Mawaziri na wabunge wa Zanzibar wanatangaza pombe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawaziri na wabunge wa Zanzibar wanatangaza pombe

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Game Theory, Jan 24, 2012.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Jan 24, 2012
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Hawa wabunge wa Baraza la wawakilishi kila kukicha wako bize kutuonyesha wao hawataki mambo ya kuharibu mila na desturi zao za kizanzibari

  haya imekuwaje wameamua kutangaza pombe?

  Tazama hizi picha:

  MICHUZI: sbl yatumia zadi ya mil 65 kuadhamini mechi ya wabunge na baraza la wawakilishi zanzibar.


  tena kwa kuonyesha ushabiki wa kutangaza pombe wao wameamua kuvaa jezi zenye kutangaza wakti wenzao toka bara waliamua kuvaa traksuti zilizokuwa plain

  Huu ndio unafiki wa BLW wa zanzibar

  Mtu anaondoka nyumbani kwake asubuhi anamwaga mkewe na n=kumpa instructions ahakikishe watoto wameenda madrasa kusoma

  ikifika mchana mtu huyo huyo anavaa jezi kutangaza pombe

  Jioni akirudi anataka kujua kama watoto walienda madrasa

  then kesho yake wanatangaza kuwa mila na desturi za mzanzibari zinaingiliwa na ni moja kati ya kero za muungano

  hawa ndio wanasiasa wa Zanzibar.

  nimeshindwa kupost picha nisaidieni
   
 2. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mbele ya fwedha hakuna Desturi wala Dasturi! Hata hivyo hawa jamaa ni Wanafiki sana, ni kama mlevi anayetema kushoto halafu anafukia kulia.
   
 3. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #3
  Jan 24, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  je wajuwa kuwa bar zinachomwa huko? au hujasikia hilo.
   
 4. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #4
  Jan 24, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kazi kwelikweli...!
   
 5. ng'wanankamba

  ng'wanankamba JF-Expert Member

  #5
  Jan 24, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 340
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Wao wenyewe walevi kama komba, tunawaona huku bara wanavyopiga ulabu.
   
 6. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #6
  Jan 24, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  unafurahia eeh?
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Jan 24, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Baa zinachomwa na watu binafsi, hapa zinazungumziwa taasisi zinazounga mkono pombe. Au hao wanaochoma baa wanatumwa na taasisi hizi?
   
 8. J

  JokaKuu Platinum Member

  #8
  Jan 24, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  ..ZNZ pombe na machangudoa wanapigwa vita kuliko madawa ya kulevya na ushoga.
   
 9. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  hii ngumu kuijibu
   
 10. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Na wewe unaunga mkono uvunjaji huu wa sheria?
   
 11. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #11
  Jan 25, 2012
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,031
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Kuna ustaz mmoja nilimkuta maeneo ya mwenge pale kwa afande kwe kitimotoz, nikamwuhoji vp yupo maeneo yale na yeye ni swala 5 tena mwezi wa ramazan? Akai eti nyama ile nyeupe(mafuta) ndo ndo haramu. Isitoshe eti kuna mtu anamsubiri.
   
 12. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #12
  Jan 25, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  mmh, priorities:
   
 13. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  [h=3]WAFANYABIASHARA YA POMBE WAPIGWA RISASI ZANZIBAR[/h]
  [​IMG]
  Mfanyabiashara Alvind Asawla aliyepigwa risasi katika paji la uso ikatokea shingoni na kumwagiwa tindikali Zanzibar, akiwa na mkewe Bimal katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jumatano iliyopita. (Na Yusufu Badi).

  WAFANYABIASHARA wawili mtu na mkewe, wamepigwa risasi na kumwagiwa tindikali huko Zanzibar kwa kuuza pombe.

  Katika uvamizi huo uliofanyika Jumatano iliyopita mwanamke Bimal Alvind (36) alinusurika kupoteza ujauzito wake wa miezi minne baada ya kupigwa risasi ya tumbo na kumwagiwa tindikali.

  Risasi hiyo ilitolewa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili bila kuathiri ujauzito huo lakini tindikali hiyo ilimjeruhi mwilini kuanzia usoni, kifuani kwenye matiti, mikono yote miwili na tumboni.

  Mumewe, Alvind Asawla (42) alipigwa risasi kichwani kwenye paji la uso katikati ya macho iliyotokea nyuma chini ya shingo na sasa amepooza upande mmoja.

  Akizungumza na gazeti hili nyumbani kwa ndugu yake Upanga wiki hii, Asawla alisema walivamiwa Jumatano iliyopita saa 10:30 jioni katika Mtaa wa Hurumzi Mji Mkongwe.
  Alisema wakati wakivamiwa, yeye na mkewe aliyeishi naye kwa miaka 17 sasa na kujaliwa watoto wawili; Priyanka (14) na Nidh (12), walikuwa wakitoka katika biashara yao wakirudi nyumbani eneo la Kiponda.

  Alisema ghafla watu wawili walimvamia mkewe na kummwagia tindikali na yeye alipokuwa akijaribu kumsaidia, watu hao walimmwagia tindikali usoni.

  Kwa mujibu wa Asawla, wakati wakitaharuki kwa hali hiyo, ghafla alitokea mtu mwingine na kumpiga risasi katika paji la uso akadondoka chini huku damu zikimtoka.

