Mawaziri kufanyiwa semina Ikulu, Dar kesho - Februari 25

Duh ukiwa unapanda jaribu kuwauliza wanaoshuka uko juu kukoje usijione fundi wa kupanda kuna wenzio walianza pia na wakashuka,aya semina elekezi kama jana na juzi naona taratibu kaka anabaki kaka natamani wale mashabiki wangerudi hapa kutueleza imekuaje.
 
...

Kweli hawa watendaji wa serikali ya awamu ya 5 pamoja na mkuu wao, mzee wa 'pushups' wanaweza kuingizwa kwenye Guiness World records kutokana na 'vioja' vyao!

Imekuwa vyema Magufuli ameligundua hilo na akaona awape semina hiyo elekezi ...!

'vioja' vinahitaji semina elekezi?
 
Jamaa walizungusha mikono hadi leo bado akili zinazunguka tuuuu hadi wamechanganyikiwa

Mna hamu iwe hivyo ila ukweli kwa upande wenu CCMscrow ndo unawatesa. CCMscrow haitakaa ibadilike MILELE!

Usisahau Chenge ni CONFIRMED na SELF DECLARED fisadi. Na list ni kubwa..... NYUMBU nyie!!
 
Mh. Magufuli hawa ndio wale mahodari wa kudokoa mstari mmoja wa biblia na kuufanyia kazi badala ya kuangalia essence! Yaani Rais asifanye kazi kwa kuwa alisema hamna semina elekezi? Humuhumu mmekuwa mnapiga kelele ooh mawaziri wanakosea na kweli esp. kufukuza wafanyakazi bila mpangilio sasa anawaita kuwaelekeza bado mnalalamika, what do you really want ? Ukweli kabisa hamsomeki!

Nyie CCMscrow mnasomeka vizuri sana. Ona Chenge ni mwenyekiti wenu wa bunge!!
 
Wakati akitangaza Baraza la Mawaziri, Rais Magufuli alisema hakuna haja na hakutafanyika semina elekezi kwao na atakayeshindwa kufanya kazi bila semina elekezi ajiondoe mwenyewe.

Hata hivyo Ikulu imeona umuhimu wa semina hiyo na imeandaa semina elekezi kwa mawaziri wote. Semina hiyo inatarajia kufanyika kesho Alhamisi, Ikulu jijini Dar es salaam.

Tofauti ni kwamba semina elekezi ya JK ilifanyika Ngurdoto, Arusha lakini semina elekezi ya Magufuli inafanyikia Dar es salaam.

Inadaiwa waandaaji wa Semina hii ni Tume ya Maadili
Muhimu sana , maana baadhi ya Mawaziri hawajawahi kuwa watumishi wa umma
 
Wote tunajiaminisha kuwa Tanzania ni nchi tajiri. Tusichojiangaisha kukiwaza ni kuwa Tanzania ni nchi tajiri wa maliasili hata mara 100 kuizidi Uingereza au mara 50 kuizidi Botswana huku tukisahau kuwa utajiri mkubwa ni wa akili.
Siku tutakayogundua kwamba hata nchi yote ikiwa jangwa lakini ina watu (tena wachache tu) wenye utajiri wa akili ndipo tutaacha ngonjera za elimu bure, mapinduzi ya viwanda na kumaliza rushwa pasipo na haki! All the best washiriki wa semina elekezi.
 
Wakati akitangaza Baraza la Mawaziri, Rais Magufuli alisema hakuna haja na hakutafanyika semina elekezi kwao na atakayeshindwa kufanya kazi bila semina elekezi ajiondoe mwenyewe.

Hata hivyo Ikulu imeona umuhimu wa semina hiyo na imeandaa semina elekezi kwa mawaziri wote. Semina hiyo inatarajia kufanyika kesho Alhamisi, Ikulu jijini Dar es salaam.

Tofauti ni kwamba semina elekezi ya JK ilifanyika Ngurdoto, Arusha lakini semina elekezi ya Magufuli inafanyikia Dar es salaam.

Inadaiwa waandaaji wa Semina hii ni Tume ya Maadili
Tume ya maadili wanataka kutoa seminar kwa mawaziri juu ya kuzingatia sheria kazi sababu timuatimua inayofanywa na mawaziri imezidi nyingine hazizingatii sheria hivyo wanahisi baadae serikali itajikuta na mzigo wa kulipa fidia iwapo wengine watagundulika kuwa walionewa. Kila waziri akilala anawaza kesho amtimue nani ili magufuri amuone kwamba mchapa kazi. Na akishampata wa kumtimua fasta anaita vyombo vya habari. Nashangaa kwenye Kila kikao ambapo jipu litatumbuliwa hapohapo kuna waandishi hukosi kuona kinasa sauti cha milardayo.com wanakipenda sana na kukitumia maana habari inarushwa fasta mtandaoni na kwenye instagram na twitter page za milardayo. Nilishangaa siku ile mwigulu nchemba kaenda kutumbua jipu kule machinjioni usiku saa kumi na mvua inanyesha lakini wakati anaongea kuna kinasa sauti cha milardayo.com nikasema duh hii kali. Siku alipoenda kwenye mgogoro was wakulima mvomero nikashangaa muda huohuo yeye mwenyewe nchemba kamtumia picha milardayo kwenye twitter page na kumwambia milardayo tayari nimewasili tukioni mvomero. Picha kibao. Sahivi wana staili ya kutembea na wapiga picha wao kabisa. Uwaziri mtamu sana kumbe.Ila wengine wanakurupuka mno katika timuatimua.
 
Ni kweli maana kina Kairuki wanatumbua bila staha..........
Huyo ndio yule alimtumbua mkuu wa chuo cha utumishi wa umma bila ganzi? Hahaha nilicheka lakini pia nilihuzunika mzee katumbuliwa jipu live hapohapo huku akiwa amekaa meza kuu kama mkuu wa chuo. Ili mradi tu social media ipate taarifa haraka. Kwanini asimfukuze kwa barua kimyakimya?
 
Shida hapa ni moja. Yaani baba akiwa kichaa sio ajabu kuona anazaa watoto wendawazimu. Waliangalizia alivyokuwa anafukuza JPM na wao wanaiga. Kumbe ukiIga kunya kwa tembo..........
Hata hivyo kama JPM tamko aliloitoa ndani ya ya miezi minne tayari amelitengua anapaswa kujitafakari. Siujui atatengua matamko mangapi kabla ya kumaliza miaka mitano? Hizi ndo taabu za kukurupuka. JPM tatizo lake hatakagi ushauri wala kutulia hata kama tunajua kuwa ana tatizo fulani kichwani. Kwani hakutambua kwamba kwa bunge aliloingia nali wengi wao si wazoefu wa majukumu aliyowapangia? Uzoefu alitaka waupate wapi wakatri waliokuwa mawaziri wengi waliangushwa kifo cha mende na utawala wao wa Kikwete!!!! awamu hii kazi ipo. Ila ninachojua CCM ni ile ile tuuuuuu!
 
Wakati akitangaza Baraza la Mawaziri, Rais Magufuli alisema hakuna haja na hakutafanyika semina elekezi kwao na atakayeshindwa kufanya kazi bila semina elekezi ajiondoe mwenyewe.

Hata hivyo Ikulu imeona umuhimu wa semina hiyo na imeandaa semina elekezi kwa mawaziri wote. Semina hiyo inatarajia kufanyika kesho Alhamisi, Ikulu jijini Dar es salaam.

Tofauti ni kwamba semina elekezi ya JK ilifanyika Ngurdoto, Arusha lakini semina elekezi ya Magufuli inafanyikia Dar es salaam.

Inadaiwa waandaaji wa Semina hii ni Tume ya Maadili
Serikali yaanza kutoa semina elekezi kwa maafisa watendaji wakuu wa serikali, maafisa waandamizi wa serikali kuu... Simu.TV - HABARI - FEBRUARI 8 | CH10 | Facebook
 
Bora wapewe hiyo semina elekezi manake walizidi sifa sana , kukurupuka na kufukuza watu kazi hawajui hata mipaka ya kazi zao. Naona baada ya semina watabadilika sana.
 
Semina elekezi kimvuli kwa mawaziri kimvuli itafanyika nyumbani
 
Kama seminar elekezi zimeanza kwa mawaziri tusubiri tuu, watumishi wote tutapata seminar elekezi tena kwa posho za vikao za kutosha tutakula na kunywa pia.... hii ndio ccm
 
Back
Top Bottom