hiyo redio huwa sisikilizi nowadayz huyo kibonde nilishauliza anapitiaga bar kwanza
coz ana mambo ya hovyohovyo allah ndo ajuaye na ndo sisikilizi tena :smash::A S thumbs_down:
Leo nilikuwa nasikiliza kipindi cha jahazi Clouds Fm, Kibonde, Kayanda na Wasiwasi walikuwa wanajadili kuhusu kufa kwa ATC, mjadala umeenda vizuri japo Kibonde alikuwa anaonekana mwenye jazba sana.......kilichonishangaza ni pale alipojidai kuwa ana machungu sana na kufikia hatua ya kutoa tusi la nguoni (k****m***m**k**)nadhani watu wazima mmenielewa, Hata wenzie aliokuwa nao niliwasikia wakicheka kichinichini kwa mshtuko walioupata na simu zikipigwa mfululizo,sasa linakuja swala la je....Clouds FM imekuwa ya kihuni namna hii kiasi ambacho imeanza kutoa matusi ya nguoni?
Nadhani kuna mliokuwa mnasikiliza pia,mtakubaliana na mimi. Kwa kweli ni fedheha.
Acha uongo, hata mimi pia nimesikiliza, hakuna sehem aliyotukana kama unavosema, hata kama angelikua ni mjinga kiasi gani asingeweza kutukana hilo tusi on air, punguza chuki.
no no no.....Kibonde simchukii kwa sababu hata nikimchukia simjui, na isitoshe mimi ni mpenzi sana wa kusikiliza Clouds, na inakuwaje leo kwa sababu nimemchukia nije niseme kuwa Kibonde ametukana wakati ni uongo?........
Acha uongo, hata mimi pia nimesikiliza, hakuna sehem aliyotukana kama unavosema, hata kama angelikua ni mjinga kiasi gani asingeweza kutukana hilo tusi on air, punguza chuki.
Shimo la taka ngumu.Acha uongo, hata mimi pia nimesikiliza, hakuna sehem aliyotukana kama unavosema, hata kama angelikua ni mjinga kiasi gani asingeweza kutukana hilo tusi on air, punguza chuki.
Mpende msipende, mkubali msikubali Kibonde yuko juu. Nina uhakika kabisa kama Tanzania tungekuwa na mfumo mzuri wa listener ratings basi kipindi cha Jahazi kingekuwa kiko juu sana katika muda wake kinapokuwa hewani (saa kumi mpaka saa moja jioni).
Kama kweli Kibonde angekuwa mbovu kama ambavyo wachache wenu mnavyotaka watu waamini basi nina uhakika kabisa wasikilizaji wa kipindi hicho wangekuwa wameshapungua tokea zamani.
Lakini inavyoelekea ni kinyume chake. Ili mtu uweze kujua na kumkasirikia kuwa leo kasema nini ni lazima u tune in kwenye kipindi cha Jahazi. Bila kumsikiliza utajuaje na (kujifanya) kukasirikia kile alichosema?
Kibonde kaza buti mwana. Uko juu. Simamia kile unachokiamini na usichoke wala kutishika kutoa maoni yako kwani wewe siyo reporter wala news anchor. Wewe ni commentator. Fani ya utangazaji kama commentator inakupa uhuru wa kutoa maoni yako kinyume na ilivyo wasomaji na waandishi wa habari ambao wanatakiwa kuandika na ku report facts.
Just remember this my brother. Dont let the haters faze you. Make your haters your motivators by becoming the number one hater aggravator in the whole wide world. I got your back son. Keep up the good work.
Hata KIU na magazeti mengine ya udaku yanasomwa na watu wengi kuliko Financial Times. Lakini hiyo haina maana kuwa hayo ni magazeti makini au ni kwa watu makini (japo mtu makini anaweza kuyasoma kwa sababu zake binafsi) kuliko Financial Times. Mwambie Kibonde aandike "article" juu ya maada yeyote ya kijamii (amekuwa kwenye mambo ya habari muda mrefu kwa hiyo anatakiwa awe na uelewa wa kawaida wa mambo yanayoihisu jamii) na aiwakilishe mahali - kwa mfano mdahalo wa kitaifa (achilia mbali wa kimataifa) uone kama itapita awamu ya kwanza ya mchujo.
amekutuma uje kumtetea? au ndio wewe mwenyewe kibonde unataka kujisafisha?tumesikiliza jahazi na tumemsikia akitoa tusi, jamaa la hovyo sana lile
Ni kweli katukana nimesikia,na wenzake wakacheka sana.
Naona Preta kanizidi spidi,nilikuwa nataka niweke hii taarifa.