  Alisema alijaribu kujikongoja kwa nia ya kuendelea kumsaidia mkewe lakini mtu huyo wa tatu alimpiga risasi ya pili mgongoni na mkewe akapigwa risasi ya tumbo.  Asawla alisema baada ya hapo hakujua kinachoendelea mpaka alipozinduka Kituo cha Polisi cha Malindi walipopatiwa PF3 na kupelekwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja walipopigwa picha za x-ray na kugundulika wana risasi mwilini.

  Baada ya kipimo hicho, Asawla alisema hospitali hiyo haikuwa na vifaa vya kutoa risasi hizo, ndipo ndugu zake waliwasaidia usiku huo na kuwasafirisha kwa ndege hadi Dar es Salaam ambapo walikimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

  Alisema mkewe alilazwa katika wadi ya Kibasila namba tatu na yeye akahamishiwa katika Hospitali ya TMJ kwa ajili ya kipimo cha CT-Scan ambacho hakikupatikana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

  Kwa mujibu wa Asawla, mke wake alitolewa risasi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na yeye kufanyiwa upasuaji wa kumtoa risasi ulifanyika katika Hospitali ya TMJ.
  Alisema anamshukuru Mungu kwa kuwa ni mzima hadi sasa kwani alipigwa risasi sehemu mbaya na kukaa nayo kwa saa zaidi ya 12 ndipo ilipotolewa kichwani jambo lililowashangaza hata baadhi ya wauguzi.

  "Nimepooza upande mmoja wa kichwa changu, sihisi jambo lolote lakini madaktari wameniambia nitarudi katika hali yangu ya kawaida polepole baada ya kufanya mazoezi," alisema.

  Alisema aliambiwa kuwa risasi hizo hazikupita katika mishipa mikubwa ndiyo maana yuko hai hadi sasa na mshipa mdogo uliomwaga damu, umefanya jicho la upande uliopooza kuwa jekundu licha ya kuona vizuri.

  Mfanyabiashara huyo alisema kuwa watu hao wamempa ulemavu wa kudumu bila kutegemea huku akiamini siyo majambazi ingawa walichukua pochi ya mkewe iliyokuwa na fedha kidogo.

  Alisema hospitalini wameambiwa tindikali waliyomwagiwa ni aina ya asidi sulfuriki (sulphuric acid) inayotumika katika magari.

  "Unajua mwizi anataka fedha na siyo kumwagia tindikali au kukupiga risasi na sisi hatukuwa na silaha yoyote; nia ya watu hawa ni kutuua kwani tumekuwa tukipata vitisho vya mara kwa mara kutokana na biashara yetu ya kuuza pombe Zanzibar," alidai.

  Alidai mara kwa mara wamekuwa wakipata vitisho ikiwemo kukuta karatasi inayomtaka kuacha biashara hiyo vinginevyo utauawa; na wamekuwa wakitoa taarifa katika vituo vya Polisi vilivyopo karibu na biashara zao.

  Alilalamika kuwa licha ya wafanyabiashara wengi wa pombe kufanyiwa vitendo vya kumwagiwa tindikali, kupiwa risasi na hata kuchomwa moto, hakuna aliyewahi kukamatwa na kuchukuliwa hatua.
  "Sisi tunafanya biashara na mahoteli makubwa ya kitalii na tunalipa kodi zote stahiki, Serikali iseme wazi kama haitaki biashara hii Zanzibar au wawadhibiti watu hawa," alisema.

  Alidai kuwa matukio kama hayo ni ya muda mrefu na mwaka 2007 wakati wa Jumatatu ya Pasaka, baba yake mzazi, Ahandillal Asawla aliyekuwa akifanya biashara hiyo alimwagiwa tindikali usoni akafariki dunia.

  "Hata baba yangu aliuawa lakini hakuna hata mtu aliyekamatwa na Serikali haikufanya jambo lolote, sasa umefika wakati Serikali itulinde tunaofanya biashara hii au itangaze kusitisha kwa manufaa yetu," alisema Asawla.

  Alisema cha kushangaza tangu ukoloni babu zake waliuza pombe kwa amani lakini sasa wanatumia pombe kama sababu za kisiasa ili kuangusha uchumi wa Zanzibar.

  Gazeti hili liliwasiliana na uongozi wa Polisi katika Mkoa wa Mjini Magharibi bila mafanikio.
  Kwanza Kamanda wa Polisi Mjini Magharibi, ACP Azizi Mohamed simu yake iliita bila majibu na simu ya Kamisha wa Polisi Zanzibar, CP Musa Musa haikupatikana pia.

  Baadaye gazeti hili lilifanikiwa kumpata Ofisa Uhusiano Polisi Zanzibar, Asha Mzule lakini alisema kuwa ni mgonjwa kwa muda kidogo hivyo hajui kinachoendelea na kutoa namba ya simu ya OCD wa Wilaya ya Mji Mpya.

  Hata hivyo OCD huyo alikataa kuzungumzia uvamizi huo wala kutaja jina lake lakini akashauri atafutwe ACP Azizi ambaye alidai yuko Uwanja wa Ndege akimsubiri Rais wa Zanzibar, Dk. Mohamed Shein anayetokea nje ya nchi.
  Namba ya ACP Azizi ilipopigwa kwa mara ya pili, haikupatikana kabisa.
   
 14. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #14
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  nashauri picha hizi wapelekewe wazanzibari kwenye forum zao kama zanzinet ili watoe majibu

  unafiki wa kutisha huu
   
 15. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #15
  Feb 1, 2012
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  double standards
   
Loading...