Mawaziri Ovyo wa CCM: Wapi Tunakosea kama Nchi?

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,850
9,405
Ni jambo lisilohitaji mjadala kwamba serikali ya awamu ya nne, hasa katika kipindi cha minne imefeli katika maeneo yote yanayohusiana usimamizi wa rasilimali za nchi kwa manufaa ya walio wengi na utawala bora kwa jumla. Tumefikia hali ambapo Serikali ya CCM haistahili tena kuendelea kushikilia dhamana na kutawala nchi. Kwa mfano, kwa muda sasa, tumekuwa na baraza la mawaziri lililokosa ‘Stability', na kupelekea utawala mzima wa nchi kuanzia ngazi ya serikali kuu hadi serikali za mitaa kuzidi kukosa mwelekeo. Tunazidi kushuhudia jinsi gani mamlaka ya nchi inavyoanza kuhama taratibu kutoka kwa viongozi wa kisiasa tuliowapa dhamana (mawaziri na wabunge) na kwenda kwa viongozi wasiotokana na ridhaa yetu ya moja kwa moja (bureaucrats – makatibu wakuu n.k). Matokeo yake ni viongozi tuliowachagua kusimamia rasilimali za nchi yetu kushindwa kufanya maamuzi wanayostahili - kisera.

Nia ya makala hii ni kujaribu kuja na mada ya kutusaidia kuachana japo kwa mara moja, na mtazamo/uchambuzi tuliouzoea wa kutoangalia mambo nje ya boksi juu ya suala la instability ya serikali ya awamu ya nne, na badala yake kuangalia suala hili kwa mapana na marefu zaidi. Ni imani yangu kwamba zoezi linaweza kutusaidia kubadilisha mawazo zaidi na kuzidi kutuandaa na mchakato wa kupata Katiba Mpya. Kama anavyohimiza Mh. Zitto, iwapo tunahitaji neno moja tu ndani ya katiba yetu mpya, basi neno hili si lingine bali "UWAJIBIKAJI."

Katika mchakato wa kuandika katiba mpya, ni muhimu tukatambua ‘trade-offs' muhimu zinazohusiana na aina mbali mbali ya mabunge ya kidemokrasia. Trade-offs nitakayo zungumzia ni ile baina ya muundo wa ‘MAJORITY DEMOCRACY' na muundo wa ‘PROPORTION (uwiano) & CONSENSUS'. Tukianzia na ‘majority democracy', hii ni system ambayo imekuwa inatumika Tanzania chini ya katiba iliyopo na chini ya serikali ya Chama Cha Mapinduzi. Kwa jinsi hali ilivyo sasa, kuna ishara zote kwamba hata ikitokea kwa mfano CHADEMA wakafanikiwa kutwaa madaraka ya nchi hii mwaka 2015, hivyo kuwa katika nafasi ya kuunda serikali, CHADEMA itaendelea na mfumo uliopo wa ‘majority democracy.' Ni kawaida kwa watu kuwa na imani kwamba muundo wa ‘majority democracy', huzaa serikali/baraza la mawaziri lenye ‘stability', hivyo kupelekea uwepo wa mazingira ya maamuzi ya haraka ya serikali – kisera, pamoja na hali ya uwajibikaji wa hali ya juu kwa upande wa chama kinachofanikiwa kuunda serikali. Sidhani kama CHADEMA wangependelea mfumo mbadala na huu iwapo wakishinda.

Nimetoa mfano wa CHADEMA mwaka 2015 kwa makusudi kabisa kwani sidhani kama nitakuwa nimekosea kutamka kwamba malengo ya CHADEMA, kama chama chochote kingine cha siasa ni kushinda uchaguzi ili kuunda serikali na kukamata Dola. Sidhani kama ni makosa kusema pia kwamba iwapo CHADEMA itashinda uchaguzi mkuu wa 2015 hivyo kupata nafasi ya kuunda serikali, nia yao itakuwa kuunda serikali/baraza la mawaziri lenye ‘STABILITY' na ‘ACCOUNTABILITY' kuliko ilivyo sasa chini ya CCM. Kama nipo sahihi, basi ina maana kwamba, iwapo CHADEMA watafanikiwa kushinda kiti cha urais na majority of seats za majimboni 2015, CHADEMA itapendelea kutawala Tanzania chini ya mfumo ule ule wa sasa chini ya CCM – yani ‘Majority Democracy' kwani wakati wote, CHADEMA wamekuwa wakionyesha umma kwamba wana uwezo wa kusahihisha mapungufu chini ya CCM. Nadhani nipo sahihi kutamka haya kwani hata kauli za wabunge wengi wa Chadema mfano – Zitto, Mbowe, Lissu na wengineo, huwa zinaelezea masikitiko makubwa juu ya jinsi gani wanavyokosa nguvu ya kuiwajibisha serikali kutokana na uchache wao bungeni. Vile vile katika kampeni za chaguzi ndogo, CHADEMA huwa wanasisitiza kwa wapiga kura umuhimu wa kuongezewa idadi ya wabunge ili wawe katika nafasi nzuri zaidi ya kuiwajibisha serikali ya CCM.

Baada ya kujadili muundo wa ‘majority democracy', sasa tugeukie muundo wa ‘proportion and consensus' ili tuweze kubaini trade offs iliyopo na ‘majority democratic system'. Huu uwiano na Consensus ni baina ya vyama vya siasa. Kama ilivyo kwa mfumo wa ‘majoritary democracy, mfumo wa ‘proportion and consensus' pia una faida na hasara zake. Kwa mfano mara nyingi mfumo huu huzaa baraza la mawaziri lisiloishi kwa muda mrefu na huzaa mazingira magumu ya maamuzi ya haraka ya serikali – kisera; lakini pia una faida zake, hasa kuzaa mazingira ambayo mchakato wa maamuzi kisera huwa ni ‘more inclusive' & ‘more fair', unaowakilisha a ‘larger' majority ya wananchi kwani wawakilishi wa vyama vyote vikubwa hushiriki kwenye maamuzi katika mazingira ya usawa na makubaliano.

Baada ya kujadili miundo hii miwili, sasa tujiulize, JE: Katika Katiba Mpya, tulenge kipi hasa:

· Kuendeleza mfumo wa sasa wa ‘Majority Democracy' kwa nia ya kuimarisha stability ya serikali/baraza la mawaziri, kuimarisha mazingira yanayozaa maamuzi ya haraka ya serikali - kisera, na kuimarisha uwajibikaji wa kwa upande wa serikali?

OR
· Kujaribu mfumo mpya wa proportion na consensus kwa nia ya kuongeza ‘inclusiveness & fairness'?

Ni muhimu hapa tukatambua kwamba ni vigumu kuwa na miundo yote miwili kwa wakati mmoja.

Muundo wa Majority Democracy & Misuko suko chini ya Utawala wa Kikwete.

Hoja ya hivi majuzi ya Mh. Zitto imeamsha hisia za wengi wetu ambao siku hadi siku, tumekuwa tunazidi kukata tamaa kutokana na utendaji mbovu wa baadhi mawaziri wa Kikwete. Hoja ya Zitto imekuja wakati muafaka. Lakini kuna tatizo moja kubwa: ni vigumu kubaini iwapo mawaziri wanaotajwa kuwa wabovu watajiuzulu, basi tutakuwa tumetatua tatizo la ‘instability' ya serikali/baraza na mawaziri. Kwa mfano, Je, Tatizo ni nini hasa:

· Instability ya baraza la mawaziri/serikali kutokana na dhana ya collective responsibility?
· Matatizo yaliyopo kwenye baadhi ya wizara?
· Mapungufu ya mfumo wa ‘Majority Democracy'?

Kwa sasa, ni dhahiri kwamba iwapo Waziri Mkuu au Mawaziri husika watajiuluzu, bado ni CCM ndiyo itakayobunda tena serikali; Pia, mawaziri wengi watarudi, na kitacho badilika pengine ni nani atapewa dhamana katika wizara ipi. Bila mkakati mzuri, hali hii inaweza pelekea mabadiliko ya mawaziri kutokea mara kwa mara katika kipindi cha miaka mitatu iliyobakia. Na hii inanipeleka kujadili suala lingine muhimu la ‘cabinet turn over'/'turnover of personel' i.e. mabadiliko ya mara kwa mara ya baraza la mawaziri, pamoja na sababu zake na athari zake katika utendaji wa serikali.

Katika kipindi cha miaka saba ya utawala wa Rais Kikwete (2005 – 2012), Rais ameunda baraza la mawaziri sio chini ya mara nne. Hii ndio ‘turn over' ya personell niliyoitaja awali. Kwa jinsi hali ilivyo sasa, kuna kila dalili kwamba ‘turnover ya personel' chini ya Kikwete itakuwa ni kubwa kuliko awamu nyingine zote tangia uhuru. Swali la kujiuliza hapa ni je, kwanini imekuwa hivi? Je ni kutokana na instability ya serikali/baraza la mawaziri au matatizo ya wizara moja moja? Ni vigumu kupata jibu la moja kwa moja, hivyo ningependa kujenga hoja kwamba pengine hii ‘high turnover of personnel in the cabinet' inatokana na Rais Kikwete kukabiliwa na ugumu wa ‘talent allocation' tangia aingie madarakani. Nitahidi kufafanua.

Tuseme nipo sahihi – then, chini ya Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya, Kikwete alianza awamu ya nne katika mazingira magumu/uncertainity kuhusu nani/kina nani ndio wenye uwezo wa kumsaidia kufanikisha kauli mbiu ya Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya. Ningependa kutumia mfano wa wizara mbili ili kuimarisha hoja kwamba pengine Kikwete alianza na nia ya dhati ya kuweka maslahi ya taifa chini ya kauli mbiu ya ari, nguvu na kasi mpya. Tuchukue Wizara ya ‘Justice & Constitutional Affairs' kama mfano. Chini ya Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya, hii ilikuwa ni moja ya wizara muhimu sana za kumsaidia Kikwete kufanikisha malengo ya maisha bora kwa kila mtanzania. Mbali ya kuitumia kuanzisha mchakato wa katiba mpya, Kikwete pia angeweza kuitumia kupanua wigo wa ‘Justice' ili kujumuisha ya the the three types of justice that operate as a triplets in any genuine democracy ambazo ni: POLITICAL JUSTICE, SOCIAL JUSTICE AND ECONOMIC JUSTICE. Kukosekana kwa moja ya haki hizi tatu ‘hudumaza' dhana nzima ya haki katika taifa.

Ndani ya malengo ya Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania, kwa vile Minister for Justice ana uwezo/nafasi kubwa to influence ‘reforms' muhimu zenye uwezo wa kuongeza haki za watanzania kiuchumi, kisiasa na kijamii, Rais angeweza kumweka waziri wa sheria au mwanasheria kuu wa serikali ambae angekuwa na imani kwamba ataweza kusimamia such reforms kwa ustadi mkubwa ili kuzidi kujenga imani ya CCM na Serikali yake kwa watanzania. Hivyo, Rais angehitaji kujenga ‘trust' na mtu mmoja na kumteua kushika dhamana hiyo muhimu. Lakini mbali ya ‘trust' ya Rais kwa mtu wa namna hiyo, pia lipo suala la uwezo (ability) ya mtu huyo – kwa mfano mawaziri wanatakiwa kuwa na utaalamu na uzoefu wa kuwawezesha kuongoza/kusimami sera kwa ufanisi wa hali ya juu, hivyo kupelekea CCM na serikali yake kufanikiwa kutekeleza kwa mfano, ilani yake ya uchaguzi kwa ufanisi zaidi.

Waziri mwingine muhimu chini ya dhana ya Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania ni Waziri wa Fedha. Rais alihitaji kuteua mtu mwenye ujuzi, uzoefu na uwezo wa kujtengeneza mazingira ya uchumi yatakayoendanana falsafa ya maisha bora kwa kila Mtanzania. Kwa mfano, kusimamia kwa ustadi mkubwa suala la mfumuko wa bei, kodi, thamai ya shilingi, kupunguza kasi ya deni la taifa na upatikanaji wa mikopo nafuu kwa wananchi. Waziri wa fedha wa kiwango hiki angeweza shirikiana na waziri wa Justice kwa kuhakikisha kwamba combination ya sera zao zingezaa economic growth (waziri wa fedha) na Social Justice (Waziri wa Justice) hivyo kufanikisha lengo la Rais la kuhakikika kuna Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania. Mbali na haya, chini ya dhana ya Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya, Rais angeweza kabisa kuja na kikosi tofauti cha mawaziri chenye uwezo mkubwa wa kisiasa/wa kujenga hoja mbalimbali, uwezo wa ku ‘negotiate' na upinzani wa ndani na nje ya CCM, ujasiri wa kukabiliana na waandishi wa habari kwa nguvu za hoja na sio hoja za nguvu, uwezo wa kusimamia sera na maamuzi ya serikali bungeni, uwezo wa kuwa ‘manage' watumishi wa umma ili wasipoteze ‘motivation', na mengineyo mengi ambayo yangepelekea CCM na serikali yake kuzidi kuwa na mafanikio katika siasa za ushindani.

Ningependa kumalizia na mambo yafuatayo: Tukiachilia mbali ukosefu wa maadili miongoni mwa baadhi ya mawaziri, hivyo kupelekea Serikali kuwa na utendaji mbovu, Je, ubovu wa serikali ya Kikwete unatokana na mambo mengine yapi?

1. Je, mwanzo wa utawala wake na hadi sasa, Kikwete anakabiliwa na wakati mgumu/uncertainity kuhusu kina nani wana uwezo wa kuwa MAWAZIRI BORA tofauti na sasa ambapo tuna BORA MAWAZIRI? Kwani the higher the uncertainty on part of the President juu ya hilo, the more likely atateua mawaziri wabovu.

2. Je, tatizo ni kwamba mchakato wa sasa wa kupata wabunge hauzai watu wenye elimu, uzoefu na utaalam wa kuwawezesha kuwa mawaziri bora? Kwani uncertainty on part of Rais kuhusu wabunge gani wanafaa kuwa mawaziri inapungua iwapo kuna a large pool ya wabunge wenye uwezo wa kuwa mawaziri bora ambao ni zao la mchakato wa uchaguzi mkuu uliojaa ushindani mkubwa lakini katika mazingira ya haki na demokrasia ya kweli.

3. Je, wabunge wenye uwezo huwa wapo wakati wote lakini kuna utamaduni wa kutowapa nafasi?

4. Je, tatizo ni umri wetu wa mdogo ndani ya Demokrasia? Kwani uncertainity on part of Rais kuhusu kina nani wana uwezo wa kuwa mawaziri bora huwa ni kubwa zaidi katika nchi zilizopo katika hatua za awali ya demokrasia. Kwa mfano, nchi yenye uzoefu mdogo na mfumo unaofuata utawala wa Baraza la mawaziri hupelekea ukosefu wa idadi ya kutosha ya wataalam, lakini pia ukosefu wa taarifa kuhusu watu gani wana sifa za kuwa mawaziri bora, hivyo kumpa Rais wakati mgumu kupata mawaziri bora kutoka miongoni mwa wabunge. Na kwa Tanzania, je, kipindi gani ndicho sahihi kuanza kuhesabu umri wetu ndani ya demokrasia miaka: 1961 (uhuru)? 1967 (ujamaa)? 1985 (soko huria)? 1992/3 (mfumo wa vyama vingi)??????

Mwisho kabisa, nimalizie kwa kusema kwamba, binafsi nina amini kwamba iwapo mchakato wa kuwapata viongozi/wenyeviti wa kamati mbalimbali za bunge ungekuwa unazingatia haki, uwazi, elimu, uzoefu na utalaam wa wagombea katika fani zao mbalimbali, hali hii ingempunguzia Rais ugumu wa kupata wabunge wenye uwezo wa kuongoza wizara mbalimbali kwa ufanisi kwa sababu Rais angekuwa na nafasi nzuri ya kuteua wabunge ambao ni wenyeviti wa kamati mbali mbali za bunge ambao wamekuwa wanaonyesha uwezo mkubwa wa kuongoza kamati zao. Kwa mfano tukiweka ushabiki wa vyama pembeni na kuangalia maslahi ya nchi, ni wazi kwamba wabunge kama Zitto, Cheyo, Kigoda, Lissu wameonyesha ‘performance' ya hali ya juu katika kamati zao, na kutoa ishara kwamba kwamba wanaweza kabisa kuwa Mawaziri Bora na sio Bora Mawaziri kwa mfano wakipata nafasi za kuongoza wizara zinazoendana na shughuli za kamati zao za bunge.

Naomba kuwasilisha.

Nadhani tatizo kubwa kuhusu kutowajibika kwa mawaziri wetu ni urafiki au uswahiba alio nao rais kwa mawaziri wake.
Waziri ni cheo cha kitaalam, pamoja na mabalozi. Tofauti na mheshimiwa Kessy anavyodai. Kwa nchi nyingi za dunia ya tatu, mawaziri huchaguliwa based on loyalty na siyo utaalam. Waziri wa nishati Marekani ni Nobel prize winner in Physics na ni mtu ambaye anaelewa sector ya nishati kitaalam na siyo kisiasa.

Kwa Tanzania, hata wajumbe wa Kamati ya bunge inayoshughulikia nishati ni wanasiasa wapiga porojo na wanukuu mahiri wa vifungu vya katiba. John Mnyika na January Makamba kwa mfano ni wapiga porojo ambao bado wanajifunza politics za sekta ya nishati, vikao vyote vya kamati za bunge vinaishia kuangalia loopholes kwenye procurements ambazo wizara husika zimefanya. Kila tukiwa na makongamano au midahalo inayohusu sekta ya nishati, huwa tunamsikiliza January as if kuwa yeye ndiye mtaalam wa nishati, while actually he is a mere conflict resolutionist. matokeo yake ni kupewa semina, safari za makongamano na vizawadi (3 months diplomas,one year masters) kutoka kwa wafadhili ambao kiukweli ni lobyists wa makampuni ya mafuta kwa mfano (they could be lobbysts wa mambo mengine).

Matokeo yake ni rais kuwajibu waandishi kuwa yeye si mungu mpaka alete mvua, while everybody knows it's our duty to ensure mvua zinaongezeka na basins zetu zipo stable ili ku-support their ecosystems n.k.
Ukijaribu kuangalia kiundani, unaweza kuona kuwa siasa zinaingia kwenye kila kitu. Kamati zote ulizozitaja sijaona walichokifanya cha maana ambacho watanzania wa leo hawakifahamu. You don't need to be an insider to realize that these people are crooks, hata kama hujui kusoma, their lifestyles tell all. Ni mafisadi wa kutupwa, where do they get that money? They don't possess any intellectual property (They don't own a patent for example), sasa hizo fedha na hayo majumba ya marumaru wanayatoa wapi? ... thats enough reason to get rid of'em, hatuhitaji mpaka Zitto au Filikunjombe atuambie hayo.

