Tunaweza kumlaumu Mbowe kumbe anashindwa kutoa mchango kwa kukosa wasaidizi wenye ueledi bungeni.Kazi kubwa ya mawaziri vivuli ni kuja na mpango mbadala kwa lengo la kuboresha mpango wa serikali,hadi sasa hakuna hata kivuli mmoja aliyeweza kuleta/kuandaa mpango mbadala.
Hili huenda limesababishwa na;
1.Jazba
2.Kutokuwa na elimu na uzoefu wa sehemu/sekta husika mfano....Mnyika hana ueledi na masuala ya nishati na miamba,Msigwa hana ueledi na mambo ya diplomasia na kimataifa,Silinde hajui masuala ya fedha na uchumi,Sugu hana ajualo kwenye tasnia ya habari.
3.Upendeleo,kupachikana wadhifa bila kujali uwezo.
Kambi ya upinza inaweza kuwa bora endapo watazingatia yafuatayo;
1.Mbowe na wenzake wajenge utamaduni wa kujisomea,si vitabu vya hadithi...bali majarida ya uchumi,maliasili ili kupata taarifa muhimu zitakazowawezesha kujenga hoja...na sio kuja na "hear say"...bungeni.
2.Waachane kutumia pesa kwenye propaganda bali waajiri wataalamu kwenye sekta kama Uchumi,Elimu,Afya,Kilimo...kwa dhumuni la kutafsiri,kuchambua na kuwapa uelewa wabunge.Mfano kama Mbowe angekuwa na mshauri wa kiuchumi asingeleta bungeni hoja ya deni la taifa kwa namna alivyohoji ni dhahiri hana uelewa nalo....mtaalamu angemuelekeza ni jambo gani la kuuliza kuhusu deni la taifa.
Nawasilisha.