Kazi ya kichwa ni kufikiri, si kufuga nywele!!!!!
Sikio la kufa halisikii dawa:flypig:Nilitegemea Mwanasheria mkuu atoe ufafanuzi wa kisheria badala ya kuzua malumbano ndani ya bunge. Nilitegemea aseme sheria inakataza nini, na inaruhusu bila ya kumtaki mwakilishi wa wananchi - personally. Lakini bado naendelea kujiuliza, kwa nini mwanasheria mkuu anaonekana kuwa ndio kiongozi wa juu bungeni? Uhuru wa bunge kama mhimili wa juu kabisa wa kuisamamia serikali uko wapi?
NB: Ninamuona @Dr F. Ndugulile hapa, niseme tu kwa nia njema, mwenendo wa uondeshaji bunge kwa sasa utawapa shida sana wabunge wa CCM 2015. Bunge limegeuka kuwa msemaji na mtetezi wa serikali, wananchi wamezibwa midomo kinyume cha sheria (ukimziba mdomo mwakilishi wa wananchi maana yake umewaziba midomo wananchi). Na kutokana na ukweli kwamba CCM ndio wengi, na uongozi wa bunge uko chini ya ccm basi itabidi wabebe lawama, wakumbane na chuki ya wananchi. Sina hakika kama wanaliona hil.
Yaani kwenye Chama Wajanja ni RA na EL, maana wamejitoa na wanaangalia Gemu kupitia luningaccm imemharibu werema, Huko nyuma hakuwa hivo, Ni Judge huyu bwana imenisikitisha sana aliingia na gia kubwa eti yeye si ccm na wakimzingua anautema uanasheria mkuu, now amekuwa ccm zaidi hata ya Nape na Mwigulu Machemba, ameishiawa kabisa akili ya kufikiri na kujibu hoja now anatukana bila hata haaya mweeeeee! ccm imeisha imebaki ni kuharibu 2 sasa.
Kinacho mtesa jaji mkuu ni ile kauli ya Tundu Lissu kuhusu majaji wasio na sifa waliochaguliwa kwa upendeleo na jk. Bila shaka kwa jinsi Werema anavyo pwaya kwenye nafasi yake naamini ni miongoni mwa hao majaji under jk umbrella.
Sikutegemea jaji mkuu anae jinasibu kuwa hana chama ana amka kumjibu mbunge wa upinzani kwa lugha inayo tafsrika kuwa ni tusi halafu naibu spika ambae ni mbunge wa ccm atetee kauli ya AG.
Baada ya tathimini kuonyesha kupwaya kwa kiti cha spika no wonder itakuja tathimini kupwaya kwa AG akiwa out weigh na Tundu Lissu. Kwa bunge hili TL ameonyesha ukomavu na ujuzi wa kisheria kuliko anae itwa Jaji mkuu.