Kitu kingine, ni impracticability of our policies. Kwa mfano Code of Ethics ya viongozi wa Tanzania (1995) inamwezesha mbunge ambaye anajua kuwa kuna ubadhirifu sehemu fulani, amshtaki mbunge au waziri kwenye ethics tribunal. But two things, the members of that ethics tribunal as stipulated in that act ni wanasiasa hao hao, hatuna independent Tribunal ya kuwashughulikia viongozi wabadhirifu. My opinion, tunge adopt sheria ya kuruhusu mahakama za kimataifa kuamua kesi za ubadhirifu just to get a conviction au innocence na kutumia penal code yetu ambayo nayo inabidi iwe harsher.

Mwisho, kisiasa inabidi mawaziri waondolewe ulazima wa kuwa wabunge, na kabla ya kupata nafasi hizo inabidi wapitishwe na Bunge. Hii pia itumiwe kwa mabalozi wetu.Siasa zikiingilia utaalam, hapo ndipo tutapoharibu.
 
Mchambuzi, umesema vizuri sana. Na binafsi ninaamini na kwa muda mrefu naamini hivyo kuwa ni makosa makubwa kwa wanaotaka mabadilikonchini kuendelea kuiangalia CCM kama chanzo cha mabadiliko hayo. Sasa hivi binafsi siamini kuwa kujiuzulu kwa Waziri au hata Waziri Mkuu ni suluhisho la tatizo letu la msingi - kushindwa kwa sera za CCM. Tatizo letu siyo tena la watu hata kidogo maana tumethibitishiwa mara kadha wa kadha sasa kuwa hata ukibadilisha watu ukaingiza wengine tatizo la msingi bado linakuwepo pale pale - CCM.
 
Kitu ambacho siku zote napingana na wewe ni kuhusisha siasa kwenye kila jambo.Hizo sera unazosema ni za CCM zimepitishwa na wabunge na viongozi wa vyama vya upinzani. Kwa mfano, Augustino Mrema hakupitisha sera za elimu, madini, banking,ulinzi, afya na madini? Hao kina Slaa wakati walipokuwa makada wa CCM hawakupitisha Programu ya Chama? ambayo ndiyo mama wa sera zetu?

Sasa just because they lost in primaries and decided to announce their candidacy from other parties ndiyo iwafanye waone muozo au ufisadi uliopo? Party politics hazitaleta mabadiliko. Ni sawa na kujirudia kulekule kwenye kubadilisha watu ambao walituletea either kwa kuanzisha au kushabika sera wanazozipinga leo hii.

Hakuna chama mbadala Tanzania, ila kuna watu mbadala.Please don't think twice, think deep.
 
Kobello:

Nakubaliana na wewe kwamba mawaziri wetu wengi ni wabovu kwa sababu hawateuliwi on merit bali sababu za kisiasa na mambo mengine yasiyokuwa na tija. Ni mara chache sana kwa hali kuwa tofauti na ukweli huu. Kwa mfano, sina uhakika kama mawaziri wengi ndani ya serikali ya sasa wana sifa, uzoefu na utaalam wa maeneo yao. Pengine exception ni Waziri Mponda na Naibu wake Nkya ndio wana background ya udaktari atleast from administration side of it, na Waziri Dr. Mathayo – Mifupo ambae ana background ya kilimo/ufugaji. Lakini pamoja na hayo, bado hata hawa wachache wenye utaalam husika, utendaji wao bado ni ovyo. Kwa mfano, Wizara ya Afya imefanikiwa kuwa na Mawaziri kutoka kila aina ya background – Madaktari bingwa kama Dr. Chiduo, Pfor. Sarungi, Prof. Mwakyusa, Dr. Mwinyi, – lakini wote hawa hawakufanya lolote la maana; Tumewahi kuwa na wengine wasio na background ya udaktari, mfano Zhakia Meghji na wengine, lakini nao hawakufanya lolote la maana; Wengi wetu tukaanza kujiuliza – pengine tatizo ni kuwa na mtaalam wa public health administration, na kwa bahati, tukampata Haji Mponda ambae ana hiyo background, lakini nae ni sifuri kabisa. Tunabaki kujiuliza, tatizo ni nini hasa?

Kuhusu Wizara ya Nishati, nakubaliana na hoja yako kwamba kinachoangaliwa ni Loyalty, sio utaalam. Ni dhahiri kwamba katika Tanzania ya leo, Professor Mwandosya ni mmoja wa watu wachache sana, pengine katika ukanda wa nchi za maziwa makuu na SADC wenye utaalam na uzoefu na masuala ya nishati na wanao tambulika na kuheshikima kimataifa. Mwandosya alikuwa Kamishna wa nishati kwa miaka mingi sana wakati wa utawala wa Nyerere; amekuwa Katibu Mkuu wa Nishati kwa muda mrefu; amekuwa mtafiti wa nishati kwa muda mrefu sana kupitia taasisi yake ya CEEST iliyopo DSM, na amekuwa anatumiwa sana na World Bank na taasisi nyingine za kimataifa kufanya tafiti mbalimbali katika nchi za maziwa makuu na SADC. Ameandika makala nyingi katika journals za kimataifa juu ya masuala ya nishati, mfano journal number one duniani on energy - ‘Energy Policy'; Taasisi yake ya CEEST hapa tunapoongea imejaa research fellows na watafiti wa PhD kutoka vyuo vikubwa vya marekani na ulaya ambao wanaelekezwa kuja kutumia facilities mbalimbali zilizopo pale; lakini pamoja na haya yote, bado hazina kama hii (Mwandosya) anateuliwa kuwa Waziri wa nchi mazingira; waziri wa Maji na Umwagiliaji, na mwishoni anachakachuliwa afya, kisa he's a political threat!

Kuhusu Mnyika, ni kweli hana utaalam wala uzoefu katika eneo la nishati lakini tusisahau kwamba yeye ni waziri kivuli tu wa Nishati, lakiji kubwa zaidi ni kwamba kwa sasa Chadema bado haina pool kubwa ya wataalam mle bungeni. Suala la January kuwa mwenyekiti wa kamati ya nishati, ni jambo lililo wazi kwamba yupo ‘on job training.'
Na kuhusu maadili ya uongozi na ufisadi, inashangaza kuona tume ya maadili inakosa meno ya kuwatafuna majangili walipo ndani ya CCM; Lakini kama hata TAKUKURU inakosa meno, ufizi wa tume ya maadili ndio utakuwa ni dhaifu kabisa hata kuotesha meno. Tatizo ta ufisadi kwa mtazamo wangu ni matokeo ya watawala wetu ndani ya CCM kurukia Azimio La Zanzibar mwaka 1992 bila ya kutambua kwamba pamoja na mapungufu mengi ndani ya Azimio la Arusha, bado lilikuwa na faida kadhaa. Wanasiasa wa CCM wao walikazania zaidi kuhalalisha mali walizoibia umma.

