..Mawaziri saba watoswa.....

Hata hii Mkuu wanatudanganya tu!

JK hawezi mtosa Dr Kawamba na Adam Malima!

Nape anajifurahisha tu
Hizi ni siasa za NAPE za maji taka. Katika utawala, CCM ina uwezo wa kuwaita na kuwaonya au kuwatimua. Hii ni Cheap popularity ya NAPE na Boss wake. Mwenyekiti wa CC ni Rais. Sasa ona hii ni nini kama si kujiangusha? Hivi hujui kuwa Rais anateua mawaziri kumsaidia kiserikali na anateua secretariat ya CCM ili imsaidie kichama? Hivi na mawaziri wakiamua kukagua uhai wa wizara zao nao wakasema Kinana na Nape watoswe? Tuache hizo, hii ni kazi ya CDM kuisema serikali ya CCM na wala si sec ya CCM kuisema hadharani serikali yao.
 
teh teh...
 
CC kama wanaona mbali wangegundua matatizo yote hayo ni Mh. Kikwete.
Kama cc ya ccm ina ubavu wamtose Kikwete kukinusuru chama
 
wale wahu wako wapi kwenye huu uzi?! Sixgate, Faiza etc. Wako wapi, waje wakatae au wakubali!! Mijitu mingine bure kabisa!
 
 
Tusubiri kama watatoswa kweli. Ajabu ni kuwa sioni wengine watakaoteuliwa wanaoweza kufanya tofauti na hawa wa sasa.
 
Angalia hii kutoka Gazeti la Mwananchi....."Kwa mfano Waziri husika hajafika kwa muda wa miaka minne na nusu mkoani Ruvuma ambako ndiko kuna ghala la chakula na tulipofika Tunduma tulikuta foleni pale mizani huku watumishi wakiwa wanafanya kazi kwa saa tisa, lakini baada ya kueleza udhaifu huo sasa wanafanya kwa saa 24,"

Hivi waziri lazima afike kila sehemu?
 
Hata hii Mkuu wanatudanganya tu!

JK hawezi mtosa Dr Kawamba na Adam Malima!

Nape anajifurahisha tu
Yaani hasa huyo Shukuru jmn, huyo anatakiwa aondolewe haraka kunusuru sekta ya elimu na Mulugo afuatie!
 
Hii cc ya maccm wangekuwa wana akili wangeanza na mwenyekiti wao maana yeye ndio alikuwa anaahidi ahidi tu hovyo hovyo. Mara kigoma kuwa dubai ya africa (tumuulize vipi?) meli mpya kureplace ilozama ziwa victoria 1999 iko wapi?? Barabara kuzunguka mlima k'njaro zi wapi?? Barabara ya arusha-mkalama-iramba i wapi??
Huyu alikuwa awe wa kwanza kuondolewa.
 
Comedy nyingine nzuri sana, Kikwete ndio Mwenyekiti WA CC halafu CC inamshauri Rais awachukulie hatua aliowateua!!!!!!
 
Baada ya hapo nimesikia vibaka wa buku 7 Lumumba wanajiandaa kuja na threads nyingi kwamba CCM ni mfano wa kuigwa kwa kufanya maamzi magumu. Hebu watazame jinsi wanavyojipanga kuleta umbeya!!

Mkuu Hiroshima,

Hii Picha na comment zake imenichekesha sana...Kumbe ndio maana upuuzi umekuwa mwingi hapa JF.
 
Kale Kachanga Ka Mkulima Lazima Katolewe Kwanza, Haiwezekani Baraza Lifeli Mara Mbili Chini Yake, Yeye Anashinda GAMBUSHI!
 

Huu ndiyo ukweli, kikwete ndiyo zigo la kutupwa. Katika familia kama watoto wameoza ujue ni uvundo wa baba unawaathili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…