uttoh2002
JF-Expert Member
- Feb 3, 2012
- 19,703
- 37,930
Leo lissu sincerely kageuka kuwa
Leo Lissu sincerely kawashauri hawa jamaa jambo la maana, kama ambavyo siku zote hawataki kusikia hii move ni mbaya kweli.
Haya ni maoni yangu.
Kwa yaliyotokea leo mahakamani ni kana kwamba mawakili wa serikali wanahisi ushahidi unaotolewa na mashahidi wa upande wao hauwezi kumtia hatiani Lissu, hivyo wameamua kutaka kuingiza ushahidi unaohusu Octoba 29, kwa nia ya kuongeza substance ya kumkuta Lissu na hatia.
Mi ninachoona hapa ni kama vile samaki anaweza kukaangwa kwenye mafuta yake mwenyewe. Maana hata kama mimi sio mwanasheria, lakini najua hii move itakuwa imempa pumzi kubwa sana Lissu ya kufichua mambo ambayo serikali kwa hii miezi minne wamekuwa wakipambana kuyaficha.
Lakini kingine ambacho serikali wanapaswa kutambua ni kwamba: ICC wanaonekana kucheza blind game, kwa kuonekana kwamba hawajayaona yaliyotokea Tanzania, na ni kama hii blind game inaenda ikifanikiwa kwasababu sasa ni kama serikali wanataka kukiweka kila kitu hadharani kupitia kesi ya Lissu.
Na kwa kweli mimi sio mwanasheria nguli, ila the moment mahakama itakubali huu ushahidi mpya wa Octoba 29 uingie mahakamani, sio tu ufawafanya watanzania mamilioni waanze kuifuatilia hii kesi, bali pia jumuiya ya kimataifa (ukijumuisha ICC) watakuwa wamepata mwanya wa kufanya validation ya ushahidi wowote ule ambao ulitumwa kwao.
Kwahiyo hii move ya kina Katuga, is not well thought. Madhara yake yatakuwa na mwangwi ambao hawatautarajia. Si kwasababu pia itamruhusu Lissu kuja na mashahidi wake wa kilichotokea Octoba 29 au?
Kwa hii move, mawakili wa serikali mtakuwa mmefanya sabotage kwa serikali ya CCM, lazima ita-back-fire kwa namna ambayo hamtaipenda.
Wenu,
MC
Leo Lissu sincerely kawashauri hawa jamaa jambo la maana, kama ambavyo siku zote hawataki kusikia hii move ni mbaya kweli.