Pia nakubaliana na wewe kwamba kuna umuhimu wa kuteua mawaziri wasiotokana na wabunge kwani chini ya mfumo wa sasa, mawaziri wamekuwa na visingizio kwamba wanao waangusha ni watendaji. Sasa imefikia wakati mawaziri ndio wawe watendaji badala ya wasimamizi wa sera. Nadhani pia ni muhimu tumfanye Rais wa nchi awe tu ni a ‘ceremonial leader', na nchi iwe chini ya waziri mkuu ambae anatajibika moja kwa moja kwa bunge.

Mwanakijiji:

Nakubaliana na wewe kwamba moja ya udhaifu wetu kama watanzania ni utamaduni na imani tuliyoijenga kwamba chanzo cha mabadiliko ya kweli ni Tanzania ni CCM. Lakini katika mazingira ya sasa, hili linaepukika kweli? Kwani hata bungeni juzi, bila ya wabunge wa CCM kuweka misimamo yao sawa, sahihi 71 za Zitto zisingepatikana. Binafsi sidhani kama mabadiliko ya kweli na ya haraka yanaweza kuja bila ya mkono wa wana CCM walioamua kujitoa mhanga na kuweka maslahi ya nchi juu ya Chama. Vinginevyo iwe ni matumaini kwamba mapambano ya sasa yaendelee kwa miaka mitatu ijayo ili ifikapo mwaka 2015, mabadiliko yapatikane kupitia sanduku la kura.
 
hakika huu ni uchambuzi makini kabisa ambao kwa yoyote mwenye akili timamu akiusoma anafunguka na kujua kinachoendelea katika nchi yetu..
 
Kuhusu waziri anatakiwa mtu wa aina gani.. hapa napingana na kobello, sio lazima awe amebobea ktk utaalam wa kitu kile kile. ila tu nakubaliana naye ktk kusema waziri sio lazima awe mwanasiasa unless wanasiasa (wabunge) hao wachaguliwe kutokana na sifa ya uongozi kama nchi za Uingereza au Canada ndipo unaweza kuwafanya wabunge wawe pia mawaziri. Na maadam tuna wataalam wachache tena kwa uchache ambao unakuta Mtaalam hajui siasa, ama mwanasiasa hana Utaalam wa uongozi ndio maana tunajikuta tumejenga madudu kama haya.

Waziri sio lazima awe kasomea udaktari ili awe waziri wa Afya hata kidogo... ila waziri lazima awe mtaalam wa uongozi (Management) na kaonyesha mafanikio sehemu yoyote alowahi kuiendesha na sio cheti cha shule au nafasi yake ndani ya chama. Naweza sema waziri ni sawa na CEO wa shirika hivyo uwaziri ni ajira inayotokana na uwezo wa mhusika kuongoza wizara ile..

Kuna kipande kidogo cha EU kilichochapishwa makhususi kwa Ureno nawaomba mkisome na mtazame challenges wanazokabiriana nazo mawaziri kisha ndio tujenge hoja zetu - Bofya

Na ndugu yangu Mchambuzi, wewe hutakiwi kuwa CCM hadi leo njoo Chadema mkuu wangu hapo ndipo panapokufaa kwa mavitu unayoangusha hapa. kobello, lazima ufahamu kwamba nchi inaongozwa na vyama vya siasa na watu kama nyie mnapokaa nje mkitegemea kuna vichwa vya watu hakuna chama basi ndio nyie mnaojenga castle kwa mchanga wa bahari. Jiunge na mawazo yako yafanye kazi kubadilisha mfumo wa kiutawala ukiwa nje ukikosoa tuuu, hutasikiwa..
 
Mkuu Mkandara,
Unajua kinachofanya wengi wetu tufikiri pengine wataalam ndio wanaotufaa ni kwa sababu ni nadra sana kwa mawaziri wetu kuchaguliwa on merit, wengi huwa ni wa ovyo ovyo kitaaluma, kielimu, uzoefu n.k. Lakini hoja yako kwamba pengine the only pre - requisite ni 'management skills', inasimama.

Kuhusu kuhamia Chadema, binafsi sina tatizo na chama hicho, kuna masuala mawili tu ndio bado im wrestling with: (1) Bado nina amini kabisa kwamba itikadi ya Chadema ina mapungufu, unless suala hilo nilifungie macho na badala yake nijikite zaidi katika harakati za kuikomboa nchi yetu na kuja kurekebishana baadae kidogo. (2) Tatizo lingine na Chadema ni kwamba haina mpango wa muda mrefu, wananchi wengi wana amini kwamba chadema ikishinda mwaka 2015, maisha bora yatakuja ndani ya miaka mitano, sana sana kumi. Sasa kama viongozi wa chadema hawawekezi katika kuwaelimisha wananchi kwamba watakaofaidika na matunda ya ukombozi kwa mfano mwaka 2015 ni watoto na wajukuu zao, haitakuwa ajabu kwa CCM kurudi tena madarakani mwaka 2020 kwa hoja mbovu kabisa mfano kwamba 'wananchi, mnaona, uongozi wa nchi sio lelemama, mmewapa hawa, wameshindwa n.k". Ni mambo machache kama haya ndio yanakatisha baadhi yetu tamaa na kusema bora kubakia na jini unalolijua badala ya kugeuka kuwa malaya wa siasa. Vinginevyo suala la kuhamia Chadema au CCK ni haki yangu ya kikatiba na ni suala ambalo lipo kichwani mwangu constantly kwani CCM kwa kweli ni 'dead man walking', ndio maana kote kinapozurura, kinaleta maafa watanzania bila ya kujali.
 
Hayo niliyoyasema yanathibitishwa na historical data. Ni waliokaa pembeni ndiyo wataoleta mabadiliko.Wakijaribu kuleta wagombea binafsi, utakuja kuniambia. Mimi ni mwna CCM, ila nipo tayari kumuunga mkono mtu yeyote mwenye idea na nia nzuri no matter which party he rpresents. Ndiyo mana unaona Zitto ana wafuasiweni kutoka CCM kuliko kutoka CDM. Huwa mnamtukana kila siku humu jamvini kisa ana practice mawazo yake ila kufuata mkondo mnaoutaka.
 
