Mauaji ya Kutisha Arusha; Binti amuua baba yake

Hossam

JF-Expert Member
Feb 10, 2011
3,410
2,000
Huko Tengeru Arusha, Binti mmoja wa miaka 33 amemuua baba yake na kumcharanga kwa panga na shoka vipandevipande kisha akamdumbukiza katika choo cha shimo siku ya Jumapili iliyopita. Alifikia uamuzi huu baada ya baba huyo kumkatalia binti huyo kuuza sehemu ya shamba lao ili akanunue corolla. Baada ya kuhojiwa aliko baba yake, binti huyo alidai 'baba kenda samunge kupata kikombe', lakini majirani baada ya siku mbili tatu walishtushwa na harufu kali kutoka katika choo cha wanafamilia hao na kulazimika kuripoti polisi tukio hilo. Polisi na wanausalama walifika eneo hilo na kuanza kazi ya kukifumua na ndipo walipobahatika kuopoa mguu na mkono; kazi bado inaendelea.
Source: MATUKIO - WAPO FM
 

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
11,019
2,000
Starehe itamweka matatani mpaka ashange mwenyewe,na nadhani huyo demu ni kabla la KIMERU (sambura)ndiyo wenye mioyo ya namna hii. Reset In Peace mzee we2.
 

JS

JF-Expert Member
Sep 29, 2009
2,066
1,250
sasa gari tu tena corrola ndo unamuua baba yako???alikuwa anafikiria kwa masaburi....too sad. RIP Mzee
 

utantambua

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,370
0
Mambo haya huwa nayaona tu ktk tv reality show inaitwa the first 48. Na nilihadaika kua yanatokea tu marekani ambapo close family members ama friends wanauana kwa kitu kidogo sana. Sasa lipo kwetu hapo arusha duh
 

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,217
2,000
Starehe itamweka matatani mpaka ashange mwenyewe,na nadhani huyo demu ni kabla la KIMERU (sambura)ndiyo wenye mioyo ya namna hii. Reset In Peace mzee we2.
Aroooo, ...Arooooo, ..Aroooo!!!!!!!
Hebu wacha hii maneno bana, una maana gani kuwa ni hilo kabila?
Itabidi tukae kama kamati kujadili kauli hii!
Kuna jirani yangu akisoma hapa ataroga mtu sasa hivi!...ohohhhhooooo!
 

pmwasyoke

JF-Expert Member
May 27, 2010
3,943
2,000
Jamii yetu kwa sasa kwa ujumla inachangia haya kutokea, kwa kuwapa heko sana vijana wanaoibukia na mali kubwa haraka haraka, bila kujiuliza wanavyozipata.
 

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,384
2,000
Wadada na magari ni lazima mujutie tamaa zenu,kama anamuua baba mzazi inakuwaje mpenzi?

Tamaa mbele na mauti..
 

BornTown

JF-Expert Member
May 7, 2008
1,718
1,250
Hii story niliisikia jana jioni kwenye redio wanadai huyo mama(binti muuwaji) alishaolewa kipindi cha nyuma akajaliwa kupata mtoto akamnyonga akafukuzwa kwa mumewe akarudi kwao na alikuwa akiishi yeye na baba yake baada ya mama yake kufariki mwaka 2001. Kuna baadhi ya majirani walikuwa wanaojiwa na mtangazaji walidai huyo dada(binti muuwaji) kuna kipindi anakuwa na matatizo ya akili, kwasasa huyo dada anashikiliwa na polisi akisubiri uchunguzi wa akili yake ili wajue kama ni mzima ama anamatatizo ya akili.

Kiukweli inasikitisha sana huyo Mzee amekufa kifo kibaya na cha mateso makali.
 

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
42,278
2,000
Arusha ni sehemu hatari sana sio mahali pakukaa kwa kipindi hiki.
Huyu jamaa lazima atakuwa mfuasi wa CDM
 

Mamndenyi

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
31,025
2,000
kwanini hakuuza hilo dude lake akanunua gari kama ana ujanja huo, kuliko kumtanguliza baba yake.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom