matumizi ya Viagra yanasababisha upofu...

matumizi ya Viagra yanasababisha upofu...

baptist

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2013
Posts
434
Reaction score
279
Watafiti nchini Australia wanadai kwamba dawa
inayotumiwa kuongeza nguvu za kiume VIAGRA
husababisha upofu baada ya mda mrefu.
Kulingana na Watafiti hao kutoka Australia, kiungo
fulani katika dawa hiyo inayotumiwa kukabiliana na
ukosefu wa nguvu za kiume,huathiri uwezo wa kuona
miongoni mwa wanaume ambao wana ugonjwa wa
macho.
Kulingana na gazeti la Nation nchini kenya,Madaktari
nchini Australia wamebaini kwamba kiungo fulani
katika dawa hiyo kinaweza kusababisha upofu
miongoni mwa wanaume wenye tatizo la ugonjwa wa
macho.
Vilevile inadaiwa kuwa dawa hiyo pia inaweza
kuwaathiri watumiaji ambao wanaona vizuri.
Utafiti huo uliofanywa katika panya,ulibaini kwamba
hata watu wasio na ugonjwa wa macho wanaweza
kuathirika.
Source; BBC
 
Kumbe ndio maana macho yangu yamekufa... Na umri huu nshaanza kuvaa maglasi..itabidi niache viagra aisee..!
 
Kumbe ndio maana macho yangu yamekufa... Na umri huu nshaanza kuvaa maglasi..itabidi niache viagra aisee..!

Pole sana mkuu sasa ukiacha kutumia performance si itakuwa ya chini sana aisee
 
Back
Top Bottom