Mkuu,

Sisi tumekosea kila kitu.
Hakuna kitu tunachofanya vizuri.
Hatuna priorities as a nation.
All we have are blue printies, no implementation.
All the institutions are in the verge of collapse
Tumekuwa kama Mbuzi, akitoka zizini ndio anajua ya siku hiyo atakula nini.
Mbaya zaidi, viongozi hawako taayri kusikiliza...
Katika Historia ya Dunia, hakuna nchi iliyodharau wasomi ikaendelea...
Tumegeuka machinga
Business as usual...
It is pity.
 
Mkuu Mkandara,
Unajua kinachofanya wengi wetu tufikiri pengine wataalam ndio wanaotufaa ni kwa sababu ni nadra sana kwa mawaziri wetu kuchaguliwa on merit, wengi huwa ni wa ovyo ovyo kitaaluma, kielimu, uzoefu n.k. Lakini hoja yako kwamba pengine the only pre - requisite ni 'management skills', inasimama.

Kuhusu kuhamia Chadema, binafsi sina tatizo na chama hicho, kuna masuala mawili tu ndio bado im wrestling with: (1) Bado nina amini kabisa kwamba itikadi ya Chadema ina mapungufu, unless suala hilo nilifungie macho na badala yake nijikite zaidi katika harakati za kuikomboa nchi yetu na kuja kurekebishana baadae kidogo. (2) Tatizo lingine na Chadema ni kwamba haina mpango wa muda mrefu, wananchi wengi wana amini kwamba chadema ikishinda mwaka 2015, maisha bora yatakuja ndani ya miaka mitano, sana sana kumi. Sasa kama viongozi wa chadema hawawekezi katika kuwaelimisha wananchi kwamba watakaofaidika na matunda ya ukombozi kwa mfano mwaka 2015 ni watoto na wajukuu zao, haitakuwa ajabu kwa CCM kurudi tena madarakani mwaka 2020 kwa hoja mbovu kabisa mfano kwamba 'wananchi, mnaona, uongozi wa nchi sio lelemama, mmewapa hawa, wameshindwa n.k". Ni mambo machache kama haya ndio yanakatisha baadhi yetu tamaa na kusema bora kubakia na jini unalolijua badala ya kugeuka kuwa malaya wa siasa. Vinginevyo suala la kuhamia Chadema au CCK ni haki yangu ya kikatiba na ni suala ambalo lipo kichwani mwangu constantly kwani CCM kwa kweli ni 'dead man walking', ndio maana kote kinapozurura, kinaleta maafa watanzania bila ya kujali.
Mkuu kuhusu Itikadi ya kusimama kati hilo ni swala dogo sana kimtazamo kwa sababu haliathiri maana nzima ya mfumo wetu kwa sababu hatuna kitu ITIKADI isipokuwa ile ya ku copy na ku paste..Kwa sababu Conservative wanatakiwa kuwa wenye mtazamo wa chimbuko la utaifa sasa siju tunaanzia wapi kutoka kwa Watenmi na Machief au Azimio la Arusha halafu Liberal ni wanaotaka mageuzi ya itikadi ile ya kwanza. ndio maana wenzetu huko Ulaya unaweza kukta chama kinaitwa Conservative au demokratic lakini kipo upande wa kushoto ama kulia..Sisi hili hatulijui na kama unataka kuhakikisha nenda katazame umoja wa vyama vya conservative utakuta majina ya vyama viijiita demokratic au Liberal.. Sisi hatuna Itikadi leo tunajiendea tu na siasa za Upinzani kama mpira wa Yanga na Simba sema hutaki kuvaa jezi ya Msimbazi.

Binafsi yangu kuna hoja nimeziweka humu ambazo zinapingana na sera za Chadema lakini haya ni mawazo yangu mimi hayawezi kuniondoa Uanachama ikiwa nakubaliana na malengo ya Chadema wanataka Taifa la aina gani hasa wanapopambana na Ufisadi.. Kwa wanaCCH wanachukulia Ufisadi ni jambo dogo sana wakati kwa miaka 50 tumeshindwa kuendelea mbele kutokana na Ufisadi na wanajua lakini kwa akili zao wanafikiria tukiongeza uzalishaji Ufisadi hauweza kuathiri uchumi wetu. Hizi fikra na ndoto kama hizi ndio zinanifanya nisiwe karibu kabisa na CCM.

Ufisadi sio kilevi ukasema watu wamekuwa addicted inawezekanakabisa kupigwa vita baada ya hapo ndipo tunaweza jiengua tukatazama ujenzi wa Taifa jipya. Huwezi taka mageuzi ya nchi ikiwa umetawaliwa, ni lazima kwanza upige vita kutawaliwa ukisha kuwa huru ndipo unatazama utaendelesha vipi uchumi wako [EMAIL=" kobello" kobello[/EMAIL], nashukuru kusikia uko CCM na ndio. Kuhusu Zitto, mkuu wangu ni demokrasia ndani ya Chadema ambayo huwezi kuiona CCM, kwa hiyo sishangai kuona unashangaa Zitto kukosolewa hapa JF, haya utayaona tu huku mkuu wangu, huko CCM ukifanya hivyo unaondolewa ktk meza ya Chukua Chako Mapema tena bila huruma tumewaona wengi wakiharibikiwa hadi maisha yao.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kuhusu Itikadi ya kusimama kati hilo ni swala dogo sana kimtazamo kwa sababu haliathiri maana nzima ya mfumo wetu kwa sababu hatuna kitu ITIKADI isipokuwa ile ya ku copy na ku paste..Kwa sababu Conservative wanatakiwa kuwa wenye mtazamo wa chimbuko la utaifa sasa siju tunaanzia wapi kutoka kwa Watenmi na Machief au Azimio la Arusha halafu Liberal ni wanaotaka mageuzi ya itikadi ile ya kwanza. ndio maana wenzetu huko Ulaya unaweza kukta chama kinaitwa Conservative au demokratic lakini kipo upande wa kushoto ama kulia..Sisi hili hatulijui na kama unataka kuhakikisha nenda katazame umoja wa vyama vya conservative utakuta majina ya vyama viijiita demokratic au Liberal.. Sisi hatuna Itikadi leo tunajiendea tu na siasa za Upinzani kama mpira wa Yanga na Simba sema hutaki kuvaa jezi ya Msimbazi.

Binafsi yangu kuna hoja nimeziweka humu ambazo zinapingana na sera za Chadema lakini haya ni mawazo yangu mimi hayawezi kuniondoa Uanachama ikiwa nakubaliana na malengo ya Chadema wanataka Taifa la aina gani hasa wanapopambana na Ufisadi.. Kwa wanaCCH wanachukulia Ufisadi ni jambo dogo sana wakati kwa miaka 50 tumeshindwa kuendelea mbele kutokana na Ufisadi na wanajua lakini kwa akili zao wanafikiria tukiongeza uzalishaji Ufisadi hauweza kuathiri uchumi wetu. Hizi fikra na ndoto kama hizi ndio zinanifanya nisiwe karibu kabisa na CCM.

