Mauaji: Nini kinamfanya mtu aamue kuua?

Mauaji: Nini kinamfanya mtu aamue kuua?

Mauaji, nini humfanya mtu aamue kumuua mtu mwingine?

Hivi karibuni tumeona visa vya mauaji vikiongezeka, hasa vile vinavyohusishwa na siasa hapa Tanzania.

Kuna maswali mengi yananijia kichwani

Je, haya mauaji hufanywa na mtu mmoja au huwa ni kundi la watu?

Ni nini hutokea kwenye akili ya mtu mpaka afikie hatua ya kumuua binadamu mwenzake?

Mimi binafsi damu inanitisha

Nikiona damu nyingi napata trauma kabisa

Sasa hawa wanaoua, tena kwa ukatili, huwa hawahisi chochote?

Anapomkata mtu, kumpiga risasi au kumchoma moto, halafu yule mtu anaomba msaada au huruma, kweli moyo hauwaumi?

Baada ya tukio, huwa hawapati mawazo, ndoto mbaya au kujilaumu?

Kuna msemo unasema, Ukianza kula nyama ya mtu huachi
Huo msemo una maana gani?

Kwa nini kuna watu wanaonekana kuua mara kwa mara bila kuacha?

Na ukimuua mtu halafu ukaiona familia yake, watoto wake au wazazi wake wanalia kwa uchungu, hilo halikugusi kabisa mpaka ukaweza kuendelea kufanya mauaji mengine?

Ukiachana na kesi ambazo mtu anahukumiwa na mahakama kwa mujibu wa sheria (na si kwa kusingiziwa), hawa wanaoua kiholela huwa hawana utu?

Hawana huruma? Hawana dhamiri? Au kuna kitu kinabadilika kwenye akili yao mpaka wanaona kuua ni jambo la kawaida?

Kila mtu atakufa siku moja(Haki hii)

Sasa kwa nini umpe mtu maumivu ya kukatwa, kupigwa risasi au kuchomwa moto wakati angekufa kwa wakati wake?

Kwa mtazamo wenu, nini hasa kinamsukuma mtu kuwa muuaji? Ni malezi, mazingira, siasa, pesa, chuki, magonjwa ya akili au kuna kitu kingine?

Karibuni kwa hoja

ShesRise_1 🤚
Miaka ya nyuma nikiwa mdogo nasoma Kuna Mzee wa makamo ( kijana Mzee)ambae alikuwa ni jirani yetu, yeye alikuwa ni muuaji wa kukodisha( ndio kazi yake) jamaa huyu alifahamika na baadhi ya watu pale kijijini kwa kazi yake hiyo. Matukio yake mengi alikuwa akiyafanya sehemu za mbali hasa huko maeneo ya usukumani.

Alikuwa akikodiwa kuua watu ambao wamefanyiana visasi, kutuhumiana mambo ya kishitikina, kudhulumiana mashamba, Biashara n.k
Sasa basi watu hawa hawana huruma hata kidogo, kwani wao wanajiona wapo kazini na wanatimza wajibu wao kama wewe uendavyo kazini kwako na kutimiza wajibu wako.

Mzee huyo alikuwa na familia kamili, mke na watoto hakuwa na kazi nyingine zaidi ya hiyo na familia yake ilitegemea kazi hiyo ya BABA " nadhani sasa unaweza kunielewa"

Mfano wewe mtoa mada siku ukikosa kazi na usiwe na pesa ya kuhudumia familia yako unajisikiaje? Ukipata dili la pesa je??

Kazi Yao ni Moja tu kuuwa tu bila kuuliza sababu.
We waone watu wanatembea hivi barabarani mnasalimiana mnacheka lkn ungewajua walivyo......!!
 
Swali fikirishi kaka
Wewe unaonaje namna gani ya kumzuia mtu asifikie maamzi ya kuua
Hapa ni lazima tushughulike na root causes, yani mfumo mzima unaoleta sababu za mauaji (chuki binafsi, visasi, itikadi n.k).

Waatu wengi ambao huwa wanaingia kwenye violence huwa wamezungukwa na mazingira ya chuki, vurugu, au propaganda zinazohalalisha ukatili, mazingira yakibadilika, uwezekano wa vitendo vya kikatili kutokea huwa unapungua kwa kiwango kikubwa.

