Shenkalwa
JF-Expert Member
- May 3, 2011
- 580
- 132
Huko Tengeru Arusha, Binti mmoja wa miaka 33 amemuua baba yake na kumcharanga kwa panga na shoka vipandevipande kisha akamdumbukiza katika choo cha shimo siku ya Jumapili iliyopita. Alifikia uamuzi huu baada ya baba huyo kumkatalia binti huyo kuuza sehemu ya shamba lao ili akanunue corolla. Baada ya kuhojiwa aliko baba yake, binti huyo alidai 'baba kenda samunge kupata kikombe', lakini majirani baada ya siku mbili tatu walishtushwa na harufu kali kutoka katika choo cha wanafamilia hao na kulazimika kuripoti polisi tukio hilo. Polisi na wanausalama walifika eneo hilo na kuanza kazi ya kukifumua na ndipo walipobahatika kuopoa mguu na mkono; kazi bado inaendelea.
Source: MATUKIO - WAPO FM
Kulingana na maelezo ya humu jf huyo binti (mwanamke) hana makosa. Kama alishawahi kuua mwanae kwa kumnyonga na akafukuzwa kwa mumewe hapana shaka amekuwa akiendeleza vitendo vya kiuwendawazimu. Kwa hiyo wale wa karibu naye walipaswa kuchukua tahadhari katika kuishi na mtu wa namna hii ambaye inaonyesha wazi kuwa wakati mwingine akili zinamzidi kiasi cha kutojua akifanyacho. Na kama alishawahi kuua mwanae uraiani alikuwa anangoja nini badala ya kuhifadhiwa kunakohusika?? Hana makosa kwa sababu si yeye ila ni uendawazimu. Hata hivyo inabidi aendelee kuhifadhiwa huko huko ili asije akaua mwingine