Ufisadi sio kilevi ukasema watu wamekuwa addicted inawezekanakabisa kupigwa vita baada ya hapo ndipo tunaweza jiengua tukatazama ujenzi wa Taifa jipya. Huwezi taka mageuzi ya nchi ikiwa umetawaliwa, ni lazima kwanza upige vita kutawaliwa ukisha kuwa huru ndipo unatazama utaendelesha vipi uchumi wako kobello" kobello, nashukuru kusikia uko CCM na ndio. Kuhusu Zitto, mkuu wangu ni demokrasia ndani ya Chadema ambayo huwezi kuiona CCM, kwa hiyo sishangai kuona unashangaa Zitto kukosolewa hapa JF, haya utayaona tu huku mkuu wangu, huko CCM ukifanya hivyo unaondolewa ktk meza ya Chukua Chako Mapema tena bila huruma tumewaona wengi wakiharibikiwa hadi maisha yao.
Sikubaliani na wewe hata kidogo. Zitto ni pandikizi la CCM, hivyo ndivyo mnavyomuita. Pia Zitto hulaumiwa openly na wazee simply because amesema ana ambition ya kuwa rais. Kuhusu Zitto kusakamwa na wanachama wenzake naweza kukupa mifano mingi tu tangu enzi za uchaguzi wa Bavicha,uchaguzi wa mwenyekiti n.k. But that doesn't really concern me.
Kujua Management pekee hakukufanyi uwe kiongozi bora wa Institution yeyote.Actually, waziri mzuri ni yule aliyebobea kwenye sekta ambayo wizara yake inasimamia.Ukimuweka kwa mfano Filikunjombe awe waziri wa kilimo, hapo ndipo utapoona maamuzi magumu yakifanywa ili kufurahisha umma na wakati huohuo kuliletea taifa hasara. Hebu angalia jinsi CDM walivyolishikilia suala la Dowans na kutusababishia hasara.
au jinsi walivyopendekeza CDM na CUF wapewe mjumbe moja mmoja kuwakilsha EALA as if hawajui kusoma.
 
Mkuu kuhusu Itikadi ya kusimama kati hilo ni swala dogo sana kimtazamo kwa sababu haliathiri maana nzima ya mfumo wetu kwa sababu hatuna kitu ITIKADI isipokuwa ile ya ku copy na ku paste..Kwa sababu Conservative wanatakiwa kuwa wenye mtazamo wa chimbuko la utaifa sasa siju tunaanzia wapi kutoka kwa Watenmi na Machief au Azimio la Arusha halafu Liberal ni wanaotaka mageuzi ya itikadi ile ya kwanza. ndio maana wenzetu huko Ulaya unaweza kukta chama kinaitwa Conservative au demokratic lakini kipo upande wa kushoto ama kulia..Sisi hili hatulijui na kama unataka kuhakikisha nenda katazame umoja wa vyama vya conservative utakuta majina ya vyama viijiita demokratic au Liberal.. Sisi hatuna Itikadi leo tunajiendea tu na siasa za Upinzani kama mpira wa Yanga na Simba sema hutaki kuvaa jezi ya Msimbazi.

Binafsi yangu kuna hoja nimeziweka humu ambazo zinapingana na sera za Chadema lakini haya ni mawazo yangu mimi hayawezi kuniondoa Uanachama ikiwa nakubaliana na malengo ya Chadema wanataka Taifa la aina gani hasa wanapopambana na Ufisadi.. Kwa wanaCCH wanachukulia Ufisadi ni jambo dogo sana wakati kwa miaka 50 tumeshindwa kuendelea mbele kutokana na Ufisadi na wanajua lakini kwa akili zao wanafikiria tukiongeza uzalishaji Ufisadi hauweza kuathiri uchumi wetu. Hizi fikra na ndoto kama hizi ndio zinanifanya nisiwe karibu kabisa na CCM.

Ufisadi sio kilevi ukasema watu wamekuwa addicted inawezekanakabisa kupigwa vita baada ya hapo ndipo tunaweza jiengua tukatazama ujenzi wa Taifa jipya. Huwezi taka mageuzi ya nchi ikiwa umetawaliwa, ni lazima kwanza upige vita kutawaliwa ukisha kuwa huru ndipo unatazama utaendelesha vipi uchumi wako kobello" kobello, nashukuru kusikia uko CCM na ndio. Kuhusu Zitto, mkuu wangu ni demokrasia ndani ya Chadema ambayo huwezi kuiona CCM, kwa hiyo sishangai kuona unashangaa Zitto kukosolewa hapa JF, haya utayaona tu huku mkuu wangu, huko CCM ukifanya hivyo unaondolewa ktk meza ya Chukua Chako Mapema tena bila huruma tumewaona wengi wakiharibikiwa hadi maisha yao.

Brand Equity ya Chadema ni nini? Je, ni uwezo wao wa ku take advantage of mapungufu ya CCM for the last 50 years ambayo ndani yake, wapo hata waliopo sasa CUF, Chadema n.k ambao huko nyuma waliyabariki? Hoja yako ya msingi naielewa kwamba tunahitaji mabadiliko lakini bado sioni Chadema italeta mabadiliko yepi hasa ukizingatia kwamba na wao wangependelea kuja tawala nchi yetu chini ya mfumo wa majoritarian democracy ambao umeiangusha CCM. Inabidi uni convince zaidi kwamba Chadema ni mbadala wa kweli wa CCM na kwamba kina viongozi wakuu wa Chadema kunywa bia na mafisadi wa CCM sio tatizo.

Kuhusu itikadi, sikubaliani na wewe. Kinachotokea nchi za wenzetu ni kucheza na spectrum ya ideology but they dont loose focus on what they stand for; in this spectrum, left end ni communism, right hand ni conservatives, na hapo kati kati ni a mixture of the two; muhimu zaidi ni kwamba hizi ideology sio kwamba ni vyama vinatunga, bali idelogy ni suala ambalo lipo kwenye jamii hata kama vyama havipo, kwa mfano jamii inayoamini kwamba ni muhimu kutahiri wanawake karne hii ya ishirini na moja, hao ni conservatives, now how do you win their votes? sidhani kama suala la itikadi ni suala la copy and paste unless wananchi hawaelewi maana ya itikadi, otherwise ni kitu wanacho practice kila siku hata bila masuala ya CCM, CUF, CHADEMA n.k.

