Matumizi na Faida za Asali katika afya ya binadamu

Kwa Wanawake wanaotaka kupunguza unene Watumie asali hebu soma hapa

Siri Kubwa ya Asali katika Suala zima la Kupunguza Unene. Unaweza kushangaa kivipi Asali inaweza kupunguza uzito wa mtu wakati ina sukari ambayo huongeza uzito? Napenda kukutoa wasiwasi kuwa sukari iliyomo kwenye asali siyo sawa na sukari unayoijua wewe. Asali ina uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo mengi sana ya kiafya mwilini na ni moja kati ya maelefu ya vyakula vya maajabu tulivyoletewa na Mungu.

Lakini kabla sijaanza moja kwa moja kueleza kuhusu asali na uwezo wake wa kupunguza uzito wa mwili, ningependa kuelezea kwa kirefu kwanza kuhusu uzito wa mwili na kanuni za kupunguza au kuongeza uzito wa mwili.

Awali ya yote, ili upunguze au uongeze uzito, unahitaji kujua mwili wako unafanyaje kazi, vitu gani vinachangia kuongeza au kupunguza uzito. Upi ni uzito wako sahihi? Mwili wako hufanyakazi kiasi gani kwa siku? Mwili wako unahitaji chakula (calories) kiasi gani kwa siku kulingana na kazi unazozifanya? Pia utajijuaje kama ni mzito sana (overweight) au mwepesi sana (underweight)?

Hivyo ili kufikia malengo ya kupunguza au kuongeza uzito, utahitaji kuwa na taarifa kamili kuhusu mwili wako (Personal Profile) ambazo zitakuwezesha kufanya mabadiliko na kuyafuatilia ipasavyo wakati wa kuanza programu ya kupunguza au kuongeza uzito.

Napenda kukutahadharisha mapema kuwa suala la kupunguza uzito kiafya halina ‘shot kati’, unatakiwa kuwa mvumilivu, kwa sababu huwezi kuona matokeo kama utapuuzia ushauri wa kuacha mazoea ya ulaji mbaya. Kama vile ambavyo hukunenepa au kukonda kwa siku moja, ndivyo ambavyo hutaweza kupunguza au kuongeza uzito kwa siku moja, hivyo usivunjike moyo mapema unapoona hufikii lengo lako mara moja.

Halikadhalika, utatakiwa kufanya mabadiliko ya chakula unachokula na wakati mwingine kukiacha kile ulichokuwa ukikipenda sana, pia lazima ujishughulishe usiwe mtu wa kukaa na kulala tu. Kabla ya kuanza programu ya kupunguza uzito, jipime kwanza kujua una kilo ngapi na jiwekee malengo kupunguza kilo, ya kuanzia wiki moja hadi kumi.

Katika kipindi hicho cha wiki 10, wiki nyingine unaweza kupunguza kilo 2, wiki nyingine unaweza kupunguza kilo 1, lakini katika wiki nyingine unaweza usipunguze hata nusu kilo, ikitokea hivyo usitilie mashaka mpango wako, endelea tu.

Katika kupima uzito, kuna vitu viwili huzingatiwa ambavyo ni uzito na urefu wa mtu. Uzito wa binadamu umegawanywa katika makundi manne: Uzito mdogo (Underweight), uzito bora kiafya (healthy weight), uzito mkubwa (overweight) na uzito wa kupita kiasi (obesity).

Ili uweze kujijua uko kwenye kundi gani, unapaswa kuujua urefu na uzito wako kwa sasa (Body Mass Index (BMI). Mfano, watu wenye urefu wa kuanzia futi 5 hadi futi 6, uzito unaokubalika ni kati ya kilo 60 na 75. Ukizidi hapo utatakiwa kuupunguza. Pia katika urefu huo ni hatari zaidi kiafya kuwa na uzito zaidi ya kilo 110. Halikadhalika, mwenye urefu huo, kuwa na uzito chini ya kilo 55 ni hatari kiafya.

Kama nilivyosema hapo awali, somo la kupunguza au kuongeza unene linahitaji uelewa mzuri ili ufikie lengo lako ulilojiwekea. Tumeshalitambua vyema suala la uzito.
 
KANUNI ZA KUPUNGUZA UZITO
Kanuni ya kwanza ya kupunguza uzito inatueleza kuwa ili mtu upunguze uzito, unahitaji kutoa kalori nyingi mwilini na kuingiza kalori kidogo (Less Calories In + More Calories Out= Weight Loss). Kwa lugha nyepesi, unapokula chakula chochote unaingiza kalori mwilini na unapofanya mazoezi au kazi yoyote unatoa kalori mwilini.

Hivyo kupunguza unene ni lazima ujinyime kula ili uingize kalori kidogo lakini ufanye sana kazi au mazoezi ili utoe kalori nyingi mwilini. Baadhi ya watu wamesema kuwa wanajinyima kula lakini hawapungui. Kujinyima kula peke yake hakutoshi kama hufanyi kazi au mazoezi yoyote ya kutoa kalori nyingi kuliko unazoziingiza mwilini mwako.

ASALI KATIKA KUSAIDIA KUPUNGUZA UNENE

Baada ya kuzingatia kanuni hiyo, hatua inayofuata ni matumizi ya asali kwa mpangilio maalum unaoweza kukusaidia kuyeyusha mafuta mwilini kwa haraka, wakati ukifanya mzoezi na kujinyima kula.

Matumizi ya asali ni rahisi sana. Kwanza kabisa hakikisha unapata asali halisi mbichi na siyo asali feki. Mjini kuna baadhi ya watu hutengeneza vitu mfano wa asali, matumizi ya asali hiyo hayawezi kukusaidia zaidi ya kukuletea matatizo mengine ya kiafya.

Kuna kampuni na maduka (kama super markets) zinazouza asali halisi, nunua asali mbichi kutoka sehemu inayoaminika. Kula vijiko viwili (vya chai) vya asali kila siku wakati wa kwenda kulala. Katika muda wa saa nne za mwanzo za usingizi, asali itayeyusha mafuta (fat) mengi mwilini sawa na kufanya mazoezi makali.

Mwanzilishi wa dayati hii ni Mike McInnes ambaye yeye ni raia wa Scottland na kitaaluma ni Mfamasia. Mtaalamu huyu aligundua kwamba wanariadha ambao hula matunda yenye virutubisho vingi vya ‘fructose’ (kama vile matunda yaliyokaushwa na asali) hupunguza mafuta mengi mwilini na huwa na stamina nyingi.

Ili kufaidi vizuri manufaa ya asali katika kukusaidia kupunguza unene na mwili kuupa nguvu, ni vizuri ukatumia asali hiyo kama ilivyoelezwa hapo juu huku ukifanya mazoezi ya viungo, angalau mara tatu kwa wiki.

Ni lazima ieleweke kwamba vitu vitatu lazima vifanyike kwa pamoja ili kupunguza unene kama unavyokusudia. Kitu cha kwanza ni kula vyakula sahihi na kwa kiasi kidogo, pili kula asali halisi na mbichi kila siku kabla ya kulala na tatu kufanya mazoezi au kazi nzito ili kutoa kalori mwilini. Umuhimu wa asali hapa ni ule uwezo wake wa kuyeyusha mafuta mwilini kwa haraka ukiwa umelala na wakati huo huo kuupa mwili stamina.

ASALI NA MDALASINI

Mchanganyiko mwingine ambao umeelezwa kusaidia sana kupunguza uzito, ni asali na unga wa mdalasini. Mchanganyiko huu ni kama kinywaji ambapo utatakiwa kuchanganya Asali, Mdalasini na maji moto kisha kunywa mara mbili kwa siku.

Ili kupata mchangayiko unaotakiwa, chukua nusu kijiko cha unga wa Mdalasini (kijiko kidogo cha chai) kijiko kimoja cha Asali (kipimo cha kijiko cha chai) na kikombe kimoja cha maji yaliyochemka.

Anza kuchanganya maji moto na unga wa Mdalasini, koroga hadi uchanganyike vizuri kisha funika na uache muda wa nusu saa ili maji yapoe. Baada ya maji kupoa, weka asali yako kijiko kimoja kisha koroga tena hadi mchangayiko wako uwe kama kinywaji.
 
Big up sana man, maana mi ninatatizo la nguvu za kiume pia. huwa najitahidi sana nisitumie vidonge vya chemicals, thanx God i hope nimepanta njia mbadala. kwa kuongezea tu ni tunda gani also linaongeza nguvu za kiume ukiacha asali maana huku kwetu asali ni mtihani mkubwa sana katika upatikanaji wake.
 
Nadhani mkubwa umetoa msaada mkubwa sana.
Thans to that.
Nakupa Faida nyingine ya asali kila siku unapoamka Asubuhi jaribu kula kijiko kimoja kikubwa cha kulia wali cha Asali kabla ya kula kitu na unapomaliza chakula cha usiku tumia hivyo hivyo kama ulivyotumia Asubuhi Fanya hivyo kwa muda

wa siku 40 Hiyo Asali itakusaidia kusafisha uchafu uliokuweko kwenye ini lako na Figo lako. Hiyo nimekupa mimi kama zawadi yangu kwako. Asali inatibu Maradhi mengi sana nikijaribu kueleza ninafikiri naweza hata kujaza page hata 10 Asali ni dawa ya kila Maradhi mkuu.
 
Some months ago nilikuwa na utaratibu huo and frankly speaking mabadiliko hayo niliyapata, every party of my body was extremely strong.
Na kutokana na kuikubali na kui promote ndiyo maan nilistuka kidogo niliposikia madhara yake kwa mimba changa.
 
Unajuwa kitu kinachoitwa Mimba? inatakiwa huyu mwenye hali ya mimba awe muangalifu sana haswa wakati wa mwanzo wa hiyo utungo wa mimba lakini ikisha kuwa kubwa basi kunakuwa na matatizo madogo tu sio makubwa kama ya mwanzo wa tungo wake haswa kuanzia hiyo mimba wiki ya 1 mpaka wiki ya 12) . Akifikisha tu mimba miezi 4 huwa kinakuwa sasani kiumbe kamili kwa hiyo matatizo yapo ila sio mengi kuliko mwanzo. Asali ni

Dawa nzuri sana kwa binadamu wote haina madhara yoyote wala Side affective mimi maisha yangu huwa natumia hiyo asali na huku nilipo ingawa nipo kwenye nchi za baridi huwezi kupata asali safi lakini natumia ili inilinde na baridi nipo kwenye nchi za baridi nakula Asubuhi ninapoamka na usiku pia Asali pia inasaidia nguvu za kiume.
 
wanajamvi naomba ushauri wenu asali mbichi ambayo haijachanganywa iwe ya nyuki wadogo ama wakumbwa inamadhara gani kwa wanawake wajawazito wenye mimba changa ( wiki 1- wiki 12) kwani nina rafiki yangu wa karibu mkewe alikuwa mjamzito hana tatizo lolote akalamba asali ya nyuki wadogo mbichi isiyochanganywa hakumaliza masaa 12 ujauzito wake ukatoka na alikuwa na mimba ya wiki 7.
Mamamkwe wake yaani mama wa mkewe akamwambia kuwa asali huwa inaharibu sana mimba hivyo hakupaswa kumpa mkewe asali kwani ndio chanzo cha mimba kuharibika, na walipokwenda kwa daktari wa kina mama alipomchunguza hawakuona tatizo lolote lilo sababisha mimba kutoka kwani mama hakuwa akisumbuliwa na kitu chochote kile.

Naomba kujua kama kuna mtu hhumu jamvini anaweza kunifafanulia kama ni kweli asali inaharibu mimba zikiwa changa!!
Nawakalisha
asali kama asali haiwezi kusababisha mimba kutoka hata siku moja sema huyo dada amechezewa kitu asichokijua na asali imekuwa kama kisababishi.watu wakitaka kukuharibia kitu kimazingara wanatafuta kwanza kisababishi ndipo wanatenda walichukusudia.kama vipi nendeni na kwenye maombi nawaambia mtajua sababu ya mimba kutoka ni nini hiyo asali ni kizugio tu cha washirikina.pia aangalie kama ana bifu na mashangazi na wakwe zake iyo itakuwa mwanzo mzuri,na ni nani alimletea hiyo asali au a;limshauri ale asali..
 
Wanajamvi nawashukuruni sana sana tena sana kwa mawazo yenu nitakachokifanya naprint coment zote nampelekea muhusika ingawa nani nimefunguka kwa matibabu ya asali. Asanteni sana
 
Mzizi mkavu, God bless you, nilienda kijijini kwenye likizo fupi, nikanunua dumu la lita 20, kila siku wakati naangalia taarifa ya habari, saa mbili usiku baada ya kutoka kazini, naweka kwenye kisosi nakula taraiibu! mi nilifuata utamu tu wa asali, kumbe nimepatia?! Thanx a lot for this useful info.
 
Umefanya jambo la maana mimi huku nilipo hakuna Asali safi mbichi na hata ukipata inaweza kufika kwa bei ya huko nyumbani ni Shillingi laki 1 huwa Asali wanachanganya na Sukari si rahisi kupata asali Safi Mbichi

mimi huwa naagiza Vijijini ndio wananiletea huku nilipo Ughaibuni Majuu natumia Asali kwa ajili ya mwili nipate joto maana baridi ya huku ni kali kuliko huko kwetu Tanzania. Nakuonea Wivu unayo Asali safi Mbichi orignal. Tumia hiyo Asali kila siku unapo amka Asubuhi

kijiko kimoja kikubwa cha kulia wali kula kabla ya kula kitu baada ya kama masa 2 ndio waweza kula chai na chakula chochote kile. Na Wakati wa usiku unapomaliza kula chakula cha Usiku tumia hiyo Asali kijiko kimoja kikubwa cha kulia wali fanya hivyo kila siku katika maisha yako ukitumia kwa njia hiyo,

inasaidia hiyo Asali kuondosha na kusafisha Uchafu uliopo kwenye Ini (Liver) na Figo (Kidney) na hapo ndipo penye matatizo makubwa ya binadamu huwa yananzia hapo kwenye tumbo la binadamu nakutakia kila la kheri . Tumia Asali GOD Bless you too.
 
Thanx a lot
 
Wana JF
Mambo mengi yanasemwa juu ya asali kama hujatambua faida ebu nikujazie zaidi. Asali ni zaidi ya dawa na chakula ndani yake kuna uhai ukila asali maisha yako yatakuwa marefu sana . Mwenyezi Mungu ameweka siri kubwa sana ndani ya asali hakuna sababu ya kuoji wewe tumia asali utapata maajabu yake kwa muda mfupi. Unaweza kufuga nyuki nyumbani na ukajipatia asali halisi penda asali mpende nyuki.
Kula na tumia na iwe chaguo lako halisi la kila siku.
 
Attachments

  • ISMANI VISIT 117.JPG
    ISMANI VISIT 117.JPG
    589.9 KB · Views: 114
Na mola wako mlezi amemfunulia Nyuki:jitengenezee majumba yako katika milima na katika miti na katika wanayo jenga watu. Qur'an 16:68

Kisha kula katika kila matunda na upite katika njia za mola wako mlezi zilizofanywa nyepesi kuzipita na kutoka matumbo yao kinatoka kinywaji chenye rangi mbalimbali ndani yake kina matibabu kwa wanadamu. Hakika katika haya ipo ishara kwa watu wanaofikiri. Qur'an 16:69
 
Swadakta umesema kweli Qur'an 16:68 haisemi maneno ya uongo asilani Qur'an ninaiamini asilimia 1000 Asante Mkuu.
 
jaman cjaelewa hapo kwny asali na ndimu,nliambiwa ni sumu ukila unaweza kufa,iweje hapo umeitaja?
Nani kakwambia Ukila asali na ndimu unaweza Kufa kuna Ushahidi wowote ule? Je kuna Mtu aliyekufa kwa ajili ya kula Ndimu na asali? Leteni ushahidi wenu sio maneno matupu tu.
 
Back
Top Bottom