Matumizi ya "h" yamekithiri

whitehorse

JF-Expert Member
Aug 29, 2009
2,565
4,426
Nimeshuhudia hii "h"ikiongezeka kwa kasi mahali isipohitajika. Kwanza ilianzia kwa wanamuziki wa bongofleva na sasa inaunguruma kote mitaani haswa kwenye kuandika ujumbe wa maneno kwa kutumia simu au barua pepe na huu ndio mwanzo wa kiswahili chetu kuingia gizani. Kwa mfano neno "utamuona mtoto" inaandikwa "hutamuona mtoto" hii ni maana tofauti na kilichokusudiwa "atakuja" "hatakuja" yaani balaa

Sent from my BlackBerry using JamiiForums
 
Mh naona huku niliko tuko nyuma sana sijawahi sikia hiyo maneno, au bdo hayajakithiri kuja "hupande" huu
 
Waborongaji wa matumizi ya h na a ni sisi wahaya..tukisema hayupo huitamka na kuiandika ayupo
tukimaanisha anakuja huitamka au kuiandika hanakuja
tatizo letu hatutaki kujifunza wala kukubali hilo ndio maana hata kabila letu huandika au kutamka M-aya
 
Aisee matumizi ya h na r na l yanakera! Unaweza kukosa mchumba bila kujijua. Ila inaweza kukukosesha kazi. Imagine ni mkataba wa kisheria ama legal document yoyote. Ni kweli tujiangalie.
 
Nilikuwa sijui kuwa wahaya wana matatizo ya aina hiyo.ila ukichunguza vizuri utagundua kuwa wahanga wa wakubwa wa tatizo hilo ni hiki kizazi kilichopitia english media kuanzia chekechea. Wako vizuri kuandika kiingereza lkn ukiona wanavyoandika kiswahili ni aibu tupu.

Nadhani hizi shule za english media hazina walimu wazuri wa somo la kiswahili na wala wanafunzi hawana mwamko wa kukazania lugha yetu
 
ni upepo tu huwa unapita mfano kuna kutumia sana "x" badala ya "s" kwa mfano sasa inaandikwa "xaxa"...lakini yalikuwepo yapo na yatakuja cha msingi yoote yatapita.............
 
ni upepo tu huwa unapita mfano kuna kutumia sana "x" badala ya "s" kwa mfano sasa inaandikwa "xaxa"...lakini yalikuwepo yapo na yatakuja cha msingi yoote yatapita.............
Hizo ni swaga... Lakini hiyzo misuse za h na a au l na r ni udhaifu kutokana ana lugha ya asili ya mtumiaji ndio mana utakuta kwenye kuandika na kutamka vinafanana lakini xaxa kwenye kutamka ataitamka vizuri tu kama sasa
 
Kuna mtu kila akitext anaandika ''Nimehamua'' yaani hizo ''h'' kibao na hana uhusiano wowote na lafudhi/matamshi..sijui ni mazoea?!!
 
Inanikumbusha nikiwa shuleni mwalimu wangu wa kihaya alikuwa anafundisha somo la Welding..sasa akawa anatusomea kama dictation tunaandika. Alisoma hivi;
"Werding is a process of joining two metars by eating" akimaanisha
"Welding is a process of joining two metals by heating"
mwanafuzi mmoja akaandika kama mwalimu alivyosoma basi wakati mwalimu anakagua madaftari akakosoa kwa kusema...
iri jamaa eti rimeandika HEATING ya kura badala ya EATING ya Moto!
Mwisho wa kunukuu!
 
Aisee matumizi ya h na r na l yanakera! Unaweza kukosa mchumba bila kujijua. Ila inaweza kukukosesha kazi. Imagine ni mkataba wa kisheria ama legal document yoyote. Ni kweli tujiangalie.

Ila hapo kwenye r na l tunahitaji maombezi wengine though hali si mbaya ila kuna ambao ni tatizo kubwa, ila mie ninaahidi kuanzia leo nimeHamua kuacha kuchanganya matumizi ya r na l
 
Tumezidi kutumiha "h" ata hambapo apastaili. Tuhache, siho poha kabisa!!
 
Inanikumbusha nikiwa
shuleni mwalimu wangu wa kihaya alikuwa anafundisha somo la
Welding..sasa akawa anatusomea kama dictation tunaandika. Alisoma hivi;
"Werding is a process of joining two metars by eating" akimaanisha
"Welding is a process of joining two metals by heating"
mwanafuzi mmoja akaandika kama mwalimu alivyosoma basi wakati mwalimu
anakagua madaftari akakosoa kwa kusema...
iri jamaa eti rimeandika HEATING ya kura badala ya EATING ya Moto!
Mwisho wa kunukuu!

nimekumbuka jamaa mmoja mkurya alitaka kujua spelling za neno kama ni 'r'au 'l' alimuuliza mwalimu kwamba hapo ni 'eroo' au 'araa',watu hatuna mbavu.
 
Matamshi inaeleweka kwamba ni athari za lugha mama!
Ila hadi kuandika?? Yaani hata ubongo na vidole vinaathirika na lugha mama??
Na kuna wengine wako mbali zaidi, wanachanganya 'ra' na 'la'....mtu anauliza hivi Lama amerara (Rama amelala)?

Inanikera sana hayo matamshi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom