kuna wengine uwa wanahandika ivyo kwa makusudi tu bira ya kukusudia.Kuna mtu kila akitext anaandika ''Nimehamua'' yaani hizo ''h'' kibao na hana uhusiano wowote na lafudhi/matamshi..sijui ni mazoea?!!
Tafadharini muhache kualibu rhugha ya taifa. Kwa kweri munakera na munahudhi sana!
Msikilize huyo msemaji AI anasema HeiHaiNimeshuhudia hii "h"ikiongezeka kwa kasi mahali isipohitajika. Kwanza ilianzia kwa wanamuziki wa bongofleva na sasa inaunguruma kote mitaani haswa kwenye kuandika ujumbe wa maneno kwa kutumia simu au barua pepe na huu ndio mwanzo wa kiswahili chetu kuingia gizani. Kwa mfano neno "utamuona mtoto" inaandikwa "hutamuona mtoto" hii ni maana tofauti na kilichokusudiwa "atakuja" "hatakuja" yaani balaa
Sent from my BlackBerry using JamiiForums
We jamaa kiboko. Umefukua kaburi la mwaka 2009!Gen-Z wengi wa Tanzania hawajui kiswahili fasaha kabisa. Utasikia mtu anasema eti "kocha ambaye ameweza kufukuzwa kazi"
Duh.Inanikumbusha nikiwa shuleni mwalimu wangu wa kihaya alikuwa anafundisha somo la Welding..sasa akawa anatusomea kama dictation tunaandika. Alisoma hivi;
"Werding is a process of joining two metars by eating" akimaanisha
"Welding is a process of joining two metals by heating"
mwanafuzi mmoja akaandika kama mwalimu alivyosoma basi wakati mwalimu anakagua madaftari akakosoa kwa kusema...
iri jamaa eti rimeandika HEATING ya kura badala ya EATING ya Moto!
Mwisho wa kunukuu!