Mkuu, naomba uelewe kwamba tunachojadili hapa ni jinsi gani Chadema inaweza kuwa mbadala wa kweli na kwamba CCM imefilisika kiuongozi. Tusaidiane the way forward lakini kwa hoja.
 
Mchambuzi,

..mimi nadhani tatizo ni JK, na wana CCM mnaona haya kutamka hilo.

..kuna key sectors ambazo Raisi hatakiwa kuweka mawaziri wa hovyo-hovyo au maswahiba zake.

..JK alipomteua Zakhia Meghji kuwa waziri wa fedha nikajua kwamba nchi hii haina Raisi.

..tatizo lingine ni kwamba serikali ya JK haina vipaumbele.
 
Nakubaliana na wewe kimsingi. Na ndio maana nikahoji kwambe je:
  • Tatizo ni JK kuwa na uncertainity on who can make mawaziri bora badala ya hali ya sasa ya bora mawaziri?
  • Je mchakato wetu wa kupata wabunge una mapungufu ambayo yanapelekea upatikanaji wa wabunge wachache wenye vigezo vya kuwa mawaziri bora?
  • Je wabunge wenye uwezo wapo lakini Rais haweki juhudi ya kutosha kuwatambua na kuwapa dhamana ya uongozi na badala yake anatumia vigezo vya uteuzi ambavyo havina tija kwa taifa?

Me nadhani point ya pili na ya tatu holds, na matokeo yake, Rais mwenyewe ndiye anakuwa chanzo cha tatizo kwani mara nyingi amesikika akisema mwenye mamlaka ya kuteua na kufukuza mawaziri ni yeye so aachiwe hiyo kazi. Alitamka hili hata wakati wa sakata la mgomo wa madaktari wakati anahutubia wazee wa DSM. Yet hatuoni mabadiliko yoyote yenye kurudisha imani ya wananchi kwa CCM na serikali yake, hivyo kupelekea ukosefu wa umakini katika maamuzi na utendaji wake kuwa ni sehemu kubwa sana ya tatizo linalotukabili sasa kama chama, na kwa vile ndicho kimeshika dola, kama taifa. Hiyo ndio hali halisi.
 
..mchakato wetu wa kupata wabunge hauna matatizo.

..mimi naamini kabisa kwamba bunge letu lina-reflect wananchi wa Tanzania.

..bunge letu lina watu wa kila aina kuanzia ma-Profesa waliobobea kitaalamu, viongozi wa dini wa kweli na wale uchwara, vijana, watoto wa "mujini", wafanyabiashara, waganga wa kienyeji etc etc.

..zaidi, Raisi amepewa mamlaka ya kuteua wabunge 10 ambao anaona watamsaidia bungeni au ktk baraza la mawaziri.

..kwa Tanzania kuna wizara 3 au 4 ambazo Raisi anatakiwa awe makini sana ktk uteuzi wa mawaziri. bila wizara hizo kufanya kazi kwa ufanisi basi hakuna cha maana kitakachoendelea nchini.

NB:

..mimi nadhani mjadala ambao utakuchangamsha zaidi ni wa nini kifanyike at this time ku-stop the bleeding.

..tufanye nini at least kuhakikisha jahazi linafika salama pwani, kwasababu kinyume chake wananchi wanaweza kuchukua hatua wenyewe.
 
JOKA KUU sijui una maana gani unaposema mchakato weetu wa kuchagua wabunge hauna matatizo. Mimi naona una matatizo makubwa sana, kwa kuwa Bunge ni mhimili muhimu sana wa dola, kwa hiyo bunge linatakiwa kuwa effective na efficient, sasa hivi hali ni tofauti sana. Bunge letu ni weak sana, ni sawa na mbwa asiye na meno. Ukiangalia CV za wabunge unaweza kushangaa kama kweli wanaweza kuwa kwenye mhimili huo. Labda ni mbunge mmoja mmoja sana akiongea unaona kweli ni mbunge, wengine ni sawa na wazugaji tu bungeni.

Inawezekana kuwa bunge letu linareflect wananchi wa Tanzania, lakini halireflect hata kidogo mahitaji ya Tanzania, watanzania au mahitaji ya kazi za bunge. Ni kweli kuna maprofesa na wenye elimu ya msingi lakini wote wanafanya kazi kwa maslahi yao na si kwa maslahi ya serikali, ndio maana bunge limekuwa mhuri tu wa serikali.

Kama hatutabadilisha quality ya bunge, basi litaendelea kuwa mhuri tu.
 
Binafsi nadhani tatizo lipo kwenye vigezo hivi ambavyo ni kwa mujibu wa katiba yetu ya nchi:
1. Lazima awe ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa miaka ishirini na moja, na ambaye anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza;
2. Awe na angalau elimu angalau ya darasa la Saba;
3. Ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;
4. Katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi hakuwahi kutiwa hatiani katika mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.
 
Mchambuzi ukichambua vigezo vyote hivyo unaweza kuona kuwa ni vigezoi vya kijinga kabisa. Cha kutimiza umri wa miaka 21 kinaeleweka kwa sababu ya naturity na kuweza kufanya analysis kiasi kabla ya kuamua. Does it make any sense kusema mbunge walau awe na elimu ya darasa la saba? kwa nini tusiseme walau shahada ya kwanza? Kuna jimbo lolote Tanzania hii leo halina graduate? Au kwanini japo tusifike diploma? Hata majimbo ya pwani ambayo watu wengi wana eli u duni nadhani wapo wenye diploma, hata kigoma kuna wenye digrii.

Is it necessary kwa mbunge kuwa mwanachama? what if watu wanataka mbunge ambaye si mwanachama

Ina maana kukwepa kulipa kodi ni kosa kubwa sana kuliko uhujumu wa uchumi, ujambazi, ufisadi, ubadhirifu etc. Na ina maana kuwa nikataka kugombea ubunge nihakikishe nakwea kulipa kidogo miaka mitano kabla ya kugombea ubunge, kabla ya hapo ntakuwa safe naweza kugombea baadaye.

Ukiangalia kwa undani utaona kuwa yote haya ni ujinga ambao tunauchekea na kuulea, ndio unaofanya bunge let liwe dhaifu, na hata baadhi ya mawaziri wanaoteuliwa miongoni mwa wabunge wawe wababaishaji.

Vigezo vya kuchagua wabunge ni sehemu moja tu tunapokosea, na hii si kwa CCM peke yake!
 
Back
Top Bottom