Rais Samia kuzindua Mkutano mkubwa wa Kilimo Afrika- Ikulu Dar es Salaam

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
325
414
Leo Ijumaa (Machi 17), Rais Samia Suluhu Hassan atazindua maandalizi ya mkutano mkubwa wa kilimo Ikulu, Dar es Salaam na hii ni kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Zuhura Yunus.

Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutano huo mkubwa wa Afrika wa masuala ya chakula na kilimo utakaofanyika Septemba 5 mpaka 8 mwaka huu.

Mkutano wa Afrika wa chakula wa Septemba unatarajiwa kuhudhuriwa na watu takribani 3,000 kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika na duniani, ikiwemo marais, mawaziri na wakuu wa taasisi za kimataifa.

Mkutano huo utaweka msisitizo kwenye Vijana na Wanawake kama Msingi wa Mfumo Endelevu wa Chakula.

Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano huo kutokana na hatua kubwa za kimageuzi ambazo serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imezichukua tangu alipoingia madarakani miaka miwili iliyopita.

Hatua hizo ni pamoja na kuongeza bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mara nne kwa mwaka wa fedha 2022/2023, jambo ambalo halijawahi kutokea tangu tupate uhuru.

Serikali ya Rais Samia pia imetambuliwa kwa mradi wake wa ubunifu wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT), ambao unalenga kuwawezesha vijana, ambao ndiyo nguvu kazi kubwa nchini, kuingia katika kilimo.

Serikali yake pia imewekeza kwenye miundombinu ya umwagiliaji, huduma za ugani, pembejeo na ruzuku ya mbolea na mbegu kwa viwango ambavyo havijawahi kufanyika miaka ya nyuma.

Serikali ya Rais Samia pia imekuwa ikitekeleza mpango wa kilimo unaojulikana kama Ajenda 10/30 yenye lengo la kufanya kilimo kiwe cha biashara na kikue kwa wastani wa asilimia 10 kwa mwaka ifikapo 2030.
 

Attachments

  • IMG-20230315-WA0000.jpg
    IMG-20230315-WA0000.jpg
    66.5 KB · Views: 5
  • IMG-20230315-WA0001.jpg
    IMG-20230315-WA0001.jpg
    66.2 KB · Views: 4
  • IMG-20230315-WA0003.jpg
    IMG-20230315-WA0003.jpg
    166.8 KB · Views: 4
  • IMG-20230315-WA0002.jpg
    IMG-20230315-WA0002.jpg
    279.6 KB · Views: 4
  • IMG-20230315-WA0004.jpg
    IMG-20230315-WA0004.jpg
    265.7 KB · Views: 3
Huyu mama kumbukizi haimhusu ila najua 2025 match 17 lazima aje chato kuwahadaa wanakanda kupata kura za huruma


USSR
Sidhani kama CCM au Chadema kuna chama kinataka kura za hao Sukuma gang, bora wangeanzisha chama chao
 
Serekali yetu ifanye kampeni maalum ya upandaji miti around all the area ambapo mwl. Nyerere dam inajengwa kwa haraka sana, naona hali ya hewa imebadilika kweli kweli, it's not a jokes
 
Anatengua ndugu zao kila siku anaweka Pwani na Zanzibar, watakuwa wajinga sn huo ndiyo ukweli.
Halafu hii ni hatari tuwe macho watanganyika hawa watu sio wazuri kwetu wana chuki na sisi wakidai nchi ina asili ya kwao Nyerere ndo aliibadilisha sasa huyu mama asije akatumika kuirejesha kiaina maana teuzi zake zina walakini.
 
Halafu hii ni hatari tuwe macho watanganyika hawa watu sio wazuri kwetu wana chuki na Sisi wakidai nchi ina asili ya kwao Nyerere ndo aliibadilisha sasa huyu mama asije akatumika kuirejesha kiaina maana teuzi zake zina walakini
Mpaka huwa najiuliza inamaana waislam hawafanyi makosa? tenguzi zote ni wakristo pekee
 
Back
Top Bottom