango gani diwani wake.
Vikao vya madiwani vingekua vinafanyika hadharani nadhani ubadhirifu mkubwa kwenye halmashuri usingekuwepo mana tungewajua wale ambao hawatoshi kupata nafasi hizo.
Kuna madiwani wa darasa la nne na wameongoza kwa miaka zaidi ya 45 . Wananchi bado wanawachagua kwa sababu ya kutojua ushindani wa kihoja kwenye vikao vya madiwani ambavyo vinafanyika gizani.
Hata mahakamani haki inatendeka kwa sababu mahakama inakuwa huru na kwa uwazi kila mtu anaruhusiwa kuingia na kusikiliza mabishano ya pande zote. Hakuna anyezuiwa kutoa ushahidi wake kwa wazi. Na nadhani kama mahakama ingekua inafanyika kwenye jengo moja tu kama lilivyo bunge kwa nchi nzima basi mahakama ingekuwa ya kwanza kuonyeshwa live kwenye vyombo vya habari.
Pamoja na kwamba mahakimu na majaji hawaombi kuchaguliwa kwa kura lakini bado kesi zinaendeshwa kwa uwazi na kusikilizwa kwa uwazi bila kificho au kuchuja habari.