dr. mume na mke siri za nini?
kwa nini kuwe na siri kati yenu?
hata mie nashangaa hizi siri za kutotaka mke/mume azijue...
kama anaona "sehemu zako za siri"
password ya atm, mpesa, tigo pesa, mnashare, hakuna ambacho mnafichana..... then simu inakuwa na siri...mmmmmmmh nashangaaa mie
Huyu msichana nampenda sana tena sana na yeye ananipenda ..huwa sipendagi kushika simu yake ila kuna siku nilishika simu yake akaichukua ghafla akafuta meseji nikamuuliza kwa nini amefuta akasema kuwa imetoka kwa ex wake na hakutaka niione..sasa nimwache aendelee kuwasiliana na ex wake ama nifanyeje?
updates!
Jamani huyu msichana kweli anayo nia njema na mimi kweli? tar 26 nilimkataza asiwasiliane na ex wake huyo bila ya kunihusha akanielewa sasa tar 29 akambeep huyo ex wake wakawa wanachati kwenye yahoo.. ..
na wameahidiana kutumiana meseji ili wawe wanachati huko yahoomessenger
kweli huyu mdada ana nia njema na mimi kweli?halafu kial saa ananinunia nikimuuliza kuhusu huyo ex wake anakuwa kama mbogo ananuna mpaka basi..eti wadau hapa kuna maisha kweli hapa??
naomba kama una matusi uachane na thread yangu nahitaji ushauri na wala sio kebehi. najua sio vizuri kukagau vitu vya mpenzi wako ila ukiona kuna kitu kimebadiliak naona ni vema kukagua .. nafanya hivi kwani natyaka nioe na huu ndio umri wangu wa kuoa so sitaki niingie mkenge .
Regards!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
updates!!
huyu mrembo nimekutana naye leo tukakaa sehemu nikamuuliza
hence nimeshapewa jibu ..i m supposed to read between lines
Ivi siri na aibu kubwa ya binadamu si utupu/uchi? Lakini kwa nini unakuwa huru kuvua nguo zako mbele ya mkeo/mumeo? Mi nadhani huyo ni mtu ambaye unaweza kushare nae siri yako kubwa, so kwenye simu kuna siri gani ambayo hutaki mwenza wako aijue?
Aisee mtu kama sio mwaminifu sio mwaminifu tu hata kama asipoweka password kwenye simu haitasaidia,mimi mume wangu hajaweka password na hanikatazi kutumia simu yake ila kuna siku nikiangalia kwenye inbox hukuti received msg na wala hukuti sent msg!kadelete kila kitu.Nilichoka siku moja nilikua natumia laptop yake nikaona yahoo messenger chat zake nusu nife kwa kihoro,usiombe kabisa kukutwa!!!!nimekoma siku hizi siangalii chochote
ww acha kumdanganya mwenzio! ww mbona hufanyi hivyo?
Umeona eeh.
Mimi wala sishangai na sina muda wa kubishana na wanaotetea usiri wa simu kwa kuwa nijuavyo mimi 99% ya wanaume ni cheaters ...kwa hiyo usitegemee watakubali simu zao ziguswe na wake zao.
Ila mimi mume wangu atafute simu ya siri kani simu yake naigusa whenever I feel like...na analijua hilo. Privacy my foot!
Eti simu ni diary...mara ngapi zinakwapuliwa na vibaka??? Kazi gani unayofanya ambayo mke hapaswi kuijua??? Unauza madawa ya kulevya???
nyumba kubwa ndio maana nilisema pale mwanzo kuwa hapa tutazunguka mbuyu bure..Nijuavyo mimi watu wote wanaofanya kazi nyeti hawaruhusiwi hata kutumia private PC kwa shughuli za kikazi... Afu watu wanakuja na cheap explanation eti siri za kazini...Kazi zenye usiri uwa zinaishia ofisini. Acha kuwadanganya wake zenu.