Dr.Chichi
JF-Expert Member
- Apr 30, 2008
- 2,393
- 637
Mchana mzima unakaa kimya wala huhangaiki kumpigia simu bf wako. Saa 7 au 8 usiku eti ndo unaanza kumpigia, asipopokea kwa sababu yuko usingizini unaanza milawama, eti kashindwa coz yuko na mwanamke mwingine, mara oooh hunipendi vinginevyo ungepokea simu yangu na mengine mengi. Acheni hizo kina dada.
Kama mwanaume ni mkware anaweza akapokea simu yako na bado wakati anaongea na wewe hiyo saa 6, au 7 usiku pembeni kipo kidosho kinaramba koni. We unaridhika eti yuko salama kumbe ukikata simu tu, mtanange unaendelea.
Simu sio mlinzi wa penzi lako kwa bf au gf wako. Ishi tu kwa matumaini upate amani moyoni mwako!
Ni hayo kwa leo!
Wasalaaam!
kawaida sana hiyo..nimeshazoea,yaani naweka headphones anaongeeeeeeeeeea we mi naitikia tu majibu kama ok,really,tats good n.k mpaka nipitiwe na usingizi ndo anakata simu otherwise nisipoongea naye full ugomvi