Issue pia ni kwamba pale ambapo sheria ni dhaifu au hazitekelezwi, uwezekano wa vitendo vya kikatili kushamiri ikiwa ni pamoja na mauaji yenyewe ni mkubwa sana kwa sababu uwajibikaji hakuna.

Hobbes aliwahi kusema ukosefu wa sheria madhubuti huwa unapelekea state of fear , yani kila mtu anakuwa na haki ya kujichukulia sheria mkononi, lakini ikiwa sheria zinatekelezwa na adhabu kali kutolewa kwa wanaofanya vitendo hivyo, mauaji yatapungua kwa kiwango kikubwa sana.
 
Miaka ya nyuma nikiwa mdogo nasoma Kuna Mzee wa makamo ( kijana Mzee)ambae alikuwa ni jirani yetu, yeye alikuwa ni muuaji wa kukodisha( ndio kazi yake) jamaa huyu alifahamika na baadhi ya watu pale kijijini kwa kazi yake hiyo. Matukio yake mengi alikuwa akiyafanya sehemu za mbali hasa huko maeneo ya usukumani.

Alikuwa akikodiwa kuua watu ambao wamefanyiana visasi, kutuhumiana mambo ya kishitikina, kudhulumiana mashamba, Biashara n.k
Sasa basi watu hawa hawana huruma hata kidogo, kwani wao wanajiona wapo kazini na wanatimza wajibu wao kama wewe uendavyo kazini kwako na kutimiza wajibu wako.
Yaani anapokua anatekeleza mauwaji anajiona yupo kazini😳
Mzee huyo alikuwa na familia kamili, mke na watoto hakuwa na kazi nyingine zaidi ya hiyo na familia yake ilitegemea kazi hiyo ya BABA " nadhani sasa unaweza kunielewa"
Mtoto: baba yupo kazini🙌
Mfano wewe mtoa mada siku ukikosa kazi na usiwe na pesa ya kuhudumia familia yako unajisikiaje? Ukipata dili la pesa je??
Nipewe dili sawa ila sio la kuua mtu
Chombezo : kuna dili lolote saivi sina pesa😂( jokes
Kazi Yao ni Moja tu kuuwa tu bila kuuliza sababu.
We waone watu wanatembea hivi barabarani mnasalimiana mnacheka lkn ungewajua walivyo......!!
Bora mengine tusiayajue kuna gharama ya kujua mambo
 
Hapa ni lazima tushughulike na root causes, yani mfumo mzima unaoleta sababu za mauaji (chuki binafsi, visasi, itikadi n.k).

Waatu wengi ambao huwa wanaingia kwenye violence huwa wamezungukwa na mazingira ya chuki, vurugu, au propaganda zinazohalalisha ukatili, mazingira yakibadilika, uwezekano wa vitendo vya kikatili kutokea huwa unapungua kwa kiwango kikubwa.

Issue pia ni kwamba pale ambapo sheria ni dhaifu au hazitekelezwi, uwezekano wa vitendo vya kikatili kushamiri ikiwa ni pamoja na mauaji yenyewe ni mkubwa sana kwa sababu uwajibikaji hakuna.
Una utu na utulivu bro umeeleweka mnoo respect 🙏
Hobbes aliwahi kusema ukosefu wa sheria madhubuti huwa unapelekea state of fear , yani kila mtu anakuwa na haki ya kujichukulia sheria mkononi, lakini ikiwa sheria zinatekelezwa na adhabu kali kutolewa kwa wanaofanya vitendo hivyo, mauaji yatapungua kwa kiwango kikubwa sana.
Wenye dhamana wanatakiwa kufanya jambo asante sana
 
Mimi kwenye kafara natofautiana na wewe. Itokee nimepewa masharti nimtoe kafara adriz de mbusii ama mdogoee Jagina Al-mukheef Tanganian Malaria 2 wala sisiti chinja nakuwawahisha faster kwa Mudi huko.
Zawadi yako hii

Zawadi yako hii

Hahahahahaaaaa wee jamaa
 
Back
Top Bottom