Mauaji ya Kutisha Arusha; Binti amuua baba yake

Huko Tengeru Arusha, Binti mmoja wa miaka 33 amemuua baba yake na kumcharanga kwa panga na shoka vipandevipande kisha akamdumbukiza katika choo cha shimo siku ya Jumapili iliyopita. Alifikia uamuzi huu baada ya baba huyo kumkatalia binti huyo kuuza sehemu ya shamba lao ili akanunue corolla. Baada ya kuhojiwa aliko baba yake, binti huyo alidai 'baba kenda samunge kupata kikombe', lakini majirani baada ya siku mbili tatu walishtushwa na harufu kali kutoka katika choo cha wanafamilia hao na kulazimika kuripoti polisi tukio hilo. Polisi na wanausalama walifika eneo hilo na kuanza kazi ya kukifumua na ndipo walipobahatika kuopoa mguu na mkono; kazi bado inaendelea.
Source: MATUKIO - WAPO FM

Kulingana na maelezo ya humu jf huyo binti (mwanamke) hana makosa. Kama alishawahi kuua mwanae kwa kumnyonga na akafukuzwa kwa mumewe hapana shaka amekuwa akiendeleza vitendo vya kiuwendawazimu. Kwa hiyo wale wa karibu naye walipaswa kuchukua tahadhari katika kuishi na mtu wa namna hii ambaye inaonyesha wazi kuwa wakati mwingine akili zinamzidi kiasi cha kutojua akifanyacho. Na kama alishawahi kuua mwanae uraiani alikuwa anangoja nini badala ya kuhifadhiwa kunakohusika?? Hana makosa kwa sababu si yeye ila ni uendawazimu. Hata hivyo inabidi aendelee kuhifadhiwa huko huko ili asije akaua mwingine

nimesoma ila nilipoona sababu ya kuua .kweli nimecheka kwa masikitko sana.........

miak 33 bado yuko kwa baba yake?

nimesoma ila nilipoona sababu ya kuua .kweli nimecheka kwa masikitko sana.........

miak 33 bado yuko kwa baba yake?

NDO AKINACHUMAULETE HAWA,SASA KAONA NO DEAL KAMRESTISHA BABAKE IN PEACE,ATANYEA DEBE MPAKA AIONEE MBINGU HAPAHAPA DUNIANI

Money is the root of all evils,utamuuaje binadamu mwenzio tena baba mzazi kisa vijisenti?jamani amani inanunuliwa ukiua amani itakuwa wapi hata ukipata corolla kila ukipanda ile damu itakuwa inakutesa.may God help us.

Mi nalia na wanawake wanaupeo mdogo wa kufikiria anafikiri ukiwa na gari ndo kazi imekwisha swala la gereji anaweka pembeni

Money is the root of all evils,utamuuaje binadamu mwenzio tena baba mzazi kisa vijisenti?jamani amani inanunuliwa ukiua amani itakuwa wapi hata ukipata corolla kila ukipanda ile damu itakuwa inakutesa.may God help us.

Jamani Mamzalendo,ktk hali 2nayoenenda majira haya ya fedha kutawala vichwa vya wa2,hakika hali c shwari hata kidogo ni wa2 wamependa pesa kushinda UTU kama Mtume Paulo alivyowaandikia watu wake ktk kile kurasa ya Waraka wa pili wa Thimoteo ya kwamba hz nyakati kama hv leo inavyoonekana ikifika hakika mjuwe ya kwmb Mwana wa Adam hayupo mbali. NAKWAMBIA YOTE YATAPITA,HATA HL LA HUYU (SAMBURA) lkn neno lililonenwa na manabii litabaki kuwa ndiyo tu. Sanasana cha kufanya ni kumlilia MUNGU ktk haki na kweli. (SAMBURA KWA KIKWE2 KIMERU NI MSICHANA AMBAYE HAJAOLEWA NA HAJAZAA BADO)

Muda huu nipo ndani ya Mahakama Kuu ya Arusha na nikabahati kumwona yule binti aliyemwua gari ya private na kutinga kwa Hakimu lakini ckupata vizuri kusikia tarehe aliyopangia ila Hakimu hakumsomea chochote.

hapo kuna mawili, kama angekuwa hana akili asingeweza kumtupa chooni baada ya kuuwa, wazo la kupanga kuuwa na hatimae kuuwa na kuficha mwili na uwezo wa kusema kaenda samunge kupata kikombe tayari hawezi kuplead insanity. angekuwa kamuuwa kamwacha hapo huku akifanya vituko vya hapa na pale bila kujielewa kafanya nn ingekuwa sawa mahakama ingechukulia alikuwa insane, mfano kwa wale wanaofanya kazi wakiwa usingizini( somnamblism) wanaweza kufanya matendo bila kujijua kama kuuwa, kufua, kuchinja hata mnyama huku wakiwa usingizini, lakini kama kwa kuuwa huko akiwa usingizni akaweza kuficha maiti na vielelezo vya damu basi huyo hawezi kusema kauwa ktk hatua ya kutojifahamu, kwa huyu mwanamke huyu alijua anafanya nn adhabu yake iko wazi kuuwawa kwa kunyongwa hadi kufa,tena upelelezi hauna haja ya kuchukua zaidi ya siku tatu.lkn kwa tz yetu atakaa hata maiak 5 utaambiwa upelelezi bado.

Back
Top Bottom