Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,871
- 155,834
MAUAJI YA MAHMOUD AL-MABHOUH
MMOJA WA VIONGOZI WA KUNDI LA HAMAS LA PALESTINA:
SEHEMU YA KWANZA:
Mahmoud al-Mabhouh (kwa Kiarabu: محمود المبحوح, Maḥmūd al-Mabḥūḥ); alizaliwa tarehe 14 Februari mwak 1961 – na kuuawa tarehe 19 Januari mwaka 2010, katika mauaji yaliyofanyika katika chumba cha hoteli huko Dubai.
Al-Mabhouh— mwanzilishi mwenza wa Izz ad-Din al-Qassam Brigades, tawi la Kijeshi la Hamas—alikuwa anatafutwa na serikali ya Israeli kwa kuwateka na kuwaua askari wawili wa Israeli mwaka 1989 pia akihusika na ununuzi wa silaha kutoka Iran kwa ajili ya kutumika huko Gaza; hii ilikuwa sababu kubwa ya kuuawa kwake.
Mauaji yake kwa sehemu yaliutikisa ulimwengu hii ni kutokana na madai kwamba yaliamrishwa na serikali ya Israeli na kutekelezwa na mawakala wa Mossad wakitumia udanganyifu na hati za kugushi za kusafiria kutoka nchi mbalimbali za Ulaya na Australia.
Picha za washukiwa 26 na majina yao mara moja ziliwekwa katika orodha ya watu wanaotafutwa na Interpol.
Polisi wa Dubai waligundua kuwa washukiwa 12 walitumia hati za kusafiria za Uingereza, huku washukiwa wengine sita walitumia hati za Ireland, wanne za Ufaransa, mmoja ya Ujerumani, na watatu za Australia. Interpol na polisi wa Dubai waliamini kuwa washukiwa hao waliiba vitambulisho vya wahusika halisi, hasa Waisrael wenye uraia wa nchi mbili. Wapalestina wawili, ambao Hamas iliamini kuwa ni maafisa usalama wa zamani wa Fatah na ambao kwa wakati huo walikuwa wameajiriwa na Fatah kama maafisa waandamizi, walitiwa mbaroni jijini Dubai, kwa kushukiwa kuwa mmoja wao aliandaa mazingira ya kilojistiki kwa timu ya wauaji. Pamoja na madai hayo ya Hamas, mamlaka za Dubai hazikusema chochote kuhusiana na tukio hilo au kuwatambua Wapelestina hao wawili waliokuwa wanashukiwa.
Kulingana na ripoti ya mwanzo, Al-Mabhouh alileweshwa kwa madawa, kisha akapigwa na shoti ya umeme na kukabwa. Luteni Jenerali Dhahi Khalfan Tamim wa jeshi la polisi Dubai Alisema washukiwa walimfuatilia Al-Mabhouh Dubai toka akiwa Damascus, nchini Syria. Waliwasili kutokea sehemu mbalimbali za Ulaya na kukaa hoteli tofauti, bila shaka kukwepa kugundulika na ukiondoa washirika wake watatu wanaoshukiwa kuwa "walisaidia kutengeneza mazingira" ambao waliondoka kwa boti kwenda Iran miezi kadhaa kabla ya mauaji, washukiwa wengine wote walitawanyika baada ya mauaji kwenda nchi mbalimbali.
Mkuu wa polisi wa Dubai alisema ana uhakika wa asiliana 99% kwamba mauaji yale ilikuwa ni kazi ya Mossad wa Israel. Tarehe 1 Machi mwaka 2010, alieleza kwamba alikuwa na "uhakika" kwamba wale wote wanaoshukiwa kufanya mauaji hayo walikuwa wamejificha nchini Israel.
Alisema kwamba Dubai wataomba hati ya kumkamata Meir Dagan, Mkuu wa Mossad, iwapo itathibitika kwamba Mossad ilijihusisha na kuwajibika na mauaji hayo. Uongozi wa Hamas nao ulisema Israel inahusika, na wakaapa kulipiza kisasi. Hamas, ambao wao binafsi walikuwa katika orodha ya Marekani kama taasisi ya kigaidi ya kigeni, pia kuorodheshwa na Jumuia ya nchi za Ulaya kama taasisi ya kigaidi ya kigeni, na pia kuchukuliwa kama taasisi ya kigaidi na serikali za Israel, na Japan, na kuchukuliwa kama tawi la Kijeshi na serikali za Uingereza na Australia, waliomba kwamba Israel nayo ijumuishwe katika orodha ya magaidi na Jumuia ya Ulaya kwa sababu ya kuhisiwa kwamba Israel walihusika na mauaji hayo.
Hata hivyo, baadaye mwezi Machi, Mkuu wa polisi wa Dubai alisema, "Sasa nina uhakika kabisa kwamba walikuwa Mossad", na akaendelea kusema "Nimempelekea Mwendesha Mashtaka wa (Dubai) maombi ya kumkamata (Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin) Netanyahu na Mkuu wa Mossad" kwa mauaji. Khalfan alisema pia kuwa Mshirika mmoja wa Hamas aliwapa maelezo Mossad. Hii ilikanushwa na Hamas ambao waliilaumu Fatah kwa kuisaidia timu ya wauaji ya Mossad.
Mwezi Machi, mwaka 2010, Waziri wa Mambo ya nchi za Nje wa Uingereza, David Miliband, alimfukuza nchini humo afisa ubalozi wa Israeli baada ya Wakala wa Makosa ya Uhalifu nchini Uingereza kugundua kuwa Israel waligushi nakala za hati za kusafiria za Uingereza.
Tarehe 24 May, mwaka 2010 serikali ya Australia ilimfukuza nchini humo afisa ubalozi wa Israeli baada ya kujiridhisha kwamba "bila shaka yoyote ile Israel ilikuwa nyuma ya mpango wa kugushi hati nne za kusafiria za Australia" zilizohusiana na mauaji hayo. Hatua kama hiyo ilichukuliwa pia na Ireland. Israel ilikataa kusema chochote kwa namna walivyokuwa wanashitumiwa kwamba vyombo vyake vya usalama vilikuwa nyuma ya mauaji hayo.
Tarehe 30 Septemba mwaka 2010, Mkuu wa polisi wa Dubai Dahi Khalfan alisema kwamba amepokea vitisho vya kuuawa kutoka kwa wakala mmoja wa ujasusi wa Israel Mossad wakimuhusisha na kitendo chake cha kufichua mipango yote ya mauaji ya al-Mabhouh, lakini pamoja na kwamba hali hiyo ilitokea ilibaki bila uthibitisho.
MAUAJI YA MAHMOUD AL- MABHOUH:

SEHEMU YA PILI:
Wasomaji wapendwa leo tunaendelea na sehemu ya pili kuhusu mauaji ya al Mabhouh mmoja wa viongozi wakuu wa kundi la Hamas.
Kama tulivyokwishakuona katika sehemu ya kwanza kuwa tarehe19 Januari, mwaka 2010, al-Mabhouh aliuawa katika chumba chake alichokuwa amepanga katika hoteli jijini Dubai, baada ya kuwa amefuatiliwa na washukiwa karibu 29 (huku washukiwa 26 ambao picha kutoka kwenye hati zao za kusafiria zikiwa zimetolewa hadharani, ambapo Wapalestina wawili walitiwa mbaroni, pamoja na mshukiwa mwingine ambaye hakujulikana jina lake naye alikamatwa pia), hao washukiwa 26 walibeba hati za kusafiria za kugushi na zenye udanganyifu kutoka sehemu mbalimbali za mataifa ya Ulaya.
Gazeti la Sunday Times liliripoti kuwa uondokaji wa al-Mabhouh kutoka Damascus kwenda Dubai katika ndege ya Emirates Flight namba 912 saa 4:05 asubuhi ya siku ya tarehe 19 Januari, mwaka 2010 ulikuwa unafuatiliwa na wakala wa ujasusi aliyekuwa chini pale uwanja wa ndege jijini Damascus.
Salah Bardawil, Mbunge wa Hamas, alisema al-Mabhouh alijiweka mwenyewe katika hatari kwa kufanya booking ya safari yake online mtandaoni na kuwajulisha familia yake huko Gaza kwa njia ya simu hoteli ambayo angefikia na kukaa katika safari yake hiyo.
Licha ya ripoti kwamba al-Mabhouh alisafiri kwa hati bandia ya kusafiria yenye jina bandia la "Mahmoud Abdul Raouf Mohammed", Hamas na maofisa wa Dubai walisisitiza kwamba al-Mabhouh aliingia katika nchi hiyo kwa utambulisho wake halisi saa 9:15 alasiri.
Kawaida al-Mabhouh angekuwa analindwa na walinzi wake, lakini kuwasili kwao kulicheleweshwa kwa sababu walinzi hawakupata tiketi katika ndege ile aliyopanda Boss wao, kwakuwa "Hakukuwa na chumba kwa ajili yao katika ndege," alisema Talal Nasser, msemaji wa Hamas jijini Damascus. "Kwa hiyo, alisafiri peke yake, na walinzi wa usalama walitegemewa kujiunga naye siku inayofuta."
Kwa mujibu wa makala ya gazeti la Ufaransa la Le Monde wakimnukuu afisa mwandamizi wa shirika la ujasusi la Ufaransa, Mossad walipanga mipango ya kumuua Mabhouh nje ya Paris. Mossad inadaiwa waliweka zamu na kituo cha kumdhibiti katika hotel kwenye kitongoji cha Bercy nje kidogo ya jiji la Paris wakiwa wametegesha kompyuta na simu za usalama.
Mkuu wa Polisi wa Dubai, Luteni Jenerali Dahi Khalfan Tamim, alieleza kwamba al-Mabhouh alipowasili Dubai alikuwa safarini kuelekea China. Alipowasili Dubai, al-Mabhouh alichukua taxi kwenda Al Bustan Rotana Hotel na alipanga chumba namba 230. Aliomba chumba ambacho kisichokuwa na kibaraza na dirisha lililozibwa, hivyo hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kuingia kupitia sehemu hizo bali kwa kupitia mlangoni tu. Aliondoka hotelini kati ya saa 10:30 na 11:00, jioni baada ya kama ya saa moja hivi toka alipowasili hotelini. Nini alifanya katika muda wa masaa matatu au manne yaliyofuatia inabaki kutokujulikana.
Mkuu wa Polisi wa Dubai alisema hakukutana na mtu yeyote katika emirate na kuwa alikwenda kufanya manunuzi tu. Wakati huo huo, timu ya wauaji walivunja na kuingia katika chumba chake. Saa 2:24 usiku al-Mabhouh alirudi chumbani, na mara nusu saa baadaye alishindwa kujibu simu kutoka kwa mkewe.
Picha kutoka kwenye kamera za usalama za hotelini zilitolewa kwa jamii kuwaonyesha washukiwa, ambao waliwasili katika ndege tofauti, na namna walivyokutana hotelini. Wakati inaonekana washukiwa waliamua kutumia vifaa binafsi vya mawasiliano miongoni mwao ili kukwepa kufuatiliwa, washukiwa hao ilidaiwa na polisi wa Dubai kutuma na kupokea ujumbe wa SMS kwa namba za simu nchini Austria. Wakati al-Mabhouh alipowasili kwenye mida ya saa 9:00 alasili, washukiwa wawili waliovalia mavazi ya tennis walimfutilia katika ukumbi ili kugundua chumba alichopanga, na pia kujua namba ya chumba hicho.
Maelezo ya Polisi wa Dubai yalidai kuwa mawasiliano yalikuwa yanafanyika na mtu wa kati (third party), ambaye alipigiwa simu kutoka hoteli tofauti na kuambiwa apange chumba 237. Kwa mujibu wa video za usalama, mtu aliyepanga chumba 237 hakuingia chumbani, lakini alionekana akimpa funguo za chumba mshirika aliyekuwa sehemu ya mapokezi ya hoteli, na mara moja akaondoka Dubai, kabla ya mauaji. Al-Mabhouh, baadaye, alitoka hotelini na wakati baadhi ya washukiwa wakiwa wamebaki wanamuangalia, ilifikiriwa kwamba mshukiwa (washukiwa) walijaribu kuweza kuingia kwenye chumba chake.
Mshukiwa mmoja aliyekuwa anaangalia alionekana kwenye video akimchelewesha mtalii mmoja aliyekuwa anataka kutoka katika lifti katika gorofa ya pili kwa wakati huo, bila shaka kuwapa nafasi watu wengine katika timu hiyo kufanya tukio. Wakati huohuo mshukiwa mwingine ilidaiwa alikuwa anamchanganya mtalii mwingine na, kwamba washukiwa wanne waliingia kwenye chumba cha muhanga na kumsubiri arudi. Ushahidi wa hili ni ukweli kuwa watu wanne waliwasili kwa lifti na kuingia njia ya ukumbini ambako chumba cha muhanga na chumba cha wauaji ndiko vilikokuwa kwa wakati huo, na watu walewale wanne walionekana wakiondoka baada ya mauaji kufanyika.
Shuguli ya usomaji ambayo ilifanyika katika vyumba vya milango ya kufuli za elektroniki za hoteli ilionyesha kwamba kulikuwa na jaribio lililofanywa kuvuruga programu ya kufuli la mlango wa elektroniki wa al-Mabhouh kwa wakati huo. Wachunguzi waliamini kwamba kufuli la elektroniki katika mlango wa al-Mabhouh huenda programu yake ilivurugwa na hivyo wauaji kuweza kuingia katika chumba chake kwa njia hiyo. Makufuli kama ya VingCard Locklink brand, yanaweza kuingiliwa na program zake kuvurugwa moja kwa moja kwenye mlango wa chumba cha hoteli.
Kwa mujibu wa Polisi wa Dubai, alifariki kwenye muda wa saa 3:00 usiku huo. Tarehe 20 Januari, mwaka 2010, siku iliyofuata, mfanya usafi wa hoteli alijaribu kuingia chumbani, lakini akakuta mlango umefungwa kutokea kwa ndani. Kisha mtu wa usalama wa hoteli aliitwa ili kuufungua mlango. Baada ya mlango kufunguliwa, mwili wa al-Mabhouh uligunduliwa kwenye kitanda. Kwenye droo karibu ya kitanda, waliweka chupa ndogo ya dawa kuonyesha kana kwamba amekufa tu kifo cha kawada.
Pichani ni chumba kimojawapo cha hoteli ya Al Bustan Rotana Hotel, Dubai nchini United Arab Emirates.
Itaendelea sehemu ya tatu.
Maka Patrick Mwasomola,
Karakata,
Uwanja wa ndege,
Dar es salaam.
Tanzania.