whitehorse
JF-Expert Member
- Aug 29, 2009
- 2,565
- 4,426
Hizo ni swaga... Lakini hiyzo misuse za h na a au l na r ni udhaifu kutokana ana lugha ya asili ya mtumiaji ndio mana utakuta kwenye kuandika na kutamka vinafanana lakini xaxa kwenye kutamka ataitamka vizuri tu kama sasani upepo tu huwa unapita mfano kuna kutumia sana "x" badala ya "s" kwa mfano sasa inaandikwa "xaxa"...lakini yalikuwepo yapo na yatakuja cha msingi yoote yatapita.............
Kuna mtu kila akitext anaandika ''Nimehamua'' yaani hizo ''h'' kibao na hana uhusiano wowote na lafudhi/matamshi..sijui ni mazoea?!!
Aisee matumizi ya h na r na l yanakera! Unaweza kukosa mchumba bila kujijua. Ila inaweza kukukosesha kazi. Imagine ni mkataba wa kisheria ama legal document yoyote. Ni kweli tujiangalie.
hafadhari yakoIla hapo kwenye r na l tunahitaji maombezi wengine though hali si mbaya ila kuna ambao ni tatizo kubwa, ila mie ninaahidi kuanzia leo nimeHamua kuacha kuchanganya matumizi ya r na l
Inanikumbusha nikiwa
shuleni mwalimu wangu wa kihaya alikuwa anafundisha somo la
Welding..sasa akawa anatusomea kama dictation tunaandika. Alisoma hivi;
"Werding is a process of joining two metars by eating" akimaanisha
"Welding is a process of joining two metals by heating"
mwanafuzi mmoja akaandika kama mwalimu alivyosoma basi wakati mwalimu
anakagua madaftari akakosoa kwa kusema...
iri jamaa eti rimeandika HEATING ya kura badala ya EATING ya Moto!
Mwisho wa kunukuu!
Inanikera sana hayo matamshi
mhaya piga ua binua "karagaza" hawezi kuacha h
nimekumbuka jamaa mmoja mkurya alitaka kujua spelling za neno kama ni 'r'au 'l' alimuuliza mwalimu kwamba hapo ni 'eroo' au 'araa',watu hatuna mbavu.