Mauaji: Nini kinamfanya mtu aamue kuua?

Mauaji: Nini kinamfanya mtu aamue kuua?

Ukifanya uhaini, ukaanza kuchoma mali za watu, kuiba mali za watu, kukata watu vidole

Wewe umevuka mipaka ya kuendelea kubaki hai unastahili kupigwa risasi na maiti yako ikatupwe mbali isionekane maana unakua ni laana hapa duniani.
 
CCM NI WAPUMBAVU SANA MKUU, LAKINI NITAKUJIBU KWA KIFUPI ANAEVUNJA UTULIVU/AMANI NA MAUAJI....

1. Anayeteka watanzania Wenzetu akina Soka, Polepole, Mdude, Chaula nk.

2. Anayepiga watu Risasi Akina TUNDU LISSU, SATIVA AKWILINA MAWAZO NK

3. Anayezuia haki ya Kikatiba ya Mikitano ya Vyama vya siasa.
(Kushiriki mikutano ya hadhara na Mikutano ya ndani.

4. Anayezuia Maandamano ambayo ni haki ya kikatiba ya Tanzania.

5. Anayezuia na Kupora Haki ya watanganyika ya kuchagua kiongozi wanaye mtaka.

6.Anayeficha Kila aina ya mikataba, Bandari, Ardhi, Dhahabu, Gesi nk.

7. Anayekandamiza uhuru wa vyombo vya Habari

CCM WAMETUONA WATANGANYIKA NI MALOFA SANA


AMKENI WATANGANYIKA.
Sawa
 
Mauaji husababishwa na mchanganyiko wa sababu za kisaikolojia, kijamii, mazingira, na kibaolojia ambazo humfanya mtu aone kuwa kutoa uhai wa mwingine ndiyo njia pekee au ya mwisho ya kutatua tatizo au kukidhi haja yake.

Hakuna sababu moja tu inayomfanya mtu aamue kumuua mtu mwingine, bali mara nyingi ni mkusanyiko wa shinikizo mbalimbali za ndani na nje.
Ooh sawa baada ya kufanya mauwaji je muuwaji hua hahisi hatia ?
Akiua anapata amani?
Na hata hajutii?
 
Jibu hili hapa "Ni malezi, mazingira, siasa, pesa, chuki, magonjwa ya akili"...
So hakuna majuto kwa muuaji ?

Maana mtu ameua mara moja then again and again 🤔
 
MONEY
POWER

RESPECT

Vyote kwa pamoja hapo juu ni sababu kubwa kwa mauaji ya kisiasa.
Hakuna namna nyingine bila kudhulumu uhai wa wengine?

Kuua wengine ili upate vyote hivyo ni roho mbaya au ubinafsi?
 
Ukifanya uhaini, ukaanza kuchoma mali za watu, kuiba mali za watu, kukata watu vidole

Wewe umevuka mipaka ya kuendelea kubaki hai unastahili kupigwa risasi na maiti yako ikatupwe mbali isionekane maana unakua ni laana hapa duniani.


Sheria inasemaje kuhusu watu hao unaosema hapa?

Wanauwawa kimya kimya au wanatakiwa kufikishwa kwenye vyombo vya Sheria?
 
Watu wana roho ngumu,,, 2022 kuna mauwaji yalitokea huko katavi ya watu wawili kukatwa shingo, huezi amini alifanya unyama alishiriki mpaka kuchimba kaburi. Baada ya siku 3 ndipo aligundulika kua ye ndie kauwa.
Walipogundua alishiriki watu
Walichukua hatua gani

Ova
 
Ooh sawa baada ya kufanya mauwaji je muuwaji hua hahisi hatia ?
Akiua anapata amani?
Na hata hajutii?
Huyo aliyetumwa kuua
Ataishi kwa kuona maluweluwe mpaka mwisho wake
Hebu jaribu kutafuta,documentary ya "the ice Man" j.klukinski
Akihojiwa akiwa jela,alikuwa anatumwa na mafia boss kufanya kazi zao za kuua
Huyu malezi yake pia yalichangia kuwa hivyo,ila jamaa alikuwa ana ukichaa kichwani
Alikuwa ana mwambia mwandishi,mara nyingi huwa anaona maluweluwe
Sema na yeye alikuja kufia jela

Ova
 
Kwa mtazamo wenu, nini hasa kinamsukuma mtu kuwa muuaji? Ni malezi, mazingira, siasa, pesa, chuki, magonjwa ya akili au kuna kitu kingine?

Karibuni kwa hoja
Hoja gani mkuu 'ShesRise', maana naona umechanganya maharage, makande, njegere, wali,n.k., ndani ya dishi hilo moja.

Maana yako ya "muuaji" ni nini?

Nikikulipa ujira unifikishie mzigo wangu nyumbani kwangu, mzigo ni wako au ni wangu?

Labda ingesaidia kidogo kufafanua mada yako ili ieleweke kwa wepesi.
Mimi ngoja nikupe mfano halisi kabisa:

Mzee Ally Mohamed Kibao aliyeuliwa kikatili kabisa.

Muuaji alikuwa ni aliyetoa amri huyo mzee auwawe; au hao wavuta bangi waliotoa roho yake na kuharibu maiti?

Ngoja nishauri: unapoandika mada kama hii, haisaidii kitu kutumia maneno meeeengi sana kama ulivyofanya hapa. Ingetosha tu kutumia mistari michache tu bila ya kumchosha msomaji wako, na kumchanganya akili.
 
Back
Top Bottom